Saturday, April 24, 2010

G-20 bado ya simama njia panda.

Iran na Zimbabwe zakubaliana kushirikiana.

Harare,Zimbabwe - 24/04/2010. Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amemaliza ziara yake nchi Zimbabwe.
Katika ziara hiyo rais wa Iran, alifungua maonyesho ya biashara katika mji wa Bulawayo baada ya kumaliza kusaini mkataba wa kiuchumi kati ya Zimbabwe na Iran.
Picha hapo juu wanaonekana rais wa Iran kushoto akiwa na mwenyeji wake rais wa Zimbabwe mara baada ya rais wa Iran kuwasili nchini Zimbabwe.
G-20 bado ya simama njia panda.
Washington, Amerika - 24/04/2010. Serikali za nchi wanachama wa kundi la G-20 wameshindwa kuafikiana kuhusu kodi za mapato katika mabenki yote duniani.
Akiongea hayo waziri wa fedha wa Kanada alisema "katika kikao walikuwepo wajumbe walio kubali na wajumbe wengine walipinga kabisa." Kikao hicho kiliitishwa ili kujaribu kutafuta njia ya kukabiliana na hali ya mzunguko wa pesa za mabenki. Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya mawaziri wa fedha wakijadiliana mara baada ya kikao kilichofanyika kutathmini hali halisi ya mzunguko wa fedha. NATO yajadili mbinu za kukabidhi madaraka kwa Waafghanistan.
Talinn, Estonia 24/04/2010. Viongozi wa NATO wamekutana nchini Estonia kujadili kwa undani jinjia gani watafanya kujiandaa kuondoa majeshi nchini Afghanistan.
Mkutano huo ulioudhuliwa na viongozi wa nchi 28, walikubaliana kwa misingi ya kuimarisha jeshi na polisi la nchi ya Afghanistan ili washike madaraka na kusimamia ulinzi wa nchi.
Akiongea mbele ya wajumbe, katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, alisema"Serikali ya Afghanistani ina endelea vizuri katika ulinzi wa nchi na hivyo kuna haja madaraka yote yawe chini ya uongozi wa serikali ya Afghanistan."
NATO inatarajia kuanza kupunguza majeshi yake nchini Afghanistan kuanzia mwaka 2011.
Vita vya Afghanistan vilinza kwa ajili ya kupambana na makundi ya ugaidi ya Taliban na Al-qaeda.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa nchi za NATO wakiwa katika mkutano kujadili mbinu mbada kuhusu Afghanistan.

Wednesday, April 21, 2010

Hatimaye mama asilia atoa ruhusa kwa ndege kuruka.

Hatimaye mama asilia atoa ruhusa kwa ndege kuruka.

Brussel,Ubeligiji - 21/04/2010. Ndege zimeanza kuruka tena angani baada ya kushindwa kuruka kutokana na mavumbi ya mlipuko wa volkano yaliyo tokea katika kisiwa cha Iceland kwenywe milima ya Eyjafllajoekull siku sita zilizo pita.
Kwamujibu wa habari kutoka kwa shirika la anga la Ulaya zinasema "bado kuna baadhi ya maeneo hali ya hewa hijawa safi kwa usafiri wa anga."
"Hata hivyo huenda safari za ndege zikaanza mapema mwisho wa wiki hii zilimalizia habari kutoka kwenye shirika hilo la anga la Ulaya".
Picha hapo juu inaonekana ndege ikielekea kutua kwenye kiwanja cha ndege cha Heathrow lilichopo Uingereza mapama hivi leo,baada ya siku sita za kushindwa kuruka angani kutokana na madhara yaliyo sababishwa na mama asilia.

Monday, April 12, 2010

Wapoland wakumbwa na msiba mkubwa

Warsaw, Poland 12/04/2010. Wananchi wa Polanda wamekumbwa na msiba mkubwa baada ya rais wa nchi hiyo na viongozi wengine wakuu wa idara mbalimbali walipo fariki kutokana na ajali ya ndege.
Rais Lech Kaczynski's na wajumbe wake walikuwa wakielekea Urusi, ambapo ndege iliyokuwa imewabeba kuanguka karibu na kiwanja cha ndege na kupoteza maisha ya watu wote waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Picha hapo juu ni ya hayati raia Lech Kacznski's, enzi za huai wak, mara baada ya kumaliza kuakagua gwaride rasmi.
Picha ya pili mi msururuwa magari ambamo moja ya gari hizo imebeba mwili wa marahemu rais wa Poland kuelekea Ikulu ya Poland.
Picha ya tatu wanaonekana awanajeshi wa Poland, wakiwa wamebeba mwili wa marehemu rais wa Poland, Lch Kaczynski' mara baada ya kuwasili nchini Poland.
Rais wa Amerika akutana na viongozi wa dunia.
Washington, Amerika 12/04/2010. Rais wa Amerika anakutana na viongozi tofauti kutoka mabara yote ya dunia katika mkutano utakao zungumzia ni njia gani zinatakiwa kuhakikisha ya kuwa siraha za nguvu za kinyuklia hazita angukia katika mikono ya Al-qaeda na wafuasi wake, kwani huenda wakazitumia katika mashambulizi.
Rais, Baraka Obama, amemefanya uamuzi huo kama ule uliofanywa na rais Franklin D Roosevelt ambaye aliwaita viongozi wa wa dunia wakati wamkutano wakutaka kuanzisha umoja wa Matifa mnamo mwaka 1945.
Akiongea rais wa Obama alisema "lazima jumuia ya kimataifa iakikishe kuwepo na usalama na ilinzi kuhakikisha siraha za nyuklia aziangukii katika mikono potofu"
Picha hpo juu wanaonekana rais Baraka Obama na waziri wa mambo ya nje wa Amerika, Hirally Clinton wakielekea kujiandaa kuwapokea viongozi wa dunia.

Thursday, April 8, 2010

Waingereza wajiaanda kuchagua waziri mkuu mpya.

Waingereza wajiandaa kuchagua waziri mkuu mpya . London, Uingereze 08/04/2010. Kampeni za uchaguzi nchini Uingereza zimeaanza rasmi, mara baada ya waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown,kutangaza rasmi ya kuwa siku ya uchaguzi mkuu utakuwa April 6 /2010. Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kisiasa. wanasema uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa ni wa kihistoria, kwa kuzingatia ya kuwa serikali iliyopo madaraka ni ya Gordon Brown, ina upinzani mkubwa sana kutoka kwa David Cameron ambaye anagombe kiti cha uwaziri mkuu kupitia chama cha Conservative. Picha hapo juu wanaonekana David Cameron kushoto na Gordon Brown kulia ambao wanagombe kiti cha uwaziri mkuu wa Uingereza katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu April 6/ 2010. Amerika na Urussi za tiliana sahihi mkataba wa kupunguza zana za kivita za kinyuklia. Prague,Cheksi - 08/04/1020. Marais wa Amerika na Urussi wametia sahii mkataba wa kupunguza uzalishaji wa nguvu za zana za kijeshi za kinyuklia. Maraias hao Baraka Obama na Dmitri Medvedev walisaini mkataba huo katika mji wa Prague uliopo Jamuhuri ya Cheksi. Akiongea mara baada ya kutia sahii, rais wa Amerika, Baraka Obama alisema " Amerika na Urussi haziwezi kufanyakazi ikiwa hazita shirikiana hasa katika maswala makubwa ambayo yana husu hali halisi ya dunia." Naye rais wa Urussi Dmitri Medvedev alisema , hii ni siku ya kukumbukwa kihistoria na itafungua ukurasa mpya na pande zote zitafaidika na mkataba huu." Picha hapo juu wanaonekana, ais wa Amerika Baraka Obama kushoto na rais wa Urussi, Dmitri Medvedev, wakisaini mkataba wa kupunguza nguvu za zana za kijeshi za nyuklia walipo kutana Prague.

Monday, April 5, 2010

Rais Raul Castro"Kuba haitatetereka kamwe."

Kiongozi wa mlango wa kulia nchini Afrika ya Kusini auwawa.

Ventersdorp, Afrika ya Kusini - 05/04/2010. Serikali ya Afrika ya Kusini imewataka wanchi wawe watulivu baada ya aliyekuwa kiongozi wa wa Wazungu wenye itikadi za mlango wa kulia kuuwawa na wafanyakazi wake baada ya mabishano kuhusu malipo ya kazi. Kwa mujibu wa mama wa mmoja wa watuhumiwa walio husika katika mauaji ya kiongozi huyo Eugene Terreblance, alisema "mwanae alimpiga chuma kiongozi huyo baada ya mabishano kuhusu malio ya kazi walioifanya tangu mwezi wa Desemba." Kufuatia tukio hilo wanancha na wapenzi wa Terreblance wamehaidi kulipa kisasi na pia wameitaka serikali kufuatilia na kuchunguza kwa makini chanzo cha kifao cha kiongozi wao. Eugen Terreblance, alikuwa mmoja wa viongozi ambao wakati wa utawala wa wazungu walio wachache nchini Afrika ya Kusini alikuwa anafanya kazi na serikali hiyo kwa ukaribu sana na hata kushukiwa kuhusika katika matukio makubwa ya kutishia amani ya wazalendo wa Afrika ya Kusini kwa ujumla. Picha hapo juu anaonekana Eugene Terreblance, enzi za uhai wake akiwa juu ya farasi kuzunguka mji ambao watu wengi watamkumbuka kwa mambo yake aliyo yafanya wakati wa uhai wake. Rais Raul Castro"Kuba haita tetereka kamwe."
Havana Kuba - 05/04/2010. Rais wa Kuba amesema ya kuwa serikali na wanchi wa Kuba hawata kubali kuyumbishwa wala kutetereka kwa njama za watu amabo wanaacha kula kwa sababu fulani. Rais Raul Castro, aliyasema haya wakati alipokuwa akiwahutubiwa wanachi wa Kuba siku ya Jumapili kwa kusema "nchi za Ulaya na Amerika zina jitahidi kwa kwakila njia kuleta matatizo ndani ya nchi," "Kuba" "kwa kuwawashawisha wapinzani wa serikali kufanya mambo yasiyo ya kawaida." Wakati huo huo mwandishi wa habari Guillermo Firinas amegoma kula kwa kudai wafungwa wa kisiasa waachiwe huru Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu, zinasema "Kuba inawafungwa wapatao 55 ambao wapo jela." Picha hapo juu anaonekana Guillermo Firinas, akipelekwa hospital ili kupata matibabu baada ya kugoma kula mpaka madi yake yatimizwe. Wananchi wa China wajawa na furaha kubwa. Shanxi, China - 05/04/2010. Watu wapata 110 wameokolewa kutaka ndania ya machimbo ( migodi) ambayo ilipasuka na kujaa maji kwa kipindi cha wiki moja iliyo pita. Watu hao walichukuliwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kuangaliwa afya zao zaidi. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Liu Dezheng alisema, " maajabu na ni kweli na imetokea kama tulivyo kuwa tunaamini na hatimaye tume fanikiwa kuwaokoa wenzetu" Viongozi na wanchi wa China wamewapongeza waokoaji wote kwa kazi nzuri waliyoifanya na nifuraha kubwa kwa wanchi wote wa China. Picha hapo juu wanaonekana wakiwa wamembeba mmoja ya wafanyakzai waliokuwa wamekwama ndani ya mgodi baada ya kumtoa ndani ya mgodi.