Wednesday, April 9, 2014

Misri nayo ya moto wa kuotea mbali kwa mashoga.

Vurugu na myumbo nchi Ukraine, Marekani yaishutumu Urusi.

Washington, Marekani - 08/04/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameishutumu serikali ya Urusi kwa kuendeleza mvurugo na myumbo wa kisiasa nchi Ukraine ambao unapelekea kugawa nchi.

Akiongea mbele ya wajumbe wa Kongresi John Kerry amesema kuwa '' mashushu, makachelo na maafisa usalama wa Urusi wapo nchi Ukraine kusaidia kuyumbisha serikali iliyopo na kuunga mkono wale wote wanao taka mgawanyiko wa nchini Ukraine.''

'' Ushaidi ni kwamba watu ambao wamevamia na kuchukua majengo ya serikali ni wale ambao wanaunga mkono kujiunga na Urusi na na pia kujitenga na serikali ya Kiev, na hii inatokana na ushawishi wa Urusi.''

Hata hivyo serikali ya Urusi imekuwa ikipinga  kwa kudai kuwa vurugu na myumbo wa kisiasa nchi Ukraine umesababishwa na ya Marekani na washiriki  kutokana na malengo na faida wanazojua wenyewe.

Mvurugona wa kuchafuka kwa amani   nchini Ukraine umekuwa  wa kichwa kuuma, tangu kuangushwa kwa serikali ya rais Viktor Yanukovich  ambapo nguvu na maandamano yalitumika na vyama vya upinzani chini Ukraine kwa msaada wa msukumo wa nchi za Ulaya Magharibi na Marekani.na kuleta upya hisia za vita baridi kati na Urusi.

Hadi sasa majimbo ya Donetski na  Kharkiv yamekumbwa na maandamano ya  kutaka kujitenga na serikali ya Kiev, pia baadhi ya watu waliovamia ofisi na majengo ya serikali kudai majimbo hayo yajiunge na Urusi.

Polisi nchini Kenya yasaka wahamiaji haramu.

Nairobi. Kenya - 08/04/2014. Polisi nchi Kenya wapo katika msako mkubwa  kuwakamata watu wote wanao ishi kinyume cha sheria nchini Kenya baada ya matukio ya  mashambuzi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa nchi humo.

Katika kufanikikisha zoezi hilo wagtu 4,000 walikamatwa katika jiji la Nairobi, japokuwa polisi wamesema '' ni watu 447 ambao kwa sasa ndiyo bado wanashikiliwa na polisi.''

Kwa mujibu wa balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Shaik Ali '' watu 82 wamerudishwa nchini Somalia baada ya kukataliwa maombi yao ya kikimbizi.''

Hatua hii ya serikali ya Kenya kufanya msako imekuja baada ya kutoa agizo kuwa watu wote walioomba ukimbizi  kurudi katika makambi ya kikimbizi.

 Agizo hilo lilikuja baada ya shambuli lililotokea katika maeneo ya Elselegh ambapo watu sita walipoeteza maisha kufuatia mashambulizi ya mabomu katika kumbi za starehe kwenye kitongoji hicho.

Kenya imekuwa inakutwa na mashambulizi ya kigaidi, baada ya kundi la Ashabab la Somali kudai kuhusika na ugaidi nchini humo kwa madai yakuwa Kenya imevamia nchini Somalia, jambo ambalo serikali ya Kenya inasema ni katika harakati za kuleta amani katika ukanda wa pembe ya Afrika.

Misri nayo ya moto wa kuotea mbali kwa mashoga.

Kairo, Misri -09/04/2014.  Watu wanne wamehukumiwa kwenda jela na mahakama jijini Kairo, baada ya  kutwa na hatia ya kufanya ushoga na kuwa kimapenzi kwa jinsia moja.

Watu hao ambao wamekutwa na kosa la kupanga na kushiriki kwa makusudi sherehe ya ushoga huku wakiwa wamevaa nguo za kike na ulimbwende wa kina mama walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minane na kupewa kazi ngumu wakati wa kipindi chote watakachokuwa jela.

Kufuatia hukumu hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la kutoka Marekani limelaani kitendo hicho na kwa kusema '' kitendo cha kufungwa watu hao ni kimyume za haki za binadamu na kitaleta mlolongo wa hukumu kama katika nchi zenye asili ya  Kiarabu.''

Nchi ya  Misri haina sheria ya kupinga ushoga, lakini mashoga na wale wote wanahusika na tabia hii huwa wanahukumiwa kwa kufuata baadhi ya vifungu ungia vya sheria .

Nchi nyingi za Afrika zimekuwa hazikubaliani na tabia ya ushoga, na hivi karibuni serikali ya Uganda ilipitisha sheria kali ya kupinga ushoga jambo ambalo  nchi za Magharibi zililaani sheria hiyo na pia kutishia kusimamisha baadhi ya misaada kwa Uganda.


Tuesday, April 8, 2014

Mwanajeshi wa Ufaransa atia chumvi kidonda cha kuhusika na mauaji ya Rwanda 1994.

Mwanajeshi wa Ufaransa atia chumvi kidonda cha kuhusika na mauaji ya Rwanda 1994.



Paris, Ufaransa - 08/04/2014. Mmoja wa makamanda waliokuwa katika kikosi cha kijeshi cha Ufaransa kilichokuwa nchi Rwanda wakati wa mauaji wa kimbari ametoa changamoto kwa serikali jiji Paris juu shutuma kutoka kwa serikali ya Rwanda.

Guillaume Ancel ambaye alikuwa kapteni  katika jeshi la Ufaransa jiji Kigali mwaka 1994 kabla  mauaji ya kimbari kuanza amesema '' niliamliwa kupakia siraha katika roli ili ziende Zaire au kwa sasa Kongo DRC na zilikuwa kwa ajili ya askari wa Rwanda ambao watakimbia na ndiyo walikuwa wahusika katika mauaji ya kimbari''

''Pia nilishauriwa kuhakikisha waandishi wa habari wasijue, na nilipo pinga swala hili niliambiwa kuwa ikiwa kama hatutashirikiana na jeshi la Rwanda la wakati hule, basi watatugeuka na tutakuwa katika hali ya mvutano nao.''

''Na hii ilitokea baada ya mauaji ya kimbari ya 7/April/1994 na  ndege iliyombeba rais  wa Rwanda Juvenal Habyalimana kuangushwa katika kiwanja cha ndege cha Kigali.''

''Kwangu nilishangaa kwa  kutokuelewa kuwepo kwa jeshi la Ufaransa kwani tayari jeshi la Umoja wa Mataifa UNAMIR lilikuwa tayari mjini Kigali.'' Aliongezea Ancel.

Tangu kutokea mauaji ya kimbari  ya mwaka 1994 nchini Rwanda, serikali ya  Rwanda chini ya rais Paul Kagame imekuwa ikizishutumu Ufaransa na Ubeligiji kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari, ambapo watu baadhi ya watu wenye itikadi kali toka jamii ya Kihutu  waliwaua watu 800,000 wa jamii ya Kitutsi na huku waangalizi  wa umoja wa mataifa wakiwa wapo na butwaa.

Monday, April 7, 2014

Rais Paul Kagame awakalia kidede waliohusika na mauaji ya kimbari.

Rais Paul Kagame awakalia kidede waliohusika na mauaji ya kimbari.

Kigali, Rwanda - 07/04/2014.
Wanachi wa Rwanda wameadhimisha kumbumbu  ya mauaji ua kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuwawa katika mauaji ambayo yalichukua zaidi ya siku miamoja.

Rais Paul Kagame, akilihutubia taifa katika kuadhimisha siku ya mauaji ya kimbari amesema " japokuwa muda umepita ukweli upo katika historia ambayo ipo na itajiandika, kwani watu au nchi hawawezi kuhonga au kulazimisha kubadirisha historia japo wawe na nguvu au kuwa nguvu kwani ukweli upo wazi"

" Na miaka 20 sasa cha muhimu ni  kuwa hawa kuwa na imani ya kusimamisha mauaji ya Wanyarwanda na wanachofanya ni kukanusha."
 "Wanyarwanda wanatakiwa kujua uhai na thamani ya mtu ambayo wenzetu hawajui nini maana yake na kuitumia vibaya."

Kabla ya kuhutubia, rais Kagame mbele wa wageni waalikwa aliwasha mwenge wa amani  ambao utakimbizwa kwa kuzungushwa nchi nzima kwa muda wa siku 90 ikiwa ni ishara ya kukumbuka siku ambazo mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994. 

Rais Paul Kagame amekuwa akizilaumu  Belgium na Ufaransa kwa kuhusika na mauaji ya kimbari yaliyo tokea nchi Rwanda mwaka 1994 na kuzitaka nchi hizo kuwa za uwazi katika ukweli, kwani histotoria ya mauaji ya Wanyarwanda itakuwa nao daima japo nchi hizo zimekuwa zikikanusha kuhusika na mauaji hayo.

Aliyekuwa rais wa Pakistani anusurika Kifo.

Rawapindi, Pakistan - 07/04/2014. Aliyekuwa rais wa Pakistani na ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya uhaini ameponea chupu chupu na jaribio la kutaka kumwua ambalo lilifanyika hivi karibuni.

Pervez Musharraf alipona hali hiyo ya kutaka kuuwawa baada ya bomu kulipuka katika daraja lililopo njia ambayo muda mchache Musharraf alitakiwa kuitumia kuelekea katika kambi ya jeshi iliyopo Rawapindi ambapo alitakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Musharafu ambaye kwa sasa anaishi nje kidigo ya jiji la Islamabadi alielekea hospital kwa kutumia njia nyingine ambayo ilikaguliwa na walinzi wake.

Kupona huko kwa Pevez Musharraf kumekuja  kwa mara ya pili, baada ya  bomu kulipuka Desemba  2003 katika maeneo ya Rawapindi baada ya msafara wake kupita katika eneo ambalo bomu lilikuwa limetegwa  na kumkosa kwa dakika chache.

Kundi la Taliban limekuwa likihaidi kumwua kiongozi huyo, ambaye alichukua madaraka kwa nguvu za kijeshi mwaka 1999 na baadaye kuwa rais tangu mwaka 2001 -2007.

Rais Assad atuma salamu kamambe  kwa rais wa Urusi.

Damascus, Syria - 07/04/2014. Rais wa Syria amefanya mazungumzo na aliyekuwa waziri mkuu wa Urusi Sergi Stepashin na kujadili ni kwa jinsi gani nchi hizo zitazidi kushikiana.

Rais Bashaar al Assad katika mazungumzo hayo alisema  " naomba kamwambie Vladmir Vladimirovich Putin kuwa mimi  nipo na sitaondoka kama alivyo ondoka rais wa Ukraine Viktor Yanukovich"

"Na hii hali ya kivita tutaimaliza na kushinda, kwani serikali yangu ipo imara na kupambana na  magaidi wanaodhaminiwa na wapinzani wenye nia mbaya na Syria kwa tamaa zao."

 Sergi Stepashim ambaye alikuwa waziri mkuu wakati wa utawala wa  rais Boris Yeltsin amesema " Assad  inaungwa mkono na watu wengi nchi Syria na hata kama kura zikipigwa leo atashida"

" Na kwa kuwa anataka kugombania uchaguzi ujao basi naimani atashida kwa kura nyingi bila shida"Alimalia Sergie Stepashin.

Urusi imekuwa nchi ambayo inaungana mkono serikali ya rais Assad, ambaye kwa sasa nchi yake ipo katika vita ambavyo vimeanza zaidi ya miaka miwili kati yaserikali na makundi ya upinzani ambayo inasadikika kuungwa mkono na badhi ya nchi za Magharibi  na nchi za Kiarabu na huku majeshi ya Assad yakiungwa mkono na kundi Hezhibollah.

Saturday, April 5, 2014

Rwanda yatimiza miaka 20 tangu mauaji ya kimbari.

Rwanda yatimiza miaka 20 tangu mauaji ya kimbari.


Rwanda chini ya Uongozi wa rais Paul Kagame imekuwa na amani na maendeleo.

Kigali Rwanda - 05/04/2014. Wananchi wa Rwanda wameadhimisha miaka ishirini tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuwawa kutokana na chuki za kijamii zilizo zilizo sambazwa na kukuzwa katika jamii nzima ya Wanyarwanda.

Mauahi hayo yalitokea wakati watu wa jamiii ya Kihutu walipowauwaa watu wa jamiii ya Kitutsi jambo ambalo lilifanya dunia nzima kushikwa na butwaa kwa kuto kuamini na huku maelfu ya Wanyarwanda wakikimbia nchi yao katika kipindi chote cha mauaji hayo.

Akiongea katika kuadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji haya, rais wa Rwanda Paul Kagame amesema " jumuiya ya kimataifa na hasa Ufaransa zinatakiwa kulaumiwa kwa kuachia mauaji hayo kutokea."

Serikali ya rais Kagame imekuwa imara katika kuhakikisha kuwa historia hii haitarudia tena nchi Rwanda kwa kupitisha sheria kali ambazo zinazuia chuki katika jamii ya Wanyarwanda. na vile vile serikali ya Rwanda imehakikisha kuwa huduma za elimu. afya na nyingine muhimu zinapatikana kwa kila mtu aishiye katika nchi hiyo.

Mauaji ya Rwanda yalitokea mwaka 1994 na kuwa ya kihistoria katika bara la Afrika kwa jamiii moja ya wwtu kutaka kuifuta jamii nyingine ya watu kwa kuwauwa kwa sababu za chuki za kihistoria.

Askofu mkuu wa Anglikani atahadhalisha kuhusu ushoga.

London, Uingereza - 05/04/2014. Askofu mkuu wa kanisa la Anglika ameonya kuwa  ikiwa kanisa hilo litaruhusu ndoa za mashoga huenda likawa na wakati mgumu na idadi kubwa  waumini wake.

Askofu Justin Welby alisema " Kwa kiasi kikubwa waumini wa kanisa la Anglikani wapo katika bara la Afrika  na wakristu  ambao wamekuwa wakidhurika ni wale ambao wanaunga mkono maswala ya kishoga."

" Na hii inaweza kutokea ikiwa kanisa litapitisha sheria ya kuruhusu mashoga."

Akiongezea Askofu Welby amesema kuwa  wakuu wa kanisa hilo  nchi Sudani ya Kusini wamemwomba kutokubadirisha misingi ya kanisa, kwani "kiwa itatokea kubadirishwa basi waumini wa Sudani ya Kusini hawata kuwa na ushirikiano na kanisa la England."

Askofu Justin Welby aliyasema haya baada ya kumaliza ziara yake kutembelea bara la Afrika ili kujione nini kinatakiwa kifanyike ili kukuza imani ya waumini wa kanisa la Anglikani katika bara hilo.

Friday, April 4, 2014

Matumizi ya mtandao yatonesha kidondo cha Marekani na Kuba.

Makao makuu ya EU yawa kiwanja cha mapambano.


Brussels, Ubeligiji - 04/04/2014. Polisi katika jiji la Brussels wamepambana na waandamanaji wanao pinga mbinyo wa  matumizi  na mapato yaliyopo katika nchi za jumuiya ya nchi za wanachama wa Ulaya 

Wakitumia majiwasha na mabomu ya kutoa machozi, polisi waliwatawanya wanadamanaji waliyo kuwa katika maeneo ya ofisi za nchi za jumuiya wa umoja wa Ulaya,huku wengi wao walikuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi tofauti vilivyopo katika nchi za hizo.

Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yanayo kosoa mwenendo mzima wa mbinyo wa matumizi na uwekezaji  ambao uongozi wa nchi za jumuiya ya Ulaya umekuwa ukikazania mbinyo huo kama njia pekee ya kuinua uchumi.

Mmoja wa kiongozi wa chama cha wafanyakazi ETUC, Emanuel Bonaciana amesema kuwa "nia ya maandamano ni kuwataka  viongozi kuja na njia mbadala ya kukuza uchumi kwa kuwekeza na ajira iliyo sawa na haki kwa wote."

Hali ya mbinyo wa matumizi na uwekezaji, umeleta hali ya mstuko kwa wananchi wa nchi za jumuiya ya Ulaya na kulaumu kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa walio wengi na wachache ndiyo wanaoifaidika na mpango huo  na hasa mabenki.

Matumizi ya mtandao yatonesha kidondo cha Marekani na Kuba.



Havana Kuba 04/04/2014.  Serikali ya Kuba imeilalamikia Marekani kwa kutumia mtandano unao fanya kazi kama  Twita ili kuaandaa mapinduzi nchini Kuba.

Msemaji wa serikali ya Kuba alisema kuwa mtandaa huo ambao una matumizi sawa na twita ulikuwa unalengo la kuhimiza wananchi wa Kuba kupingana na "serikali ya Kuba kwa kuwa ni ya kikomunisti"

Hata hivyo serikali ya Marekani imepinga kuhusika na njama hizo zakuhimiza wananchi wa Kuba kupingana na serikali yao, bali Marekani imekubali kuwepo na mtandao huo kama twita ambao ulikuwana madhumini ya kuwasaidia wa Kuba katika mawasiliano na ujenzi wa demokrasia.

Msemaji wa serikali ya Marekani Marie Harf amesema kuwa "hii siyo siri kwani mradi huo ulikuwa na nia ya kuweka uwazi ukuzaji wa demokrasia na ulikuwa wa miaka mitatu ambapo ulighalimu dola za $1.2 millioni na ulipitia na kudhaminiwa kwa kutumia wakala tofauti"

" Na hatukusambaza maswala ya kisiasa" Alimaliza Marie Harf.

Hata hivyo shirika la habari la AP limeripoti kwa kusema " mradi huu ulibuniwa kuzunguka vikwazo vya kimtandao vilivyo wekwa na serikali ya Kuba kwa kutumia makampunu yenye ubia na shell chini ya uongozi wa USAID shirika ambalo huwa linatoa misaada kwa masikini duniani"

Mzozo wa Kuba na Marekani ni wamuda na kuwa ni moja ya mzozo baridi ambao unaanzia 1962 na kupelekea Marekani kuwa na vikwazo na Kuba tangu kipindi hicho.

Wapalestina na Waizrael wampa kichwa kuuma John Kerry.

Rabat, Moroko - 04/04/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amesema kuwa kuna nia kubwa ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya kati ya Waizrael na  Wapalestina japo kwa sasa  kuna ugumu umejitokeza.

Waziri John Kerry aliyaongea hayo mjini Rabat Moroko, kwa kusema kuwa "hali ya mazungumzo yakuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina inahitaji kuangaliwa kwa njia zote za umakini kwa kuzingatia kwa sasa pande zote mbili simechukua hatua ambazo zinaleta ugumu wa kuendeleza mazungumzo ya kuleta amani."

Kutamka kwa waziri John Kerry kuhusu ugumu wa mazungumzo ya kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael kumekuja baada ya Uingozi wa Wapalestina  kusaini kwa pamoja kutaka kujulikana kama taifa , ambapo hapo awali ilikuwa ni moja ya makubaliano yaliyowekwa katika ya Izrael na Palestina.

Uongozi wa Palestina pia  umedai "Izrael imevunja mkataba wa makubaliano wa kuwaachi huru wafungwa wa Kipalestina waliopo katika jela za Kiizrael na kusitishwa kwa utanuzi wa ujenzi wa makazi ya Waizrael katika maeneo ya Wapalestina."

Hata hivyo kwa mijibu wa wachunguzi wa maswala ya amani ya mashariki ya kati wanadai kuwa kama "Kama serikali ya Izrael ingekubali kuaachia wafungwa wa Kipalestina, basi kungesababisha kuvunjika kwa serikali ya waziri mkuu Benyamin Netanyahu, jambo ambalo waziri Netanyahu limemletea ugumu kutimiza ahaadi ya kuwaachia wafungwa hao wa Kipalestina."

Mpango wa kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael umekuwa nawakati mgumu kwa muda mrefu  kwa serikali ya Marekani, jambo jitihada zimekuwa zikifanyika kwa hali na mali ili amani iwepo kati ya Wapalestina na Waizrael.