Saturday, January 18, 2014

Rais Yoweri Kaguta Museven awapa hafueni mashoga.

Rais Yoweri Kaguta Museven awapa hafueni mashoga.

Kampla, Uganda - 18/01/2014. Rais wa Uganda, Yoweri |Mseven, amkataa kusaini muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda.

Akiandika kupinga kwa sasa kutia sahii rais  Museven amesema " kweli ushoga si kitu cha kawaida na wanatakiwa kuokolewa na siyo kuhukumiwa."

Kitendo cha rais Museven kupinga kutia sahii muswada huo, kimetafsiliwa kuwa, ni kugopa msukomo wa kimataifa, ambapo ingepelekea kuleta mvutano kati ya serikali yake na mashirika ya kimataifa yanayo unga mkono ushoga ambapo mashirika hayo yanaushawishi mkubwa kimataia na kuweza kusababisha myumbo wa serikali ya Uganga kimataifa.

Thursday, January 16, 2014

Kesi ya Rafiki Hariri yaanza na kuhamishia masikio ya Walebanoni jijini Hague.

Kesi ya Rafiki Hariri  yaanza na  kuhamishia  masikio ya Walebanoni jijini Hague.

Hague, Uhollazi - 16/01/2014. Mahakama maalumu inayoshughulikia kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanoni Rafiki Hariri imeaanza rasmi jijini Hague Uhollanzi ambapo watu wanne wanatuhumiwa kuhusika katika mauaji hao.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya watu nne  Mustafa Badreddine, Salim Ayyash, Hussin Oneissi na Assad Sabra  ambao pia inasadikiwa kuwa ni wanacham wa kundi la Hezbollah kundi ambalo linashutumiwa kuhusika katika mauji ya Rafiki Hariri.

Hata hivyo kesi hiyo imeanza huku watuhumiwa kutokuwepo mahakamani na jaji David Re kuamua kuwa kesi itaendelea kwa "watuhumiwa kukana kosa hilo."

Rafiki Hariri, na watu wengine 22 waliuwawa mwaka 2005, baada  milipuko ya abomu kutoe katika eneo ambalo walikuwepo na kundi la Hezbollah kushutumiwa kuhusika na mauaji hayo, japo kundi hilo limekana  kuhusika na  mauaji hayo na pia kuipinga mahakama hiyo.

Hata hivyo baada ya kuuwawa kwa Hariri, jeshi la Syria lililazimika kuondoka nchini Lebanoni ambapo jeshi hilo lilikuwa likilinda amani nchi  Lebanoni.

Monday, January 13, 2014

FIFA ya Sepp Blatter yafanya alicho takiwa kupewa Pele.

FIFA ya Sepp Blatter yafanya alicho takiwa kupewa Pele.

Zurich, Uswizi - 13/01/2014. Edson Arantes Nascimento alimaarufu kama Pele, ametunukiwa zawadi maarumu ya mpira wa dhahabu  na kutambulika kuwa yeye  ndiye alikuwa mchezaji bora wa dunia katika karne 20 na mpa sasa hakuna ambaye amamesha wahi kuvunja rekodi yake ya usakataji wa soka na ufungaji wa magoli duniani kote hadi sasa.

Akiongea baada ya kupokea zawadi hiyo ya mpira wa dhahabu, ambao umeanzishwa kwa mara ya kwanza, Pele alisema "sasa naona ndoto yangu imekamilika, kwani nimekuwa na wivu kuona wengine wakitunukiwa na hivyo kwa sasa nina kombe vyote nilivyo kuwa navihitaji"

Sepp Blatter ambaye ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu FIFA akimsifu Pele alisema" Hakuna mchezaji ambaye amemfikia Pele katika historia ya mpira wa miguu duniani.
"Amefunga magoli zaidi ya alfu moja na kuwafanya watu wapende mchezo wa mpira wa miguu pote duniani na kwa uwezo wake wakusakata soka, na ni mchezaji wa karne ya 20"

Pele hakuweza kupata zawadi hii ya mpira wa dhahabu kwa kuwa mchezaji bora wa dunia enzi za uchezaji wake,  kwa sababu alikuwa hajawahi kucheza ligi za Ulaya japo alikuwa akitikisa dunia kwa umairi wake wa kusakata soka na kuwanyanyasa mabeki na makipa kugalagala na kurudi nyavuni kuotoa mpira ulio tikisa nyavu.


Cristiano Ronaldo atunzwa mpira wa dhahabu kwa mara ya pili.

Cristiano Ronaldo atunzwa mpira wa dhahabu kwa mara ya pili.

Zurich, Uswizi - 13/01/2014. Mchezaji wa Real Madrid  Cristiano  Ronaldo amechaguliwa kuwa mcheaji bora wa dunia wa mwaka 2013

Cristiano Ronaldo 28, amechaguliwa  kwa kura 1,365  na kuwashinda wachezaji wenzake wawili Lionel Messi  1,205 wa timu ya Barcelona.



 Na Frank Ribery 1,127 wa Buyen Munich ambao walifikia fainali katika uchaguzi huo.

Akiongea baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2013, Cristiano Ronaldo alisema, " sina cha kusema, na nawashukuru wachezaji wenzangu, uongozi kwa jumla, kwani kupata tunzo hili siyo rahisi."

Tuzo hili la kuwa mchezaji bora wa dunia litakuwa ni la mara ya pili katika maisha yake Cristiano Ronaldo ya kimpira kufuatia la kwanza alilopata mwaka 2008.



Areal Sharon alazwa nyumba yake ya milele.

Areal Sharon alazwa nyumba yake ya milele.

Tel Aviv, Izrael - 13/01/2014. Mamia ya Waizrael wameudhuria mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu na amiri jeshi wa nchi hiyo Areal Sharon.

Mazishi ya waziri Areal Sharon yalifanyika katika shamba leke  kwenye eneo la jangwa la Negev.

Waziri mkuu wa sasa wa Izrael Benyamin Netanyahu ambaye aliongoza mazishi kwa niaba ya serikali, alisema " Sharon ni moja ya komanda wa Kiizrael ambao watakumbukwa kwa kuitete Izrael na Wajuishi "












Mazishi ya Areal Sharon yameudhuliwa na makamu wa rais wa Mareakani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergi Levrov, aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Brair na viongozi wengi kutoka sehemu tofauti duniani kasoro viongozi kutoka Afrika na Amerika ya Kusini.

Areal Sharon 85, alifariki kutokana na kuugua kwa  baadhi ya viongo vyake vya ndani ya mwili, na hii ilitokana hapo mwanzo wa mwaka 2006 kupata ugonjwa wa kiaharusi ambao ulimsababishia kulazwa kwa muda wa miaka saba.

Saturday, January 11, 2014

Waziri wa ulinzi wa Uingereza hausishwa na mateso wafungwa Irak.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza hausishwa na mateso ya wafungwa Irak.

London, Uingereza - 11/01/2014. Shirika la kutete haki za binadamu na katiba ya Ulaya lenye makao yake nchini Ujerumani limeiomba mahakama inayoshughulikia makaosa ya jinai ICC, kuchunguza matendo ya uvunjwaji wa haki za binadamu uliofanywa na viongozi wa serikali wa Uingereza.

Likiataja shirika hilo limesema "Geoff Hoon ambaye alikuwa waziri wa ulinzi na katibu mkuu  Adam Ingram kuwa walihusika kwanjia moja au nyingine katika mateso na mantendo yaliyo kuwa yanakuiuka haki za binadamu kati ya mwaka 2003 na 2008 na kuvunja sheria ya Geneva ya kulinda wafungwa wa kivita."

Hata hivyo watu hao ambao wanashukiwa kufanya makosa hayo wamekana kuhusika na makosa hayo.

Kesi hiyo ambayo ina kurasa 250,  ilikabidhiwa kwa ICC, huku ikiwa na makosa 85 ambayo inasemekana yamevunjwa  na viongozi hao, na hivyo kuomba wachunguzwe.

Wakati wa vita vya Irak, wanajeshi wa Uingereza walishutumiwa kwa kuhusika katika kutesa wafungwa wa kivita, ambapo Geof Hoon alikuwa ndiye mkuu wa wizara ya ulinzi ya nchi ya Uingereza.





Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael hatupo naye tena kimwili.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael hatupo naye tena kimwili.

Tel Aviv, Izrael - 11/01/2014. Wanachi wa Izrael wamekubwa na msiba mkubwa kufutia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu na amiri jeshi wa nchi hiyo kutokea leo hii.

Ariel Sharon 85, ambaye alikuwa amelazwa hospital kwa muda mrefu, baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi mwaka 2006  na ambapo  ulisababisha akupata madhara ndani ya viongo vya mwili wake na kupelekea kifo.

Shlomo Noy, ambaye ni msemaji wa hospital ambayo alikuwa amalazwa Sharon alisema " matibabu ya kila aina yalifanyika ili kummponya Sharon, lakini haikuwezekana na hivyo hatupo naye tena."

Msemaji wa familia ya Areal Sharon, Yoram Ravid amesema " kwa kuwa Sharon alikuwa ni mwanajeshi na hivyo naimani mazishi yake yafafanywa kwa taratibu za kijeshi."

Areal Sharon, atakumbukwa kwa hisia tofauti, kwa wengine kumwita shujaaa na wengine muuaji.

Kufuatia kifo cha Areal Sharon, Viongozi mbali mbali duniani wametuma salamu zao za rambi rambi kwa watu na serikali ya Izrael.

Friday, January 10, 2014

Risasi zalipuka baada rais Michel Djotodia kutagaza kuachia urais.

Risasi zalipuka baada ya rais Michel Djotodia kutagaza kuachia urais.


Bangui, Afrika ya Kati - 10/01/2014.  Rais wa mpito wa Afrika ya Kati ameachia madaraka baada ya serikali yake kushindwa kuhimili vishindo vya mvurugano wa kisiasa nchi humo.

Tangazo hilo la rais Michel Djotodia kuachia madaraka limetolewa, huku mkutano wa kuleta amani ukifanyika nchini Chad.

Baada ya kutangazwa kujiudhuru kwa Djotodia, milio ya risasi ilisikika katika sehemu tofauti jiji Bangui, na kambi ya wakimbizi  Kikiristu 100,000 iliiingiwa na nderemo, na huku hakukuwa na hata mmoja wa wapiganaji wanaomuunga mkono Djotodia mitaani.

Kufuatia habari za kujiudhuru Michel Djotodia, waziri Ufaransa Ulinzi wa Jean-Yves le Drian amesema " tunatarajia kuwepo na uongozi mpya ambao utaiongoza Afrika ya Kati hadi kipindi cha uchaguzi na kuunda serikali itakato ongoza nchi kwa  kufuata sheria."

Afrika ya Kati nchi ambayo ilikuwa koloni la Ufaransa, imekumbwa na mvurugo wa kisiasa ambao umepelekea kuleta matabaka ya kidini kati ya Waislaam na Wakristu ambayo  kwa sasa makundi hayo yanapigana.
Na tangu kuanza kwa vurugu za kisiasa nchini Afrika ya Kati,  maelfu ya watu wamesha poteza maisha, mali zao na hata kukimbia na kuchukua ukimbizi nje ya nchi ya Afrika ya Kati.

Thursday, January 2, 2014

Mwaka 2014 waanza kwa Wakenya kujeruhiwa na bomu.

Mwaka 2014 waanza kwa Wakenya  kujeruhiwa na bomu. 



Mombasa, Kenya - 02/01/2014. Mlipuko wa  bomu umetokea  baada ya watu walio kuwa kwenye pikipiki kurusha bomu katika hotel moja mjini Mombasa.

Akiongea kuhusu shambulizi hilo, Evans Achoki ambaye ni mkuu wa tarafa ya Kwale alisema " nilisikia mlipuko uliotokea katika hotel kwa jina Tandoori na baadaye nilipofika pale nilikuta watu wamejeruhiwa"

Kuthibitisha mlipuko huo, msemaji wa polisi Jack Ekakuro amesema " watu 10 wamejeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu na kwa sasa majeruhi wapo hospital kwa matibabu."

Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu, tangu nchi hiyo ilipoamua kulisaidia jeshi la serikali ya Somalia katika harakati zake za kupambana na kund la Al Qaeda. Na kundi hilo la al Qaeda kuhaidi kufanya mashambulizi nchini Kenya.

Mwaka 2013 haukuwa mwaka wa heri kwa Wairak.


New York, Marekani 02/01/2014. Umoja wa mataifa umetoa taarifa kuwa mwaka 2013 umekuwa mwaka ambao mauji kwa Wairak yalizidi kulinganishwa na miaka ya nyuma nchi humo.

Ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa "watu wapatao 8,868  wamepoteza maisha yao, na mauaji ya kutisha yametokea mwezi wa Desemba 2013 ambapo watu 759 ambapo 69 kati yao walikuwa ni walinzi na  maafisa usalama wa taifa."

Mauaji mengi yanayo tokea nchini Irak yamekuwa ni ya kisiasa au ya kimakundi  ambayo yanahusisha Washia na Wasuni, ambapo wamekuwa wakivutana katika  kuongoza nchi,  tangu kuangushwa kwa utawala wa Saadam Hussein na jeshi la Marekani na washiriki wake miaka 10 iliyopita.

Wednesday, January 1, 2014

Hali ya afya ya waziri mkuu wa zamani wa Izreal ipo tete.

Hali ya afya ya waziri mkuu wa zamani wa Izreal ipo tete.

Jerusalemu, Izrael 01/01/2014. Afya ya aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael, Ariel Sharon inazidi kudorola siku hadi siku toka alipofanyiwa upasuaji wa na kuwekewa mirija ya kupitishia chakula mwezi Septemba mwaka jana.

 Amir Marom, ambaye ni msemaji wa hospital ya Hashomer alipo lazwa Sharon alisema kuwa " nikweli hali ya Sharon siyo nzuri kiafya na madakitari bado wapo wanafuatilia afya yake kwa ukaribu."

Kwa mijibu wa habari zinasema kuwa hali ya afya ya Ariel Sharoni ilianzakudhoofika  mara baada ya viungo vyake vya ndani ya mwili  kushindwa kufanya kazi vizuri. Lakini hazikueleza lini matatizo hayo yaliianza.

Waziri mkuu Arel Sharon 85 ambaye ni mwanzilishi wa chama cha Kadima, alilazwa hospital tangu mwaka January 4, 2006, baada ya kupata ugonjwa wa kiharusi, ambao ulimsababishia kutoka katika ulingo wa siasa nchi Izrael. 

Balozi wa Palestina auwawa kwa bomu.
Prague, Czecheslovakia - 01/01/2014. Balozi wa Palestina nchini  Czecheslovakia, ameuwawa kwa  bomu kwenye jengo analo ishi katika jiji la Prague.

Akithibitisha kuwepo na mlipuko wa bomu, msemaji wa polisi Andrea Zoulova amasema "balozi Jamal al Jamal   alifariki mara baada ya kufikishwa hospitali"

Na habari kutoka kwa ofisi ya mambo ya nje ya nchi  ya Wapalestina imesema " mlipuko wa bomu ulitokea wakati balozi, Jamal al Jamal alipo kuwa akijaribu kufungua kabati iliyokuwa imeletwa kutoka ofisi za zamani za ubalozi huo"

Hata hivyo serikali ya nchi Czechslovakia haija thibitisha kuwa mlipuko huo unahusika na ugaidi.