Monday, March 30, 2009

Mkutano wa nchi za wanachama wa jumuiya za nchi za Kiaarabu waanza kwa vishindo"Rais wa Sudan audhuria mkutano".

Wapenzi wa soka wapotezamaisha"Fifa yataka maelezo".

Abdjan, Ivory Coast - 30/03/09. Zaidi ya watu 22 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana wakati walipotaka kuingia uwanjani kuangalia mpira kati ya timu yao ya taifa na timu ya taifa ya Malawi katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya kuingia katika fainali ya kombe la dunia litakalo fanyika nchini Afrika ya Kusini mwakani.
Kufuatia mkasa huo,shirikisho la mpira wa miguu duniani,FIFA, limeitaka chama cha mpira cha Ivory Coast, kutoa maelezo kuhusu mkasa huo ambao umesababisha mauaji na majeruhuhi ya watu.
Picha hapo juu ni alama ya shirikisho la mpira wa miguu duniani,ambalo linasimamia michezo yote ya mpira wa miguu duniani na kupanga sheria za mchezo huo.
Picha ya pili wanaonekna polisi wakiwa wamembeba mmoja ya watu alijeruhiwabaada ya kukanyagwa wakati akijaribu kuingia uwanjani kuangaria mechi kati ya timu ya taifa lake na timu ya taifa ya Malawi.
Waziri wa mambo ya ndani aponea chupuchupu.
Mogadishu, Somalia - 30/09/09. Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdirahman Ali, amenusurika kupoteza maisha baada ya gari alilo kuwa akisafiria kukanyaga bomu na kulipuka na kupoteaz maisha ya walinzi wake katika kitongoji kimoja katika mji wa Mogadishu.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, jina limehifadhiwa ,alisema inaelekea hili shambulizi lilikuwa limemlenga waziri huyu.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja ya wapiganajiwa moja ya kundi linalo pingana na serikali ya Somalia.
Mkutano wa nchi za nchi wanachama wa jumuiya za nchi za Kiaarabu waanza kwa vishindo"Rais wa Sudan audhuria mkutano".
Doha, Katar - 30/03/09. Mkutano mkuu wa kuwakutanisha viongozi na marais wa nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu, umeanza rasmi nchini Katar, ili kutafuta ni jinsi gani nchi hizi zita weza kutatua matatizo yanayo zikabili nchi zao.
Katika mkutano huo, ambao umekuwa una malumbano mengi ya kisiasa, hasa baada ya mahakama ya kimataifa inayo shughulikia kesi za uarifu na mauaji iliyipo nchini Uhollanzi kutoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar Al bashir, ili ashitakiwe kwa makosa ya jinai.
Wakihutubia mkutano huo kwa nyakati tofauti, viongozi wa Syria na Libya, walisema imekuwa jambo la aibu kwa nchi za Kiaarabu kushindwa kushirikia na baadhi ya nchi wanchama wa nchi hizo kuwa vibaraka wa nchi za Ulaya na Amerika.
Katika mkutano huo, rais wa Misri, hakuudhulia mkutano huo, na kwa mujibu wa chunguzi wa maswala ya kisiasa wanasema hii ni kutokana na hali halisi iliyopo eneo la Mashariki ya Kati.
Picha hapo juu ni ukumbi wa mkutano ambamo viongozi wa nchi za jumuia wanachama wa nchi za Kiaarabu wanakutana.
Picha ya pili anaonekana rais wa Libya, Muammar Ghadaffi, akuongea na viongozi wenzake wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya ya nchi Wakiarabu mji Doha.
Picha ya tatu ni rais wa Syria, Bashar al Assad, aliongea na kukumbusha makubaliano ya amani katika eneo la Mashariki ya Kati bado kutimizwa hivyo ni lazima nchi za kiaarabu ziungane kuhakikisha mkataba huo unafikiwa na kukamilishwa.
Picha ya nne, anaonekana rais wa Sudan, Omar al Bashir, akiwasili katika mkutano wa viongozi wa nchi za Kiaarabu unaofanyika nchini Katar Doha.
Chuo cha polisi cha shambuliwa nchini Pakistan.
Rahore,Pakistan - 30/03/09 - Mashambulizi yametokea katika kituo cha kufunzia polisi kilichopo Rahore na kusababisha mauaji na majeruhi ya polisi walio kuwa katika majengo hayo.
Chuo hicho kilikuwa na watu wapatao 800, ambao walikuwa katika chuo hicho kwa ajili ya mfunzo ya polisi.
Hata hivyo kwa msemaji wa serikali na mkuu wa operasheni hiyo Majr General Athar Abbas,alisema makamanda waliweza kuwashinda watu walioteka nyara majengo hayo na baadhi yao walikamatwa na wapo chini ya mikono ya serikali.
Picha hapo juu, wanaonekana na baadhi ya polisi na maafisa usalama wakiwa wamemshikilia mmoja ya mtuhumiwa ambaye anasadikiwa kuwa mmoja ya watu walio leta maafa katika chuo cha mafunzo ya polisi cha Rahore.
Picha ya pili wanaonekana wafanyakazi, zima moto na huduma ya kwanza wakiwa wamembeba mmoja wa watuwalio jeruhiwa wakati wa mashambulizi yaliyo tokea katika chuo cha polisi.
Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari kizimbani nchini Kambodia.
Phnom Penh, Kambodia - 30/03/09.Mahakama ya ualifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa iliyopo nchini Kambodia, imeanza kusikiliza kesi ya mauaji ya kimbari yaliyo fanyika mapema miaka ya 1970s, ambapo zaidi ya watu wapatao million 1.7 waliuwawa na baadhi ya viongozi wa kundi la Khmer Rouge.
Majaji watano, wataanza kusikiliza kesi zidi ya aliyekuwa mmoja wa kiongozi, wa kundi la Khmer Rouge, Kaing Guek Eav au kwa jina jingine Duch anashitakiwa kwa kuhusuka na mauaji hayo ya kimbari wakati alipo kuwa mkuu wa jela moja nchini Kambodia.
Kaing Guek Eav au Duch,mwenye miaka 66,anashitakiwa kwa makosa ya kubaka, kuua kwa makusudi,na kutesa watu bila hatia kati ya miaka 1975-1979.
Picha hapo juu, anaonekana, Kaing Guek Eav au Duch, akiwa mahakamani kusikiliza kesi zidi yake zikisomwa.
Picha ya pili anaonekana, Kaing Guek Eavau Duch,akiwa amezungukwa na wanasherika ambao wapo kusikiliza kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari zidi ya mteja wao.

Sunday, March 29, 2009

Rasi wa Brazil,azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.

Rais wa Brazil, azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.

Sao Paulo,Brazil -28/03/09. Rais wa Brazil, Lula da Silva, amezilaumu nchi za tajiri duniani kwa kuleta hali mbaya ya kiuchumi, wakati alipo kutana na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ambaye yupo nchi Brazili kwa ziara ya kiserikali.
Rais Lula da Silva, alisema yakuwa wazungu wenye macho ya bluu, ndiyo wakulaumiwa, kwa kusababisha mporomoko wa uchumi, kwani hakuna, watu weusi wala waindi ambao wameleta maafa haya ya kiuchumi duniani, na hivyo nchi masikini zisilazimishwe kulipa hasara iliyo sababishwa na watu hawa wenye machoi ya bluu.
Rais, Lula, aliongezea kwa kusema ya kuwa, mporomoko wa uchumi duniani, umeweka wazi ni jinsi gani baadhi ya watu wanavyo fikiria wao ni bora na kumbe sivyo.
Hata hivyo waziri wa Uingereza, Gordo Brown, alisema hivi sasa ni wakati wa kushirikiana kutafuta njia ya kutatua matatizo haya ya kiuchumi.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Brazil, Lula da Silva, akiongea na wandishi wa habari, mara baada ya mkutano na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Picha ya pili, anaonekna waziri mkuu wa Uingereza, akimwangalia kwa makini, rais wa Brazili, wakati akiongea kuhusu hali halisi, kwa nini uchumi umeporomoka.
Urussi kushirikiana na NATO kuijenga Afghanistan.
Moscow, Urussi-28/03/09.Serikali ya Urussi, imesema ipo ytayari kushirikiana na NATO,ili kuijenga Afghanistan.
Akisema hayo , waziri wa mambo ya nje wa Urussi,Sergei Lavrov,alisema haya wakati wa mkutano unaozungumzia hali halisi ya Afghanistan, uliofanyikia Mocsow, na kusema ya kuwa serikali ya Urussi inatizama kiundani ni jinsi gani itashirikiana na NATO, ili kuijenga upya Afghanistan.
Picha hapo juu ni baadhi ya wanchi wa Afghanistan, wakiwa katika moja ya shamba lao wakiangalia matunda, ambayo huwa wanauza na kupata kipato cha kila siku, lakini kutokana na zao hili, ndimo madawa ya kulevya hutengenezwa, na jumuia ya kimataifa imekuwa inatafuta njia mpya ya kuijenga kiuchumi Afghanistan, ili wananchi wasitegemee zao hili.
Jacob Zuma,azilaumu nchi za Magharibi.
Johannesburg,Afrika ya Kusini-28/03/09.Mwenyekiti wa chama tawala cha Afrika ya Kusini Jacob Zuma, amezilaumu nchi za Magharibi, kwa kushindwa kuisaidia Zimbabwe., kwa kudai ya kuwa ni njia moja wapo ya kushinikiza rais wa Zimbabwe ili akubaliane na mabadiliko.
Jacob Zuma, alisema hii si sawa , kwani rais Robert Mugabe amekuwa madarakani, kwa kipindi kirefu kama rais wa Zimbabwe, na hivyo sivyo kama wanaovyo ona nchi za Magharibi, bali hali ya wanchi wa Zimbabwe ndito ya muhimu, kwani katika kupiga kura kila mwananchi alipiga kura, na siyo kila mwananchi alipiga kura kwa rais Mugabe au waziri mkuu ,Tsvangirai.
Hata hivyo , Jacob Zuma, alisema kuukubali kushirikiana kwa rais Mugabe na Tsvangirai,ni mwanzo wa mageuzi yatakayo waletea wa Zimbabwe manufaa na Maendeleo.
Picha hapo juu, anaonekna , Jzcob Zuma ,akiwa kavalia vazi la kiasili la Kizulu, wakati wa sherehe za kuazimiasha kumbukumbu ya Mfalme Shaka Zulu.
Picha ya pili ni viongozi wa Zimbabwe, rais Robert Mugabe na waziri mkuu, Morgen Tsvangirai wakipeana mkono mara baada ya kukubaliana kushirikiana kuongoza serikali na wananchi wa Zimbabwe kwa pamoja.
Sudan ya shuku Israel kwa mashambulizi nchini mwake.
Kartoum,Sudan-28/03/09. Serikali ya Sudan,imesema huenda mashambulizi yaliyo fanywa katika eneo moja lililopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, lilifanywa na Israel na kupoteza maisha ya watu 40.
Mashambulizi hayo yalioyo tokea mapema mwezi wa kwanza na wapili mwaka huu 2009.
Hata hivy msemaji wa serikali ya Sudan, alisema yakuwa mashamulizi hayo mwanzo yalizaniwa yamefanywa na Amerika, lakini , baadaye serikali ya Amerika ilikanusha madai hayo.
Aliendelea kwa kusema, msemaji huyo wa serikali ya Sudan, yakuwa bado wanachunguza kwa makini, lakini huenda mashambuliz haya yalifanywa na Israel,kwani hapo awali Israel ilidai yakuwa kua siraha, zina pitia Sudan kupelekwa Ukanda wa Gaza.
Picha hapo juu, inaonyesha ramani,ni jinsi gani mashambulizi yalivyo vyanywa ikiwa ni Israel iliyafanya.
Picha ya pili ni ya moja ya gari, ambalo lilishamuliwa na makombora ya liyoshambulia eneo lililopo Kaskazini Mashariki mwa Sudan, bilia serikali ya Sudan kufahamishwa.
Japan yawa tayari kuzuia chombo cha anga cha Korea ya Kaskazini.
Tokyo, Japan-28/03/09.Serikali ya Japan, imepitisha amri ya kulitaka jeshi la ulinzi wa anga kujiandaa kuzuia chombo cha anga kitakacho rushwa na Korea ya Kaskazini.
Uamuzi huo umekuja mara baada ya Korea ya Kaskazini kutangaza ina mpango wa kurusha chombo chake angaani kati ya Aprili 4 na 8 mwaka huu 2009.
Uamuzi huu unakuja baaada ya serikali ya Japan, kuona ya kuwa kitendo cha Korea ya Kusini, kutaka kurusha roketi hiyo ni hatari kwa Japan.
Picha hapo juu, inaonekana meli ya kijeshi ya Japan, iliyo na mitambo tayari kuzuia chombo cha anga cha Korea ya Kaskazini.
IAEA-Shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia duniani la vutana kupata kiongozi mpya.
Vienna, Austria - 28/03/09.Shirika la umoja wa Mataifa linalo shughulikia maswala ya nguvu za nyuklia limeshindwa kumpata mkurugenzi wake mkuu, katika uchaguzi uliochukua mzunguko mara tano kwa kipindi cha siku mbili.
Uchaguzi huo unafanyika,ili kumpzta mkurugenzi mpya, atakaye ongoza shirika hilo , baada ya mkurugenzi wa sasa Mohamed El Baredei ambaye anatarajiwa kujiuzuru.
Wagomea waliogombea kuwa wakurugenzi wa shirika hilo,Abdul Samad Minty wa Afrika ya Kusini na Yukiya Amano, hawakuweza kushinda baada ya kushindwa kupata kura zinazo hitajika ili kuwa mkurugenzi wa shirika hilo.
Picha hapo juu, ni ya mkurugenzi wa sasa wa shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia, Mohamed El Baredei,ambaye anatajariwa kujiuzuru kutoka madarakani.

Sunday, March 22, 2009

China kujiandaa kushindana na nguvu za kiaanga.

Mchezaji wa mpira wa miguu apigwa risasi kiwanjani.

Baghdad,Irak-22/03/09.Polisi nchini Irak wamesema mmoja ya mchezaji wa mpira wa miguu, alipigwa risasi ya kichwa na kufa hapo hapo wakati alipo kuwa anaijiandaa kupiga mpira wa adhabu ndogo.
Msemaji wa polisi, Mej,Muthanna Kharid, alisema mchezaji huyo wa timu ya Buhairat, alipigwa risasi na moja ya mshabiki wa timu pinzani ya Sinjar wakati zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika.
Katika mechi hiyo timu ya Sinjar, ilikuwa inaongoza kwa goli moja.
Hata hivyo, shabiki huyo alikamatwa na polisi mara moja, alimalizia kusema haya masemaji wa Polisi.
Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ya wapenzi wa mpira wa miguu wakishangilia mara baada ya timu yao kushinda kombe la matifa ya Asia wakati walipo rudishwa kushiriki mashindano ya kimataifa.
China kujiandaa kushindana na nguvu za kiaanga.
Beijing, China, 22/03/09.Makubaliano kati ya China na Muungano wa Ulaya, kuhusu ujenzi wa pamoja wa chombo cha kuruka angani Galileo, kutoleta zao mafanikio, yameifanya China kuamua kujenga chombo chakuruka angani peke yake .
Kuamua kwa Chini kuendelea na ujenzi huo, kutaifanya China kuwa na uwezo sawa wakianga na nchi kama Amerika na Urussi.
Kutoleta mafanikio ya kushirikiana kujenga chombo hicho, kumekuja hasa kwa kuzingztia swala la usalama ambalo lililtwa na moja ya nchi mwanachama wa Muungano wa Ulaya.
Picha hapo juu, inaonekana moja ya chombo kinaruka kuelekea ngani , kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano.
Vita vya Gaza vyaleta mjadala katika jamii nchini Israel.
Jerusalem. Israel 22/03/09.Habari zinazo endele kutolewa na baadhi ya askari wa jeshi la Israel, kuhusu hali halisi ya vita kati ya Israel na Palestina, mapema mwisho wa mwaka 2008 hadi mwazo wa mwaka 2009, zinazidi kuleta hali ya wasiwasi na mvutano hivyo na kuleta mjadala mkubwa katika jamimii nzima ya Israel na kuhusu imani na ulinzi wa nchi.
Hii ina kuja baada ya ya baadhi ya watu kujadili kuwepo kwa vita hivi kwani vinakwenda kinyume na matakwa ya kidini,na wengine wana sema hii ni lazima kulinda taifa la Israel,kwani ni taifa teule na ni lazima walilinde kwa hali na mali.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya askari wa Israel wakiwa wamesima kwa pamoja kabla ya kuendelea na mapambano na kundi la Hamas kwenye eneo la ukanda wa Gaza.
Rais wa Sudan ashauriwa kuto kuhudhuria mkutano.
Khartoum,Sudan 22/03/09. Shule moja ya kidini nchini Sudan imemshauri rais wa Sudan,Omar Al bashir , kuto safiri nchini Katar, kuhudhuria mkutano wa nchi wanachama wa jumuia ya nchi za nchi za Kislam unaotarajiwa kuanza 30,03/09.
Shule hiyo Ulema, imesema hatuapendele rai Omar Al Bashir, kwenda huko kwenye mkutano, badala yake aende mwakilishi wake atakaye chaguliwa na serikali..
Hii onyo limetolewa, baada ya mahakama ya ianayo shughulika makosa ya jina na iliyopo nchini Uhollandi, kutowa kibali cha kukamatwa kwa rais huyo wa Sudan, ili ashitakiwe.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Sudan Omar Al Bashir, akishangalia kwa kucheza moja ya ngoma za kiasili za Sudan, wakati alipo tembelea katika jimbo moja nchini Sudan.
Picha ya pili wanaonekana, baaadhi ya wananchi maelfu wamekuja kumlaki, rais Omar Al bashir,alipo kwenda kuwatembele kwenye maeneo yao.

Saturday, March 21, 2009

Nchi zaanza kulegeza vukwazo nchini Zimbabwe"Misaada yaanza kutolewa

Nchi zaanza kulegeza vikwazo nchini Zimbabwe."Misaada yaanza kutolewa".

Stockholm, Sweden - 21/03/09.Serikali ya Sweden, imesema itatoa kiasi cha million $ 10.5 kwa serikali ya Zimbabwe, kwa ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Uamuzi huo wa Sweden, kuipatia serikali ya Zimbabwe, pesa umefuatia wa ule wa serikali ya Australia kutoa msaada wa pesa mapema mwamzoni mwa mwezi tatu/2009, baada ya ya kuridhika na hai halisi ya kisiasa inavyo endelea nchini Zimbabwe.
Picha hapo juu, anaonekna rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akiongea katika moja ya sherehe nchini Zimbabwe, mara baada ya chama chake kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja na chama cha upinzani cha MDC, kinacho ongozwa na waziri mkuu Morgan Tsvangirai.
Amerika na Iran bado zawekeana vitendawili.
Tehran,Iran 21/03/09.Kiongozi mkuu wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei, amesema yakuwa Iran ipo tayari kushirikiana na Amerika, ikiwa Amerika itabadilisha mwelekeo wake kuhusu Iran.
Kiingozi huyo wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei,aliya sema haya wakati alipo kuwa akizungumza mbele ya maelfu ya Wairan waliokusanyika kusherekea siku ya kuanza mwaka mpya wa Iran.
Hatua ya kiongozi wa Iran kuongea hayo , imekuja baada ya rais wa Amerika, Baraka Obama, kuongea swala la Iran wakati alipo kuwa akiongea mbele ya vyombo vya habari mapema wiki hii.
Kwa kipindi kisicho pungua miaka 30, uhusiano kati ya Irana na Amerika, umekuwa siyo mzuri,tangu Iran ilipo wateka nyara baadhi ya wafanyakazi wa kibalozi wa Amerika, walio kuwa nchini Iran, wakati wa mageuzi ya kisiasa ya mwaka 1978.
Picha hapo juu anaonekana rais, wa Amerika Baraka Obama, akiongea wakati alipo kuwa akiongea mbele ya vyombo vya habari.
Picha ya pili,anaonekana kiongozi wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei, akiongea wakati wa kuakaribisha mwaka mpya wa Wairan.
Usalama wa waweka amani Darfur mashakani.
Darfur,Sudan 20/03/09. Mmoja ya walizni wa amani kwenye maeneo ya Darfur, amepigwa risasi na kufa wakati wakiwa ulinzi kwenye kwenye maeneo ya Nyala.
Mashambulizi hayo yalitokea wakati watu wapatao wanane, waliojifunika uso, waliwashambula walinzi hao kwa ghafla wakati walipo kua katika doria, alisema msemaji wa (UNMID -UN Afrika Union force ) Kamal Daiki.
Hata hivyo akueleza ni askari huyo ametokea nchi gani.
Picha hapo juu anaokana askari wa UNAMID, akiwa ameshikilia mtutu, huku mbele yake kuna mtoto mdogo wa kike akiwa anamwangalia kwa makini.
Muungano wa nchi za Ulaya kutoa fedha mara dufu.
Prague,Czech -20/03.09.Viongozi wa muungano wa Ulaya, wamekubaliana kwa pamoja kuongeza mara dufu, fedha ili kuinua hali ya kiuchumi inalo likabili bara hili.
Akiongea haya waziri mkuu wa Czech,Mirek Topolanek,ambaye ndiye rais wa sasa wa muungano huu, alisema nchi za muungano wa ulaya zimekubaliana kutoa billion $68, wakati walipo kutana ijumaa ya wiki hii Brussel kuzungumzia hali halisi ya kiuchumi ya nchi za muungano huo.
Picha hapo juu wanaonekna viongozi wa muungano wa Ulaya wakipongezana mara baada ya kumaliza mkutano mjini Brussel siku ya ijumaa 18/03/09.
Baba aliyezaa na mtoto wake ahukumiwa kifungo cha maisha.
Viena,Austria - 20/03/09.Mahakama ya mji wa St Poelten, imemuhukumu kifungo cha maisha Josef Fritzl mwenye miaka 73, kwa kumkuta na hatia ya kumteka nyara, kumfanya mtumwa na kumweka kinyumba mtoto wake wa kike kwa kipindi kisicho pungua miaka 24 na kumzalisha watoto na mmoja ya watoto hao kufa kutokana na kukusa matibabu.
Kitendo hicho cha Josef Fritzl,kiliishangaza na kustua dunia, hasa jamii ya watu wa Ulaya kwani si kitu chakawaida katika jamii, alisema mmoja ya wakazi waliokuwa wakiishi karibu na Josef Fritzl.
Josef Fritzl, alitubu makosa yake mbele ya mahakama, baada ya mtoto wake wa kike kutoa ushaidi mbele ya mahakama,na ndipo kulimfanya akubali makosa, kwani mara ya kwanza alikuwa amekana makosa yake.
Picha hapo juu anaonekana, Josef Fritzl, akisindikizwa na polisi kueleka jela, baada ya kupata hukumu ya ke ya kukua maisha jela.
Picha ya pili, anaonekana mwanasheria wa Josef Fritzl,bwana Rudolf Mayer, akiongea mbela ya waandishi wa habari, mara baada ya kukumu zidi ya mteja wake.

Wednesday, March 18, 2009

Madagasca yapata rais mpya."Achukua ofisi akiwa kijana wa miaka 34"

Jaji arudishwa ofisini" Maandamano na siasa za mvutano bado nchini Pakistan.

Lahore,Pakistan-18/03/09.Kurudishwa madarakani kwa aliyekuwa jaji mkuu wa zamani wa Pakistan, Iftikhar Chaudhry, kumeleta hali ya joto katika siasa ya Pakistan.
Kwa mujibu wa msemaji mmoja wa mabo ya kisiasa nchini Pakistan, alisema wanachi wanangojea nini kitatokea na baada ya kuarudishwa kazini jaji huyo, kwani kuna baadhi ya kesi zinazo wakabili viongozi wa nchi hasa katika ngazi za juu za nchi. Picha hpo juu, anonekana jaji mkuu wa Pakistani, Iftikhar Chaudhry, ambaye kuchelewa kurudishwa kwake ofisini, kumeleta machafuko nchini Pakistan na mvutano wa kisiasa kuwa mkubwa.
Picha ya pili ni ya rais wa Pakistan,Asif Ali Zardari, ambaye amekuwa na wakati mgumu tangu achukue ofisi kama rais wa Pakistan, na hasa kwa kuchelewa kumrudisha ofisini jaji Iftikhar Chaudhry kama jaji mkuu.
Picha ya tatu, wanaonekna baadhi ya wanchi wa Pakistan, wakifuatilia kwa makini hali ya kisasa nchini mwao, kwa kupita magazeti.
Madagasca yapata rais mpya."Achukua ofisi akiwa kijana wa miaka 34".
Antananarivo, Madagasca-Mahakama nchini Madagasca,imepitisha Andy Rajoelina kuwa rais wa Madagasca, siku moja baada ya kupewa madaraka ya kuwa rais wa nchi hiyo.
Andy Rajoelina, amechukua madaraka, baada ya rais, Marc Ravolamanana , wa Madagasca kulaumiwa ya kuwa hakutimiza matakwa ya kidemikrasia na kurazimishwa kujiuzuru kutoka madarakani.
Picha hapo juu anonekana, rais mpya wa Madagasca Andy Rajoelina, akiongea na wananchi mapema kabla ya kuteuliwa kuwa rais mpya.
Picha ya pili, anaonekana rais, wazamani wa Madagasca, Marc Ravolamanana, akiongea na wananchi,mapema kabla ya kulazimishwa kuondoka ofisini kama raisi.
Urussi kuongeza nguvu za kijeshi ifikapo mwaka 2011.
Moscow, Urussi- 18/03/09.Rais wa Urussi, Dmitry Medvedev, ameagiza ongezeko la kujenga na kuimarisha nguvu za kijeshi la Urussi lifanyike ili kukabilina na ongezeko la nguvu za NATO.
Tamko hilo, limekuja baada ya kuongezeka kwa ukubwa wa jumuia ya NATO, kwa kufatia baadhi ya nchi zilizo kuwa katika jumuia ya shikisho la nchi za Urussi, kujiunga na NATO na nyingine zipona mpango wa kujiunganga na jumuia ya NATO.
Kwa mujibu wa agizo hili,limesema ni lazima ifikapo 2011, jeshi la Urussi liwe na uwezo wa kiteknolojia na nguvu za kijeshi za kisasa.
Picha hapo juu, anaonekna rais wa Urussi,Dimitry Medvedev, akiongea na moja ya wakuu wakijeshi wa Urussi mapema hivi karibuni.
Czeck yakaata ardhi yake kutumika kujengea mitambo ya kijeshi.
Prague,Czeck-18/02/09.Serikali ya Czeck imetangaza kusimamisha mpango wake wakuirusu serikali ya Amerika, kujenga mitambo ya kunasia mawasiliano na mitambo mingine ya kijeshi.
Akiongea hayo, waziri mkuu wa wa Czeck,Mirek Topolanek, alisema kuamua kusimamisha mpango huo kwani, mswada huo utakataliwa endapo litapelekwa katika bunge.
Picha hapo juu anaonekana,waziri mkuu wa Czeck, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.
Papa awaomba watu kubadilisha tabia zao.
Yaounde,Kameroon-17/03/09.Papa Benedict wa XVI, amewasili nchini Kameroon, ikiwa ni moja ya ziara yake katika bara la Afrika.
Katika ziara yake alisema yakuwa, aliaagizia jamii kujiepusha na uzinzi, kwani maatumizi ya kondom (Mipira ya kuvaa kabla ya kufanya mapenzi) haisaidi kuepusha kuenea ukimwi.
Lalazima ni watu kubadilisha tabia, na kungoja hadi hapo watakapo oa au kuolewa.
Baada ya ziara nchini, Kameroon. Papa Benedict ataelekea nchini Angola.
Picha hapo juu, anaonekana, Papa Benedict, akiwasalimia watu waliokuja kumlaki wakati alipokuwa akitembea kuwasalimia wanachi wa Kameroon.
Picha ya pili, anaonekna rais wa Kameroon, Paul Biya, akimkaribisha, Papa Benedict wakati alipo wasili nchini Kameroon.

Sunday, March 15, 2009

Nawaz Sharif avunja amri ya kifungo"Aongoza maandamano".

Mawaziri wa fedha wakutana kujadili hali ya uchumi wa dunia. London,Uingereza - 15/03/09.Mawaziri wa nchi 20 zenye uchumi mzuri, wamekutana nchini Uingereza li kujadili hali halisi ya kiuchumi na kuhaidi kuokoa dunia na tatatizo ya kifedha. Kwa mujibu, wamkutano huo,mawaziri hao wameamua kwa pamoja yakuwa watasaidiana kuinua masoko ya dunia li kuepuka zaidi matatizo ya baadaye. Picha hapo juu wanaonenaka mawaziri wa fedha wa nchi 20, zenye uchumi mzuri walipo kutana mjini London ili kujadili hali halisi ya kiuchumi ya duniani na kutoa uamuzi bora. Hali ya siasa, nchini Madagasca ni tete"Rais akubali kura za maoni". Antananarivo, Madagasca - 15/03/09.Rais wa Madagasca, Marc Ravalomanana, ametangaza ya kuwa yuko tayari kuitisha kura ya maoni nchini humo, ili kumaliza mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo. Rais, Marc Ravalomanana, aliyasema hayo mbele ya watu wapatao 5,000,kwenye ikulu ya nchi hiyo. Hata hivyo , kiongozi wa wa chama cha upinzani nchini humo, Andy Rajoelina,amemtaka rais Marc Ravalomanana, aachie madaraka, kwani amshindwa kuongoza nchi kwa kufuata misingi ya kidemokrasia, na anaongoza nchi kinyume na sheria na kuwa dikteta. Picha hapo juu wanaonekana,baadhi ya wanajeshi wakiwa katika doria,baada ya kuchukua madaraka ili kutuliza ghasia. Picha, ya pili anaonekana, rais Marc Ravalomanana, akiwahutubia watu walio kuja kumsikiliza, kuzungumzia swala la kisiasa nchini humo ambalo lipo tete. Wafanyakazi wa shirika la misaada waachiwa huru. Darfur,Sudan - 15/03/09.Wafanyakazi wa shirika la madokta wasio na mipaka(MSF) Medicins Sans Frontires, ambao tekwa nyara siku siku ya jumatano, wameachiwa huru. Wafanyakazi hao wananao tokea nchi za Itali na Kanada waliachiwa jana kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Sudan Kwa kudhibitisha, maelezo hayo ya seikali ya Sudan, msemaji wa (MSF) linalo tokea nchini Ubeligiji ,Erwin van t'Land, alisema ya kuwa ni kweli wafanyakazi wenzao wamaachiwa huru. Picha hapo juu, yanaonekana makazi ya wakimbizi wa ndini wa Sudan, ambo ni wanachi wa Sudan, wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo, na msaada mkubwa wa matibabu umekuwa ukitolewa na mashirika haya ya kimataifa. Nawaz Sharif, avunja amri ya kifungo."Aongoza maandamano".

Lahore, Pakistan, -15/03/09. Kiongozi wa chama kukubwa cha upinzani nchini Pakistan, Nawaz Sharif, amevunja amri ya aloyo wekewa ya kifungo cha ndani, baada ya ya kuongoza maandamano kuelekea mjini mkuu wa Pakistan Islamabad.
Bwana, Nawaz Sharif, ambaye ni kiongozi wa chama cha Pakistan Muslim League Nawaz (PML-N) anaongoza watu wapatao 10, 000, kuelekea mjini Islamabad, watasimama katika vijiji tofauti na miji kabla ya kufika jiji Islamabad. Maandamano haya yanafanyika kuunga mkono madai ya wanchi wanao dai yakuwa aliyekuwa jaji mkuu wa arudishwe kazini,kwani ilikuwa ni moja ya makubaliano na ahadi zilizo tolewa na serikali iliyopo madarakani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Picha hapo juu anaonekna , Nawaz Sharif,akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuanza kuongoza maandamano kuelekea jijini Islamabad.
Picha yai pili, wanaonekna baazhi ya watu wakipambana na polisi,wakati wa maandamano yanayo endelea karibu nchi kote Pakistan.
Picha ya tatu wanaonekana mamia ya wanchini wakiwa njiani wakitokea Lahore, kuelekea jijini Islamabad, huku wakiongozwa na na Nawaz Sharif.
Vikwazo kwetu ni mchezo wa kitoto"Asema rais wa Iran".

Tehran,Iran - 14/03/09.Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amesema kuendelea kuwekewa vikwazo kwa nchi yake ni mchezo wa kitoto,kwani hakutazuia nchi kundeleza utaalamu wa kutumia nguvu za nyuklia kwa ajili ya matumizi ya umeme na teknolojia.

Rais, Mahmoud Ahamadinejad, aliyasema hayo wakati walipo kuwa akizindua mtambo mpya wa kutengeneza nguvu za gasi uliopo kusini mwa Pars nchini Iran.

Maelezo haya ya rais wa Iran, yalikuja mara baada ya rais, wa Amerika Baraka Obama, kutangaza ya kuwa Amerika itaiwekea Irana vikwazo zidi kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.

Picha hapo juu anaonekana rais wa Irana , Mahmoud Ahmadinejad,akihutubi wakati wa uzinduzi wa mtambo mya wa gasi, kwenye mji wa Pars nchini Iran..