Tuesday, December 30, 2014

Marekani yataka nguvu za kijeshi kutumika nchini JD Kongo.
 

Kinshasa, JD ya Kongo - 30/12/2014. Wanajeshi wa umoja wa mataifa waliopo nchini JD Kongo, wametakiwa kutumia nguvu za kijeshi, ikiwa kundi la apiganaji wa DFLR ( Democratic Force for the Liberation of Rwanda) litashidwa kusalimisha siraha walizo nazo itakapofikia January 2.

Russ Feingold, ambaye ni mwakilishi wa Marekani katika ukanda wa Maziwa makuu amesema "
"Ikiwa kutatokea ucheleweshaji wa kukabidhisha siraha, kundi la DFLR ndilo litakalo faidika, huenda wakazitumia siraha hizo katika ukiukaji wa haki za binadamu. 

"Hivyo  jeshi la umonja wa mataifa - MUNUSCO, lipo tayari pindipo hili nilisemalo litatokea ili kukabiliana na kundi hilo, na napenda hili lieleweke kuwa nguvu za kijeshi zitatumika."

 Kundi la DFLR ambalo ni la Wahutu wenye mlengo mkali na wanaopingana na serikali ya Kigali, wamekuwa wakishutumiwa kwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na inaaminika bado kuna wapiganaji 1400  ambo bado wanashirikiria siraha zao.

 Iran yadai haita buruzwa katika mazungumzo ya kinyulia.
Tehran, Iran - 30/12/2014. Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zalif, amesemakuwa Iran itasimama imara katika majadiliano yake kinyuklia  yatakayo anza 15/01/2015.

Akiongea Javad Zalif alisema " bado kuna upana ambao unatakiwa kipunguzwa katika mazungumzo hayo. Hatupo tayari kusukumwa sukumwa.

"Tutakuwa Imara kama mwanzo na la muhimu ni kuhakikisha vikwazo vyote vinaondolewa kama tulivyo sema hapo awali. Nakama hakutakuwa na makubaliano, Iran ipo tayari kwa hali na mali kukabiliana na lolote litakalotokeo."

Mazungumzo hayo ya Iran na mpango wake wa kuendelea na muzalisha nyuklia yanangojewa, kwani matokeo ya katika mkutano huo yanaweza badirisha sura ya dunia katika ulimwengu wa kinyuklia.
 
Mazungumzo ya kinyuklia ya Iran  yanajulikana kamaya nchi 5+1 ambayo yanajumuisha Urusi, Marekani, China, Unigereza na Ufaransa. 

Uingereza kupingwa muswaada wa Wapelestina UN.
New York, Marekani - 30/12.2014. Uingereza imetamka kuwa itapinga muswaada wa Wapalestina  walio uwakilisha umoja wa mataifa, ambao unaitaka Izrael kusimamisha chukuaji wake wa ardhi ya Wapelestina kinguu, na kurudisha maeneo yote wanayo miliki Waizrael.

Mark Lyall, ambaye ni balozi wa Uingereza wa Umoja wa mataifa ameseama kuwa " jibu la Uingereza ni hapana kwa muswaada huo.

"Kwani lugha ambayo imetumika inaleta walakini, hasa kuongezeka kwa lugha ya wakimbizi, na hivyo kunaugumu katika sualazima la hali hiyo."

Matamshi hayo ya Uingereza, yamekuja baada ya hapo awali Marekani kutamka kuwa inapinga muswaada huo wa Wapalestina kwa kuwa haukuelezakuhusu usalama wa Izrael

Muswaada wa Wapalestina umekuwa ukipigiwa chepuo na Jordan, ambapo  inataka kura ya kupitisha muswaada huo ipigwe siku ya Alhamis, jambo ambalo kwa sasa linaelekea kuwa na ugumu. Kwani Uingereza na Marekani zaweza tumia kura zao za vito kupinga muswaada huu.
 


Talibani waikejeli NATO.

Wapalestina wawakilisha muswaada wao uhuru umoja wa Mataifa

New York, Marekani - 29/12/2014. Jumuiya ya nchi za muungano wa Kiarabu, zimekubaliana kwa pamoja muswaada uliyo letwa na serikali ya Wapelestina kwenye umoja wa mataifa, ambao unataka Izrael kusitisha vitendo vyake vya kuchukua ardhi ya Wapalestina kinguvu, na kutoka katika maeneno yoye iliyo yachukua kinguvu ifikapo 2017, jambo ambalo Marekani na Izrael zimepinga.

"Ni suala la kuwaunga mkono Wapalestina ni muhimu, na ndio maana nchi za muungano wa nchi za Kiarabu zimeunga mkono muswaadahuo.
Alisema balozi wa Dina Kawar, ambaye ni balozi wa Jordani wa Umoja wa Mataifa.

"Kutakuwa na mazungumzo na wajumbe wa Palestina, nini kifanyike na lini kura zipigwe, ili kupitisha muswaada huo." aliongezea Kawar

Muswaada huo wa Wapalestina, ulipingwa na Marekani na Izrael, kwa madai kuwa hauelezei kuhusu hali ya Amani ya Izrael.

Hata hivyo wajumbe wa Palestina wamesema kuwa katika muswaada huo, lipo suala la majadiliano ya miji ya West Bank, Mashariki ya Jerusalem na Ukanda wa Gaza, miji ambayo michoro yake ya kiramani ilibadirika baada ya vita vya Mashariki ya Kati vya 1967.

Hatung'oi buti nchini Sudani ya Kusini, asema raia Museven.

Kampala, Uganda - 29/12.2014. Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseven, amesema kuwa jeshi la Uganda litaondoka nchini Sudani ya Kusini pindipo Amani ya kudumu itakapo patikana.

Akiongea kuhusu hali ya Amani ya Sudani ya Kusini, rais Museven alimeam, "tatizo si la  Uganda, tatizo ni Amani ya kudumu inayo takiwa nchini Sudani ya Kusini.

Kunatakiwa hali ya utulivu na Amani iwepo, kwani jeshi la Uganda haliwezi ondoka na kuachia mwanya wa vurugu kurudia.

Serikali ya Uganda iliamua kupeleka jeshi lake nchini Sudan ya Kusini, baada ya kutokea mvutano wa madaraka kati ya rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar, jambo ambalo lilileta kuvurugika kwa Amani.

Hata hivyo Riek Machar, amekuwa akidai kuwa jeshi la Uganda linatakiwa kuondoka nchini Sudani ya Kusini,kwa kuhisi kuwa lina unga mkono utawala wa SPLM uliopo chini ya raia Salva Kiir.

Talibani waikejeli NATO.

 
Kabul, Afghanistani - 29/12.2014. Kundi la Taliban la Afghanistan limekejeli  kuondoka kwa NATO ni dalili ya kushindwa kwao, na kwamba kundi hilo ndilo lililo ibuka na ushndi, baada ya kampeni ya kivita iliyochukua miaka 13.

"NATO na washiriki wake wamekunja bendera katika mazingira ya kushindwa, na kukabidhi madaraka ya kiulinzi kwa serikali ya Afghanistan, ni jibu kuwa Taliban wameshinda, kwani mpaka leo sisi bado tupo. Alisema msemaji wa Taliban Zabihulla Mujahid.

"Na Kuanzia sasa Taliban itashika usukani, na wale waliofikiliwa kuachiwa madaraka watashughulikiwa kama tulivyo lishughulikia jeshi la NATO na washirikia wake na sasa wanakimbia." Aliongezea  Mujahid.

Vita zidi ya kundi la Taliban vilianza mwaka 2001, vikiwa na madhumuni ya kuungamiza utawala wa Taliban, na kusababisha vifo wanajeshi karibu 3,500, na pia kuleta hasara kijamii nchini Afghanistan na watu wengi kupoteza maisha yao.

 

Monday, December 22, 2014

Muhammad Ali alazwa hospitalin.


Obama alaani mauaji ya Polisi.



New York, Marekani - 21/12/2014. Rais wa Marekani Barack Obama amelaani mauaji ya polisi wawili katika jiji la New York, ambao walikuwa wakishika doria ndani ya gari lao. 

Kamishna wa polisi wa New York Bill Bratton, amesema "Ismaaiyl Brinsley, mwenye umri wa miaka 28, aliwapiga risasi kichwani polisi hao bila kuwepo onyo lolote. Na kabla ya hapo Brinsley ambaye anaasili ya kiafrika, alimpiga risasi mchumba wake wazami kabla ya kuwauwa  polisi hayo wa mji wa Brookyl."

Mauaji ya polisi hao wawili, yametoke,  wiki chache baada ya  maandamano ya watu wenye hasira, kupinga vitendo vya polisi kuhusika na matukio ya polisi kuwauwa watu weusi ambao hawakuwa na silaha. 

Ismail Brinsley alijiua mwenyewe kwa risasi baada ya kukimbilia kwenye kituo cha treni zinazopita chini ya ardhi. 

Polisi imesema alikuwa ameweka ujumbe kwenye mtandao wa wake kuwa alipanga kuwauwa "nguruwe" wawili kama hatua ya kulipiza kisasi kifo cha Eric Garner, Mmarekani mweusi aliyeuawa kwa kukabwa koo na polisi.

 Rais wa Misri amfuta kazi Mkuu wa ujasusi

Kairo Misri - 21/12/2014. Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi leo amemfukuza kazi mkuu wa upelelezi  Jenerali Mohamed Farid el- Tohamy aliyeteuliwa siku chache tu baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani Mohamed Mursi mwezi Julai mwaka jana. 

Jenerali Khaled Mahmoud Fuad Fawzy ambaye alikuwa msaidizi wa Farid el Tohany ndiye aliyeteuliwa kuchukua nafasi yake. 

Hata hivyo hakuna sababu zozote zilizo elezwa za kufukuzwa kazi kwa Jenera Farid el 
Tohan.

Wakati huo huo, Misri leo imekifungua  mpaka wa Rafah, ambao utawawezesha  wakazi wa Ukanda wa Gaza, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miwezi miwili kuweza kuingia na  kutoka Misri. 

Misri ilifunga mpaka wa kuingia Gaza, Oktoba 25 baada ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu katika eneo la Sinai kuwauwa wanajeshi wake 33.




Marekani  kuchunguza uvamizi wa mtandao wa Sony.


Marekani ,Washington -21/12/2014 Rais wa Marekani Mabaka Obama, amesema kuwa Marekani inachunguza ili kuweza kujua kama Korea ya Kaskazini inahusika na ushambuliaji wa mtandao wa Sony, na kama ikigundulika ilihusika, basi hatua za kisheria zitachukuliwa.

Obama alisema, "tunalianagalia hili  suala la kushambuliwa kwa Kampuni ya Sony kwa makini, nakuwa kila sheria ya kukabiliana na jambo hili zipo tiyari.

"Kwani hatufanyi maamuzi kwa kupitia vyombo vya habari, bali ukweli utakapo patikana basi sheria zitafuata."

Mazungumzo hayo ya rais Obama yamekuja  baada ya Korea ya Kaskazini kukanusha kuhusika na mashambulizi ya kimtandao kwa kampuni ya Sony, na kuitaka  Marekani  kuonyesha ushirikino ili kulitafutia ukweli suala la uvamiaji wa mtandao wa kampuni ya Sony.  


Muhammad Ali alazwa hospitalini.

 

Kentaki, Marekani - 21/12/2014. Aliyekuwa bingwa  ndondi kwa uzito wa juu duniani Muhammad Ali  mwenye miaka 72, amelazwa katika hospitali ya mji wa Loiseville ili kutibiwa  homa ya mapafu. 

Bob Gunnell, ambaye ni msemaji wa Ali, alisema " Ali anatibiwa na kundi la madaktari wake na yuko anaendelea vyema.

Mohammed Ali, ameshakuwa hospitali kwa siku moja na anatarajiwa kuruhusuhusiwa kutoka hopitalini baada ya Madaktari kulidhika na mwenendo wa afya yake .



 


 


 

Saturday, December 20, 2014

Liberia yasifiwa na Ban Ki-moon zidi vita vya Ebola.


Nchi za Africa zatakiwa kushirikiana na mahakama ya ICC.



Mahakama kimataifa inayo shugulikia makosa ya jina (ICC)  imeanza mkutano wake wa siku tatu, jiji New York,Marekani,  ambapo umeghubikwa na mfukuto wa kwanini mahakama hiyo imekuwa ikiiandama bara la Afrika tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo mwaka 2002.

Akiongea katika ufunguzi huo rais mpya wa Baraza la mataifa wanachama wa ICC, Sidiki Kaba, ambaye ni Waziri wa sheria wa Senegal,Alisema " Naomba kuwepo na ushirikiano barani  Afrika, ili kubadili mawazo potofu yanayo haribu mahakama hiyo ya ICC.

"Nana penda  kusisitiza kwamba malalamiko ya nchi wanachama  yanapaswa kusikilizwa, na kutafutiwa ufumbuzi." Aliongeza Kaba.


Mkutano huo ambao unajumuisha nchi wanachama 122, Pia uliudhuliwa na wajumbe kutoka Palestina ambapo walikubaliwa rasmi kuwa waangalizi katika mkutano.

 Na kwa mujibu wa Mahakamaya ICC  uamuzi huo wa kuruhusu kuwepo kwa Wapalestina ni hatua moja muhimu ambayo inafungua njia kwa Wapalestina  kujiunga kama mwanachama kamili wa mahaka hiyo ya uhalifu ya kimataifa.



Liberia yasifiwa na Ban Ki-moon zidi vita vya Ebola.


Serikali ya Liberia, imepongezwa kwa juhudi zake katika kupambana na ugonjwa wa Ebola, Pongezi hizo zilitolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban KI-moon, ambaye yupo nchini humo ili kuona ni hatua gani zimefikiwa katika kupambana ugonjwa wa Ebola.


Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Ban Ki-moon kutembelea Liberia, tangu ugonjwa wa Ebola ulipozuka ambao hadi sasa umeshaua watu zaidi ya 7000 katika eneo zima la Afrika ya Magharibi.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya kuiuzuru Irak. 

Mkuu wa  kitengo kinacho  shughuli masuala ya  kigeni ya Umoja wa Ulaya  Federica Mogherini anatazamiwa kuizuru  Iraq  wiki ijayo  kwaajili ya kufanya  mazungumzo na  viongozi wa serikali na pia kukutana na viongozi wa  serikali ya Kikurdi.

Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema  kuwa Mogherini  atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri mkuu Haider Al-Abadi,  na baadaye  siku ya Jumanne atakuwa na mazungumzo na rais wa jimbo la Kurdi, Masoud Barzani katika mji wa Irbil.

Ziara hiyo za Mogherini itakuwa na madhumuni ya kuona ni kwa jinsi gani  Umoja wa Ulaya, utasaidia katika kupambana na kundi na dola la Kiislaam ,  ambapo hadi sasa Umoja wa Ulaya  umeshatoa  euro milioni 20 kusaidia kutatua matatizo ya kiutu ambayo yamesababishwa na kundi hilo wapiganaji wa IS wanaoshikiria maeneo kadhaa nchini  Iraq.


Waziri Frank Walter Steinmeier aonya kuhusu Urusi.


Waziri wa mambo ya nje ya nchi  wa  Ujerumani Frank Walter Steinmeier,ameleezea wasiwasi wake kuhusu msukumo uliyopo wa  vikwazo kutoka kwa nchi wanachama wa nchi za umoja wa Ulaya kuwa  hutahatarisha na kuiyumbisha Urusi, ambapo wimbi lake litaleta mtikiso katika bara la Ulaya.

Walter Steinmeier alisema kuwa, kushuka kwa tahamni ya Lubo, fedha inayo tumika Urusi, hakutakuwa na faida kwa nchi za Ulaya, hivyo ni bora kuwepo na uangalizi katika sheria za kuweka vikwazo kwa Urusi.

Mazungumzo hayo ya Steinmeier, yamekuja baada kikao cha wakuu wanchi za jumuiya ya Ulaya, kuionya Urusi kuwa kama haitabadiri msimamo wake dhidi ya Ukraine, nchi za Umoja wa Ulaya hazita sita kuongeza  vikwazo zidi ya Urusi.




Thursday, December 18, 2014

Uimara wetu ndio kitisho kwa wapinzani asema rais Vladmir Putin.

Wabunge nchi Kenya watwangana.

Nairobi, Kenya - 18/12/2014. Wabunge nchini Kenya, wametwangana na kutupiana usoni nyaraka zilizo andikwa muswaada  wa kiulinzi na kiusalama kwa madai kuwa unakwenda kinyume na haki za wananchi Wakenya.

Vurugu hiyo ambayo ilianzishwa na wabunge wa kundi la upinzani, kwa kudai kuwa kupitishwa kwa muswaaada huo, kutafanya nchi ya Kenya kuwa taifa la kipolisi.

"Muswaada huu utafanya uhuru wa Wakenya kuwa hatarini, na watakao faidika ni matajiri ambao wapo na karibu na serikali tawala ya Jubilee."  Alisema Moses Wetangula, kiongozi wa wabunge wapinzani.

Sheria hii iliyopitishwa, imewapa uwezo maafisa usalama kuwa na uwezo wa kuwaweka kizuizini washukuwa wa ugaidi kwa kipindi cha mwaka mmoja, kurekodi mawasiliano na kufatilia nyendo za uandishi wa habari na pia kuwawekea vizuizi katika kazi zao za kiandishi.

 Muswaada huo wa kiusalama na kiulinzi, umepitishwa kutokana na kuongezeka kwa mashambuliz ya kigaidi nchini Kenya kutoka kwa kundi la Alshabab ambalo ni mkondo wa kundi mama la Alqaeda.

 Uimara wetu ndio kitisho kwa wapinzani asema raia Putin.

Moscow, Urusi - 18/12/2014. Rais Vladmir Putin, ametangaza kuwa kushuka kwa thamani Lubo, fedha ambayo inatumika nchini Urusi, kunasababishwa na  myumbo wa uchumi wa kimataifa na kuwa uchumi wa nchi hiyo utakuwa imara baada ya miaka miwili.

Akionya rais Putini alisema "Japo vikwazo vilivyo wekwa na nchi za Ulaya na Washiriki wake vinachangia, Urusi kama taifa tutaweza imarisha uchumi wetu na tupo imara hakuna wa kututishia wala wa kutuyumbisha."

Kuhusu suaa la Ukraine na Crimea, rais Putin amehaidi kuwa Urusi haita yumbishwa na itabaki na msimamo wake ambao iliiuweka toka awali.

Kwenye mkutano huo wa Rais Putin, waandishi wa habari 1200 waliudhuria. Na ni wa kwanza  kwa tangu thamani ya pesa ya nchini hiyo kushuka ghafla katika masoko ya kifedha. Jambo ambalo limesababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta, ambayo huwa yanachangia kwa kiasi kikubwa cha uchumi wa Urusi.
  
Wapiganaji wa M23 watoroka kutoka katika kambi ya jeshi nchini Uganda. 

Kampala, Uganda - 18/12/2014.Wapiganaji 1000 wa kundi la M23 waliokuwa katika kambi ya kijeshi ya Bihanga nchini Uganda, wametoroka baada ya ya kudhainia kuwa hali ya usalama wao ni mdogo pindipo watakapo rudishwa nchini JD Kongo.

Akiongelea kuhusu kutoroka huko, Bertrand Bisimwa, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi la M23, alisema "Wapiganaji hao walikimbia  baada ya kukataa kupanda lori la kijeshi ambalo lilikuwa tayari kuwapeleka uwanja wa ndege ili kuelekea makwao, jambo ambalo lilifanya wanajeshi wa Uganda kufyatua risasi na kuwaumiza baadhi ya wapiganaji wa M23."

Kitendo cha kuwarudisha kwa nguvu wapiganaji wa M23 nchi JDKongo ni kukiuka masharti ya amani yaliyowekwa hapo mwanzo wa makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini KOngo."Added Bisimwa.

Hata hivyo msemaji wa wa jeshi la Uganda Kanali Paddy Ankunda, amesema kwa kupitia mtandao wa twitter kuwa jeshi la Uganda lipo linawasaka wapiganaji hao wa M23 ambao wamekimbia.

Kufuatia kukimbia huko kwa wapiganaji 1000 wa M23, kumekuwa ma wasiwasi kuwa huenda wapiganaji hao wakarudi na kujiunga na baadhi ya makundi ambayo bado yanapingana na jeshi la serikali la JC Kongo.