Thursday, September 29, 2011

Ujerumani yaingeza nguvu sarafu ya Euro.

Mahakama kuendelea kusikiliza kesi kuhusu kifo cha Michael Jackson.

Los Angeles, Marekani -29/09/2011. Mahakama katika jiji la Los Angeles, bado inaendelea kusikiliza kesi zidi ya mganga Conrad Murrey, ambaye anashutumiwa kwa kosa la kusababisha kifo cha nyota na bingwa wa musiki ya pop Michael Jackson.
Kesi hiyo ambayo imeanza hivi karibuni, baada ya uchunguzi kumalizika ili kujua nini kilimwua bingwa huo wa musiki
Hata hivyo muuguzi huo Conrad Murray amekana kosa hilo na kesi bado inaendelea kusikilizwa.
Ujerumani yaiongeza nguvu ya sarafu ya Euro.
Berlin, Ujerumani-29/09/2011.Bunge la Ujerumani limeidhini kwa kura mswada wa serikali ya nchi hiyo kuikomboa sarafu ya euro ambayo ilikuwa ipo mashakani kutoka na myumbo wa kiuchumi fedha uliyopo katika nchi wanachama wa jumuia ya Ulaya.
Matokeo ya kura 523 yaliyo unga mkono muswada huo, yalimpa uhai mkubwa Kansela Angela Merkel, kwani hapo mwanzo wa majadiliano ya muswada huo ilionekana ya kuwa itakuwa vigumu kupitishwa.
Kufuatia uamuzi huo wa Ujerumani kuilinda sarafu ya euro, masoko ya fedha katika bara la ulaya yalionekana kufanya vizuri kwa hisa kupanda.
Ujerumani imekuwa nchi pekee katika nchi wananchama wa jumuia ya Ulaya ambayo imekuwa inasimamia sarafu ya eoro kwa hali na mali.
Waganga na wauguzi wahukumiwa kwenda jela Bahrain.
Manama, Bahrain - 29/09/2011.Maganga na wauguzi ambao walishiriki kuwatibu watu walioumia wakati wa maandamano ya kupinga serikali wamehukumiwa vifungo vya miaka tofauti kati miaka 5 na 15 jela.
Waganga hao na wauguzi ambao walikuwa katika hospitali ya Sulmania, wanashutumiwa kuwa kwa kuwatishia walinzi wa usalama kwa kutumia siraha, visu na vifaa vingine vya kufanyia upasuaji.
Msemaji wa wizara ya habari ya Bahrain Sheikh Mubarak Abdulaziz Khalifa alisema "waganga hao na wauguzi walifanya kitendo cha kigaidi kwa kuwazuia walinzi wa usalama wasifanye kazi zao na kushiriki katika maandano kinyume na sheria."
Hata hivyo wauguzi hao walikana makosa hayo na kuomba shirikisho la wauguzi kuingilia dunia kuingilia jambo hili kwa kudai "nikinyume na sheria za uuguzi."
Mpinzani wa serikali ya Bahrain Matar Matar alisema " serikali ainatakiwa kutatua matatizo yaliyopo na hasa ya kisiasa kwani ndiyo chanzo cha kutoluwa na amani."

Tuesday, September 27, 2011

Serikali ya mpito ya Libya kutoendelea na kesi ya mtuhumiwa wa ajali ya ndege Pan Am 103.

Serikali ya mpito ya Libya kutoendelea na kesi ya mtuhumiwa wa ajali ya ndege Pan Am 103.

Tripol, Libya - 27//09/2011. Waziri wa sheria wa serikali ya mpito ya Libya ametangaza ya kuwa kesi zidi ya aliyekuwa mtuhumiwa katika kesi ya kulipuliwa ndege ya Pan Am 103 iliyo tokea Lockerbie haitaendelea na imefungwa.
Waziri Mohammed al-Alagi alisema " Abdel Basset al-Megrahi alisha hukumiwa na kuachiwa na koti kutokana na hali yake kwa makubaliano ya serikali za Skotilandi na Britishi, hivyo hawezi kushitakiwa marambili kutokana na kosa hilo."
Al Megrahi alikutwa na hatia ya kuhusika katika kulipua ndege ya Pan Am 103 liyokuwa imebeba watu 250 na kuhukumiwa mwaka 2001 kwa kosa la kusababisha vifo vya watu 260 kati yao 11 walikuwawa baada ya ndege kudondoka katika eneo walilo kuwepo.
Kuchiwa kwa Abdel Basset al-Megrahi kulileta mvutano mkubwa kati ya serikali za Uingereza, Marekani na ndugu wa raia walio uwawa katika ajali hiyo.
Iran na Sudan zazidi kudumisha uhusiano kwa ukaribu zaidi.
Khartoum, Sudan - 27/09/2011. Rais wa Iran yupo ziara nchini Sudan, ili kudumisha uhusiano uliyopo kati ya Iran na Sudan.
Katika ziara hiyo, rais wa Iran Mahamoud Ahmadinejad atatiliana sahii mikataba na serikali ya Sudani katika nyanja za uchumi, kukuza uhusiano wa kijeshi uliopo na wa kisiasa.
Iran ni moja ya nchi ambazo zinauhusiano wa karibu na serikali ya rais Omar Hassan al Bashir, ambapo serikali yake inapingwa na nchi za Ulaya Magharibi na Marekani kwa kuwekewa vikwazo vya kibiashara na kiuchumi.
Rais Al Bashir anaunga mkono sera ya Iran ya kuwa na mitambo ya kinyuklia, japo nchi za magahribi zinapinga kitendo hicho, kwa madai Iran inampango wa kutengeneza mabomu ya nyuklia.

Mshindi wa Nobel ya Laureate mama Wangari Mathai hatuko naye tena.

Mshindi wa Nobel ya Laureate mama Wangari Mathai hatuko naye tena.

Nairobi, Kenya 27/09/2011. Wananchi wa Kenya wamkutwa na msiba baada ya kuondokewa na aliyekuwa mtetezi na mwanzilishi wa kitengo cha kuboresha mazingira nchini humo kinacho julikana kama Green Belt Movement Bi Wangari Mathai.
Wangari Mathai ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kutunikiwa nishani ya Nobel Laureate, alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani katika hospital jijini Nairobi.
Msemaji wa familia ya Bi Mathai alisema " tumepata masikitiko makubwa na majonzi kwa kuondokewa na mama yetu mpendwa, ndugu yetu, na mpenda haki."
Bi Wangari Mathai atakumbukwa kwa kuongoza maandamano ya kupinga serikali ya Kenya kutaka kuongeza mawaziri na pia kuwa mfano bora kwa wanawake wote wa Afrika katika kupigania haki, pia na kuongoza katika nyazifa mbalimbali serikalini ikiwemo uwaziri.

Sunday, September 25, 2011

Rekodi ya mbio za marathoni za Berlin ya vunjwa.

Rekodi ya mbio za marathoni za Berlini ya vunjwa.

Berlin, Ujerumani 15/09/2011. Mwana riadha Patrick Makau amevunja rekodi ya dunia ya mbio za marathoni iliyokuwa ikishikiliwa na mwanariadha Haile Gabreselassie wa Ethiopia.
Patrick alivunja rekodi hiyo kwa muda wa masaa 2 dakika tatu na sekunde 38.
Mwanariadha huyo aliwaongoza katika kipindi cha kumalizia mbio na huku Wakenya wenzake walishikiria nafasi ya pili na ya tatu katika mbio hizo.
Akiongea baada ya mbio hizo Partick alisema " sikujua kama siku kama ya leo inaweza kuwa kama ilivyo tokea nichofanya nilikuwa nimekuja kushindana na kushinda."
Haile Gabrselassie ambaye naye alishiriki mashindano hayo kwa kukimbia hadi kufikia km 35 na kujitoa.
Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakiwika katika mbio na kuliletea taifa la Kenya sifa nyingi kila mwaka.
Dmitry Medvedev apendekeza Vladmir Puttin kugombea kiti cha urais wa Urusi.
Moscow, Urussi- 25/09/2011. Rais wa Urusi amemtangaza rasmi waziri mkuu wake Vladimir Puttin kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Dmitry Medvedev alisema " ninayo furaha kuwatangazia ya kuwa napendekeza waziri mkuu Vladimil Puttin kugombea kiti cha urais katika uchaguzi unaokuja na sina wasiwasi wowote wa kuwa na mashaka kwani naamini ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza nchi yetu."
Baada ya kutangazwa kwake kugombea kiti cha urais, Vladimir Puttin alisema " nipo tayari kuongoza Urussi kwa kusaidiana na wanzangu na Dmitry Medvedev atakuwa waziri mkuu kama tukishinda uchaguzi."
Huku wakishangiliwa na wanachama wa chama tawala cha United Russia walioudhuria katika mkutano mkuu wa chama hicho uliyo fanyika jijini Moscow, viongozi hao walionyesha ukaribu wa zaidi hata wakati walipokuwa wakiingia katika ukumbi wa mkutano.
Ufalme wa Saud Arabia watoa ruhusa kwa wanawake kupiga kura.
Riadh, Saudi Arabia - 25/09/2011. Mfalme wa Saud Arabia ametoa ruhusa kwa wanawake wote aliopo nchini Saudi Arabia kugombea nafasi za uongozi katika ngazi za manispaa na ruhusa ya kupiga kura.
Mfalme Abdullah bin Abdulaziz al Saud alisema " hatutaki kuwatenga wanawake kwani wao ni sehemu ya jamii baada ya makubaliano kufikiwa na kamati ya uongozi ya kifalme."
Kufuatia maelezo ya ya Mfalme, wanawake wote raia wa Saudi Arabia wataruhusiwa kikamilifu kushiriki katika uchaguzi wa manispaa utakao fanyika mwakani.
Inaaminika zaidi ya wanawake 5,000 huenda wakashiriki katika harakati za kupiga kura na kugombea uongozi katika manispaa 285 zilizopo nchini humo.

Friday, September 23, 2011

Wapalestina wakabidhi ombi la kutaka kutambulika kama taifa kwa Ban Ki-moon.

Wapalestina wakabidhi ombi lao la kutaka kutambulika kama taifa kwa Ban Ki-moon.

New York, Marekani - 23/09/2011. Rais wa Wapalestina amehutubia mkuutano mkuu wa umoja wa mataifa na kudai Palestina itambulike kama nchi huru pia kukabidhi maombi hayo kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Mahmoud Abbas akihutubia alisema " tunaweza kaa na kuzungumza na Izrael kwa kufuatia mkataba wa makubaliano ya mpaka mwaka 1967,na kusimamisha ujenzi wote unaoendelea katika maeneo ya Wapalestina, kwani mazungumzo ya hapo awali yalikwama kutokana na Izrael kutokuwa na nia ya kufanya mazungumzo mwaka jana Septemba."
Rais huyo wa Wapalestina alimaliza hotuba yake hiyo kwa kushangiliwa na viongozi wakuu wa nchini na wajumbe wote waliokuwemo ndani ya jumba la mkutano.
Hata hivyo waziri mkuu wa Izrael Binyamin Netanyahu ambaye naye alihutubia katika mkutano huo alisema " siwezi kuleta amani peke yangu, nasiwezi bila wewe Abbas, kwani sisi wote ni watoto wa Abraham."
"Inabidi Waizrael wafanye uamuzi busara kwa kukubali ya matakwa ya Wapalestina na vilevile Wapalestina lazima wafanye uamuzi busara kwa kukubaliana na matakwa ya Waizrael." aliongezea Netanyahu.
Hata hivyo ombi la Waplestina litachukuwa muda kabla ya kufikiwa muafaka wake na kikao cha kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
Rais wa Iran azilaumu nchi za Magharibi.
New York, Marekani - 23/09/2011. Rais wa Iran amezilaumu nchi za magharibi kwa kutumia uwezo walionao kuvuruga amani na kusababisha myumbo wa uchumi duniani.
Mahmoud Ahmadinejad akihutubia katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa alisema " nguvu za kijeshi zimekuwa zikitumika na mataifa ya magharibi pasivyo halali"
Pia mashabulizi ya Sept 11 ni ya kimiujiza, ingefaa Osama bin Laden akamatwe ili afikishwe kwenye sheria na tungejua ukweli, kwani kitendo cha kumwua hakikuwa na mantiki yoyote " alisisitiza rais Ahmedinejad.
Hata hivyo wakati akihutubia, viongozi wa nchi za magharibi walitoka nje ya jumba la mkutano baada ya rais huyo wa Iran kuanza kuzishambulia nchi hizo na hasa nchi ya Izrael.
Zambia yapata rais wa tano tangu kupata uhuru.
Lusaka, Zambia -23/09/2011. Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambia ameshinda kiti cha urais kwa kumpita mpinzani wake wa chama tawala cha MMD- Movement for Mult-party democracy.
Michael Sata ambaye aligombea kiti cha urais kupitia chama cha Patriotic Front alishinda kwa kupata asilimia 43 za kura zidi ya mpinzani wake Rupia Banda.
Akihutubia baada ya matokeo ya uchaguzi, rais mpya wa Zambi Michael Sata alisema " wananchi wa Zambia wamesema na lazima tuwasikilize na huu ni wakati wa kuwa pamoja katika kuijenga nchi, kwani sisi vizazi vya zamani lazima tuwape mwelekeo mzuri wa kujenga nchi hawa vijana wa vizazi vipya."
"Na haidi kiweka Zambia kwanza na kupambana na rushwa" alisema rais mpya wa Zambia Michael Sata.
Rais Michael Sata ni rais wa tano tangu Zambia kupata uhuru mwaka 1964

Thursday, September 22, 2011

Mauaji ya kutisha yatokea Burundi.

Mauaji ya kutisha yatoke Burundi.
Bujumbura, Burundi - 22/09/2011.Kamishna mwenyekiti wa umoja wa Afrika amelaani matukio ya mauaji ya watu 40 yaliyo tokea hivi karibuni nchini Burundi.
Dr Jean Ping alisema " kitendo kilicho fanyika ni cha kinyama na umoja wa Afrika utaendelea katika jitihada za kuunga mkono kuwepo kwa amani nchini Burundi."
Mauaji hayo ambayo yametokea maeneo ya Gatumba, yameleta mshituko mkubwa kwa wanchi wa Burundi, na kutaka serikali ifanye kila njia kuwakamata wale wote walio husika, ilikuweza kuurudisha imani kwa wanachi.
Wanawake wawili wahukumiwa kwa kuvaa baibui nchini Ufaransa.
Paris
Ufaransa - 22/09/2011. Mahakama jijini Paris imewatoza faini wanawake wawili kwa kosa la kuvaa baibui zinazo funika hadi uso.
Wanawake hao walitozwa jumla ya euro 200 na mahakama hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria inayo zuia mavazi hayo.
Hata hivyo faini hiyo ililipwa na mfanya biashara mmoja na kusema " nadhani uhuru wa mtu ni muhimu sana, na sikubaliani na sheria iliyo wekwa kwani inakwenda kinyume na katiba ya Ulaya, nna wanawake lazima wawe huru hata wanapo tembea."
Faini hiyo imekuwa ya kwanza tangu kupitishwa kwa sheria ya kukutaza mavazi ya baibui inayo funika hadi usi, jambo baadhi ya wananchi wa Ufaransa wanapingana lao.

Waizrael na Wapalestina watakiwa kukubalina ili kufikia muafaka wa amani

Waizrael na Wapalestina watakiwa kukubaliana ili kufikia muafaka wa amani.
New York
, Marekani - 21/09/2011. Rais wa Marekani amelihutubia balaza la umoja wa mataifa ya kuwa mgogoro kati ya Waizrael na Wapalestina utamalizwa kwa makubaliano yao wenyewe.
Baraka Obama alisema " Mgogoro uliyopo kati ya Waizrael na Wapalestina hunahitaji makubaliano ya pande zote mbili, hivyo lazima yawepo mazungumzo ili kuleta amani"
" Na uhusiano wa Amerika na Izrael hautatikishwa kamwe na haswa katika swala la ulinzi na usalama wa Izrael." Aliongezea Obama.
" Wapalestina wanatakiwa kuwa na taifa lao, na ndiyo maana Marekani imekuwa itoa misaada ya kuwasaidia Wapalestina ili kujenga taifa lao."
Hotuba ya rais Obama, imetangulia kabla ya rais wa Wapalestina Mohmoud Abbas ajatangaza ombi la wa Wapalestina kutaka kuwa wanachama wa Umoja wa Mataifa na kutambulika kama taifa hapo siku ya Ijumaa wiki hii.
Hata hivyo serikali ya Marekani imesema " itapinga kitendo cha Wapalestina kutaka kuwa taifa ikiwa ombi ilo litawakilishwa kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa."
Mgogoro wa Waizrael na Wapalestina umekuwa wa muda mrefu na wakuleta vichwa kuumu kwa jumiya ya kimataifa.

Saturday, September 17, 2011

Mahaka ya kutete haki za binadamu yaombwa kuwashitaki viongozi wa Kanisa.

Mahakama ya kutete haki za binadamu yaombwa kuwashitaki viongozi wa Kanisa
. Chikago, Marekani - 17/09/2011. Kundi la kimataifa linaloshughulikia haki za wale wote aliotendewa maovu na kanisa Katoliki, limetaka kesi ifunguliwa zidi ya viongozi wa kanisa hilo. Kundi hilo limepeleka malalamiko yake kwenye mahakam ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kwa msaada wa wanasheria wa kujitokea na kudai ya kuwa vitendo vilivyo fanywa watumishi wa kanisa Katoliki vinatakiwa kufuatiliwa kisheria na viongozi walio husika na kuficha siri lazima wafikishwe mahakamani kujibu mashitaka. Hata hivyo wanasheria wa kimataifa wana sema "itakuwa vigumu kwa mahakama hiyo kufuatilia kesi hiyo kutokana na baadhi ya vifungu vya sheria vilivyopo kuhusu uhalali wa kuendesha kesi hiyo." Papa Benedekt alisha zungumzia hali hiyo na kusema "nikitendo cha aibu kilicho fanywa na watumishi wa Kanisa la Katoliki na kuhaidi yakuwa atalishughulikia kwa undani zaidi."
Kanisa Katoliki limekuwa na wakati mgumu katika miaka ya hivi karibuni,baada ya kugundulika ya kuwa baadhi ya watumishi walikuwa wanashiriki katika vitendo vya kulawiti.
Serikali ya mpito ya Libya yakubaliwa Umoja wa mataifa. New York ,Marekani - 17/07/2011.Umoja wa mataifa umepitisha muswada wa kuikubali serikali ya mpito ya Libya kama mwakilishi wa nchi hiyo. Kukubalika huko kwa serikali ya mpito ya Libya kumekuja baada ya viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Uturuki kufanya ziara za kiserikali nchini Libya kwa mara ya kwanza, tangu kuangushwa kwa serikali ya Muammar Gaddafi hivi karibuni. Mwakilishi wa Urusi katika umoja wa mataifa alisema " niwajibu wa jumuiya ya kimataifa kwa kushirikiana na umoja wa mataifa kuisaidia Libya ili kujenga miundo mbinu ya kisiasa ili kuweza kukuza demokrasia na kuleta amani nchini humo." Hata hivyo vikwazo vya anga bado vitaangaliwa kwa makini, japo kuwa Urusi inataka vikwazo hivyo viondolewe haraka iwekezekanavyo ili kurahisisha maendeleo ya ujenzi wa Libya. Wapalestina kudai utaifa wao New York. Lamalla, Marekani - 17.09.2011.Mamia ya Wapalestina wameandamana karibu miji yote iliyopo Palestina kuunga mkono uamuzi wa serikali kwenda Umoja wa Mataifa kudai haki ya Utaifa wa Wapalestina. Rais wa baraza la Wapalestina aliwa wahakikishia Wapalestina ya kuwa atafanya kila linalo takiwa ili kuliomba baraza la Umoja wa Mataifa kuunga mkono kwa Wapalestina kukubalika kuunda taifa huru la Kipalestina. Akikisisitiza hoja hiyo, rais Mohmoud Abbas alisema " kuna nchi zaidi ya 120 zimekubali kuunga mkono ombi letu, kufuatia hotuba ya rais Baraka Obama, aliyoitoa mwaka 2010 kwenye mkutano mkuu wa umoja wa mataifa ya kuwa mwaka 2011 tutakuwa wanachama kamili wa umoja wa mataifa." Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alikubaliana na hoja ya Wapalestina kwa kusema " swala la Wapalestina linaeleweka na makubaliano ndiyo njia nzuri ya kuleta amani." Rais Mohmoud Abbas anatarajiwa kuwakilisha ombi lake hilo, baada ya hotuba ya tarehe 23. Septemba mwaka huu katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa.

Monday, September 12, 2011

Watanzania waanza maombelezi baada ya ajali ya boti.

Bomba la mafuta la lipuka nchini Kenya na kuleta maafa makubwa.
Nairobi, Kenya - 12/09/2011.Watu 63 wamepoteza maisha yao na wengine zaidi ya 110 kijeruhiwa vibaya baada bomba la mafuta kupasuka na kuanza kuvuja na baadaye kuwaka moto katika eneo la viwanda la Lunga Lunga.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "inaminika moto huo umetokea baada ya kipande cha sigara kudondoka katika moja ya tundu kikilopo kwenye bomba hilo."
Msemaji wa polisi Erick Kiraithe alisema " huenda vifo vikaongezeka kutokana ajali hiyo."
Bomba hilo ambalo limepita katika maeneo anayo kaliwa na watu , lili kuwa lina vuja na kuwafanya wakazi wa maeneo hayo kwenda kukinga mafuta, jambo ambao limesababisha watu wengi kujeruhiwa na wengine kupoteza maisha baada ya mafuta hayo kushika moto na kulipuka.
Watanzania waanza maombolezi baada ya ajali ya boti Unguja.
Unguja, Zanzibar -12/09/2011. Wananchi wa kisiwa cha Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wamenza maombelezi kwa muda wa siku tatu baada ya ajali ya boti iliyo kuwa imebeba abiria kuelekea Pemba kuzama na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Boti hiyo ambayo ilikuwa imebeba watu wapatao 800 na mizigo kwa kiasi kingi, ilizama kilomita chache baada ya kutoka bandari ya Unguja.
Kwa mujibu wa habari zina sema "boti hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 600, lakini ilikuwa imelizidisha watu pamoja na mizigo kabla ya kuondoka na kufanya baadhi ya abiria kuamua kushuka kutokana na wingi wa watu.
Mmoja wa abiria waliokuwemo kwenye boti hiyo Yahya Hussein alisema " nilihisi kuna matatizo baada ya kuanza kuona meli inakwenda alijojo na mwendo wa kuyumba na nikaona bora niliruke wakati meli inaanza kuzama na shukuru ubao nilioshikilia ndoyo uliyo niokoa nisizame."
Nayo serikali ya Tanzania imeunda tume ya uchunguzi kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na vile vile kutoa misaada ya kifedha na mali ili kuwafariji waliopotelewa na ndugu na jamaa zao kutokana na ajali hiyo.
Baraka Obama na George Bush waudhuria siku ya kumbukumbu ya Sept/11.
, Marekani - 12/09/2011. Rais Baraka Omaba wa Marekani amewaongoza wananchi katika maombelezi ya kuadhimisha miaka 10 tangu kufanywa kwa mashambulizi ya kigaidi jijini New York.
Baraka Obama alisema "hakuna kitu kitautikisa au kubomboa umoja wa Wamarekani na daima tutakuwa pamoja."
"Na tutapambana na ugaidi hadi tuutokomeze, na tutazidi kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao katika kulitetea taifa letu na kuenzi yote waliotufanyia.
Sherehe za kumbukumbu za kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na mashambulizi yaliyofanywa kwenye majengo ya marefu yaliyo kuwa katikati ya jiji la New York ambapo zaidi ya watu 2900 waliuwawa na magaidi kwa kushirikiana na kundi la Al Qaeda na kuharibu malizingira ya jiji hilo, ziliudhuriwa pia na aliyekuwa rais wakati wa mashambulizi hayo George Bush na viongozi wengine wa serikali.

Thursday, September 8, 2011

ZANU-PF yakansha madi ya kuwa Robert Mugabe anasatani.

ZANU-PF yakanusha madai ya kuwa rais Robert Mugabe anasatani.
Harare, Zimbabwe - 08/09/2011.Msemaji wa chama tawala ZANU-PF nchini Zimbabwe amekanusha habari za uvumi ya kuwa rais wa nchi hiyo anasaratani ya muda mrefu.
Habari kutoka kwenye chama hicho zinasema " habari zilizo tolewa na Wikileaks ya kuwa gavana wa benki kuu ya Zimbabwe aliongea faragha na balozi wa Marekani Christopher Dell mwaka 2006 ya kuwa rais Robert Mugabe anasumbuliwa na saratani ambayo imesambaa karibu mwili mzima siyo kweli."
"Kama ilikuwa mwaka 2006 ndiyo walifanya mazungumzo hayo mbona mpaka leo yupo mzima na hakuna hata siku alionekana yupo dhaifu." habari kutoka ZANU-PF zilisema.
Ukanushi wa habari hizo , umekuja baada ya mtandao wa Wikileaks kutoa habari ya kuwa rais Robert Mugabe anasadikiwa kuwa na ugonjwa wa saratani.
Kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya awasili nchini kwa mara ya kwanza.
Libya, Libya - 08/09/2011. Kiongozi wa serikali ya mpito iliyo leta mapinduzi ya kijeshi nchini Libya amewasili nchini Libya kwa mara ya kwanza tangu kuanza mapinduzi hayo.
Mohmoud Jibril aliwasili nchini Libya ili kuangalia maendeleo na kuzungumza na wapiganaji waliongoza katika kuing`oa serikali ya Muammar Gaddafi.
Katika mikutano tofauti aliyo udhulia na kuhutubia, Mohmoud Jibril alisema "kazi ya kuikomboa Libya bado na haitakuwa vizuri tukiaanza kulumbana kisiasa, kwani mbele yetu bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuijenga upya Libya."
Wakati huo huo, wapiganaji wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi walifanya mashambuli zidi ya jeshi la wapinzani karibu na maeneo wanayo shikilia, baada ya kiongozi huo kutangaza yakuwa yupo nchini Libya na akatoa wito waendelee kupambana na wapinzani.
Vita kati ya wapiganaji wa serikali ya mpito na wale wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi yamekuwa yakiiendelea kwa muda wa miezi sita tangu harakati za mapinduzi kuanza nchini humo.

Monday, September 5, 2011

Njaa yazidi kutishia maisha ya Wasomalia.

Izrael yakataa kuomba msamaha kwa Uturuki.
Tel Aviv, Izrael - 05/09/2011. Waziri mkuu wa Izrael imekataa kuomba msamaha kwa serikali ya Uturuki
Binyamin Netanyahu alisema " hatuna haja ya kuomba msamaha, ingawaje tunasikitika kitendo cha watu kupoteza maisha, kwani jeshi letu lilibidi lijilinde kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na watu waliokuwemo kwenye meli hiyo, natumaini tukaweza kumaliza swala hili kimsingi, kwani Izrael haijawahi kutaka kukosana na Uturuki."
Maelezo hayo wa waziri mkuu wa Izrael yamefuatia ripoti iliyo tolewa na umoja wa mataifa kuhusu chanzo cha vurugu zilizo tokea kwenye meli iliyo kuwa imewabeba wana harakati wanao unga mkono Wapalestina, baada ya jeshi la Izrael kuivamia meli hiyo wakati ikielekea Gaza mwaka 2010 Mei.
Kutokana na tukio hilo serikali za Uturuki na Izrael zimefunga uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo.
Wapinaji wa NTC nchini Libya wangoja amri baada ya mazungumzo kushindikana.
Bani Walid,Libya -05/05/2011. Mazungumzo kati ya jeshi linalo muunga mkono Muammar Gaddafi na jeshi serikali ya mpito yamekwama baada ya kutofikia makubaliano.
Mazungumzo hayo ambayo yalikwama baada ya wapiganaji wanao muunga mkono Muammar Gaddafi kukataa kusalimu amri.
Mkuu wa majadiliano wa serikali ya mmpito Abdallah Kanshil alisema " tumeshindwa kufukia makubaliano na sasa uamuzi tume waachia viongozi wetu waamue la kufanya."
Kuvunjika kwa mazungumzo hayo huenda kufanya jeshi la serikali ya mmpito lilipo km 10 kuanza mashambulizi katika mji wa Bani Walid, jambo ambalo linashukiwa litaketa maafa makubwa.
Kesi zidi ya Jacques Chirac kuendelea.
Paris, Ufaransa - 05/09/2011. Mahakama nchi Ufaransa imeamuru kesi zidi ya rais Jacques Chirac iendelee ijapokuwa hatakuwepo mahakamani kutokana na matatizo ya kiafya.
Chirac 78 anakabilwa na kesi ya kutumia pesa za umma vibaya wakati akiwa meya wa jiji la Paris.
Jaji Dominique Pauthe alitoa amri hiyo kwa kusema " hakuna haja ya kuwepo kwa mshitakiwa na kesi inaweza kuendelea."
Jacques Chirac wakati wa utawala wake alipinga kitendo cha kuvamiwa kwa nchi ya Irak na kama akikutwa na hatia anaweza kufungwa kifungo cha hadi miaka 10 na faini ya euro 150,000.
Njaa yazidi kutishia maisha ya Wasomalia.
Mogadishu, Somalia -05/09/2011. Mamia ya wananchi wa Somalia wamepoteza maisha kutokana na njaa na ukame uliyoikumba nchi hiyo.
Habari kutoka shirika la umoja wa mataifa linalo shughulikia lishe kwa ajili ya Somali zinasema " robotatu ya nchi ya Somalia imekumbwa na ukame na kusababisha njaa ambao imepelekea watu zaidi kupoteza maisha wengi wao wakiwa watoto wadogo."
Kufuatia hali hiyo, kitengo cha kutathmini hali ya lishe nchini Somalia kimeomba mashirika ya kimataifa kutoa mchango wao, au huenda zaidi ya watu 400,000 wakapoteza maisha kwa kipindi cha miezi michache kutoka sasa.
Somalia ni nchi moja wapo ya zile nchi zilizo kumbwa na ukame katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.
Kesi zidi ya mpinzani wa serikali ya Rwanda kuendelea.
Kigali Rwanda -05/09/2011. Jaji wa mahakama nchini Rwanda ameamuru kesi zidi ya kiongozi wa upinzani Victoire Ingabire iendelee.
Jaji Alice Rilisa aliamuru kesi iendelee, baada ya mwanasheria kwa upande wa mshitakiwa kupinga ombi la upande wa mwanasheria wa serikali la kutaka kuongezewa muda ili kukusanya ushahidi zaidi.
Iain Edward wakili wa upande wa mshitakiwa aliomba mahakama kuruhusu kuendelea kwa kesi kwa kusema " mwendesha mashitaka wa serikali alisema wapo tayari kuuendelea na kesi na wanaushahidi wa kutosha tayari kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo inakuwaje wanataka waongezewe muda zaidi?"
Victoire Ingabire ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani nchini Rwanda cha Unified Democratic Force anashitakiwa kwa kwa kueneza chuki za kikabila, kukana kutokea mauaji ya kimbari nchini humo na kula njama za kutaka kununua siraha kwa ajili ya kutaka kuleta machafuko nchini Rwanda, na kama akikutwa na hatia huenda akafungwa kifungo cha maisha.

Sunday, September 4, 2011

Wanariadha wa Kenya hawana mpinzani duniani.

Muammar Gaddafi alishirikiana CIA na MI6.
Tripol, Libya - 04/09/2011.Jumuiya ya kutete haki za binadamu zimeilaumu serikali ya Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na serikali ya Muammar Gaddafi wakati alipo kuwa madarakani.
Habari zilipo patikana zinasema "serikali ya Muammar Gaddafi ilikuwa ikishirikiana na makachelo wa CIA na MI6 na hata kuweza kutoa habari za wapinzani wa Gaddafi ambao walikuwa wanashukiwa ni magaidi, jambo ambalo lilifanya Walibya waliokuwa wamekimbia utawala wa Muammara Gaddafi kurudishwa nchini humo kwa mahojiano ili kuweza kujua kama ni magaidi au wanashirikiana na Al Qaeda."
Makaratasi zenye ripoti hizo yalikutwa kwenye ofisi inayo sadikiwa ilikuwa ya aliyekuwa mkuu wa usalama Moussa Koussa, ambaye kwa sasa anaishi nchini Katar baada ya kutoraka kwa kupitia Uingereza.
Muammar Gaddafi alikuwa mmoja wa viongozi walioshirikiana na Uingereza na Marekani katika kupambana na ugaidi na hasa kundi la Al Qaeda tangu vita rasmi vilipo tangazwa zidi ya ugaidi duniani baada ya mashambulizi ya 11/Sept 2001.
Angola ya kumbwa na vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa.
Luanda, Angola -04/09/2011. Watu zaidi ya 23 wamekamatwa jijini Luanda baada ya kufanya maandamano ya kutaka rais Jose Eduardo dos Santos ajiudhulu.
Maandamano hayo yalianzia kwenye viwanja vya uhuru ili kuelekea kwenye ofisi za rais, kwa kuwa na lengo la kudai rais Jose Eduardo dos Santos aachie madarakani na watu walio kamatwa na kuwekwa kizuizini waachiwe huru.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka shirika la habari la Ureno Lusa zinasema " kuna baadhi ya watu wameumia vibaya wakiwemo waandishi wa habari, baada ya polisi na mafisa usalama kutumia nguvu katika kuzuia maandamano hayo."
Maandamano hayo yanakuja baada ya wanchi na viongozi wa upinzani nchini humo kudai ya kuwa "serikali ya Angola imekuwa haifanyi jitihada za kupambana na rushwa."
Angola inawananchi wapatao 16 milllion ambao wengi wao wanaisha chini ya dola 2 kwa siku.
Wanariadha wa Kenya hawana mpinzani duniani.
Daegu, Korea ya Kusini - 04/09/2011. Timu ya wanariadha wa Kenya wameweza tena kwa mara nyingine kuwanyanyu wananchi wa Afrika ya Mashariki na kuipatia sifa kubwa Kenya kwa kuweza kushinda medali za dhahabu kwa wingi kwenye mashindano ya riadha ya dunia nchini Korea.
Wanariadha hao wa Kenya wameweza kunyakua medali saba, na kukamlisha idadi ya medali kumi na sita katika mashindando hayo ambayo yanaisha wiki hii.
Vivian Cheruiyot ambaye ni mmoja ya washindi wa medali zilozo ipa sifa Kenya na Afrika ya Mashariki alisema " ushindi wetu unatokana na ushirikiano mkubwa tulionao wanariadha wa Kenya."
Wanariadha wa Kenya wamekuwa wanashinda mashindano mengi ya kimataifa na kuipatia Kenya sifa kila mwaka wanapo shiriki mashindano ya riadha popote duniani.
Dominique Strauss-Kahn arudi nyumbani akiwa huru.
Paris, Ufaransa - 04/08/2011. Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha (IFM) duniani
amewasili nchini Ufaransa baada ya kesi ya ubakaji zidi yake kufutwa hivi karibuni.
Dominique Strauss Kahn, aliwasili jijini Paris na kupokelewa na baadhi ya watu waliokuja kumlaki na hakuweza kuongea na waandishi wa habari.
Hata hivyo Strauss Kahn anakabiliwa na kesi nyingine iliyo funguliwa zidi yake na na mwandishi mmoja kwa madai "alitaka kumbaka miaka ya nyuma."
Kwa mujibu wa wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa wa Ufaransa wanasema "kesi hizi zimemwalibia kwa kiasi kikubwa Dominique Strauss Kahn katika kampeni yake ya kutaka gombea urais nchini Ufaransa na itabidi atumie busara ili kuweza kurudisha matumaini yake ya kutaka ugombea urais."
Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa unatarajiwa kufanyika hapo mwakani.
Muuguzi akanusha uvumi kuhusu Muammar Muammar Gaddafi.
Mogolnoye
,Ukraine -04/09/11. Mmoja wa wauguzi wa Muammara Gaddafi amekanusha madai yaliyokuwa yameenea ya kuwa kiongozi huyo Libya alikuwa na uhuusiano wa kimapenzi na baadhi ya wauguzi na walinzi wake wa kike.
Oksana Balinskaya muuguzi aliyekuwa wa Muammar Gaddafi alisema " nashangaa kusikia uvumi huo, kwani hakuna hata siku moja kati yetu alikuwa anamtibu (Dady) Muammar Gaddafi peke yake, muda wote tulikuwa tumezungukwa na watu, kama si walinzi basi watu wa falimia yake."
"Tulikuwa tuna mwita dady, kwani alivyo kuwa na ukarimu, muda wote alituuliza kama tuna shida au tunataka kitu tuseme, hivyo siwezi kusema vibaya juu yake, bila yeye nisingeweza kua hapa nilipo kimaisha nitasikitika kama akiuwawa au kukamatwa."
Oksana Balinskaya ni mmoja ya wauguzi ambao walikuwa nchini Libya ili kufanya kazi ya uuguzi wakati wa utawala wa Muammar Gaddafi ambaye ameng'olewa madarakani hivi karibinu.

Friday, September 2, 2011

Umoja wa Ulaya kuibana zaidi serikali ya Syria.

Polisi wazuia maandamano ya kimageuzi nchini Uganda.

Kampala, Uganda-02/09/2011. Serikali ya Uganda imepiga marufuko maandamano yaliyo kuwa yamepangwa ili kuungamkono mageuzi ya kisiasa yanayo endelea katika bara la Waarabu.
Uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya habari kupatikana ya kuwa "uenda maandamano hayo yakaleta chuki kati ya jamii na kuwa mwazo wa mvurugo wa amani ndani ya nchi."
Hata hivyo msemaji wa polisi Vicent Sekate alisema " maandamano hayo yamezuiliwa kutokana na kukusa sehemu ya kuyafanyia."
Hivi karibuni rais Yoweri Museni alisema " mgeuzi yanayo tokea Kaskazini mwa Afrika yanaweza leta athari kubwa kwa bara la Afrika na kusababisha mvutano wa madaraka na kijeshi."
Serikali ya Uganda imekuwa na wakati mgumu kisiasa kutokana na joto lililomo nchini humo la kutaka serikali ya rais Yoweri Museni kufanya mabadiliko ya kiuchumi.
Umoja wa Ulaya kuibana zaidi serikali ya Syria.
Brussels, Ubeligiji -02/09/2011. Umoja wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya zimeamua kwa pamoja kuiwekea vikwazo serikali ya Syria kutokana na kukiuka haki za binadamu.
Uamuzi huo umekubalika na viongozi wa jumuia ya Ulaya ili kuibana serikali ya Syria chini ya rais Bashar al-Assad ambayop inapambana na wapinzani wanaotaka mageuzi ya kisiasa nchi humo.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alisema " tunatakiwa kuiwekea vikwazo serikali ya Syria kwani vitendo vinavyo fanywa na serikali hiyo havikubaliki."
Vikwazo hivyo ambavyo ni kuzuia ununuzi na uuzwaji wa mafuta ya Syria na kuongeza vikwazo vya usafiri kwa wale wote wanaohusika katika serikalia ya rais Assad vimesha tayarishwa na vinasubiri kujadiliwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hizo na baadaye kupitishwa.
Machafuko nchini Syria yamezidi kuongezeka, kufuatia mageuzi ya kisiasa yaliyo likumba bara la Waarabu hivi karibu.
Uturuki yapunguza uhusiano na Izrael.
Ankara, Uturuki -02/09/2011. Serikali ya Uturuki imeamua kupunguza uhusiano uliopo kati yake na serikali ya Izrael.
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu aliyaongea hayo muda mfupi kabla ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon kukabidhiwa ripoti kuhusu tukio la jeshi la Izrael na wanaharakati waliokuwa wanelekea maeneo ya Gaza ili kupeleka misaada ya kiutu.
Serikali ya Uturuki imekuwa ikiitaka serikali ya Izrael kuomba msamaha baada ya raia wa Uturuki kuuwawa katika boti zilizokuwa zunaelekea Gaza hapo siku za nyuma.
Pia Uturuki imefunga ofisi zake za kibalozi nchini Izrael na kumtaka balozi wa Izrael nchini humo aondoke mara moja na kusimamisha ushirikiano wa kijeshi uliopo kati ya nchi hizi mbili.
Mvutano kati ya serikali ya Uturuki na Izrael ulizidi kuwa wa wasiwasi baada ya jeshi la Izraeli kufanya mashambulizi kwenye maeno ya Gaza miaka miwili iliyo pita na watu wengi kupoteza maisha na malinyingi kuharibiwa.

Thursday, September 1, 2011

Kenya hawatakuwa wanavaa nywele za bandia kwenye mahakama.

Kesi zidi ya machafuko ya Kenya yaanzwa kusikilizwa.
Hague, Uhollanzi -01/09/2011.Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi ya ukiukwaji wa haki za biadamu imeanza kusikiliza kesi zidi ya viongozi wanaoshutumiwa kuhusika na mauaji na machafuko yaliyo tokea nchini Kenya mwaka 2007 baada ya uchaguzi.
Washitakiwa hao ni waziri wa elimu William Ruto na ambaye alikuwa natarajiwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini Kenya.
Katika kesi hiyo " jaji wa mahakama hiyo alisema kesi hizo zidi ya washukiwa hao ipo kwa kusikilizwa na kuwapa nafasi washutumiwa kujitetea."
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa washitakiwa wanasema" hatuna wasiwasi na ukweli utaonekana kama hatna makosa."
Kesi zidi ya Ruto na wenzake inatarajiwa kuchukua muda kabla ya hukumu kutolewa.
Kenya hawatakuwa wanavaa nywele za bandia kwenye mahakama.
Nairobi, Kenya 01/09/2011. Majaji nchini Kenya hawatakuwa wanatumia maneno ya "my lord or my lady" katika mahakama nchini huma, baada ya madiliko kufanywa katika wizara ya sheria hivi karibuni.
Jaji mkuu Willy Mutunga alisema " kuanzia sasa majaji watakuwa wanatumia maneno ya Muheshimiwa or your honour na hii ndi itakuwa lugha ya mawasiliano kati ya wana sheria na mahakama na hawataruhusiwa kuvaa nywele nyeupe za bandia kichwani na vilevile kutakuwa na vazi rasmi la kuvaa wakati wa kuendesha kesi kotini."
Uamuzi huo umekuja baada ya majaji na wanasheria kutaka mabadiliko ya kisheria na mazingira ya koti yabadilishwe.
Ugonjwa wa mafua ya ndege na kuku kutishia afya za watu tena.
Geneva, Uswisi - 01/09/2011. Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya kilomo na chakula (FAO) limeonya kuenea kwa ugonjwa wa mafua ya ndege na kuku.
Habari zinasema "ugonjwa wa mafua ya ndege na kuku (H5N1 unaelekea kusambaa nchini China na Vietnam na huenda ukafika Kambodia na nchi zilizopo kwenye ukanda wa Peninsula.
Ugojwa wa mafua ya kuku na ndege ni ugonjwa ambao una madhara katika jamii na umesha poteza maisha ya watu karibu kila sehemu duniani.
Sarkozy na Cameron wasimia mkutano wa Libya nchini Ufaransa.
Paris. Ufaransa - 01/09/2011. Mataifa sitini yanakutana nchini Ufaransa ili kujadili ujenzi na mipango ya kuijenga upya nchi ya Libya ambayo uchumi wake umeharibika kutokana na vita katika harakati za kung'oa madarakani Muammar Gaddafi.
Mkutano huo ambao umeitishwa na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, unatarajiwa kuitambua rasmi serikali ya mpito na kujadili njia ya kuwasaidia wa Libya ili kuinua uchumi wao.
Mustafa Abdel Jalil mwenyekiti wa serikali ya mpito alisema " tutaweka wazi muswada wetu wa kuunda katiba mpya na kujiandaa na uchaguzi baada ya miezi 18."
Habari kutoka kwenye mkutano huo zinasema " mkutano huo utakuwa wa hali ya juu, kwani nchi ambazo zilisaidia katika harakati za kumng'oa Muammar Gaddafi madarakani zitakuwa na wakati mgumu katika kujaribu kuweka masrahi yao mbele, hasa baada ya serikali ya mpito kusema zile nchi zilizo saidia katika mapinduzi zitapata malipo bora."
Mkutano huo wa Paris unafanyika wakati Muammar Gaddafi ametangaza tene kupitia TV na radio za nchini Syria ya kuwa atapambana hadi kufa na kuwataka wale wanao muunga mkono kupigana hadi mwisho.