Monday, February 28, 2011

Brussels, Ubeligiji - Jumuia ya Ulaya imekubaliana kwa pamoja kumwekea vikwazo kiongozi wa Libya kufuatia matukio ya nayo endelea kutokana na maandamano ya kupinga uongozi wa serikali.
Vikwazo hivyo vilivyo pitishwa ni pamoja na ununuzi wa siraha, kuzuiliwa kusafiri, na pesa zote ambazo zilikuwa zimewekwezwa na familia yake.
Serikali ya Misri ya mzuai Hosni Mubaraka na familia yake kusafiri.
Kairo, Misri - 28/02/2011. Serikali ya Misri imezua familia ya rais wa zamani wa Misri kusafiri nje ya nchi kufuatia uchunguzi unaoendelea.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari msemaji wa mwanasheria mkuu wa serikali Abel el Saeed alisema " serikali imeamua kumzuia Hosni Mubaraka kutoka nje ya nchi yeye na familia yake kufuatia uchunguzi dhidi ya yake.
Rais Hosni Mubaraka, alitolewa madarakani baada ya wanachi wa Misri kuandamana kumtaka atoke madarakani kutokana na kutoridhishwa na uongozi wake wa miaka 32.
BMW na Citreon kuunangana kibiashara.
Geneva, Uswiss - 28/02/2011. Makampuni ya magari ya BMW na Peugeot Cirtoen yamekubaliana kuungana kibiashara ili kutengeneza aina mpya ya gari itakayo endana na teknolojia mpya.
Akongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa PSA Peugeot Citreon Phillipe Varin alisema " huu ni mwanzo na muungano huu utaiwezesha jumuia ya Ulaya kutengeneza magari ya kisasa ambayo yataendana na teknologiajia mpya."
Utengenezaji wa magari hayo ambayo yatajulikana kama magari ya Hybrid yata leta ajira kwa watu wapatao 400.

Saturday, February 26, 2011

Umoja wa mataifa kuwekea vikwazo serikali ya Libya.

Umoja wa mataifa kuwekea vikwazo serikali ya Libya. New York, Marekani - Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imekutana ili kujadili muswada wa kuiwekea vikwazo serikali ya Libya.

Uamuzi huo wa umoja wa mataifa umekuja baada ya serikali ya Libya chini ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kutumia nguvu kuvunja maandamano ambayo yanapinga serikali yake.
Kwa mujibu wa habari kutoka katika kamati hiyo ya umoja wa mataifa zinasema " serikali ya Libya inatumia nguvu zake za dola kimyume na kusababisha vifo na maafa katika jamii nzima ya Walibya."
Hali ya kiusalama nchini Libya imebadilika na kuwa uwanja wa vita mara baada ya maandamano ya kumtaka kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kutika madarakani jambo ambalo kiongozi huyo amekataa.
Picha hapo juu anaonekana kiongoziwa Libya Muammar Gaddafi akiwahutubiwa wananchi kwa mara ya tatu tangu kuanza maandamano ya kumtaka aachie madaraka.
Hali ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda ikatokea.
Abidjani, Ivory Coast-26/02/2011. Milio ya risasi imesikika katikati ya jijila Abidjani na kuwafanya wakazi wake kukimbia kwenye maficho huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa akionya kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Mapigano hayo ambayo yalikuwa kati ya kundi la rais wa sasa wa nchi hiyo Laurence Gbagbo na Alassane Ouattara.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zimasema " halisiyo shwali katika jiji hilo."
Hali ya machafuko ilianza mara baada ya uchaguzi mkuu kufanyika na Gbagbo kudai yeye ndiye aliye shinda uchaguzi na huku mpinzani wake Ouattara kudai yeye ndiye mshindi wa uchaguzi huo.
Picha hapo juu ni viongozi wa makundi yanayo pigana nchini Ivory Coast, Watara kushoto na Gbagbo kulia

Thursday, February 24, 2011

Rufaa ya mwanzilishi wa WikiLeaks yakataliwa.

Rufaa ya mwanzilishi wa WikiLeaks yakataliwa.

London, Uingereza - 24/02/2011. Mahakama jijini London imetupilia mbali rufaa ya mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks ambayo inapinga kupelekwa kwake nchini Sweden ili kujibu mashitaka.
Jaji Howard Riddle alisema " tumuma zidi ya mshitakiwa ni za kisheria na zinatakiwa zijibiwe kisheria hivyo inatakiwa mshitakiwa akajibu mashitaka."
Akiongea baada ya hukumu mwanasheria wa mshitakiwa Julian Assange alisema " tutakata rufaa dhizi ya uamuzi huu."
Juliana Assange ambaye amekuwa shubiri katika jamii ya kidipromasia baada ya mtandao wake WikiLeaks kutoa siri za viongozi na mabalozi wanapo kutana kila mara.
Mahakama ya kimataifa ya muhukumu miaka 27 jela mkuu wa zamani wa Polisi wa Serbi.
Hague, Holland 24/02/2011. Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za Yugoslavia imemuhukumu aliyekuwa mkuu wa polisi Serb kwa miaka zaidi ya miongo miwili.
Vlastimir Djordjevic alihukumiwa na baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kushiriki machafuko na mauaji ya Kosovo Albania.
Akitoa hukumu jaji Kevin Parker alisema " unahukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa kukutwa na makosa ya kuhusika na mauaji ya watu 724 wa Kosovo Albania na kuleta mgawanyiko wa jamii katika eneo hilo."
Vlastimir Djordjevic alikamatwa mwaka 2007 huko Montenegro maada ya kukimbia na mafichoni kwa muda wa miaka minne.

Tuesday, February 22, 2011

Muhammar Gaddafi asema hatoki madarakani

Muhammar Gaddafi asema hatoki madarakani. Tripol, Libya - 22/02/2011. Rais wa Libya melihutubia taifa la Libya na kusema hataondoka nchi na yupo tayari kufa kwa ajili ya nchi yake.

Kanal Muhammaar Gaddafi alisema, " mimi ni shujaa na mpiganaji kutoka kwenya turubai, nipo tayari kufa na nitapigana hadi mwisho, mimi siyo rais uacha madaraka, mimi ni mpiganaji."
Akiongea kwa hasira aliongezea " wale wote wananifata naawagiza wawakamate watu wote wanlioleta machafuko na wafikishwe kwenyw sheria."
"Nitahakikisha tunasafisha kila nyumba kama wasipo jisalimisha."
"Kama Libya ita yumba itakuwa makao ya Al-Qaeda."
Maandamano siyo kuaribu na siyo waasi wa nchi.
Rais wa Libya aliyasema hayo baada ya Walibya kuandamana kumtaka aachie madaraka na kuruhusu mabadiliko ya kisiasa.
Manoari za Kiiran zapita Suez Kanal kwa mara ya kwanza.
Suez Kanal, Misri - 22/02/2011. Manoari mbili za kijeshi za Iran zimepita kwa mara ya kwanza kwenye mfereji wa Suezi Kanal. Meli hizo zimepita muda wa saa tisa na dakika arobaini na tano kwenye mfereji huo na zinategemewa kurudi mwezi Tatu mwaka 2011.
Meli za Iran zimepita kwenye mfereji huo kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa serikali ya Hosni Mubaraka.
Kufuatia kupita kwa meli hizo serikali ya serikali ya Izrael imesema " tunatizama kwa uangalifu mwenendo huo wa Iran."
Uongozi wa Suez Kanal uliripoti ya kuwa Meli za Iran zimepita kwenye eneo hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.
Rais wa Urussi aonya kuhusu mapinduzi katika nchi za Kiarabu.
Moscow, Urussi - 22/02/2011.Rais wa Urusi ameonya ya kuwa mabadiliko ya kisiasa yanatotokea katika nchi za kiarabu yanaweza kuleta athali kubwa.
Rais Dmitry Medveded alisema " siafiki na jinsi viongozi wa nchi za magharibi ambao wamekuwa wana unga mkono mapinduzi ya kisiasa yanayo tokea katika nchi za Kiarabu, kwani yanaweza kuleta machafuko na kugawa nchi hizo ambapo matokeo yake yatakuwa mabaya kwa muda mrefu."
Akiongezaa " Inawezekana nchi hizi zikaja kutawaliwa na viongozi ambao wataleta maafa katika jamii. alisema rais Medved.
Maoni ya rais wa Urussi yamekuja kufuatia machafuko na mabadiliko ya yanayoendelea katika nchi za Kiarabu ambayo yameishitua dunia.

Friday, February 18, 2011

Milipuko yatokea nchini Tanzania

Milipuko yatokea nchini Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania - 18/02/2011. Milipuko ya mabomu imeua zaidi ya watu ishirini na kuleta maafa makubwa kwenye kambi moja ya jeshi iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Saalam.
Mlipuko huo ambao ulitokea usiku wa kuamkia Jumatano na kusababisha wenyeji wa maeneo hayo kukimbia mji wao kwa uwoga.
Milipuko hiyo iliyo tokea katika kambi ya jeshi iliyolo Gongo la Mboto wilaya ya Ilala imesababisha maafa makubwa kwa jamii.
Mizengo Pinda alisema " milipuko hiyo imeleta maafa makubwa na huenda baadaye maafa yakaongezeka kutokana na hali halisi iliyo sababishwa na milipuko hiyo."
Milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi la Gongo la Mboto imetokea kwa mara ya pili baada ya milipuko uliyo tokea mwaka 2009 ambapo watu wapatao 27 walipoteza maisha yao.
Wamisri washangilia wiki moja tangu kuondoka Hosni Mubaraka.
Kairo, Misri - 18/02/2011. Maelfu ya wananchi nchini Misri wameandamana ili kushangilia kuanguka kwa utawala wa Hosni Mubaraka.
Rais Hosni Mubaraka ambaye alikuwa rais wa Misri kabla ya kuamua kuachia madaraka baada ya wanachi kuandamana kutaka serilikali ya Mubaraka iachie utawala.
Hata hivyo kulikuwa na maandamano mengine yalifanyika katika jiji la Kairo kuunga mkono Hosni Mubaraka kwa madai ameiniua nchi na kuleta amani.
Rais Hosni Mubaraka, alitoka madarakani baada ya maandamano ya siku kumi na nane ambayo yalimlazimisha kuachia madaraka ya urais.

Wednesday, February 16, 2011

Kachero alidanganya kuhusu uwezo wa Saddam Hussein.

Kachero alidanganya kuhusu uwezo wa Saddam Hussein. Berlin, Ujeruman - 16/02/2011. Wabunge nchini Ujerumani wameonya ya kuwa hunda kachero aliyejulikana kwa jina la Curveball akawekwa kizuizini mara baada ya kusema ya kuwa alidanganya.

Curveball jina la kazi, ambaye ni raia wa Irak amesema ya kuwa alitoa habari za uongo kwa makachero wa Amerika na washiriki wake ya kuwa rais wa Irak Saddam Hussein alikuwa na siraha za sumu ambazo ni zakuangamiza.
Raia huyo wa Irak, Rafid Ahmed Alwan, ambaye aliongea na gazeti la Guardian na kudai ya kuwa alidanganya ili rais Saddam Hussein atolewe madarakani.
Rafid Ahmed Alwan alisema " labda nilikuwa sawa au sikuwa sawa lakini nilipewa nafasi ya na hivyo nikaitumia ili Saddam Hussein atolewe madarakani na mimi na familia yangu tunajidai kwa kuchangia mageuzi ya kisiasa na kuleta demokrasi nchini Irak."
Curveball alikimbia kutoka Irak mwaka 1995 wakati wa utawala wa marehemu rais Saddam Hussein.
Serikali ya Libya ya macho yake kwa waandamanaji.
Benghazi, Libya - 16/02/2011. Polisi nchini Libya wamepambana na waandamanji ambao walikuwa wamendamano na kuelekea kituo kikuu cha polisi.
Katika maandamano hayo, polisi waliumia gasi na zana nyingine ili kuwatawanya waandamanaji ambo watu wapatao kumi na nne kuumia wakiwmo polisi.
Maandamano yaliyo fanyika nchini Libya yamefuatia maandamano yaliyo fanyika nchini Tunisia na Misri na kufanya serikali za chini hiyo kuondoka madarakani.
Waganda waajianda na uchaguzi wa rais.
Kampala, Uganda - 16/02/2011. Viongozi wa vyama tofauti vya siasa nchi Uganda wanamalizia kampeni zao za mwisho kabla ya uchaguzi siku ya Ijumaa.
Uchaguzi huo ambao matokeo yake yata wezesha wanchi wa Uganda kupata rais ambaye watamchagua baada ya muda wa rais wa sasa wa Yoweri Museni kumalizika.
Mpinzani wake wakuu wa rais wa sasa Yoweri Museni ni Kiiza Basigye ambaye amekuwa akimlaumu Musseven kwa kutoleta mabadiliko kwa wanchi wa Uganda.
Kufuatia uchaguzi huo serikali ya Uganda imetangaza kuwa siku ya Ijumaa itakuwa sikuku ya kitaifa.

Monday, February 14, 2011

Wasafiri wa anga wapata chombo kipya.

Wasafiri wa anga wapata chombo kipya.

New York, Amerika 14/02/2011. Kampuni ya ndege ya Boeing imezindua ndege mpya ambayo itakuwa hewani hivi karibuni.
Boeing imesema ndege "hiyo 747-8 Intercontinental itakuwa ikisafiri mwendo mrefu na waki huo ikitumia mafuta kiasi".
Ndege hiyo ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 467 ambao watakuwa wameongezeka kwa abiria 51 tofauti na ndege ya sasa 747.
Serikali ya Algeria yafuta amri ya dharula.
Algiers, Algeria 14/02/2011. Serikali ya Algeria imetangaza kusimamisha amri ya dharula ambayo ilikuwa imewekwa kwa kipindi cha miaka kumi na tisa.
Waziri wa mambo ya nchi za nje Mourad Medelci amesema " serikali imeamua kutoa amri ya dharula kama ilivyo haidiwa na rais Abdelaziz Bouteflika hiv karibuni."
Amri ya dharula iliwekwa mwaka 1992.
Kuondolewa kwa sheria hii imekuja baada ya serikali kuwa na wakati mgumu hasa kutoka kambi za nyama pinzani.

Sunday, February 13, 2011

Rais wa zamani wa Pakistani ashitakiwa.

Kiongozi wa Palestina ajiudhulu kazi yake. Ramallah, Palestine - 13/02/2011. Msemaji mkuu wa serikali ya Wapalestine amejiudhulu katika kazi yake baada ya habari zilizo patikana kwenye vyombo vya habari zimetokea kwenye ofisi yake. Saeb Erakat, ambaye amekuwa msemaji mkuu wa serikali ya Wapalestina kwa muda mrefu, amekuwa akiandamwa na mlolongo wa lawama ya kuwa amekuwa hafanya kama anavyotakiwa hasa katika majadiliano ya kuleta amani na Waizrael. Habari ambazo zilipatikana kwenye vyombo vya habari hivi karibuni zimeonyesha jinsi gani viongozi wa Palestina wanavyo jadiliana katika majadiliano ya amani na Waizrael ambayo yamesimama kutokana na tofauti za misimamo. Rais wa zamani wa Pakistani ashitakiwa.

Islamabad, Pakistan - 13/02/2011. Mahakama nchini Pakistan imetoa kubali cha kumtaka aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo kukamatwa ili ajibu mashitaka ya kuwa alihusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
Musharaff, ambaye alikuwa rais wa Pakistan na amiri jeshi mkuu wa nchi hiyo, anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Benazir Bhutto.
Habaria kutoka kwa viongozi wa serikali zinasema " uchunguzi ulio fanywa unaonyesha kwa njia mojo au nyingine uongozi wa serikali ya Musharaff uliyo kuwepoe wakati wa mauji ya Benazir Bhutto unahusika."
Hata hivyo, upande wa Musharaff unakanusha madai hayo na kusema ni habari za uvumishi ndizo ambazo zimetumika na Musharaff hausiki na mauaji hayo.
Pervez Musharaff anatarajiwa kuwasili mahakamani tarehe 19 Februari 2011 ilikusikiliza kesi dhidi yake.

Saturday, February 12, 2011

Rais wa Misri Hosni Mubaraka ajiudhuru urais.

Rais wa Misri Hosni Mubaraka ajiudhuru urais. Kairo, Misri - 12/02/2011. Sherehe, shangwe vigeregere vilivyo andamana na vilio vilisikika nchi zima mara baada ya makamu wa rais wa Misri Omar Suleiman kutangaza ya kuwa rais Hosni Mubaraka amejiudhuru na kukabidhi madaraka mikononi mwa jeshi.

Akiongea kwa muda wa sekunde thelathini, makamu wa rais alisema " rais Hosni Mubaraka ameamua kujiudhuru na kuanzia sasa na amekabidhi madaraka yote kwa kamati itakayo ongozwa na jeshi."
Rais Hosni Mubaraka, ambaye ametawala Misri kwa miaka 30, amejiudhuru baada ya msukumo mkubwa kutoka kwa waandamanaji ambao walikuwa wanadai atoke madarakani.
Maandamano yaliyo mfanya rais wa Misri kuachia madaraka yamechukua siku kumi nane, na kusababisha maafa makubwa ja kijamii na kiuchumi.

Wednesday, February 9, 2011

Wakili wa Charles Taylor aondoka mahakamani.

Wakili wa Charles Taylor aondoka mahamani.

Hague, Uhollanzi - 09/02/2011. Mwanasheria anaye mtetea aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor ametoka mahakamani baada ya ya majiji wanaosikiliza kesi hiyo kukataa ripoti iliyo wakilishwa wakati wa mwisho.
Mwanasheria huyo kutoka Uingereza alisema " Ikiwa mahakama na sisi hatuelewani, inakuwa vigumu kuamini na wamezuia kwa asilimia 90 utetezi wa mteja wangu?"
Charles Taylor anatuhumiwa kwa makosa ya kukiuka haki zabinadamu kwa wanachi wa Sierra Leone.
Waziri mkuu wa Itali kuenda akasimama kizimbani.
Milan, Itali- 09/02/2011. Waziri mkuu wa Itali huenda akajikuta amesimama kizimbani baada ya wanasheria kufungua kesi dhidi yake kwa madai ya kutumia cheo chake vibaya.
Silvio Berlusconi, ambaye ni waziri mkuu anatuhumiwa kwa kwa kufanya mapenzi na msichana ambaye hajafika miaka kumi nane.
Mahakama jijini Milan, imeombwa ifungungue kesi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kashfa hio.
Hata hivyo waziri mkuu Silvio Berlusconi amekuwa akikanisha kashfa hizo zidi yake na kusema " ni za kisiasa, wapinzani wake ndiyo wanao shikilia madai hayo ili kumchafulia jina lake."
Kampuni ya magari ya Toyota yapata hafueni.
Washington, Marekani -09/02/2011. Kampuni ya magari ya Toyota imepata hafueani baada ya ripopti ya uchunguzi kuonyesha yakuwa matizo yaliyokuwemo kwenya magari yake hayakusababishwa na mtiririko wa umeme kwenye gari.
Akiwakilisha ripoti ya uchunguzi iliyo fanywa na wanasayansi wa NASA, waziri wa mawasiliano Ray LaHood alisema "matatizo ya kuongezeka kasi ya gari wakati waundeshaji hayakusabaishwa na mtiririko wa umeme bali matatizo ya kiufundi - makeni."Baada ya ripo ti hiyo kutolewa uongozi wa kampuni ya magari ya Toyota, ulisema tutajitahidi kuimarisha magari yetu na tupo tayari kusilikiza mawazo ya wateja wetu ili kuhakikisha usalama wa kila mteja wetu.''
Kampuni ya magari ya Toyota ilipata msukosuko hivi karibuni baada ya baadhi ya wateja wake kudai yakuwa magari take yana matatizo.

Saturday, February 5, 2011

Thamani ya Euro kuimarishwa kwa kila hali.

Thamani ya Euro kuimarishwa kwa kila hali. Brussels, Ubelgiji 05/02/2011. Mkutano wa viongozi wa jumiya ya Ulaya umeamua kuahakikisha thamani ya pesa ya Uero in tengemaa.

Kanselah wa Ujerumani Angela Markel alisema " kwa kushirikiana na nchi wanachama wa jumuia ya Ulaya Ujerumani na Ufaransa tutailinda Uero siyo kipesa tubali pia kiuchumi na kisiasa na kuifanya iwe madhubuti katika mashindano na kuinua uchumi kwa pamoja."
Uamuzi wa viongozi wa jumuia ya Ulaya kuilinda sarafu ya Euro, kumekuja baada ya myumbo wa kiuchumi wa nchi wanachama.
Waandamanaji nchini Misri bado kushikiria msimamo wao.
Kairo, Misri -05/02/2011. Waandamanaji nchini Misri bado wanashikiria haja yao kutaka rais sasa kutoka madarakani.
Wakiongoea kupinga ombi la mkuu wa jeshi la kuwataka warudi majumbani, waandamanaji walisema "hatuwezi kuondoka hapa tulipo mpaka rais Hosni Mubaraka ametoka madarakani."
Hata hivyo jumuia ya kimataifa bado inasugua vichwa ni kwa jinsi gani wataweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa uliopo nchini Misri kwa kuzingztia nchi yenyewe ni kiungo muhimu katika eneo zima la mashariki ya kati.
Wakati maandamano ya kumpinga rais Mubara yanaendelea, bombo la kupisha gasi kuelekea nchi Jordani lilipasuka na kunamadai ya kuwa bomba hilo limelipuliwa na watu wasio julikana.
Bomba hilo lililopo Ghuba ya Sinai liliupasuka na kusababisha wimbi kubwa la moto kuelekea hewani na kuathiri usambazaji wa gasi kuelekea nchini Jordani,
Picha hapo juu ni picha ya poto ulio lipuka mara baada ya bomba la gasi kuasuka na kuathiri usambazaji wa zao la gasi kuelekea nchini Jornan.
Pichaya pili hapo juu inaonyesha waandamanaji waliopo katikati ya jiji la Kairo kwenye viwanja vya Tahrir kwa siku ya kumi na mbili tangu kuanza maadamano ya kutaka rais Mubaraka aachie madaraka.

Wednesday, February 2, 2011

Rais Mubaraka kutogombania urais tena.

Rais Mubaraka kutogambinia urais tena.

Kairo, Misri- 02/02/2011. Rais wa Misri ametangaza yakuwa hatagombea tena kiti cha urais tena na kusema atatoka madarakani baada ya kuhakikisha mabadiliko yana fanyika bila matatizo.
Rais Hosni Mubara alisema " sitagombea tena urais na sikutarajia kugombea tean kiti cha urais. Serikali itahakikisha kuwa hali ya sasa itakuwa shwari na nahaaidi ya kuwa sitakakimbia nchi na nita kufa hapa nyumbani na kuzikwa hapa, Mirsi ni nchi yangu nimeipigania na hivyo sitaondoka."
Mubaraka amehutubia kwa mara ya pili tangu kuanza maandamano ya kupinga serikali yake.

Tuesday, February 1, 2011

John Kerry ataka rais wa Misri kuachia madaraka. New York, Marekani - 01/02/2011. Mbuge na kiongozi muhimi katika chama cha Demokratik cha Marekani amemtaka rais wa Misri kujiudhuru.

John Kerry alisema " Mubaraka lazima akubaliane na matakwa ya wananchi na raia wa Misri kwa ajili ya usalama na kulinda hadhi ya Wamisri na mtoto wake asigombanie kiti cha urais wakati wa uchaguzi, pia Marekani inatakiwa kuangalia mbele na kujua ya kuwa kipindi cha Mubaraka kimekwisha."
John Kerry amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka Marekani kutamka wazi ya kuwa rais Mubaraka aachie madaraka.
Picha hapo juu ni ya mbuge John Kerry, ambaye amekuwa wa kwa kutamka wazi kuwa rais wa Misri Hosni Mubaraka atoke madarakani.
Rais wa zamani wa Haiti kurudi nyumbani.
Port au Price, Haiti - 01/02/2011.Serikali ya Haiti imekubali kumpa kibali cha kurudi nyumbani aliye kuwa rais wa nchi hiyo ambaye alikimbilia Afrika ya Kusini.
Jeans Bertrand Aristide aneyeishi ukimbizini nchi Afrika ya Kusini amekuwa akisema kila mara yupo tayari kurudi nyumbani ikibidi kufanya hivyo.
Ira Kurzban, mwanasheria wa wa Aristide amesema " ninacho fahamu ni kwamba rais Jeans Bertrand Aristide amepewa pasipoti tayari kurudi nyumbani na kamati ya serikali ya Haiti."
Kurudi kwa Aristide kutakaribiana na uchaguzi wa mara ya pili wa kumchagua rais wa Haiti ambao utafanyikahivi karibuni.
Picha hapo juu ni ya rais wa zamani Jean Bertrand Aristide ambaye anatarajiwa kurudi nyumbani kutoka ukimbizini.
Mfalme wa Jordani avunja serikali.
Aman Jordan - 01/02/2011. Mfalme wa Jordani amevunja serikali baada ya kushindwa kuimarisha uchumi wa nchi na kusababisha wananchi kuandama.
Maandamano hayo ambayo yamefanyika zaidi ya wiki, yalianza baada ya kupanda kwa mafuta na bei ya vyakula.
Habari kutoka ofisi ya mfalme zinasema " mkuu wa jeshi wa zamani Marouf Bakhit ambaye aliyewahi kuwa waziri mkuu hapo awali amechaguliwa kuwa kuunda serikali mpya baada ya serikali ya Samir Rifai kushindwa kuimarisha uchumi."
Wananchi wa Jordan wamekuwa wakilalamikia serikali kwa kushindwa kuimarisha uchumi na kusababisha maisha ya raia kuwa magumu.
Picha hapo juu ni ya Mfalme wa Jordan ambaye amevunja serikali baada ya kushindwa kuongoza wananchi na kuinua uchumi Jordan.