Tuesday, January 31, 2012

Marekani yadai utawala wa rais Bashar al Assad wa Sryia utaanguka muda si mrefu.

Senegal yaingia katika mtego wa demokrasi na vurugu katika bara la Afrika.

Dakar, Senegal-31/01/2012. Maalfu ya wananchi nchini Senegal , wakiongozwaa na viongozi wa vyama vyaupinzni wana endelea kuandamana ili kupinga uamuzi wa mahakama kuu kumruhusu rais wa sasa Abdoulaye Wade kugombea kiti cha urais kwa mara ya tatu.
Maanamno yao ambayo yameaanza siku hivi karibuni yamesha poteza maisha ya watu wawili  baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano ambayo yalizuiliwa na polisi na kusababisha vurugu.
Uongozi wa chama cha upinzani June 23 Movement - M23 umewataka wananchi "kuandamana bila kufanya vurugu."
Vurugu za kisiasa nchini Senegal zimekuja baada ya mahakama kuu nchini humo kutoa ruhusa kwa rais Abdoulaye Wade kugombea kiti cha urais na kuwaazuia baadhi yawagombea akiwemo Yousuf Ndour kwa kutotimiza masharti ya uchaguzi.

Marekani yadai utawala wa rais Bashar al Assad wa Syria utaanguka muda si mrefu.

Washington, Marekani - 31/01/2012. Serikali ya Marekani imedai ya kuwa serikali ya rais Bashar al Assad inakaribia kuanguka.
Matamshi hayo ya Marekani yamekuja wakati jumuiya ya nchi za Kiarabu zimewakilisha  muswada ili se rais Bashar al-Assad aachie  madaraka ili kuwezesha kuundwa kwa serikali ya mpito itakayo andaa uchaguzi wa halari nchini Syria.
Msemaji wa Ikilu ya Marekani Jim Carney alisema " kuanguka kwa serikali ya Bashar al- Assad kupo njiani kwani haina tena utawala katika nchi nzima ya Syria."
Hata hivyo serikali ya Urussi imedai " mswada huo wa nchi za Kiarabu inafungua njia ya vita vya wenyewe kwa wenyewe."
Syria imekumbwa na mvurugo wa kisiasa tangu kuibuka kwa mwamko wa kisiasa katika nchi za Kiarabu ambao ulianzia nchi Tunisia.


Makamu wa rais wa Irak aonya kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Irak.


Irbil, Irak - 31/01/2012. Makamu wa rais wa Irak ambaye yupo ukimbizini katika jimbo la Kikurdishi ameonya yakuwa Irak inawezza kurudi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Makamu wa rais Tariq al-Hashimi alisema " Hali iliyopo nchini Irak kwa sasa inatisha na inaelekea kukaribisha vita vya wenyewe kwa wanyewe, kwa Waziri Mkuu Nuri al-Maliki anaielekeza nchi yangu kwenye hali ya kuwepo vita kati yetu wenyewe kwa wenyewe."
"Nashangaa kusikia ya kuwa Irak ni bora kwa sasa, na Marekani inawezaje kujisifia kutokana na hali iliyopo nchini Irak? Wakati hali bado ni tete kila sehemu, Irak kutokuwa na amani kutaathiri maslahi ya Marekani."
Makamu wa rais Tariq al-Hashimi yupo ukimbizini katika jimbo la Wakurdishi, baada ya kushutumiwa kuhusika katika njama ya kutaka kuleta machafuko ndani ya serikali.


Nchi wanachama wa muungano wa Ulaya wakubaliana kudhibiti sarafu ya Euro.

Brussels, Belgium - 31/01/2012.  Nchi za muungao wa jumuiya ya Ulaya zimekubaliana kwa pamoja kudhibiti matumizi ya fedha kwa nchi wanachama katika kikao ch wakuu wa nchi hizo walipo kutana nchi Belgium.
Katika mkutano huo viongozi hao wa nchi 25 walikubli na kutia sahii mkataba wa kudhibiti, ili kuepusha hali iliyoo tokea hivi karibuni ya kuyumba kwa mfumo wa kifedha katika nchi za muungano huo.
Rais wa muungano wa nchi hizo za Ulaya Herman Van Rompuy alisema " nivizuri tumeweza kutimiza na kukubaliana kwa pamoja na hi itasaidia kuimarisha sarafu ya euro katika soko la kimataifa."
katika mkataba huo nchi mbili Uingereza na Jamuhuri ya Chezch zimekataa kusaini mkataba huo kutokana na sababu za ambazo nchi hizo zinasimamia kwa manufaa ya nchi zao.




Sunday, January 29, 2012

Vionngozi na Marais wa Afrika wakutana nchini Ethipia.


Adis Ababa, Ethiopia - 29/01/2012. Viongozi na Marais wa Afrika wanakutana nchini Ethiopia katika mkutano wa kwaza tangu kuuwawa kwa  rais wa Libya Muammar Gaddafi ambaye alikuwa mmoja wa viongozi maarufu katika jumuiya ya mungano wa viongozi wa bra la Afrika.
Rais wa Benin Thomas Boni Yayi  ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho cha viongozi wa muungano wa nchi za Afrika alisema " tumekutana hapa ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayo likumba bara la Afrika hasa nchini Somalia, Sudan, Senegal na Niger, kwani yankuwa yakileta shida na matatizo kwa wanachi wa maaeneo hayo na bara la Afrika kwa Ujumla."
Naye katibu mkuu wa umoja wa Matifa Ban ki -Moon ambaye ameudhuria mkutano huo  alisema  " inapaswa serikali za Afrika ziepukane na ubaguzi wa kijinsia na kuwapa raia wake haki sawa."
Hata hivyo kufuatia hotuba hiyo ya Ban ki- Moon, hakuna maoni yaliyo tolewa na kutoka kwa viongozi wa Afrika ambao hapo mwanzo baadhi ya nchi wanachama wa muungano huo wa Afrika hawakukubaliana na jambo   hili hasa linapo kuja kuhusu swala la ushoga wakati waziri mkuu wa Uingereza alipo lizungumzia kwa mara ya kwanza nchini New Zealand wakati wa mkutanao wa nchi zilizo tawaliwa na Uingereza.

Uzalisha wa mafuta Sudan kuwa na mgogoro kati ya wassudan.

Juba, Sudani ya Kusini - 29/01/2012. Serikali ya Sudani ya Kusini imeamua kussimamisha uzaliashaji wa mafuta hadi hapo itakapo fikia makubaliano na serikali ya Kartoum.
Stephen Dhiue Dau waziri wa madini na nishati wa  udani ya Kusini alisema " kufuatia majadiiliano yaliyo fanyika hivi karibuni kati ya serika ya Juba na Kartoum na kutofikiwaa makubaliano itakuwa vigumuu kuendelea na uzalishaji.
"Katika mkutano huo, serikali ya Kartoum inatakiwa kukubaliana na serikali ya Juba katika maswala ya uzalishaji wa mafuta na kuondoa majeshi yake yaliyopo katika mpaka wa maeneo ya Abyei." Aliongezea waziri Stephen Dhieu Dau.
Mvutano kati aya serikali ya Juba na Kartoum zimekuwa zikivutana tangu Sudani ya Kusini kujitenga na serikali kuu ya Kartoum mwaka jana.


Wakaguzi wa maswala ya kinyuklia wawasili nchini Iran.


Tehran, Iran - 29/01/2012. Wakaguzi wa mswala ya kinyuklia wameawasili nchini Iran kwa ziara ya siku tatu, ili kukagua ni kwa kiasi gani Iran inazalisha zao hilo la kinyuklia kulingana na vipimo vyakimataifa.
Herman Nackaerts ambayye ni kiongozi anaye ongoza msafara wa wajumbe wa shirika linalo simamia maswala ya kinyuklia alisema " tunatumaini serikali ya Iran itashirikiana nasi kwa kila hali ili kupa uhakika wa mpango wao wa kinyuklia."
Katika ziara hiyo wajumbe hao wa shirika ya umoja wa mataifa linalo shughurikia maswala ya kinyuklia watafanya mazungumzo na  waziri wa mambo ya nje ya Iran Ali-Akbar Salehe.
Ziara hiyo ya wajumbe wa shirika la kimataifa linalo shughurikia maswala ya kinyuklia inafanyaka wakati nchi za jumuiya ya Ulaya na Marekani zimeiwekea vikwazo  Iran kwa madai inakiuka viwango vyauzalishaji wa viwango vya nyuklia na kuwa na mpango wa kutengeneza siraha za kinyuklia.

Saturday, January 28, 2012

Bill Gate ahaidi kutoa dola za Kimarekani 750 kwa ajili ya kupambana na Ukwimwi.

Serikali ya mpito ya Libya yatakiwa kusimamisha unyanyasaji.


Misrata, Libya - 28/01/2012. Serikali ya mpito ya Libya imetakiwa kukabiliana na kusimamisha   unyanyaswaji ambayo wanafanyiwa watu wote ambao walikamatwa na kuwekwa kizuizini.
Mkuu wa shirika linalo simamia haki za binadamu la umoja wa mataifa  avi Pilay lilisema " watu wote ambao wamekamatwa  kwa kushukiwa kuhusika au kusaidia serikali ya rais Muammar Gaddafi wamekuwa wakiteswa, kubakwa na wengine kufikaia kupoteza maisha, hivyo hatua za haraka zinahitajika kuhakikisha vitendo hivyo visimamishwe mara maoja.
"Hali ya unyanyaswaji kwa watu waliokuwa kizuizini imekuwa ikitokea karibu kila sehemu nchini Libya."
Na mkuu wa jeshi la mji wa Misrata Ibrahim Beitelmel alisem " nafikiri hili shirika la kutetea haki za binadamu na hawa waganga  wana jambo la siri  na au uhusiano na Muammaar Gaddafi, kwani hali kama hiyo siyo kubwa kama wanavyo tangaza."
Kufuatia hali hiyo, shirika la waganga wasiyo na mipka la kutoka Ufaransa - Medicins Sans Frontieres limesimamisha shughuli zake kutokana na kuendelea kwa hali ya unyanyaswaji kwa watuu waliowekwa vizuizini.
Inaaminika ya kuwa idadi wafungwa na watu waliowekwa kizuizini inazidi 8,500, kwa madai walikuwa wakishirikiana na serikali ya  Muammar Gaddafi.

Mganga alihusika katika kutoa habari alipo Osma Bin Laden.






Washington, Marekani - 28/01/2012.Waziri wa ulinzi wa Marekani amelaumu kitendo cha serikali ya Pakistani kumweka kizuizini mganga aliye saidia kukamatwa kwa Osama Bin Laden.
Leon Panetta alisema  "nakuwa na mashaka na kitendo cha serikali ya Pakistan kumweka kizuizini Shikal Afridi kwa makosa ya jinai ambayo anadaiwa kuyafanya, kwani Shikal, alisaidia katika kupartikanakwa Osama bin Laden.
"Dr Shakal Afridi amekuwa akifanya kazi na serikali yeetu katika jitihada za kumtafuta Osama bin Laden, na kwa utaalamu wake aliweza kukusanya DNA ambazo zilisaidia katika harakati za kumtafuta  kiongozi huyo wa Alqaeda  na hatimaye aliuwawa."
"Na bado naamini ya kuwa kulikuwa na baadhi ya viongozi nchini Pakistani walikuwa anajua wapi Osama bin Laden alipo kabla ya jitihada za ziada kuchukuliwa na serikali ya Marekani.
Uhusiano wa Marakani na Pakistan umekuwa ukizorata kwa muda sasa, jambo ambalo limekuwa likileta kutiliana mashaka kati ya nchi hizo mbili hasa katika maswala ya kiusalama.

Mahakama yaruhusu rais Abdoulaye Wade kugombea tena kiti cha urais.




Dakar, Senegal - 28/01/2012. Mahakama kuu nchini Senegal imetoa uamuzi ya kuwa rais wa sasa anaweza kugombea kitu cha urais kwa mara ya tatu kwa kufuatia sheria ya nchi inavyo sema.
uamuzi wa mahakama ulisema "Rais Abdoulaye Wade 85, ambaye ameruhusiwa kugombea kiti cha urais, baada ya kutimiza mashrti ambayo yanatakiwa mgombea kuyatimiza."
Kufuataia uhamuzi huo wa mahakama, maelfu ya wanchi wa Senegal wameandamana kupinga jambao ambalo limesababisha polisi wa kuzuia ghasia kutumia nguvu  kuwatawanya waandamanaji.
Naye mwanamuziki maarufu duniani Youssou Ndour, ambaye alikuwa anatarajiwa kugombea kiti hicho cha urais, na aliyekuwa mpinzani mkubwa katika kupinga kitendo cha rais Wade kugombea tena kiti cha urais amezuiliwa kugombanaia kiti hicho.
Uchaguzi wa urais nchini Senegal unatarajiwa kufanyaika Februari 36.


Bill Gate ahaidi kutoa dola za Kimarekani 750 kwa ajili ya kupambana na Ukwimwi.


Davos, Uswisi - 28/01/2012. Mmilikiwa wa kampuni kubwa ya mtandao duniani alihaidi kutoa kiasi cha  million 750 za dolla za Kimarekani ili kusaidia kupambana na ugonjwa wa ukimwi.
Bill Gate alihaidi fedha hizo kwa kusema "ingawa tupo na wakati mgumu wa kiuchumi, tunatakiwa tusisahau ya kuwa kuna  watu ambao wanaitaji misaada ili waweze kujisaidia kujijenga kimaisha.
Na kutoa misaada ni wajibu wetu ya hali na mali."
Mchango huo ambao umehaidiwa na Bill Gate utaambatana na misaada ya kwanza ya dola za Kimarekani million 650 ambayo Bill Gate na  mke wake Melinda waliitoa kwa kupitia shirika lao la kimisaada Bill and Melinda Founddation ambalo limekuwa likisaidia katika kupambana magonjwa ya kifua kikuu na magonjwa mengine yanayo husiana na kifua kikuu.
Bill Gate ni mmoja ya wafanyabiashara wanao uhuzuria mkutano unaoendelea nchini Uswisi ambao unawakutanisha viongozi wa dunia ili kujadili maenedeleo ya kiuchumi duniani.

Friday, January 27, 2012

Pevez Musharraf achelewesha nia yake ya kurudi Pakistan.

Etienne Tshisekedi bado alia na rais Joseph Kabila. 


Kinshasa, Jamuhuri ya Kidemokrasia Kongo - 27/01/2012. Mpinzani wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Etien Tshisekedi amewaagiza wadau nawale wote wanao muunga mkono kuendela kuandamana hadi hapo watakapo fanikiwa nia yao.
Etienne Tshisekedi ambaye ni kiongozi  wa chama cha Unino Democracy and Social  Progress (UDPS), na anapinga kwa madai ya kuwa rais wa sasa Joseph Kabila hakushinda uchaguzi,na hastahili kuwa rais wa nchi na kudai yeye ndiye aliyeshinda uchaguzi na anatakiwa aongoze nchi.

Pevez Musharraf achelewesha nia yake ya kurudi Pakistan.



Islamabad, Pakistan - 27/01/2012. Aliyekuwa rais wa Pakistan na ambaye anaishi nchi Uingereza, amechelewesha nia yaa ke ya kurudi nyumba Pakistan, kwa kutishiwa kukamatwa.
Pevez Musharraf ambaye alikuwa rais wa Pakistan na mkuu wa jeshi mwaka , ambaye baada ya kuachia madaraka 2008 aliamia Uingereza na baadaye mapema miaka miwili alitangaza kurudi nyumbani ili kugombania kiti hicho cha urais tena kwa kupitia chama chake All Pakistan Muslim League.
Msemaji wa chama ambacho Pevez Musharraf angegombania kiti cha urais Muhammad Ali Saif alisema " Uamuzi wa kuchelewesha kurudi nyumbani kwa Pevez Musharraf ni uamuzi ambao chama kilimlazimisha kufanya hivyo baada ya kukaa kikao kwa muda wa masaa  mawili, jambo ambalo Pevez Musharraf alikuwa amelipinga.
"Na chama kitaamua lini Pevez Musharraf atarudi nyumbani Pakistan."
Uamuzi wa  kuimzuia Pevez Musharaf asirudi Pakistan, umekuja baada ya bunge kupitisha uamuzi ya kuwa akirudi nyumbani lazima akamatwe.


Viongozi wa dunia waagiziwa kutupia macho swala la wakimbizi duniani.


Davos, Uswis - 27/01/2012. Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalo shughulikia hali na maswala ya wakimbizi amewaagiza viongozi walioudhuria kwenye mkutano wa kutasmini hali ya uchumi dunia ya kuwa wasifunge milango na kulitupia macho swala la wakimbizi ambalo linaongezeka kila siku.
Antonio Guterres alisema " hali ya kutokuwepo na utulivu na amani na vita vimekuwa vikiwaacha mamilioni wakiwa wanaishi katika maaisha ya kikimbizi na magumu.
Wakati vita na vurugu watu wanashindwa kujenga maisha yao, katika nchi yao na kukumbilia maaeneo yaliyo na amani jmbo ambalo watu wengi wamekuwa naa wakati mgumu, kwa mfano zaidi ya watu 350,000 ambao wameacha makazi hasa katika nchi za Sudan na Somalia."
Viongozi kutoka nchi tofauti duniani wanakutana ili kujadili haali halisi ya uchumi duniani.

Monday, January 23, 2012

Kenyatta Ruto na wengine wawili wahitajika kujibu kesi zidi yao na mahakama ya Hague Uhollanzi.

Kenyatta Ruto na wengine wawili wahitajika kujibu kesi zidi yao na mahakama ya Hague Uhollanzi.

Hague, Uhollanzi - 23/01/2012. Mahakama inayo shugurikia kesi zinazo kiuka haki za binadamu iliyopo nchini Uhollanzi imewafungulia kesi viongozi wanne kutoka Kenya ili kujibu tuhuma zinazo wakabili katika kuhusika na vurugu na mauji yaliyo fanyika mkwa 2007 kabla na baada ya uchaguzi.
Kwa mijibu wa habari kutoka mahakama hiyo zinasema wailio funguliwa kesi ni " Makamu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta 50, aliyekuwa waziri wa Elimu William Ruto 45, Joshua Arap Sang 36 ambaye alikuwa mtangazaji wa redio na katibu wa mawaziri Francis Muthaura."
Hata hivyo washitakiwa wote wamekanusha madai hayo na kudai ya kuwa wwatashirikiana na mahakama hiyo na ukweli utajieleza.
Naye William Ruto amedai yakuwa kesi hiyo haita mzuia kugombani kiti cha urais na kusema " kesi hii ni kishangazo kwangu na naamini ukweli utaonekana na naomba wapinzani tukutane kwenye uchaguzi na wananchi waamue."
Kufunguliwa kesi zidi ya Wakenya hao kumekuja baada ya mwanasheria mkuu wa mahakama ya kimataifa  Luis Moreno Ocampo kumaliza kufanya uchunguzi wake.

Syria yapinga miswada ya jumuiya yaa nchi za Kiarabu.


Damascus, Syria 23/01/2012. Serikali ya Syria imezilaumu nchi za jumuiya za Kiarabu na kupinga miswada yote ambayo imetakiwa itimize.
Serikali ya Syria imesema " kitendo cha nchi za jumjuiya za Kiarabu kupitisha miswada hiyo ni kuingilia mambo ya ndani ya Syria  na haitokubaliana na ma miswada hiyo."
Miswada iliyo pitishwa ni kwamba rais Bashar al Assad achie madaraka na kukumkabidhi makamu wake ili aandae mpango wa uchaguzi na kupanga serikali ya mpito na lazima Syria ihakikishe yakuwa mauaji yanasimamishwa na maandamano yaruhusiwe.
Kwa mujibu wa muswada wa nchi za jumjuiya ya kiarabu, zililikuwa zimepanga yakuwa mabadiriko ya siasa nchi Syria yangekuwa kama yale ya Yemen.


Nchi za jumuiya  ya Ulaya zaiwekea vikwazo vya mafuta Iran


Brussels Ubeligiji - 23/01/2012. Nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya zimekubaliana kwa pamoja kuiwekea vikwazo Iran kwa kukubaliana kutonunua mafuta yanayo toka Iran.
Makubaliano hayo yemefikiwa nna nchi hizo ili kuilazimisha Iran kuachana na mpango wake wa kuendelea na uzalishaji wa nyuklia jambo ambalo nchi za laya na Marekani zinahisi ya kuwa Iran inampango wa kutengene siraha za kinyukli.
Vikwazo hivyo vya nchi za jumuiya ya Ulaya vimekuja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo Iran katika maswala ya fedha na mabadiriko ya kibenki kati ya nchi hizo.
Mwakilishi wa jumuiya ya Ulaya katika maswala ya kigeni Catherine Ashton alisema " nchi zote 27 za jumuiya  ya Ulaya zimekubaliana kuiwekea vikwazo Iran ili kuishinikiza kuachana na mpango wake wa kuzalisha nyuklia."
Msemaji wa mambo ya kigeni wa Iran Ramin Mehmanpaarast alisema " vikwazo zidi ya Iran havitaifanya  nchi hiyo kusitisha mpango wake kuzalisha nyuklia na Iran itaibuka kuwa mshindi na nchi za Ulaya ndizo zitaathirikaa."
Iran ambayo hapo awali ilitangaza kuwa ikiwa vikwazo vitawekwa na kuathiri uuzaji wa mafutaa yake basi watafunga mfereji uliopo katika Ghuba ya Strait Hormuz.



Sunday, January 22, 2012

Wakenya waombwa kutulia kufuatia uamuzi wowote utakao tolewa na ICC

Wakenya waombwa kutulia kufuatia uamuzi wowote utakao tolewa na ICC.


Nairobi, Kenya - 22/01/2012. Serikali ya Kenya imewataka wanchi wake wawe na hali ya kuwa watulivi kabla na wakati wamatokea ya uamuzi wa mahakama ya kimataifa inayo shughurikia kesi zidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu kutoa uamuzi wake kama baadi ya viongozi wa nchi hiyo watashitakiwa.
Katibu mkuu wa maswala ya usalama wa Kenya Francis Kimemia alisema " nimuhimu kwa rais kuwa na amani hasa katika kipindi hiki.
"Kwani pia ikiwa viongozi hao watashitakiwa watakuwa na fursa ya kukata rufaa." Alimalizia Kimemia.
Mahakama ya kimataifa ianayo shughulikia kesi zidi ya ukiukwaji wa haki za binadamau iliyopo nchini Uholanzi chini ya mwana sheria mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno - Ocamp, ilifanya uchunguzi zidi ya mauaji na machafuko yaliyo tokea nchi Kenya kabla na baada ya uchaguzi wa mkwa 2007, na kuwataka baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa vilivyo shiriki uchaguzi huo wahojiwe kwa uchunguzi zaidi.
Kufuatia uamuzi huo Uhuru Kenyatta Williamu Ruto na viongozi wengine waliwasili nchi Uholanzi na kufanyiwa mahojiwano na mahakama hiyo ambayo inatarajia kutoa uamuzi wake kama kuna kesi zidi ya watu viongozi hao.

Mmoja  wa viongozi wa serikali ya mpito ya Libya  ajiudhulu. 

Bengazi, Libya - 22/01/2012. Mji wa Bengazi umekumbwa na maandamano baada ya wanachi ambao kudai  ya kuwa serikali ya mpito haiwasikilizi hoja jambo ambalo limelazimisha kijiudhulu kwa makamu wa serikali ya mpito.
Abdul Hafez Ghoga alisema " nimeamua kujiudhulu kwa manufaa ya taifa na naamini  nisinge penda kuwa kikwazo na sababu ya kuleta hali yakuto elewana katika kujenga taifa letu."
Abdul Hafez Ghoza ambaye alishambuliwa wakati alipo tembelea chuo kikuuu cha Bengazi, anasadikiwa ya kuwa alikuwa mmmoja ya watu wa karibu wa Muammar Gaddafi.

Rais Ali Abdullah Sareh ajiudhuru urais na kuondoka nchini.

Sanaa, Yemen  - 22/02/2012. Rais wa Yemen amelihutubia taifa la Wayemen kwa mara mwisho akiwa kama rais wa nchi hiyo kabla ya kujiudhuru kiti hicho cha urais na kuondoka kuelekea Oman.
Rais Ali  Abdullah Sareh katika hotuba yake alisema "nomba msamaha kwa yale yoye yaliyo tokea wakati wa utawala wangu wa miaka 33.
"Na kwa  uwezo wa Mungu nitaenda  Marekani kwa matibabu na baadaye nitarudi Sanaa kuongoza chama changu."
Rais Ali Abdullah Sareh ameamua kujiudhuru baada ya bunge la Yemen kupitisha mswaada wa kumlinda ashitakiwe kutokana na makosa yaliyo tokea wakati wa utawala wake, jambo ambalo baadi ya watu wa Yemen wanalipinga na kutaka wale wote waliofanya makosa lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Rais Ali Abdullah Sareh na serikali yake imekumbwa na vurugu kufuatia vuguvugu la mageuzi ambalo limevumisha upepo katika nchi zote za Kiarabu na kuyumbisha serikali yake.

Saud Arabia yatangaza kuwatoa wajumbe wake katika kamati inayo kagua  nchi Syria.

Riyadh, Saud Arabia - 22/01/2012. Serikali ya Saud Arabia imeamua kuwatoa wajumbe wake ambao wanashiriki katika kuangalia hali halisi ya amani na mvurugo unao tokea nchini Syria.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi  wa Saud Arabia mwana wa Kifalme Saud al Faisal alitangaz na kusema " tunatoa wajumbe wetu kwani tunaona serikali ya Syria haitilii mkazo kupunguzwa kwa mauaji na vurugu ambazo zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu na tunaomba jumuiya ya kimtaifa izidi kuisisiza  serikali ya Syria kuleta amani na kukubalia mabadiriko."
Uamuzi wa serikali ya Saud Arabia kuwatoa wajumbe wake katika kamati inayo simamia uangalizi nchi Syria iumekuja  wakati shirikisho la muungano wa nchi za Kiarabu zikiwa zimekubaliana mpango mwingine wa kuongeza muda wakukaa kwa mwezi mmoja zaidi ili kuendele kuangalia na kukagua  hali halisi ya Syria kisiasa Syria na kutoa masharti kwa serikali ya Syria iwaachie watu wote walio jela, kuandaa uchaguzi kwa katika muda wa miezi na kuondoa wanajeshi wake wote waliopo mitaani, kuruhusu maandamano yasiyo leta vurugu, kuhakikisha mauji yanasimamishwa na rais Bashir al Asad kuachia madaraka kwa makamu wake ili kuandaa uchaguzi.

Saturday, January 21, 2012

Mashindano ya kugombea kombe la nchi bingwa katika bara la Afrika ya anza.

Mashindano ya kugombea  kombe la  nchi bingwa  katika bara la  Afrika ya anza.


Malabo, Equqtorial Guinea - 21/01/2012. Mashindano ya mpira wa miguu yanayo zikutanisha nchi za Kiafrika zilizo fauru kuingia kwenye fainali za kugombea ubingwa wa Afrika katika mchezo wa mpira wa miguu yameanza rasmi nchini Equatorial Guine katika jiji la Malabo.
Katika ufunguzi wa mashindano hayo wenyeji timu ya taifa ya Equarorial Guinea watafungua mashindano hayo kwa kukwaana na timu ya taifa ya Libya.
Sauti za mavuvuzela zimekuwa zikisikika kila kona ya jiji la Malabo tayari kwa kuwakaribisha watu wote anao shiriki katika mashindano hayo hasa timu za mpira wa miguu za mataifa yanayoshiriki.
Mashindano hayo yametayarishwa na nchi mbili Gabone na Equatorial Guinea.

Chama cha Kiislaamu cha shinda uchaguzi nchini Misri.


Kairo, Misri - 21/01/2012. Matokeao ya uchaguzi uliyofanyika nchini Misri yameipa chama cha Kiislama ushindi mkubwa zidi ya vyama vingine ya siasa.
Chama cha Muslim Brotherhood Freedom kimeshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 47 ya viti katika bunge lijalo la nchi hiyo.
Uchaguzi huo ni wa kwanza tangu kuangushwa kwa madarakani amliyekuwa rais wa Misri Husni Mubara mwaka jana, kutoka na maandamano makubwa yaliyo fanyika nchini humo.

serikali ya Nigeria yatangaza hali ya hatari katika mji wa Kano.

Kano, Nigeria - 21/01/2012.Serikali ya Nigeria imetangaza hali ya hatari na kuweka vizuizi katika mji wa Kano kufuatia milipuko ya mabomu iliyo sababisha mauaji ya watu 126 na wengine kujeruhiwa vibaya.
Kundi la Boko Haramu limedai ya kuwa limehusika na milipuko hiyo.
Kufuatia milipuko hiyo, serikali ya Nigeria imefunga mipaka inayo pakana na Niger na Kamerooni kwa madai ya kuwa mipaka hiyo imekuwa ikitumika na makundi kama Boko Haram.

Kiongozi wa kundi Hamas Khaled Meshaal la  kutogombani  uongozi tena. 

Ghaza, Palestina - 21/01/2012. Kiongozi wa kundi la Hamas ametangaza ya kuwa hatagombea tena kiti cha uongozi wa kundi hili ambalo amekuwa kiongozi tangu mwaka 2004.
Khaled Meshaal alisema hayo wakati alipo kutana  na jopo la viongozi wa kundi Hamas na kusema " nimeamua kutogombea uoangozi huo kutokana na sababu za kibinafsi na hata hivyo nitazidi kutumikia chama changu cha Hamas na watu wa Palestina."
Khaled Meshaal alichukua uongozi wa kundi la Hamas baada ya kifo cha Abdel Aziz al Rantisi, ambaye aliuwawa na jeshi la Izrael.

Yemeni yapitisha sheria ya kulinda rais asishitakiwe akitoka Madarakani.


Sanaa, Yemen - 21/01/2012. Bunge nchini Yemen limepitisha mswada ambao utamlinda rais asiweze kushitakiwa
Sheria hiyo ambayo ilichelewa baada ya rais wa Yemen kutaka mabadiliko yafanyike ili kumpa nafasi ya yeye na wenzake ambao walikuwa wanaongoza serikali kuwekewa nguzo ya kisheria ambayo itawalinda washishitakiwe baada ya kutoka madarakani.
Waziri wa habari  Ali al Amrani alisema " sheria hii imepita na itasaidia kuleta na kufikia malengo ya amani na mabadiriko ya kisiasa ambayo ndiyo kilio cha wananchi wa Yemen." 
Kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo, rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh atajihudhuru na kutoka katika kiti cha urai ambacho amekikalia kwa muda miaka 33.

Madagaska yamkatalia rais wazamni kurudi nchini mwake

Madagaska, Antananarivo - 21/01/2012. Ndege ambayo ilikuwa imembeba aliyekuwa rais wa zamni wa Madagaska  na aliyetolewa madarakani mwaka 2009 na kukimbilia ukimbizini nchini Afrika ya Kusini ilikataliwa kuingia anga la Madagaska.
Rais Marc Ravalomanana ambaye alikuwa akielekea nchini mwake baada ya kukua ukimbizini nchini Afdrika ya Kusini, alijikuta akikataliwa kuingia nchini Madagasca.
Kwa mujibu wa serikali ya Madagaska zinasema "ikiwa Marc Ravalomanana atarudi nchini Madagaska atakamatwa na jambo hili linaweza kuleta vurugu katika nchi, kwani watu ambao wanamuunga mkono wanasubiri kitendo hicho."
Hata hivyo, Marc Ravalomanana alisema " nataka kurudi nyumbani ili kuongoza na kuleta mabadiliko ya kisiasa yenye amani na siyo kuleta vurugu."
Marc Ravalomanana amekuwa akitaka kurudi nchini mwake,lakini serikali ya Madagasca imekuwa ikimkatalia kwa kuhofia ya kuwa kurudi kwake kunaweza kuleta mchafuko wa amani.

Wednesday, January 18, 2012

Janga la njaa laanza kunyemelea nchini Sudan.

Janga la njaa laingia nchini Sudan.

Kordofan, Sudan - 18/01/2012. Mwakilishi wa serikali ya Marekani anayeshughulikia maswala ya Sudan ameonya ya kuwa kuna watu zaidi ya milllion moja watakumbwa na janga la njaa nchini Sudani.
Princeton Lyman alisema "ikiwa huduma za kijamii hazitafikishwa  kwa haraka katika maeneo ya Kusini kwa Kordofan na mto Nile Bluu, basi hali itakuwa mbaya kiasi watu kufa na njaa hadi ikifika mwezi Machi."
Nafikili imefikia wakati wa Afrika kusema kwa sauti moja katika swala hili na kutoruhusu swala hili kutokea na ni wajibu wa viongozi wa Afrika kuleta amani na usalama kwa wanchi wao ili misaada iweze kutolewa kirahisi pindipo inapo itajika na dunia nzima lazima ilitizame tatizo hili."
Balozi wa Sudan nchini Afrika ya Kusini Ali Yusuf Alsharif alisema "hali ineweza kuwa mbaya kuliko Somalia, na hasa nguvu zisizo na busara zinapo tumika kwani zinafanya hali inakuwa tete na kuweka wakati mgumu kwa kila pande."
Princetone Lyman aliyasema hayo nchini Afrika ya Kusini, na kusisi tiza mashirika ya kimataifa yaruhusiwe kufanya kazi zake za kutoa misaada, jambo ambalo serikali ya Sudan imekuwa ikidai yakuwa maeneo hayo ni ya hatari kwa mashirika ya kimataifa.

Vyama vya wafanyakazi vyasimamisha mgomo nchini Nigeria.


Lagos, Nigeria - 18/01/2012. Jiji la Lagos na majimbo mengine nchini Nigeria yamekuwa na utulivu baada ya vyama viwili vya wafanyakazi kukubaliana kusimamisha mgoma ambao ulikuwa umepangwa kutokana serikali kukubali kupunguza bei ya mafuta.
Vyama hivyo Nigeria Labor Congress na Trade Union Congress vilikuwa vimeitisha mgomo kwa wanachama wake kutokana na kitendo cha serikali kutaka kusimamisha rudhuku katika mafuta jambo ambalo lilileta vurugu karibu nchini nzima ya Nigeria.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kutangaza ya kuwa serikali itapunguza bei ya mafuta.
Ningeri nchi mojawapo inayo zalisha mafuta kwa wingi duniani, lakini imekuwa namatatizo ya zao hilo jambo ambalo limefikia hata kusababisha hali ya kiusalama katika maeneo yanayi chimbwa zao hilo kuwa tete.


Izrael haina mpango wa kufanya mashambulizi nchini Iran kwa sasa.




Tel-Aviv, Israel - 18/01/2012. Waziri wa ulinzi wa Izrael  ametamka ya kuwa mashambulizi zidi ya mitambo ya kinyuklia ya Iran hayapo kwenye meza yake na serikali haina mpango huo.
Waziri wa ulinza Ehud Barak alisema " uamuzi wa kuyashambulia maeneo yaliyo na mitambo ya kinyuklia nchini Iran ni kitu ambacho si cha ukaribu na cha kuzaniwa kwa sasa, hivyo na nisingependa kuwapa muda maalumu."
Hata hivyo Ehud Barak alishindwa kuelezea kama Iran inauwezo wa kutengeneza bomu la kinyuklia kwa kusema "sijui na siwezi kuthibitisha hilo."
Waziri wa ulinzi Ehud Baraka aliyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na radio ya kijeshi ya jeshi la Izrael.

Benki ya dunia yaonya kuibuka kwa myumbo wa uchumi duniani.




New York, Marekani 18/01/2012. Benki ya dunia imetahadharisha ya kuwa huenda dunia ikakumbwa tena na myumbo wa kiuchumi ambao utaleta madhara kuli ilvyo tarajiwa.
Onyo hili limekuja baada ya habari kutoka benki hiyo kusema " madeni yanayo zikumba nchi za Ulaya, msukosuko wa usambazaji wa mafuta na soko la kifedha kutokuwa na muhimiri imara ndizo zitakuwa sababu ya kuyumba kwa uchumi wa dunia."
Myumbo wa uchumi duniani umekuwa ikileta vichwa kuuma kwa wakuu wa nchi na viongozi wa sekta mbalimbali kwa muda sasa na bado wapo mbioni kutafuta ufumbuzi wa swala hilo.

Tuesday, January 17, 2012

Watanzania ni wachangamfu na wanamatumainai ya maisha.

Watanzania  ni wachangamfu na wanamatumaini ya maisha.

Dar er Salaam, Tanzania - 17/01/2012.Shirika linalo chunguza tabia na maisha ya binadamu wanavyo ishi  katika mazingira tofauti limeripoti ya kuwa wanchi wa Tanzania watu wachangamfu, wacheshi na furaha kwa ujumla na kuwa na matumaini makubwa kimaisha.
Shirika hilo The Legatum Prospertity Index limeasema " Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na Kati na watu  waishio nchi Tanzania  wanauwezo wa kukabiliana na hali iliyopo, jambo ambalo linawapa matumaini ya kimaisha kwa kila siku na kuwa na furaha ya kimaisha."
"Tanzania pia ni nchi yenye amani na watu wake wanaweza kujitafutia, wanashirikiana kwa hali na mali kiti ambacho kinaleta furaha kwa jamii nzima." lilisema shirika hilo lenye makao makuu nchi Uingeraza Londo.

Somalia Puntland kuanza kuchimba mafuta.


Puntland, Somalia - 17/01/2012. Shirka moja la kutoka Kanada limeaanza kuchimba ili kutafuta vyanzo vya mafuta katika eneo lili Kaskazini mwa Somalia kenye  jimbo la Punland.
Shirika hilo lijulikanalo kama Canadian Africa Oil,  limeaanza uchimabaji huo kwa makubaliano na serikali ya Punland jimbo la Somalia lililo jitenga na Serikali ya Kuu Somalia.
Issa Farah mkurugenzi mkuu wa madini na nishati alisema " huu ni mwanzo wa mabadiliko kwa Wasomalia wote kwa kuzingatia Somalia imekuwa na matatizo tangu mwaka 1991 na fikili baada ya miaka 10 Somalia itakuwa imebadilika kiuchumi kwa kiasi fula."
Uchimbaji wa kutafuta vyanzo vya mafuta hayo utaanza kwa kuchimbwa mita 38000 ambapo inatarajiwa kufikia mafuta amboyo yanakadiliwa kuna mapipa zaidi ya bilion 4.

Uingereza yakataliwa kumridisha kwa nguvu Abu Qatada nchini Jordani.


London, Uingereza - 17/01/2012. Mahakama ya kutetea haki za binadamu ya nchi za jumuiya ya Ulaya imepinga ombi la serikali ya Uingereza la kutaka mmoja wa dau wa Osama bin Laden arudishwe nchi Jordani.
Mahakama hiyo ilikataa abu Qatada kuridishwa kwa nguvu nchini Jordani ambapo anakabiliwa na kesi za uhaini, kwa kuwa kuna uwezekano haki zake za kibinadamu zikavunjwa na serikali ya Jordani.
Mahakama ilisema " tumeona ya kuwa Abu Qatada akirudisha nchini Jordani huenda akateswa na kupewa adhabu ambazo zinakwenda na kinyume na haki za bibanadamu."
Abu Qatada, anayejulikana kwa jina la Omar Mohammed  Othman alipata ruhusa ya kuishi nchi Uingereza  1993 baada ya kukumbia to  Jordani kwa kuwa serikali ya nchi hiyo ilikuwa inamuhusisha na tukio la kulipuliwa kwa shule ya Waamerika iliyopo nchini Jordan na Jerusalem Hotel.

Saturday, January 14, 2012

Uchaguzi wa mkuu wa Kenya 2012 mikononi mwa Mwai Kibaki na Raila Odinga.



Uchaguzi wa mkuu wa Kenya  2012 mikononi mwa Mwai Kibaki na Raila Odinga.


Nairobi, Kenya - 14/01/2012. Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa uamuzi ya kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo  ufanyika mwaka 2013 au kama ukitakiwa kufanyika mwaka huu itategemea makubaliano ya serikali ya muungano.
Jaji Mumbi Ngugi akiwa na majaji wenzake David Majanja na Isaac Lenaola alisema " Jopo hili la majaji limekubaliana kwa pamoja ya kuwa uchaguzi mkuu ufanyike mwaka 2013 Machi, na kama serikali itakubali baraza la mawaziri livunjwe mapema basi uchaguzi unaweza fanyika mwaka huu."
Na inabidi makubaliano hayo yawe kimaandishi


Angola yawapiga jeki Wareno kibiashara.


Luanda Angola - 14/01/2012 - Wafanya biashara wanaotoka nchini Angola wamekuwa na wakati mzuri wa kunua hisa na kufanya bishara zao nchini Ureno kutokana na nchi hiyo kuyumba kiuchumi.
Ureno ambayo ilitawala Angola miaka ya nyuma kabla ya Angola kupata uhuru 1975, imejikuta ikipigwa jeki na Angola katika sekta tofauti za kibiasha baada ya wafanya bishara kutoka nchi hiyo kuanza kufanya biashara na kuwekeza nchini humu katika baadhi ya mabenki.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kiuchumi wanasema " Wareno wengi sasa wanaamia Angola katika harakati za kutafuta kazi na wakati huo huo kuuza na kununu bidhaa nchini Angola."
Angola na Ureno zimekuwa na historia ya karibu kwa kuzingatia nchi hizo zina watu ambao kwa njia moja au nyingine wanauhusiano wakaribu sana kijamii,


100% - Namuunga mkono   Baraka Obama hadi mwisho




Johannesburg, Afriak ya Kusini 4/01/2011. Mwana mama maharufu duniani kwa vipindi vyake maili alivyokuwa akivitangaza wakati wa kipendi chake cha TV nchini Marekani ameudhihirishia umma ya kuwa yupo pamoja na rais Baraka Obama kwa hali na mali.
Oprah Winfrey alisema " nina muunga mkono Baraka Obama kwa hali na mali na kwa kluzingatia kazi ngumu aliyonayo na jitihada zote ambazo ameonyesha katika kuinua maisha ya watu wote nchini Marekani kwakuzingatia wakati mgumu iliyopo na nikiongozi mwenye uewezo."
Na kama akiitaji huduma zangu nipi tayari kutoa huduma hizo wakati wowote, kwani niliyo hakuna asiye fahamu sifa za Baraka Obama hasa kwa wananchi wa Marekani kwani ameleta mabadiliko makubwa sana.
Oprah Winfley aliyasema hayo baada ya kumaliza kutoa zawadi ya vyeti kwa wanafunzi wa kwanza  walio maliza shule ambayo aliijenga nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuinua na kusaidia wasichana wasio na uwezo.

Friday, January 13, 2012

Marekani yaomba msamaha kwa Waafghanistani.


Eric Cantona ataka kugombea urais wa Ufaransa.


Paris, Ufaransa - 13/01/2012. Aliyekuwa mchezaji maarufu wa timu ya Manchester United ametangaza wiki hii  nia yake ya kugombea urais wa Ufaransa unao tarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Eric Cantona 45 alifanya uamuzi huo na kuandika barua kwa Mameya ili kupata sahii 500 ambazo zitamwezesha kugombea uchaguzi wa rais.
Eric Cantona ambaye atakumbukwa  mmnamo mwaka 1995, arimrukia mmoja ya wapenzi wa mpira wa miguu aliye mtupia maneno machafu wakati Cantona akiwa uwanjani akicheza mechi.
Wanachi wa Ufaransa wanatarajia kufanya uchaguzi wa raia hivi karibu, ambapo rais wa sasa Nicolas Sarkozy atagombea tena kiti hicho kwa mara ya pili.

Kundi la al Shabab lafanya mauaji nchini Kenya.


Gerille, Kenya - 13/01/2012. Kundi la al Shabab limefanya mashambulizi na kuwauwa watu sita na kuteka nyara watu watatu.
Watu walio uwawa ni polisi wanne, mfanyakazi mmoja wa serikali na raia mmoja baada ya kushambuliwa kwa sisasi katika mji wa Gerille uliopo karibu na mpaka wa Kenya
Mkuu wa polisi wa Gerille Leo Nyangosa alithibitisha habari za mashabulizi hao na kuuwawa kwa watu sita na wengine kutekwa nyara na kundi la al Shabab.
Kundi la al Shabab limedai ya kuwa mashambulizi hayo ni kisasi kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuvamia nchini Somalia.
Jeshi la Kenya liliingia nchini Somalia miezi mitatu iliyopita ili kupambana na kundi la al Shabab ambalo linapingana na serikali ya Somalia na kuhusika na kuteka nyara baadhi ya watalii waliokuwa wamefanya utalii nchini Kenya.


Marekani yaomba msamaha kwa Waafghanistani.


Washingtone, Marekani - 13/01/2012.  Waziri wa ulinzi wa Marekani amemtaka radhi rais wa Afghanistani, baada ya picha za video zilizo sambazwa katika mitanado ambazo zinaonyesha baadhi ya wanajeshi wa Marekani wakikojolea miili ya watu walio kufa.
Waziri wa ulinzi Leon Panetta alisema " nimeziona hizo picha na kitendo hicho kinasikitisha na kinakwenda kinyume na maadili ya jeshi la Marekani na wale waliohusika katika kufanya kitendo hicho wamesha fahamika na watachukukiwa hatu kali."
Naye rais wa Afghanistan Hamid Karzai alisema " hiki nikitendo cha kusikitisha na lazima kilaaaniwe."
Wanajeshi hao ambao walionekana wana kojelea miili ya watu ambao hawajulikani kama ni wapiganaji wa Taliban au raia wa kawaida.
Kitendo cha wanajeshi huenda kikazidi kuleta ugumu kwa wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Afghanista ili kuimarisha ulinzi na kuwaandaa Waafghanistan kujilinda wenyewe baaada ya jeshi la Marekani kuondoka nchini humo.