Saturday, May 24, 2014

Papa Francis aanza ziara nchi za Mashariki ya Kati.

Jacob Zuma ala kiapo kuwa rais kwa mara ya pili mfululizo.

Pretoria, Afrika yaKusini - 24/05/2014. Rais Jacob Zuma  ameaapishwa kwa mara nyingine kuwa rais wa Afrika ya Kusini ikiwa ni muhula wake wa pili kama rais wanchi hiyo.

Baada ya kuapishwa rais Zuma  alisema " kipindi hiki cha uongozi wangu wa miaka mitano tutahakikisha tunainua uchumi na maisha ya jamii kwaujumla."

Katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi, rais Jacob Zuma, amelaumiwa kwa kukosa kuinua maisha ya wananchi walio wengi ambao inasadikiwa hali ya umaskini imekuwa ikiongezeka kwa haraka kila kukicha.

Katika sherehe hiyo, marais na viongozi mbali mbali waliudhulia kuapishwa huko wakiwemo, rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na Goodluck Jonathan.

Rais Jacob Zuma amechukua kiti cha urais chini ya chama cha ANC ambapo kilishinda uchaguzi mkuu uliyofanyika Mei 7 na kuwa chama pekee kinacho ongoza nchi tangu Afrika ya Kusini tangu kukomeshwa kwa serikali ya ubaguzi wa rangi miaka 20 iliyopita.

ICC Hague yatoa hukumu jela miaka 12 kwa German Katanga

Hague, Uhollanzi - 24/05/2014.Mahakama ya kimataifa ICC, inayo shughurikia makosa ya jina na ukiukwaji wa haki za binadamu imemuhukumu kwenda jela aliyekuwa mkuu wa majaeshi ya upinzani nchi Kongo DRC, German Katanga.

German Katanga 36, ambaye alikutwa na makosa ya kuuza siraha ambazo zimetumiwa katika mauaji ya mamia ya watu manamo  mwaka 2003.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Bruno Cotte alisema " mahakama inakuhukumu miaka 12 kwenda jela kutokana na makosa ambayo umekutwa nayo."

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo, wakili wa Katanga amekata rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama.

German Katanga amekuwa ni kiongozi wa pili kuhukumiwa na mahakama ya ICC baada ya mahakama hiyo kumuhuku jela aliyekuwa mkuu wa majeshi ya upinzani Thomas Lubanga mwaka 2012.

Papa Francis aanza ziara nchi za Mashariki ya Kati.

Amman, Jordan - 24/05/2014. Mkuu wa kanisa Katoli dunia Papa Francis amewasili nchi Jordan ikiwa ni moja ya nia yake ya kukuza uhusiano wa karibu na wakazi wa Mashariki ya kati.

Akiongea mara baada ya kuwasili nchini Jordani na kuongoza ibada katika uwanja mkubwa ulipo Amman  Papa Francis alisema " nimatumaini yangu kuwa amani na utulivu utakuwepo kwa wakazi wa eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia nzima, na nawashukuru wananchi wa Jordani kuwa mstari wa mbele katika kuleta amani na kutoa msaada na vile vile kuwa weka kilauhudi ili kumaliza mzozo wa Waizrael na Wapalestina."

Papa Francis alipokelewa na  Mfalme wa Jordan Abdullah II wakati alipo wasili nchi Jordani na baadaye alitembelea katika hekalu la waumini wa Orthodox na vile vile kutembelea kambi ya wakimbizi kutoka  Syria.

Papa Francis katika ziara yake hiyo, ameambatana na wakuu wa dini ya Kiislam na Kiyahudi kutoka  Argentinana ikiwa ni katika jitihada zake za kutaka kuwepo na uhusiano wa karibu na waumini wa dini nyingine.

Siku ya Jumapili atatembelea mji wa Bethlehem - West Bank na kuongoza ibada katika eneo ambalo inaaminika ni mahali alipo zaliwa Yesu Kristu.

Thursday, May 22, 2014

Iran yadai ipo tiyari kwa majibu ya kivita.

Uchaguzi wa urais nchi Malawi wawa tumbo joto kwa rais Joyce Banda.

Lilongwe, Malawi - 22/05/2014. Rais wa Malawi Joyce Banda na ambaye anagombania tena kiti cha urais, amekutwa na wakati mgumu  baada ya kashfa kuibuka  kuwa wa Malawi imepoteza mamilioni ya pesa kutoka hazina kuu wakati wa uongozi wake.

Huku akiwa anasubiri mataokeo ya uchaguzi mkuu ambapo  zaidi ya watu wapatao millioni 7 wamepiga kura, rais Joyce Banda alilalamikia mfumo mzima wa uchaguzi kwa kudai kuwa ''kumekuwa na ukiukwaji wa kimsingi wa mwenendo mzima wa uchaguzi na mitandazo ya kuhesabia kura kuvurugwa kimakusudi.''

''Na mimi sihusiki na wizi wa millioni ya dola za Kimarekani zinazo tajwa.''

Malawi inakadiliwa kupoteza zaidi ya dola  million 30, na pia serikali ya rais Joyce Banda iliwekewa vikwazo vya misaada na na pesa kutoka nchi wafadhili tangu kutokea sintofahamu katika uongozi wake.

Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi mkuu wa Malawi Maxon Mbendera amepinga kauli hiyo ya rais banda kwa kusema '' hakuna ukiukwaji wa sheria uliovunjwa na mitandao ipo safi, na kama ingetokea tatizo basi tunayo plan B ya kluhesabu kura kwa mkono.''

Rais Joyce Banda, amekuwa na wakati mgumu kutoka kwa wapinzani wake ambao wanaongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Malawi  Peter Mutharika Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kwa pamoja nchini Malawi ulinafanyika siku moja kwa mara ya kwanza tangu Malawi kupata uhuru 1962.

Iran yadai ipo tiyari kwa majibu ya kivita.

Tehran, Iran - 22/05/2014. Serikali ya Iran imesema kuwa  itakuwa ni makosa makubwa kwa Izrael kufanya mashambulizi nchini Iran kwani  majibu ya Iran baada ya kushambuliwa yatakuwa hayana mfano.

Onyo hilo limetolewa na mkuu wa maswala ya kijeshi na ushirikiano wa kiulinzi Brigedia Ramezan Sharif kwa kusema ''Natumaini Izrael haitafanya makosa kama hayo, na wakuu wa wanchi hiyo wenye busara wanajaribu kuzuia hatua hiyo kwa kujua kuwa Iran itajibu mashambulizi ambayo dunia nzima itastuka.''

Kuongea kwa mkuu huyo wa jeshi la Iran, kumekuja baada ya kudai kuwa vitisho vinavyo fanywa na baadhi ya viongozi wa Izrael vinaangaliwa kwa makini.

Mvutano na vitisho kati ya Iran na Izrael vimekuwa vimekuwa vikiendelea huku Izrael ikidai Iran izuiwe kuendelea na mradi wake wa kinyukilia kwa madai unania ya kutengeneza mabomu yatakayo tioshia amani kwa Irzael na mashariki ya kati nzima.

Na wakati huo huo Iran kudai kuwa mradi wake wa kimnyuklia ni wa kimaendeleo ya kisayansi, na pia kudai Izrael kuweka wazi kuwa ina siraha za kinyuklia jambo ambalo mpaka sasa Izrael haija liweka wazi.

China na Urusi zawaweka ngumu Umoja wa mataifa.

Washington, Marekani - 22/05/2014. China na Uruusi zimepiga kura ya veto kwa kupinga muswada wa kutaka serikali ya Syria kupelekwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Kura hiyo ya veto immepigwa  baada ya Ufaransa  kuwakilisha muswada huo ambao unaishutumu serikali ya Syria kuhusika na ukiukwaji wa haki za minadamu na makosa ya jinai.
Muswada huu ambao uliungwa mkono na nchi 58, uligonga mwamba uliowekwa na China na Urusi kwa madai kuwa ulikosa baadhi ya ukweli.

Akiongea baada ya kura hiyo ya veto, balozi wa umoja wa mataifa wa Urusi Vitaly Churkin alisema '' uamuzi wa kupiga kura ya veto ni mzuri kwani unania ya kupunguza mlolongo wa kuendelea vita nchini Syria ambao umekuwa ukichochewa kila kukicha.''

Syria imekuwa katika vita vya wenyewe kwa kwa kipindi cha miaka mitatu na zaidi na inakadiriwa watu zaidi ya 175,000 wamecha poteza maisha na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa.


Wednesday, May 21, 2014

China na Urusi zasaini mkataba wa karne.

China na Urusi zasaini mkataba wa karne.

Beijing, China - 21/05/2014. Urusi na China zimesainia mkataba wa biashara wa malighafi mafuta ambao utatudu kwamuda wa miaka 30.

Makubaliano hayo  kufanya biashara pamoja katika sekta ya malighafi mafuta yamechukua miaka kumi ya majadiriano na hatimaye  kufikia makubaliano, ambapo kuanzi sasa  shirika la uzalishaji wa malighafi mafuta la Urusi Gazprom na la China CNPC kwa pamoja yatafanya bishara ambayo itagharimu $ 400 billion.

Mkurugenzi mkuu wa Gazprom Aleksey Miller lisema " mkataba wa makubaliano na matumzi yatakavo fanyika itabaki ni kati ya Gazprom na CNPC katika makubaliano ya kibiashara."

Mkataba wa Urusi na China umeitwa mkataba wa karne, kwani utasaidia nchi hizi mbili kuwa karibu zaidi jambo ambalo nchi za muungano wa Ulaya na Marekani zitauchunguza na kuwa makini na nchi  hizi mbili.

Kitendo cha Urusi kusaini mkataba na China  kibiashara ya malighafi mafuta kimetafsiliwa kuwa  ni ushindi mkubwa kwa rais Vladmir Putin, kwani kutokana na mgogoro wa Ukraine, Urusi imejikuta ikivutana na nchi za muungano wa jumuiya ya Ulaya na Marekani na hata kufikiwa Urusi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Friday, May 16, 2014

Kenya yashambuliwa tena na mabomu.

Kenya yashambuliwa tena na mabomu.

Nairobi, Kenya - 16/05/2014.Wakazi wa jiji la Nairobi walishikwa na mstuko mkubwa baada ya milipuko ya mabomu kutokea kwenye soko la Gikomba ambalo ni la pili kwa ukubwa na maarufu kwa uuzaji wa nguo na bidhaa ndogo ndogo.


Akiongea baada ya tukio hilo, rais wa Kenya. Uhuru Kenyatta amesema "tutawatafuta pale walipo wale 
wote wanao husika au kuandaa kuvurga amani nchi Kenya, kwani wanafanya vitendo vya kishetani "

" Naamini kwa ushirikiano wa pamoja tutashida vita hivi zidi ya ugaidi." Asisitiza rais Kenyatta.

Milipuko hiyo ya mabomu ambayo imesababisha mauaji ya wati 12 na kujeruhi watu 90, imetokea wakati wananchi wa Kenya hasa wakazi wa jiji la Nairobi wakiwa bado na jeraha la kulipuliwa kwa eneo la maduka ya kisasa la Westgate ambapo watu 67 waliuwawa mwishoni kwa mwaka jana baada ya wapiganaji wa Al Shabab kuvamia eneo la maduka hayo.

Kenya imekuwa inakumbwa na milipuko ya mabomu ambayo kundi la Al Shabab limekuwa likidai kuhusika na  na mashambulizi yanayo tokea nchini humo ikiwa ni kupinga kitendo cha serikali ya Kenya kupeleka jeshi lake nchi Somalia ili kupambana na kundi la Al Qaeda

Hata hivyo serikali ya Kenya imekasirishwa na kitendo cha Uingereza kuwakataza raia wake kutokwenda Kenya na kuwataka wale walipo Kenya kuondoka kwa madai kuwa hakuna uhakika wa usalama wa raia hao wakati watakapo kuwa  Kenya.

Nchi mwenyeji wa kombe la dunia 2014 yavutana na wananchi.

Sao Paulo, Brazil - 16/05/2014.Waandamanaji wamepambana na polisi nchi Brazil kwa kupinga kitendo cha serikali kuaandaa michuano ya kombe la dunia, huku wanachi   walio wengi wakiwa na maisha ya kimasikini.

Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika miji tofauti nchi humo, kuliwafanya polisi kutumia mabomu ya machozi ili kupambana na waandamanaji waliokuwa na asira huku waki imba kudai maisha bora na huku wakipindua magari yaliyokuwa barabarani pia kuvunja baadhi ya maduka.

Mmoja wa waandaji wa maandamano hayo Luana Gurther alisema " serikali inatakiwa kutumia pesa katika kujenga hospitali, shule, nyumba na kusaidia kuinua maisha ya watu, badala ya kutumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kombe la dunia."

Maandamano hayo yamekuja baada ya hali ya maisha kuwa juu, na huku bei ya vitu kupanda bei kwa asilimia 50% .

Brazili itakuwa mwenyeji wa kombe la dunia  la mwaka huu wa 2014 na pia michuano ya michezo ya  Olimpiki ya 2016.

Umoja wa mataifa wadai ukiukwaji wa haki za binanadamu ni mkubwa nchini Ukraini.

Geneva, Uswisi - 16/05/2014. Umoja wa mataifa mestushwa na hali ya  uvunjwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchi Ukraini,  baada ya kupokea  ripoti yenye kurasa 37 ambayo imetolewa na shirika la kutete haki za binadamu la Umoja wa mataifa.

Akiongea kuhusu hali hiyo, mkuu wa kitengo cha kutete haki za binadamu Navi Pillay amesema " uvujwaji wa haki za binadamu nchi Ukraine umekuwa ukifanywa kwa wale watu ambao wamekuwa wakiandamana bila kufanya vurugu na pia na wale wasiohusika katika vurugu na huku polisi wa serikali wakiwa wanaangalia au wakati mwingine kushiriki katika kufanya matendo ya unyanyasaji."

" Hii pia imekuwa ikitokea kwa waandishi wa habari kupigwa kutekwa nyara na hata jeruhiwa kwa makusudi." Aliongezea Pillay.

Naye aliyekuwa Kansela wa Ujerumani kati ya 1074-1982 Helmut Schmidt, ameilaumu  muungano wa nchi za Ulaya kwa kusema " Nchi za muungano wa Ulaya zinavyofanya katika mgogoro wa Ukraini zinatishia kuzuka kwa vita na Urusi, kwani  kadri siku zinavyo kwenda na hali hii inazidi kuwa mbaya  na hali kama hii ilitokea mwaka 1914."

Mazungumzo hayo ya kuzilaumu nchi za muungano wa Ulaya yaliyo fanywa wakati  Kansella Helmut Schmidt alipo ongea  na gazeti la Bild hivi karibuni, ili kuona mwono wake wa hali halisi ya ushiriki wa muungano wa nchi za Ulaya katika mgogoro wa Ukraini.

Marekani yadai ikoma macho na Iran.

Al-Quads, Izrael - 16/05/2014. Marekani imeihakikishia Izrael kuwa haitaruhusu Iran kutengeneza bomu la nuklia.

Matamshi hayo yaliongewa na waziri wa Ulinzi wa Marekani  Chuck Hagel, ambaye yupo nchini Izrael kwa ziara ya kiserikali wakati  apokutana na waziri mkuu wa Izrael  Benjamin Netanyahu katika jiji la Jerusalem ambalo kwa kiarabu linajulikana kama Al-Quads.

"Napenda kuwahakikishia kuwa  Marekani ipo macho kwa kila hali ili kuhakikisha Iran haitengenezi bomu lolote la nyuklia, na kama Iran itaendelea kutosikia basi hatua kali zitachukuliwa kufuatia sheria za kimataita."

Akizungumzia kuhusu matamshi hayo ya waziri Chuck Hagel, mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia na mwandishi wa habari wa Iran Hamid Golpira amesema"Izrael imekuwa ikikanusha kuwa haina mabomu ya nyuklia wakati ukweli unajulikana kuwa Izrael ina mabomu ya nyukila yapatayo 200, na mpaka sasa haitaki kuweka wazi japo jumuiya ya kimataifa inalikua hili, ikiwemo  Marekani."

Mvutano kati ya Marekani , washiriki wake na Iran kuhusu masuala ya kinyuklia umekuwa ukipigwa danadana katika kila vikao vinavyo fanywa vya  5+1  vya nchi za Iran, China, Ujerumani, Marekani, Ufaransa na Uingereza. kwa kutoa majibu ya sintokubaliana kila baada ya mikutano

Wednesday, May 14, 2014

Umoja wa mataifa waingia doa na mapambano ya Ukraine.

Jaji aamuru mwanariadha akapimwe akili.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 14/05/2014. Jaji  anayesikiliza kesi ya mauaji nayo mkabili mkiambiaji Oscar Pistorius, ametoa amri ya kuchunguzwa akili kwa mwanariadha huyo ili kuweza kupata kufahamu uwezo wake wa akili na ufahamu.

Akitoa amri hiyo Jaji Thokozile Masipa alisema " mshitakiwa anatakiwa kuangaliwa kiakili kwani, itasaidia mahaka kujua ni kwa kiasi gani haya makosa yalifanyika, kwa maana hali ya kutambua akili na ufahamu wa mtu si kazi ya mahakama."

"Matatizo ya akili yanatakiwa kuangaliwa na siyo jambo la kulifumbia macho." Aliongezea Jaji Masipa.

Uamuzi huo wa Jaji Masipa wa kutaka Oscar Pistorius kuchunguzwa akili umekuja baada ya kusikiliaza mwenendo mzima wa kesi na pia kwa upande wa utetezi kutaka uchunguzi huo ufanyike kwa kutokana na historia ya maisha ya mshitakiwa.

Oscar Pistorius, ambaye ni mwanariadha wa kwanza kushiriki katika mbio za Olimpiki jumla za mwaka 2012 London akitumia miguu bandia, alikili kumwua bila kukusudia mpenzi wake Reeva  Steenkamp katika siku ya wapendanao dunia.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael ahukumiwa kwenda jela.


Jerusalem, Izrael - 14/05/2014. Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael amehukumiwa kwenda jela kwa muda wa miaka sita na kutakiwa kulipa faini ya Euro 210,000.

Ehud Olmert ambaye alikuwa waziri mkuu mwaka 2006, alikutwa na hatia ya kuhusika katika kula  rushwa wakati alipo kuwa meya wa jiji la Jerusalem.

Akitoa hukumu, Jaji David Rosen alisema, " kuwa kiongozi anaye ongoza jamii na kukabidhiwa dhamana ya wananchi ni lazima awemfano bora kwa jamii, na kitendo cha kukubali kula rushwa lazima kikomeshwe kwa kiongozi yoyote aliyehusika kwa kuadhibiwa vikali."

"Makosa aliyokutwa nayo Olmert yalikuwa kukubali kula mlungura katika harakati za kuandaa mipango mji, na pia pesa nyingi kutumika kiholera katika kutangaza baadhi ya miradi na vilevile kutoa unafuu wa kodi kinyume na sheria na hata kushinikiza baadhi ya sheria kuundwa ili kutoa ubukheri kwa wahusika katika ujenzi wa  jiji la Jerusalem."

Kesi ya Ehud Ormert imechukua zaidi ya miaka miwili,na uchunguzi  ulianza rasmi kufanyaki mwaka 2010 na baadaye kuonekana  Olmert alikuwa muhusika mkuu katika suala zima la matumizi mabaya ya pesa wakati wa utawala wake kama meya wa jiji la Jerusalem na kumfanya alijiudhuru 2008 uwadhifa wake wa uwaziri mkuu, baada ya polisi kuanza matayarisho ya kumfungulia kesi.

Umoja wa mataifa waingia doa na mapambano ya Ukraine.

New York, Marekani - 14/05/2014. Umoja wa Mataifa umekutwa na wakati mgumu wa kujibu maswali baada ya helikopta yenye nembo ya UN kuonekana kutumika katika mashambulizi nchi Ukraini.

Habari kutoka katika ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon zimesema, " nikinyume na sheria kutumia vifaa au helikopta ya umoja wa mataifa katika mapambano yoyote na hii inaleta sura potofu kwa jamii nzima ya kimataifa kuhusu ufanisi wa umoja wa Mataifa."

"Vifaa, ndege na helikopta za Umoja wa Mataifa huwa vinatumika katika kusaidia na kuokoa watu walio katika hali ya hatari na maafa, hivyo serikali ya Kiev imevunja sheria na kwenda kinyume na mkataba wa umoja wa amataifa na tunalaani itendo cha kutumia vifaa vya Umoja wa Mataifa katika mapambano ya kivita."

Hata hivyo waziri wa ulinzi wa  Ukraine imekanusha kutumia helikopta ya umoja wa mataifa katika mapambano yake na wapinzani ambao wanataka kujitenga na serikali ya Kiev, na alipo ulizwa kuhusu helikopta yenye nembo ya UN kuonekana kufanya mashabulizi akili kataa kulizungumzia swala hilo tena.

Helikopta yenye rangi nyeupe Mil Mi-24 imeonekana ikitumika katika mashambuzi ya kuwashambulia wapinzani wa serikali  ya Ukraine, ambo wanapinga uhalali wa serikali ya sasa ambayo iliingia madarakani baada ya mapinduzi yaliyo mng'oa rais Victor Yanukovych  Februari mwaka huu 2014.

Mapambano ambayo yanaendelea nchi Ukraine yamekuwa baada ya majimbo ya Donetsk na Lugansky kupiga kura ya maoni ya kujitenga na serikali ya Kiev, jambo ambalo Kiev inalipinga.

Tuesday, May 13, 2014

Msuruhishi wa machafuko ya Syria atundika madaruga juu.

Waumini wa dini waajiliwa kupigana na ugaidi nchi Marekani.


New York, Marekani - 13/05/2014. Polisi katika jiji la New York wamekuwa wakiwaajili watu wenye imani na dini Kislaam tangu kutokea mashambulizi ya Septemba 11.

Likilipoti habari hizi, gazeti la New York Times  limeandika "Kamati ya usalama iliamua kuwaa ajili waumini hao wa dini ya Kiislaam katika hotel na kwenye Miskitiili kuweza kujua na kupata habari mapema kabla, kwani  maeneo hayo yamekuwa yakitumika katika mikutano na pia kuajili watu kujiunga na makundi ya kigadi."

Likiongeza katika ripoti hiyo limeandika kuwa " wengi wa waajiliwa wamekuwa wale wanao toka nje ya Marekani."

Akithibitisha kwa kuwepo kwa uajili huo, mkuu wa kitengo cha kupamana na ugaidi John Miller alisema " Tunaangalia watu ambao wanaweza kutupatia undani wa ugaidi kutoka sehemu tofauti duniani jambo ambalo litasaidia kupambana na ugaidi kwa urahisi."

Hata hivyo kufuatia uamuzi wa polisi kuajili watu wenye imani na dini ya Kiislaam, malalamiko yamekuwa yakitolewa na wahusika kwa kudai inabidi washirikiane na polisi kwani hawana njia nyingine.

Gazeti la New York Times limelipoti habari hizi kufuatia sheria ya uhuru wa habari.

Msuruhishi wa machafuko ya Syria atundika madaruga juu.


New York, Marekani 13/05/2014.Lakhdar Ibrahimi ambaye  aliyeteuliwa na umoja wa mataifa kuwa mkuu katika kusuruhisha suala la uleteji wa amani na mapatano katika myumbo wa kisiasa na vita kati ya Wasyria ametangaza kujiudhuru ifikapo mwisho wa tarehe 31/05/2014.

Akitangaza kutaka kujiudhuru huko katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema "Lakhdar Ibrahimi atajiudhuru"

Hata hivyo Ban Ki-moon haueleza ni nini kilicho mfanya msuruhishi huyo kutaagaza kujiudhuru wakati hali ya Syria bado ni tete.

Akiongea baada ya habari kutangazwa Lakhdar Ibrahimi alisema " nimekuwa nafikirika kujiudhuru  kila kukicha na sasa muda umefika wa kutangaza rasmi siku ya kujiudhuru kwangu."

Lakhdar Ibrahimi toka kuteuliwa kwake kushughulikia suala la machafuko ya Syria amaekuwa na wakati mgumu wa kuwapatanisha wapinzani wa serikali na serikali ya rais Assad, jambo ambalo lilimfanya akili na kuomba radhi kwa wananchi wa Syria kuwa hali bado ni tete katika kufikia makubaliano kwa pande zote mbili.

Kujiudhuru kwa Ibrahimi kumekuja wakati serikali ya rais Bashaar Assad imekuwana nguvu zaidi kuliko wapinzani na kufanikiwa kuuchukua mji wa Alepo ambao ulikuwa makao makuu ya wapinzani wa serikali na huku rais Bashar Asaad akiwa katika kampeni ya kugombea tena kiti cha urais kwa miaka saba ijayo, ambapo anatarajiwa kushinda kwa wingi wa kura.

Matokeo ya kura za maoni nchini Ukraine yawa kitendawili.


Moscow, Urusi - 13/05/2014. Matokeo ya kura ya maoni ya kutaka kujitawala kwa majimbo ya  Donitsk na Lugansk yamezidi kuleta kicha kuuma kwa uongozi wa nchi za jumuiya ya Ulaya na Marekani na huku Urusi ikiwa inachukua muda kutathmini nini kitatokea.

Kufuatia matokeo ya kura za maoni katika majimbo hayo,  serikali za majimbo hayo yameitaka Urusi kukubali kuziunganisha katika serikali ya shirikisho na kuwa sehemu ya Urusi.
Naye msemaji  wa rais Dmitry Peskov akjibu kuhusu maombi ya majimbo hayo amesema "Urusi Urusi bado natafakali kwa makini juu ya maombi hayo."

Matokeo ya kura katika majimbo hayo ya Donietsk na Lugansk yame pelekea viongozi wa majimbo hayo kutangaza kusimamisha maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao ulitarajiwa kufanyika hivi karibuni jambo
ambalo Marekani imetishia kuwa " ikiwa hakutafanyika uchaguzi mkuu, vikwazo zidi ya Urusi vitazidishwa."

Kura zamaoni ambazo  zilipigwa siku ya Jumapili na  kwa wingi wa kura za asilimia 90 za kuunga mkono kwa majimbo ya Donetsk na Lugansk kujitenga na serikali ya Kiev,yameleta mitazamo tofauti.

Urusi imeshiria msimamo wake kuwa machafuko na mauaji yanayo endelea nchi Ukraine ni sababu ya serikali ya Kiev kushindwa kujua la kufanya, kwani imekuwa ikiongozwa na nguvu za nje badala ya kukaa na kufanya mazungumzo na wapinzani wa serikali na wakati huo huo Marekani na washiriki wake wakuu jumuiya ya Ulaya, kupinga na kulaani matokeo pia kutanganza kutoyatambua,

Monday, May 12, 2014

Wanajeshi wa kukodiwa watumika nchi Ukraine


Serikali ya Nigeria yapinga matakwa ya kundi la Boko Haram.

Maiduguri, Nigeria - 12/05/2014. Kundi la kigaidi la Boko Haram, limesambaza na kuzimeonyesha video za wasichana wa shule iliyowateka karibuni wiki nne zilizo pita.
Video ya kwanza ilikabidhiwa kwa shirika la habari la Ufaransa AFP na baadaye kuanza kuonekana katika mitandao tofauti ambapo wasichana hao walionekana wa kiswali.

Akiongea baada ya kuonyeshwa kwa video hiyo ya wasichana hao, mkuu wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau alisema " wasichana hawa watashikiliwa hadi hapo wanachama na wapiganaji wa Boko Haram watakapo achiwa huru"

 Naye mwakilishi wa BBC aliyepo Nigeria John Simpson amesema "kubadili nia huko kwa kundi hilo la Boko Haram kumeo nyesha kuwa kundi hilo lipo tiyari kuongea kuhusu kuachiwa kwa wasichana hao."

Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002 na toka hapo limekuwa likifanya mashambulizi zidi ya raia na ikiwa ni njia ya kuonyesha kupingana na mwenendo wa serikali ya Nigeria.

Jina Boko Haram linamaana ya kuwa  elimu na utamaduni wa kutoka nchi za Magharibi ( Ulaya na Marekani) ni marufuku kufuatwa na  wanchi wa Nigeria hasa wale walipo katika jimbo la Maiduguri

Wanajeshi wa kukodiwa watumika nchi Ukraine.


Donetsk, Ukraini - 12/05.2014. Maafisa usalama wa jimbo la Donetsk wamethibitisha madai yaliyotolewa na gazeti la Bild am Sonntag la Ujerumani   kuwa wanajeshi mamluki wa kukodiwa kutoka shirika la ulinzi  linaloitwa Xe Services lenye makao yake nchini Marekani  wameletwa nchi Ukraine ili kusaidiana na jeshi katika harakati za kupambana na wanapingana wanaopingana na serikali ya sasa ya nchi hiyo.

Mapema April 29/2014 gazeti la Bild  am Sonntag lililipoti kuwa kitengo cha usalama cha Ujerumani (BND) kilimpa maelezo Kansela Angela Merkel kwa kumweleza kuwa wanajeshi wa kigeni wa kutoka shirika la Xe zamani lililo julikana kama Blackwater na washiriki wake wapo nchi Ukraine tayari kusaidiana na serikali ya Kiev.

Maafisa hao wa usalama wamesema kuwa kuna idadi ya wanajeshi 400 mamluki ambao wapo nchi ni Ukraine na baadhi yao wameonekana kushiriki katika operesheni nzima ya kupambana na  wapinzani wa serikali ambao serikali ya Kiev inadai kuwa wanaungwa mkono Urusi, japo Urusi imekuwa ina kana kuhusika na hali ya machafuko yaliyopo nchini Ukraine na kwa kudai serikali iliyopo ndiyo ya kulaumiwa kutokana na machafuko yaliyopo nchini humo.

Nguvu za kisayansi katika jeshi la Iran za zidi kuonekana.


Tehra, Iran -12/05/2014. Iran imefanikiwa kutengeneza ndegeaina ya drone, ndege ambazo huwa zinaendeshwa bila rubani  ikiwa ni njia moja ya nchi hiyo ya kuweza kwenda sambamba na nchi nyingine ambazo zina ndege za aina hiyo.

Ndege hiyo ilionyeshwa kwa wataalamu wa kijeshi kutoka Urusi ambao walikuwa nchi Iran kikazi na kuelezwa kuwa "drone hiyo ambayo imetengenezwa kwa kufanana  na za Kimarekani, itakuwa na uwezo wa kurekodi maelezo ya picha na mienendo yoyote itakayo agiziwa kufanya na wataalamu wa  drone hizo"

Iran imekuwa na mikakati mikubwa ya kujiendeleza kisayansi na kiteknologia na vile vile kuhakikisha inaongeza nguvu zake za kijeshi tangu nchi hiyo ilipo kuwa na vita na Irak katika miaka ya 1980-89, na baadaye kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

 Na kutokana na vikwazo hivyo, Iran ilianza kuonyesha umairi wake wa kisayansi katika kijeshi mnamo mwaka wa 1992 baada ya kufanikiwa kutengeneza vivaru cha kivita, mizinga na ndege za kivita ikiwa kama njia ya kujihami.