Mmmhh mambo bado magumu uwanja wa nyumbani.
Waasimu wawili wa jadi Liverpool na Arsenal, hivi karibuni,walitoka suruhu 1-1, hivi karibuni walipo pambana nyumbani kwenye uwanja wa Liverpool.
Baadhi ya wachezaji walilizika na suruhu hiyo, kwani mpambo huu mpaka kipyenga cha mwisho ilikuwa vigumu kuamua ni nani ataibuka mshindi.
Mlinzi wa Liverpool Jamie Carragher, amesema kunahaja ya timu yao kutafuta dawa kutibu, tatizo hili la kushindwa kushinda uwanja wa nyumbani, aliongeza kwa kusema wapinzani wao Arsenal walikuwa wanonekana kila kona ya uwanja, hali hii iliwauiwa vigumu kuweza kushinda mpamabano huu.
Pichani hapo juu ni ma timu kochi wakiwa na sura tofauti za kuhimiza vijana wakaze kamba.
Kulia ni Arsene Wenge, akitumia mikono kupiga makofi kukumbushia stahili fulanai ambayo inaelekea vijana wamesahahau, na kushoto ni bwana Rafael Benitez akichungulia kwa makini jinsi gani vijana wanavyo menyana kulinda hadhi yao uwanja wa nyumbani, kwani wageni wa Arsenal wanapamba motoooooo.
Moroko kupata nguvu za Kinyuklia hivi karibuni.
Serikali ya Ufaransa imetangaza rasmi yakuwa itaanza hivi karibuni kuisaidiaserikali ya Morroko kujennga mitamabo ya kutoa nguvu za kinyuklia, kwa ajili ya kungeza ufanisi katiak nyanja za nishati na teknolojia,.
Akitangaza rasmi alipo zuru hivi karibuni nchini Moroko, rais wa Ufaransa bwana Nicolas Sarkorzy, alisema ushirikano uliopo kati ya Moroko na Ufaransa ni wa kufaakuigwa ili kuleta maendeleo kijamii duniani kote.
Pichania ni mfalme wa Moroko Mohamed VI akijiandaa kumpokea rais wa Ufaransa bwana Sarkorz.
Uchaguzi nchini Kenya waja kwa vishindo ya uzawa wa maeneo.
Wannchi wa Kenya , watafanya uchaguzi wao mwaka huu 2007, mwezi wa desemba tarehe 27.Matamshi yahaya yalitolewa hivi karibuni na rais wa jamuhuri ya Kenya bwana Mwai Kibaki.
Rais Kibaki, atashiriki katika kugombani akuchaguliwa kuwa rais kwa awamu ya pili, huku atachuana na wapinzani wake mkubwa, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, aMchungaji Pius Muiru.
Kutokana na wachunguzi wa uchaguzi huu na hasili ya mgombea ndiyo inaangaliwa sana, hasa kutokana na vyama vikuu ambavyo wanachama wake wanavutana. Bwana Kibaki akiongoza chama kijulikanacho kama Part of National Unity(PNU) na wachama wake wengi ni watu wa kabila la Kikiyu.
Bwana Odinga ataongoza chama kijulikanacho kama Orange Democrqatic Movement ( ODM), ambaye asili yake ni kutokea kabila la Waluo.
Rais Putin nitakuwa waziri mkuu, kama tukishinda.
Rais wa Rusia bwan Vladamir Putin, ametangaza ya kuwa atakuwa waziri mkuu wa Rusia baada ya kumaliza muda wake kama rais wa Rusia.
Bwana Putin alisema haya alipo kuwa akiongea kwenya mkutano wa chama,United Russia.
Aliendelea kwa kusema atakuwa mstari wa mbele katika kampeni za uchaguzi utakao fanyika hivi karibuni.
Hapo juu pichani ni bwana Putin akiongea hivi karibuni.
Rais Mugabe nitaudhuria mkutano wa Ureno, wabaya wetu ni Uingereza
Rais wa Zimbabwe bwan Robert Gabriel Mugabe, amesema yakuwa atahudhuria mkutana kati ya viongozi wa bara la Afrika na Ulaya utakao fanyika Lisbon Ureno, mwishoni mwa mwaka huu.
Aliyasema haya hivi karibuni alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, alisifu viongozi wa SADC kwa kuwa kidete kupinga shinikizo la umoja wa Ulaya ya kuwa nani awepo na nani asiwepo,pia aliongeza ya kuwa kuna mambo mengi ambayo hayapendezi kwe jamii ya kima mataifa na hakuna,siku moja wamesha shinikizwa kuchagua nani aahudhulie kwenye umoja wa mataifa.Bali utaona dunia ina kaa kimya tu.
Aliongeza kwa kusema, Zimbabwe inamatatizo na serikali ya Uigereza, kwani serikali ya Uingereza imekataa kukamilisha mikataba waliyowekeana na serikali ya Zimbabwe, kuhusu matatizo ya ardhi.Na Zimbabwe haina matatizo na Ulaya yote
Hakukuwa na mikakati imara, ya kukabiliana na mabadiliko nchini Irak.
Maneno ya waziri mkuu amstahafu wa Uingereza bwan Tony Blair, siku tano tu baada ya kuanguka kwa utawala wa Saddam Huseein, ya kuwa Irak, itakuwa pahali pa usalama na bora kwa wa Irak na eneo zima kwa ujumla. yameoneka kupingwa na wadadisi wa mambo. Hii imetokana na hali halisi iliyopo nchni Irak kwa sasa.
Kwani kuanza kwa vita vya Irak, miaka minne iliyo pita hadi sasa, ni kitu ambacho Washington ,a London, hawakutegemea ya kuwa vita hivi vinge sumbua kwamuda mrefu,haya ni maelezo ya mmoja wa wakosoaji wa vita vya Irak aliyasema hivi karibuni.Akiongezea kwa kusema ya kuwa
kuanza kwa vita, bila kufuata misingi iliyo wekwa toka enzi za Napoleon, ni makosa ambayo yalifanyika.
Kwani," Napoleon alisema usichukue hatua ya kwanza bila kujua nini kinafuata, au kupanga kukabiliana na na matokeo yake.
Msemaji huyu alisema yakuwa vita vya Irak, vilipangwa na kuvamia nchii hii, kwa kujua ya kuwa Sadam akisha toka madarakani wairak watasidia katiak kujenga nchi yao. Na hii hali iliyopo ya kuwepo na vikundi tofauti ambavyo vina hatarisha usalama wa Irak, hakikutarajiwa.
Pichani hapo juu, ni rais George Bush wa Amerika alipo tembelea UK na bwana Tony Blair wakati alipo kuwa bado waziri mkuu wa Uingereza,wakiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi nchini Irak.
Maneno ya mwisho ya Diana Malkia wa Wailes kabla ya kifo chake.
Shahidi ambaye alikuwepo wakati wa ajali ya Diana na Dodi El Feyed, amesema ya kuwa wakati alipo kuwa akisaidia katika kuokoa maisha ya Diana, alisikia Diana akisema Mungu wangu Mungu wangu mara kwa mara.
Shaihidi huyu ambaye anajulikana kwa jina bwana Damian Dalby,aliyasema haya alipo kuwa akitoa ushahidi, mbele ya wachungizi wanaochunguza ajali mbaya ambayo ilisababisha kifo cha Diana na Dodi El Feyed.
Ajali hiyo ilitokea jijini Paris, 31/Agusti/1997 kwenye daraja lijulikanalo kama Pont d'Alma.
Pichani hapo juu ni picha ya gari ambayo Diana na Dodi walipata nayo jali na kusababisha vifo vyao, ambavyo mpaka sasa bado kuna utata kuhusu ajali hiyo.
Mwandishi wa habari marufu atunikiwa nishani.
Mwanadishi wa habari na mtangazaji wa cnn, bi, Christine Amanpour, ametunukiwa nishani, na Malkia wa Uingereza kutokana na kazi yake anavyo ifanya kiadirifu.Zawadi hii ambayo ilianzishwa mwaka 1917 na Mfalme George V, kwaajili ya kuwatunukia watu amabo wamesaidia kuilinda na kupigania Uingereza wakati wa vita vya kwanza vya dunia.
Bi Christine Amanpour, alikuwa na tabasamu kubwa alipo pokea nishani hii, ambayo ina rangi za blue na msalaba wa dhahabu na michirizi ya rangi nyekundu,na una motoo KWA AJILI YA MUNGU NA MFALME.
Vilevile bi Christine ni moja ya waanzilishi wa cnn london ambayo imeanzishwa hivi karibuni.
Bi, Christine Amanpourni mmoja kati wa waandishi waliokuwa wakilipoti enzi za vita vya Bosnia na Elsagovina, vilivyo tokea ulaya mashariki,na ametangaza matukio mengi amabayo ya mejili hapa duniani.
Hapo juu bi Christine Amanpour akionyesha nishani aliyo pokea kutoka kwa malkia Elizabeth.
Belguim ya waonya wanunuzi wa almasi kwa magendo.
Msemaji mmoja wa mawakili hao amesema, ununuzi huu umekuwa ukisaidia kendelea kwa matatizo na vita vya wenyewekwa wenyewe, katika bara la Afrika kwa muda mrefu, na tunatarajia kukabidhi koti kesi hizi karibuni.
Kutokana na uchunguzi uliofanywa, imegundulika hivi karibuni,serikali ya Belguim., ilitaifisha kiasi cha faranga( Fedha) zipatazo Euro million 14, ambazo zilitokana na mauzo ya almasi haramu, amabazo zinaaminika zilitokea almasi hizi zilitokea nchini Ivory Coast, moja ya nchi ambayo vita vya wenyewe kwa wenyewe bado vinaendela, kuigawa nchi hiyo kataiak sehemu kubwa mbili.
Ajiunguza baada ya kuchoka na ubaguzi.
Hivi karibuni nchini, kwenye mji wa Luxenburg nchini Belguim, mwana mama mmoja,mwenye wototo watatu, alijimwagia mafuta aina ya petrol, na kujiwasha moto, kwa madai ya kuwa ubaguzi umezidi,mjini hapo.
Mwana mama huyo alijiwasha karibu na waandishi wa habari, na kuleta mshtuko mkubwa, mjini hapo, na hasa wakati wa maandamano hayo yalioandaliwa kuelezea hali hii ya ubaguzi inavyo wakela.
Hata hivyo, hivyo wafanyakazi wa zima moto na watu wa huduma ya kwanza waliwahi kufika na kuokoa maisha ya mama huyu, aliye julikana kama Maggy.D.Mufu.
Mwana mama huyu alikimbizwa kwenye hospitali ya Bon Secours mjini Metz , ambapo anaendelea na matibabu zaidi.
Hapo juu ni mwana mama Meggy alipo kuwa amejiwasha kupinga ubaguzi, mjini Luxenburg Belguim, na hapo wanaonekana watu wakijaribu kumvua nguo zake ili moto usimzuru zaidi.