Kwaheri 2011 kwa mafundisho, karibu 2012 kwa wema barani Afrika.
Mwaka 2011 utakumbukwa na Waafrika kama mwaka ambao ulikuja na majonzi na furaha ya kihistoria, hasa kwa kizazi cha tatu cha bara la Afrika.
Kizazi cha tatu cha Afrika, ni wale wote waliozaliwa miaka ya 70 hadi miaka ya 90 tangu Afrika ipate uhuru kutoka kwa wakoloni na mwaka 2011 na chini ya uongozi wa demokrasi wameongozwa na kubadika kuliko walivyo tarajia.
Kizazi hiki cha tatu cha Waafrika waliozaliwa miaka ya 70 na hadi 90 wameweza kuona mabadiliko ya kijamii, kisayansi, kiuchumi na siasa ambayo wengi hawakutarajia kuyaona kwa muda mfupi wa maisha walioishi kulinganisha na baba mama, mababu na mabibi waliopigania uhuru.
Mwaka 2011 mengi yametokea, hasa kubwa katika swala la kisiasa chini ya kiongozi demokrasi na kuleta mauaji na machafuko katika bara la Afrika tangu uhuru.
Kizazi hiki cha tatu ambacho wengi wana miaka kati 45 na 20 chini ya kiongozi demokrasi ambaye amewafanya kujitambua yakuwa wanahitaji mabadiliko na kuanza kuyatekeleza kwa njia tofauti.
Yaliyofanyika kimabadiliko chini ya kiongozi demokrasi yameonekana na sehemu ya matokeo yake yameaanza onekana na mengi matokeo yapo njiani yanakuja.
Jambo ambalo lapaswa kukumbukwa na kizazi cha tatu cha Afrika tangu uhuru ni kwamba swala la uangalifu na umakini utazamwe kwa undani ni kwa jinsi gani kiongozi demokrasi anavyo ongoza katika kuleta mageuzi.
Na vile vile ieleweke ya kuwa binadamu ameumbwa kuwa na tofauti, na kama hizo tofatuti zikifanyiwa kazi kwa lengo moja mazuri yatafanyika na kuleta haki na amani.
Kwani naimani yakuwa kizazi cha tatu cha bara la Afrika tangu uhuru kina lengo la kuleta maendeleo katika bara la Afrika.
Na kwa viongozi waliopo ningependa kuwakumbusha yakuwa kuongoza ni mthiani mkubwa ambao ipo siku watapata majibu yao kama walifauru au walishindwa.
Ikumbukwe kuwa wazazi wetu, mababu na mabibi walipo kuwa wanapigania uhuru walikuwa wanajua wafanyalo, hivyo basi kizazi cha tatu cha Afrika chini ya kiongozi demokrasi umakini unatakiwa ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa.
Yaliyo tokea mwaka 2011 chini ya kiongozi demokrasi yameleta matokeo ambayo lazima kuyatafakari kwani mtutu wa bunduki na nchi ya mkuki siyo chanzo cha haki sawa kwa wote.
Hivyo basi mabaya yaliyo tokea mwaka 2011 yawe ni fundisho na yasirudiwe na tuanze mwaka 2012 kwa malengo mazuri.
Kwaheri 2011 kwa mafundisho na karibu 2012 kwa wema barani Afrika.
Mungu Ibariki Afrika.
Mungu wabari wale wote wapendao Haki na Amani duniani.
Kwaniaba ya launite.blogspot.com tunawatakia heri ya mwaka mpya 2012 na Mungu atubariki wote. Amina
Mhariri.
Saturday, December 31, 2011
Kwaheri 2011 kwa mafundisho, karibu 2012 kwa wema barani Afrika.
Posted by Kibatala at Saturday, December 31, 2011 0 comments
Marekani na na nchi za UAE zakubaliana kikataba ya kiulinzi.
Washington, Marekani - 31/12/2011. Serikali ya Marekani na umoja wa shirikisho wa nchi za Kiarabu United Arab Emarates zimekubaliana kuwekwa mitambo ya kiulinzi katika nchi za UAE.
Makubaliano hayo ambayo yalisainiwa 25/12/2011, yatiwezesha Marekani kuweka mitambo yake ya ulinzi katika nchini hizo.
Msemaji wa serikali George Little alisema "mkataba huo ambao utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani $3.48billion na itasidia kuimarisha ulinzi katika nchi hizo."
Mkataba huu utawezesha kuwekwa kwa mitambo ya kuzuia mabomu, mitambo ya mashabulizi 96, rada na mitambo mingine ya kiulinzi.
Marekani na umoja wa shirikisho wa nchi za Kiarabu zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa muda mrefu jambo ambalo limeziwesha nchi hizi mbili kushirikiana katika maswala ya kiuchumi na kiulinzi.
Jeshi la Ethiopia laingia nchini Somalia.
Beledweyne, Somalia - 31/12/201. Jeshi la Ethiopia limefanikiwa kushikiria mji wa Beledweyne kutoka mikononi mwa kundi la Al-Shabab.
Kundi la Al Shabab limedai kuyaondoa majeshi yake katika eneo hilo baada ya kuzingirwa na jeshi la Ethiopia.
Kwa mujibu wa wanchi waliona wanajeshi wa Ethiopia walisema " tumeona magari ya kijeshi yakizunguka zunguka hapa mjini tangu jana."
Habari kutoka jeshi la Ethiopia zinasema "jeshi la Ethiopia limeamua kuisaidia Somalia baaday ya serikali hiyo ya Somalia kuomba msaada."
Wakati huo huo habari kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Somalia zinasema " serikali ya Somalia imetangaza ukombozi na kuhaidi kupambana na kundi la Al-Shabab kwa kila hali na tutaomba kila msaada kwa nchi majirani ili tuweze kulinada nchi yetu na kuliangamiza kundi la Al-Shabab."
Kundi la Al-Shabab limekuwa likipambana na serikali ya Somalia kwa muda mrefu jambo ambalo limeifanya serikali kushindwa kufanya shuighuli zake za kusaidia wananchi na kuijenga nchini.
Kim Jong Un ateuliwa rasmi kuwa kiongozi wa Korea ya Kaskszini.
Kim Jong Un ambaye aliongoza mazishi ya baba yake na kuhusishwa na maswala ya serikali kabla ya baba yake Kim Jong Il kufariki ameteuliwa rasmi kuwa kiongozi wa chama tawala cha wafanyakazi ana ambacho ndoyo kinacho ongoza nchini hiyo.
Kuteuliwa huko kwa Kim Jong Un atakuwa kiongozi wa jeshi na kuwa na madaraka ya juu katika nchi hiyo.
Kwa mujibu wachunguzi wa mambo ya kisiasa na maswala ya ulinzi wanadai huenda mrithi huyo akawa mgumu kushirikiana naye kwa kuzingatia ya kuwa amezungukwa na watu waliokuwa wanafanya kazi na baba yake.
Posted by Kibatala at Saturday, December 31, 2011 0 comments
Friday, December 30, 2011
Rais Hugo Chavez atilia wasiwasi Marekani kuhusu kuugua ugonjwa wa tarasini-kansa.
Posted by Kibatala at Friday, December 30, 2011 0 comments
Thursday, December 29, 2011
Iran na Marekani zavutana kwa maneno juu ya ghuba ya Strait Hormoz
Homs,Syria -29/12/2011. Mmoja wa wajumbe wanaoakagua hali ilivyo nchini Syria kutokana na vurugu za kisiasa na ambaye raia wa Sudan ameongelea hali ilivyo hadi sasa nchini Syria.
Jenerali Mohamed Ahmed Mustafa al Dabi alisema "ingawa sehemu nyingine zilikuwa za kuoesha yakuwa kulikuwa na machafuko, lakini tulivyo fika maeneo mengi hayukuonekana kutisha na hali ilikuwa shwali na hatukuona vifaru vya jeshi ili tuliona gari za jeshi, na ningependa mkubuke ya kuwa hii ilikuwa siku ya kwaza tangu tuanze uangalizi wetu."
Hata hivyo maoni ya Jenerali Dabi yalitiliwa wasiwasi na nchi za Magharibi kwa kusema ya kuwa maoni ya ke ni ya mwazo tu."
Nazo habari kutoka ofisi za umoja wa nchi za Kiarabu zilisema, "maoni ya Jenerali Mohamed Mustafa Dabi yanathaminika kwani ni muhimu kwa kuzingatia yeye nimwanajeshi na mwana diplomasia vilevile."
Syria imetembelewa na wakaguzi 50 wa nchi za jumuiya ya Kiarabu, ili kutathmini hali halisi ya matatizo ya kisiasa yanayo endelea nchini humo.
Posted by Kibatala at Thursday, December 29, 2011 0 comments
Monday, December 26, 2011
Miaka 20 yatimia tangu kuvunjika kwa USSR.
Pakistani na China kushirikiana kiukaribu zaidi.
Isamabad, Pakistan - 26/12/2011. Serikali ya Pakistan na China zimehaidi kushirikaiana kikamilifu ilikudumisha uhusiano uliopo.
Hayo yaliongelewa na rasi wa Pakistani Asif Ali Zardari na mgeni wake mwakilishi wa serikali ya China kamishna Dai Bingguo.
Kukutana huko kumekuja katika kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wa China na Pakistani.
Beijing na Islamabad zilitiliana sahii mkataba wa kibiashara wa $1.6 billion ambapo nchini hizi mbili zitaweza kubadilishana kibisahara na kupunguza kutegemea mzunguko wa pesa.
Uhusiano wa China na Pakistan umekuwa wa karibu saana na hata kufikia kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika mji wa Jhelum uliopo Pakistan.
Brazil yakuwa kiuchumi na kuipita Uingereza.
Rio de Janairo Brazil - 26/12/201. Kitengo kinacho shughulikia maswala ya uchunguzi wa uchumi duniani Centre Economics and Business Research CEBR kimetangaza matokeo ya maendeleo ya kiuchumi duniani.
CEBR imeripoti " Brazil imekuwa nchi ya sita kiuchumi na kuipita nchi ya Uingereza kutonaka kukua uchumi kwa 7.5% sambamba na mipango mbinu ya uzalishaji wa bidhaa zinazo tumika na kuuza vitu vyake hasa nchini China na kuagizia vitu vichache kutoka nje ya nchi (Brazil)."
Kitengo hicho kimetabiri ya kuwa huenda Urusi ikakuwa kiuchumi ifikapo mwaka 2020 kwani kwa sasa ni ya tisa na nchi za Ulaya huenda zikadondoka kiuchumi ifikapo 2020.
Syria yahaidi kushirikiana na wajumbe wa jumuiaya ya nchi za Kiarabu waliopo nchini humo.
Damascus, Syria - 26/12/2012. Wajumbe wa umoja wa nchi za Kiarabu wamehakikishiwa kupata ushirikiano wa kila aina kutaka serikali ya Syria.
Habari kutoka serikali ya Syria zinasema " serikali itashirikiana kikamilifu katika kuahakikisha ya kuwa mipango yote iliyo pendekezwa na umoja huo zinafuatwa."
Mkurugenzi wa maswala ya unangalizi wa Mashariki ya Kati Haisham Jaber alisema "habari zinazo tolewa na vyombo vya habari zinaelezea vifo vya watu , lakini havielezei ya kuwa pia makundi ya upinzani ya wanajeshi ambao wanapigana na serikali, na nibora kutenganisha kati wa wanajeshi wapinzani na raia na hii ndiyo inaweza kuwa chanzo cha ugumu wa kazi kwa wajumbe wa jumuiya ya Kiarabu waliopo nchini Syria."
Wajumbe hao ambao waliwasili nchini Syria, wamekuwa na wakati ngumu, kutokana na hali ya mvutano wa kisiasa na misimamo na malengo ya vyama vya upinzani vinavyo pinga serikali ya Syria iliyopo chini ya rais Bashar al Assad.
Miaka 20 yatimia tangu kuvunjika kwa USSR.
Moscow, Urusi - 26/12/2011. Wanchi waliokuwa katika shirikisho la nchi za United Soviet Socialist Repiblic USSR wanaadhimisha miaka 20 tangu kuvunjika kwa shirikisho hilo.
Shirikisho hilo ambalo liliundwa 1922 lilivunjika chini ya uongozi rais Mikhail Gorbachev na nchi zote ambazo zilikuwa katika shirika hilo kuwa nchi huru na kuanza kujijenga ka nchi.
Hata hivyo waziri mkuu wa sasa wa Urusi Vladmir Putin alisema "kuvunjika kwa shirikisho hilo ni moja ya makosa ya kihistoria ya karne ishirini na ishirini na moja." Waziri mkuu Putini aliyasema haya wakati alipo kuwa rais wa Urusi.
Hata hivyo wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanadai kuvunjika kwa USSR, hakukuwa kama mapinduzi, bali ilikuwa ni utengano wa amani ambao matokeo yake yanaonekana mpaka sasa.
Posted by Kibatala at Monday, December 26, 2011 0 comments
Papa Benedikt aongoza misa ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Posted by Kibatala at Monday, December 26, 2011 0 comments
Saturday, December 24, 2011
Uhuusiano wa Uturuki na Ufaransa wazidi kuwa na mvutano.
Hali ya kisiasa nchini Kongo JK yazidi kuleta utata.
Kinshasa, Kongo JK - 24/12/2011. Maafisa usalama nchini Kongo JK wamepambana na waadau na wale wanao muunga mkono kiongozi wa upinzani wa nchini hiyo Etienne Tshisekedi.
Mapambano hayo yametokea wakati wa maandalizi ya kumwapisha kiongozi huyo, kwa kudai Etienne Tshisekedi ndiye mshindi rasmi na anatakiwa ahapishwe awe rais.
Hata hivyo kwa mujubu wa habari zilizo patikana zinasema "Etienne Tshisekedi aliapishwa katika makazi yake."
Matokeo ya uchaguzi nchini Kongo JK yameteta mvutano kufuatia ripoti za jumuiya za kimataifa ya kuwa uchaguzi huo ulikuwa na matatizo.
Katika uchaguzi huo rais wa sasa wa Joseph Kabila alitamkwa kama mshindi kwa kupata kura 49% za kura na mpinzani wake Etienne Tshesekedi kupata 32%.
Joseph Kabila aliapishwa hivi karibuni kuwa rais wa Kongo JK na ataongoza nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Uhuusiano wa Uturuki na Ufaransa wazidi kuwa na mvutano.
Ankara, Uturuki - 24/12/2011. Serikali ya Uturuki imeishambulia kwa maneno serikali ya Ufaransa na kudai pia kuwa Ufaransa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Algeria.
Uamuzi huu wa serikali ya Uturuki kufanya hivyo, umekuja baada ya bunge la Ufaransa kupiga kura kutambua ya kuwa mauaji ya Armenia yaliyo fanyika nchini Uturuki ni ya kimbari.
Waziri mkuu wa Uturuki Recep yayyip Erdogan alisema "mauaji yaliyo fanywa na Ufaransa nchini Algeria kuwanzia mwaka 1945 ni ya kimbari na yatambulike hivyo pia."
Ikiwa rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ahajui kuhusu mauaji hayo ya kimbari, ni bora amuulize
baba yake Paul Sarkozy ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana nchini Algeria 1940."Aliongezea waziri mkuu Reccep Erdogan.
Mvutano kati ya Ankara na Paris ulizidi kuwa mbaya baada ya kura hiyo na serikali ya Ututuki kutangaza kufunga mahusiano na Ufaransa.
Kuba kuachia wafungwa wa kisiasa.
Havana , Kuba - 24/12/2011. Rais wa Kuba amatangaza msamaha kwa wafungwa wapatao 3000 wakiwemo wafungwa 86 kutoka nchi za kigeni 25.
Rais Raul Castro alitangaza hayo wakati alipo kuwa akihutubia baraza la sheria la nchi hiyo na hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais Raul kutoa msamaha tangu kuchukua madaraka kutoka kwa kaka yake Fidel Castro.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa mabo ya kigeni ya Kuba walisema " uamuzi wa serikali ya Kuba kutoa msamaha kwa wafungwa hao ni katika mpango wa kujiaanda na ziara ya Papa Benedikt XVI ambayo anatarajiwa kuifanya hapo mwakana."
Uamuzi huu wa kuachia wafungwa wa kisiasa na wengine nchini Kuba kumekuja wakati nchi nyingi za Ulaya ya Magharibi na Amerika bado zinawasiwasi na serikali ya Kuba kutokana na msimamo wake wa kisiasa.
Maafisa usalama wa Nigeria wapambana na kundi la Boko Haram.
Abuja, Nigeria - 24/12/2011. Watu wapatao 61 wamepoteza maisha na makazi kuharibiwa kutokana na mashambulizi yanayo endelea kati ya jeshi serikali na kundi la Boko Harama.
Mashambulizi hayo ambayo yameaanza baada ya milipuko ya mabomu katika jimbo la Borno na Yobe na kuleta huharibifu mkubwa.
Kwa mujibu wa habari kutoka heneo hilo simasema " mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wakuu wawili wa polisi wakati wapambano hayo."
Kundi la Boko Haram limekuwa likipambana na serikali ya Nigeria kutokana nambishano wa tofauti wa siasa.
Na kutokana na vurugu za kisiasa nchini Nigeria watu wapatao 450 wameshapoteza maisha yao.
Posted by Kibatala at Saturday, December 24, 2011 0 comments
Thursday, December 22, 2011
Jiji la Dar-es- Salaam nchini Tanzania la kumbwa na mafuriko.
Adis Abeba, Ethiopia - 22/12/2011. Mahakama jijini Adis Ababe imewakuta na hatia waandishi wa habari kutoka Sweeden na kosa la uhaini kwa kuwakamata katika kundi la wapiganaji wanao pinga serikali la Ogaden.
Johan Persso na Martin Schibbye walikamatwa mwezi wa Julai wakati jeshi la serikali ya Ethiopia lilipo kuwa likipambana ba kundi la Ogaden na baadaye kushitakiwa kwa kukutwa makosa ya kuingia nchini Ethiopia kiyume na sheria na kutoa msaada wa kundi la kigaidi.
Waaandishi wa habari hao wanatarajiwa kuhukumiwa vihi karibuni kabla mwisho wa mwaka na wanaweza kukaa jela miaka 18.
Hata hivyo serikali ya Sweden imeitaka serikali ya Ethiopia kuawachia waandishi wa habari hao, kwani walikuwa wanafanya kazi zao bila makosa.
Rais wa Urusi atangaza mpango mpya wa mfumo wa siasa nchini Urussi.
Rais Dmitry Medvedv alisema " serikali ya Urussi haitakubali machafuko yanayo letwa na watu wenye itikadi kali kwa kutumia mlango wa neno demokrasia na hatuta ruhusu watu wanamna hiyo kuwa na nafasi."
"Nchi inataka mabadiliko ya kisiasa yenye demokrasi bora na siyo vurugu, hii inahitajika ili kufungua ukurasa mpya ambapo kila raia wa Urussi atakuwa na haki sawa na kila chama kitapata nafasi katika demokrasi itakayo wafaa raia wa Urussi."Alimalizia rais Medvedev.
Hotuba hiyo ya rais Dimitry Medvedev, imekuja siku chache baada ya uchaguzi wa wabunge uliyo fanyika nchini humo na kuleta wasiwasi mkubwa kufuatia matokeo ya uchaguzi huo na watu kuandamana.
Jiji la Baghda nchini Irak lashutushwa milipuko ya mabomu iliyo leta maafa.
Baghdad, Irak - 22/12/2011. Jiji la Baghdad limekumbwa na milipuko ya mabomu ambayo yamesababisha maafa makubwa na kuleta hali ya wasiwasi kwa wakazi wa jiji hilo.
Kwa mujibu wa mashahidi walisema " kunametokea milipuko zaidi ya kumi na mbili tofauti katika jiji hilo."
Habari kutoka wizara ya ndani ya Irak zinasema " watu wapatao 63 wamefariki dunia na wengine 176 kujeruhiwa vibaya kutoka na milipuko hiyo iliyo tokea sehemu tofauti ndini ya jiji la Baghdad."
Milipuko hiyo imetokea siku chache baada ya jeshi la Marekani kuaanza kuondoka nchini Irak na wakati huo huo kukiwa na mvutano wa siasa katia ya waziri mkuu Nour al Marik Shia na makamu wa rais Tarik al Hashim Sunni ambaye yupo ukimbizini katika eneo linalo ongozwa na Kurdish.
Posted by Kibatala at Thursday, December 22, 2011 0 comments
Monday, December 19, 2011
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini afariki dunia.
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini afariki dunia.
Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 19/12/2011. Kiongozi wa Korea ya Kaskazini amefariki dunia siku ya Jumamosi wakati akiwa njiani kutoka katika jiji la Pyongyang.
Kim Jong-Il 69 alifariki kwa kugonjwa wa moyo kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya nchi hiyo.
Mtangazaji wa luninga ya taifa ya Korea ya Kaskazini alisema " tumepoteza kiongozi mpendwa wa chama na nchi na ni uchungu kwa taifa ziama."
Kwa mujibu wa habari kutoka Korea ya Kaskazini zinasema, mtoto wake wa kiume Kim Jong-Un 28 ndiye aliyechaguliwa kushika nafasi ya baba yake.
Kim Jong Il alichukua uongozi wa Korea ya Kaskazini mwaka 1994 baada ya baba yake Kim Il Sung
kufariki dunina.
Kufuatia kifo cha kiongozi huyo, nchi za Magharibi zimetoa matazamo tofauti na kutaka uongozi mpya kujitaidi kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.
Syria yakubali kusaini mkataba wa makubaliano na jumuiya Kiarabu.
Kairo, Misri - 19/12/2011. Serikali ya Syria imekubali kutia saini mkataba wa makubaliano jumuiya ya nchi za Kiarabu ambao utaruhusu waangalizi wa jumuia hiyo kuingia nchi Syria ili kuangalia hali halisi ya kisiasa nchini humo.
Makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na waziri msaidizi wa mambo ya nje wa Faisal al Maqgad na latubu msaidizi wa jumuiya ya nchi za Kiarabu Ahmed Ben Helli jijini Kairo nchi Misri.
Waziri wa mabo ya nje wa Syiria Walid Muallem alisema " Syria imesaini makubaliano hay baada ya kuona yana manufaa kwa nchi na hayaingilii mambo ya ndani ya nchi."
Makataba wa makubaliano hayo umekuja siku chache kabla ya jumuiya nchi za Kiarabu kuamua kupeleka swaka la Syria katika balaza la usakama la Umoja wa Mataifa.
Posted by Kibatala at Monday, December 19, 2011 0 comments
Friday, December 16, 2011
Luis Moreno Ocampo atatizwa na vifo vya Muammar Gaddafi na mwanae
Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac ahukumiwa miaka miwili.
Posted by Kibatala at Friday, December 16, 2011 0 comments
Wednesday, December 14, 2011
Rais Baraka Obama awakaribisha wanajeshi kutoka Irak.
Posted by Kibatala at Wednesday, December 14, 2011 0 comments
Saturday, December 10, 2011
Papa Benedikt kufanya ziara nchini Kuba.
Posted by Kibatala at Saturday, December 10, 2011 0 comments