Rais, Baraka Obama, kafanikiwa alimia 65% kwa muda wa siku 100, ofisini. Washington, Amerika - 30/04/09. Rais wa Amerika, Baraka Obama, ametimiza siku 100,tangu kuwa rais wa Amerika. Kwa mujibu wa wachunguzi wa mabo ya kisiasa na kiuchumi, wanasema rais, Baraka Obama, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kukamilisha kwa asilimia zaidai ya 65% kwa ya le yote aliyo yasema wakati wakampeni za uchaguzi wa rais mapema mwaka jana. Moja ya mamba ambayo rais , Obama ameyatimiza, ni kufungwa kwa jela, ya Guantanamo Bay,kutia sahii kuzuia kuteswa kwa wafungwa au mtuu yoyote kinyume na sheria za haki za binadamu,kusaidia kuyakwamua kifedha makampuni makubwa ya magari kama GM(General Motors) nchini Amerika na kurudisha uhusiano mzuri na nchi nyingi ikiwemo, Venezuela. Picha hapo juu anaonekna, rais wa Amerika Baraka Obama,akionyasha vidole ya kuwa mambo ni kuelekea mbele, kabla ya kuanza kuongea na waandishi wa habari na kujibu maswali. Jeshi la Uingereza kuanza kurudi nyumbani kuanzia leo. Basra,Irak - 30/04/09.Jeshi la Uingereza limemaliza muda wake wakuu kaa nchini Irak, kama jeshi la ulinzi na kulinda amani. Hii ina fuatia , baada ya ya waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown,kusema haya siku ya alkhamisi wiki hii wakati alipo kutana na waziri mkuu wa Irak,Nour al Maliki, ya kuwa jeshi la Uingereza litajea nyumbani. Jeshi hilo la Uingereza limekuwa nchini Irak kwa kipindi cha miaka sita (6). Kwa mujibu wa habari kutoka kwenye jeshi la Uingereza, zina sema ni wanajeshi 400 watakao baki, kwa ajilii ya kutoa mafunzo kwa Wairak. Picha hapo juu wanaonekana, wanajeshi wa jeshi la Uingereza wakiwa wanatoa heshima zao kwa wanajeshi wenzao waliopoteza maisha katika vita nchini Irak, vilivyo anza mwaka 2003.
Thursday, April 30, 2009
Jeshi la Uingereza kuanza kurudi nyumbani kuanzia leo.
Posted by Kibatala at Thursday, April 30, 2009 0 comments
Monday, April 27, 2009
Mafua ya nguruwe yaiweka dunia njia panda.
Mafua ya nguruwe yaiweka dunia njia panda.
Posted by Kibatala at Monday, April 27, 2009 0 comments
Thursday, April 23, 2009
Hali ya ukame nchini Kenya huenda ikaleta maafa kwa jamii"UN"
Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Amerika lawamani. Washington, Amerika 23/04/09.Aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Condoleezza Rice,inesemekana ndiye aliyetia sahii kuanza kutumika kwa njia ambazo zilikwenda kinyume na haki za binadamu wakati watuhumiwa waliokamatwa kama wahujumu na watu hatari kwa Amerika wakati wa mahijiano katika gereza la Guantanamo Bay. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana, zinasema Bi Rice, alitia sahii ruhusa hiyo mwaka 2002, wakati akiwa mshauri wa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Picha hpo juu, anaonekana, Bi Condeelezza Rice, akiongea katika moja ya vikao wakati alipo kuwa akifanya kazi katika ofisi ya mambo ya ndani ya Amerika. Wahisani wakubali kuisaidia Somalia. Brussels, Ubeligiji - 23/04/09. Kundi la waihisani wamekubaliana kwa pamoja watachanga kiasi cha US$250 million, ili kuisadia Somalia kujenga na kurudisha hali ya kiusalama nchini humo. Wahisani hao walikubali kwa pamoja kutoa mchango huo,kwa kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano kuzungumzia hali halisi ya Somalia, hasa kufuatia kuku kwa uharamia. Picha hapo juu wanaonekana, rais wa Somalia, Sheikh Sharif Ahmed ,na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, wakati wa mkutano huo uliofanyika nchini Ubeligiji na wahisani na Umoja wa Mataifa. Uhusiano wa Amerika na Venezuela kuanza upya. Caracas, Venezuela - 19/04/09. Serikali ya Venezuela, imesema ya kuwa itafungua ofisi zake za kibalozi nchini Amerika, ikiwa ni ishara ya kuonyesha yakuwa Venezuela inahitaji kushirikiana na Amerika. Hayo yalizungumzwa na rais wa Venezuela , Hugo Chavez, wakati alipo kutana na rais wa Amerika, Baraka Obama,kwenye mkutano, ulio zishirikisha nchi zililizopo katika bara la Amerika nchi Trinidad na Tobago. Uhusiano wa Venezuela, haukuwa mzuri wakati wa kipindi cha utawala wa rais George Bush, hata kufikia, kufungwa kwa ofisi zote za kibalozi kati ya nchi hizi. Pcha hapo juu ,anaonekana , rais wa Amerika Baraka Obama na rais wa Venezuela, Hugo Chavez, wakiwa wameshikana mikono, wakta rais Hugo Chavez, alipo kuwa akimkabidhi rais Baraka Obama kitabu cha historia ya Watu wa Latini Amerika na maisha yao hadi hivi leo. Picha hapo juu, wanaonekana marais , Hugo Chavez kuliana rais, Baraka Obama kushoto wakiwa mwameshikana mkono wakati walipo kutana nchini Trinidad na Tobago ili kuzungumzia hali ya kiuchumi ya Amerika. Algeria yalaumiwa na Morocco kwa kutaka kuvuruga amani. Rabat, Morocco - 19/04/09. Serikali ya Morocco imeilaumu serikali ya Algeria, kwa kusaidia wapiganaji wa POLISARIO, kuingia karibu na mpaka wa Morocco na kufanya mashambulizi ambayo ayakuleta madhara. Kwa mujibu wa habari zilizo toka ofisi za mambo nchi za nje za Morocco, zilisema wapiganaji hao walipiga risasi ovyo hewani. POLISARIO, ni kundi lililopo kusini magharibi mwa Morocco linalo pigania kujitenga na Morocco. Picha hapo juu ni ramani ya Afrika ya Kaskazini Magharibi,na kusini mwa ramani hiyo, kunaonekana,eneo la Sahara ya Magharibi, ni eneo ambalo kwa muda mrefu linamvutano na mgogoro mkubwa huko kaskazini magharibi mwa bara la Afrika. Hali ya ukame nchini Kenya huenda ikaleta maafa kwa jamii."UN".
Harare, Zimbabwe - 17/04/09. Viongozi wa vyama pinzani nchini Zimbabwe,Robert Mugabe wa NAZU PF na Morgan Tsvangirai wa MDC, wamechelekea kwa pamoja siku ya uhuru wa Zimbabwe hivi karibuni, tangu kuanzishwa kwa serikali ya muungano.
Sherehe hiyo ambayo ili udhuliwa na viongozi wote wa serikali na baadhi mabalozi huwa inaadhimishwa kila tarehe 17/04/09 ya kila mwaka.
Katika sherehe hiyo, rais,Robert Mugabe , aliwataka wananchi waungane kwa pamoja, kujenga nchi na kuulunda nchi yao
Picha hapo juu ni ya bendera ya Zimbabwe, nchi ambayo ulipata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Posted by Kibatala at Thursday, April 23, 2009 0 comments
Sunday, April 19, 2009
Makampuni yaliyo shiriki katika ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini yanaweza kushitakiwa.
Ukame wa waanza kusogelea Afrika ya Magharibi. Akkra, Ghana - 19/04/09.Wataalamu wa sayansi ya mazingira nchini Ghana wamesema huenda ikawa na hali ya ukame zaidi hapo mbeleni, kwa kufuatia uchunguzi wa kisayansi uliofanywa kwa kulinganisha karne ya 20 na karne tuliyo nayo sasa. Kwa mujibu wa kituo kimoja cha sayansi kilichopo nchini humu(Ghana) kinasema hii ni kutokana na utafiti uliofanywa katika ziwa Bosumtwi lililopo nchini Ghana. zimeonyasha tofauti kubwa kulingana na za karne za nyuma. Hata hivyo, wanasayansi walisema yakuwa,bado itachukua muda hali kuwa mbaya zaidi kwa kuzingatia mvua na maeneo ya kijiografia yaliopo katika nchi hizi. Picha hapo, juu ni ya ramani ya Afria ya Magharibi, eneo ambalo wanasayansi wanasema hali ya ukame inalinyemelea kwa mbali.
Posted by Kibatala at Sunday, April 19, 2009 0 comments
Thursday, April 9, 2009
Swala la nguvu za nyuklia ni kitendawili kwa Iran, Amerika na washiriki wake.
Kim Jong Il, achaguliwa kuwa rais wa Korea Kaskazini tena.
Posted by Kibatala at Thursday, April 09, 2009 0 comments
Wednesday, April 8, 2009
Rais wa zamani wa Peru aongezewa miaka 25 zaidi kukaa jela.
Tetemeko la ardhi la leta maafa nchini Itali.
Posted by Kibatala at Wednesday, April 08, 2009 0 comments
Sunday, April 5, 2009
Baraka .H.Obama atangaza kupunguzwa kwa siraha za nyuklia duniani.
Korea ya Kaskazini yarusha chombo chake angani.
Posted by Kibatala at Sunday, April 05, 2009 0 comments