Tuesday, November 29, 2011

Kenya yatoa kibali cha kukamatwa ria

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo apelekwa Hague.

Hague Uhollanzi 29/11/2011. Aliyekuwa rais wa Ivory Coast na ambaye alitolewa madarakani kwa nguvu Laurent Gbagbo amewasilishwa jijini Hague tayari kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Lucie Bourthoumieux ambaye ni mwanasheria wa wa rais huyo alisema " Laurent Gbagbo amesha pekekwa nchini Uhollanzi."
Gbagbo alifunguliwa mashitaka na mahakama inayo husika na "utetezi wa haki za binadamu na makoso ya jinai."
Hata hivyo msemaji wa Gbagbo Abdon George Bayeto alisema " hii siyo haki kwa kitendo cha kumpeleka Laurent Gbagbo Hague kwani tukumbuke alishinda kwa 48% na hii italeta myumbo wa siasa na amani kuwa tete kati ya wa Ivory Coast."
Laurent Gbagbo alitolewa madarakani na kundi la chama cha mpinzani wake Alassane Ouwattara ambaye ndiye rais wa sasa wa Ivory Coast.
Mganga aliyekuwa akimtibu Michael Jackson afungwa miaka minne.
Los Angeles, Marekani - 29/11/2011. Mahakama jijini Los Angeles imemuhukumu mganga Conrad Murray 58 aliyekuwa mtabibu wa Michael Jackson jela miaka minne baada ya kukutwa na kosa la kuua bila kukusudia.
Akitoa hukumu hiyo Jaji Michael Pastor alisema " Conrad alikuwa na wajibu wa kufatilia maadili ya kitabibu lakini hakufanya hivyo na hukumu hii ina mstahili kutokana na kosa hili."
Mganga Conrad Murray alikutwa na kosa hilo wiki tatu zilizo pita baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa zaidi ya wiki sita
Aliyefanya mauaji ya kutisha nchini Norway adaiwa kuwa anaugonjwa wa Akili
Oslo, Norway - 29/11/2011. Mahakama inayo shughulikia kesi zidi ya muuaji aliye uawa watu 77 nchini Norway imeamua awekewe mtu wa kuchunguza ugonjwa wa akili.
Uamuzi huo umekuja baada ya mwanasheria kutoa ripoti ya kuwa Anders Behring Breivik anaugonjwa wa akili na hivyo apelekwe kwenye nyumba inayo shughulikia wagonjwa wa akili ili kutazamwa zaidi.
Anders alifanya mauaji makubwa nchini Norway mwezi wa saba, wakati alipo kwenda kuwashambulia vijana waliokuwa kwenye mkutano wa chama cha Labour cha inchi hiyo.
Wanafunzi wavamia ofisi za Ubalozi wa Uingereza nchini Iran.
Tehran, Iran - 29/11/20. Kikundi cha wanafunzi vijana nchini Iran wamevaamia ofisi za ubaalozi wa Uingereza na kuchoma bendara na kuharibu maeneo na mafaili ya kiofisi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema " waandamanaji hao walitumia mabomu ya petrol, na kuchoma moto baadhi ya makaratasi ya kiofisi na huku wafanyakazi wa ofisi hiyo ya kibalozi ya Uingereza wakikimbia kuokoa maaisha yao."
Vijana hao walikuwa walisikika wa kisema "kifo kwa Uingereza, Izrael na Marekani na washiriki wake."
Serikali ya Uingereza imelaani kitendo hicho.
Hata hivyo polisi walifanikwa kuwatawanya vijana hao na kuhakikisha wafanyakazi waliokuwepo ndani ya jengo la ofisi hiyo ya kibalozi wapo salama.
Mahakama nchini Malasyia yawakuta na makosa Tony Blair na George Bush.
Kuala Lumpur, Malaysia 29/11/2011. Mahakama inayo shughulikia makosa ya kivita na ukiukwaji wa haki za binadamu iliyopo nchini Malaysia imewakuta waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair na aliye kuwa rais wa Marekani George Bush.
Kesi hiyo iliyo sikilizwa kwa muda wa siku nne kuanzia 19-22 Novemba kwenye mahakama ya Kuala Lumpur-The Kuala Lumpur War Crimes Tribunal or KLWCT, ilitoa uamuzi wake huo baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo iliyo letwa na wanasheria Gurdeal Singh Nijar na Francis Boyle, kwa kusema " tumewakuta na hatia Tony Blair na George Bush kwa kosa la kuondoa amani na kusababisha mauaji kutokana na vita vya Irak."
Hata hivyo katika kesi hiyo watuhumiwa hawakuweza kuwepo, ijapokuwa "mahaka imedai yakuwa watuhumiwa walipewa nafasi yakujitetea lakini hawakutokea wala kutuma wawakilishi wao."
Akiongea baada ya hukumu hiyo, mwanaharakati anaye pinga vita Mahathir Mohamed alisema " juhudi za mahakama zinazidi kuonekana na kukua ili kupambana na muundo mbinu wa kivita ambao umekuwa ukitumika vibaya na tutaendelea kupambana."
Mahakama hiyo ya Kuala Lumpur, imekuwa ikivilaumu vyombo vingine vya sheria kwa kushindwa kutekeleza sheria zinavyo sema, na kusababisha mashaka zidi ya jamii.
Kenya yatoa kibali cha kukamatwa rais wa Sudani.
Nairobi, Kenya - 29/11/2011. Serikali ya Kenya imetoa kibali cha rais wa Sudani kukamatwa pindopo atakanyaga nchini humo tena.
Akitoa kitambulisho hicho Jaji Nicolas Ombija alisema " rais Omar al Bashir atakamtwa ikiwa atakanyaga mguu wake nchini Kenya, kwani anahitajiwa na mahakama ya kimataifa iliyopo nchini uhollanzi ili kujibu mashitaka yanayo mkabili ya ukiukwaji wa haki za binadamu."
Uamuzi huo wa kutoa kibali cha kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar al Bashir umekuja baada ya mahakama ya kutetea haki za binadamu iliyopo nchi Uhollanzi, kuilaaumu serikali ya Kenya kw kushindwa kumkamata rais huyo wa Sudani wakati alipo tombelea Kenya mwezi wa nane 2010.

Tuesday, November 22, 2011

Luis Moreno-Ocampo awasili nchini Libya kwa mazungumzo.

Luis Moreno-Ocampo awasili nchini Libya kwa mazungumzo.

Benghazi, Libya - 22/11/2011. Mwanasheria mkuu wa koti ya kimataifa inayo husika na makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu amewasili nchi Libya ili kujadili na viongozi wa serikali ya mpito ni kwa jinsi gani kesi ya mtoto wa Muammar Gaddafi itaendeshwa.
Mwanasheria huyo Luis Moreno Ocampo alisema "huu ni mwanzo na wale wote ambao walio tenda makosa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria."
Luis Moreno Ocampo amewasili na msaaidizi wake Fatou Bensouda nchini Libya, huku serikalli ya mpito ikitaka kesi zidi Saif al-Islaam Gaddafi ifanyike nchini Libya, jambo ambalo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaa dai ya kuwa "hakutakuwa na haki katika kuendesha kesi, kwa kuzingatia mazingira yaliyopo."
Hata hivyo serikali ya mpito imesema "Saif al-Islaam atapata kila msaada katika kusikiliza kesi yake."
Saif al Islaam alikamatwa wakati akikimbia kutoka nje ya Libya hivi karibuni.

Monday, November 21, 2011

Viongozi wa upinzani wa serikali ya Syrria wakutana na serikali ya Uingereza.

Uispania yapata waziri mkuu mpya.

Madrid, Uispania - 21/11/2011. Chama chenye maadili ya mrengo wa kulia kimeshinda uchaguzi nchi Uispania.
Chama hicho People Party -PP, kimefanikiwa kupata viti kwa wingi kuliko vyama vingine vyenye idadi ya 186 kati ya 350 katika bunge.
Akihutubia baada ya ushindi huo, kiongozi wa chama hicho Mariano Rajoy 56, alisema " bado kuna wakati mgumu wa kuinua uchumi na hakutakuwa na maajabu na hivyo hakuna haja ya kuhaidi, na tutafanya kila njia kutatua matatizo yaliyopo."
Spain nchi ambayo inamatatizo makubwa ya ukosefu wa kazi, na zaidi ya million tano ya watu hawana kazi, wangi wao wenye umri kati ya miaka 25-46
Viongozi wa upinzani wa serikali ya Syria wakutana na serikali ya Uingreza.
London, Uingereza - 21/11/2011. Viongozi wapinzani wa serikali ya Syria wamekutana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza ili kujadili hali halisi ya kisiasa iliyopo nchini Syria.
Viongozi hao wa upinzani wamekuta na serikali ya Uingereza ili kuishinikiza serikaali ya rais Bashar al Assad, ili alete mabadiliko ya kisiasa nchini Syria.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alisema "Rais Assad lazima aelewe ya kuwa viongozi wa serikali ya upinzani wanatambulika na wapo tayari kuleta mageuzi."
Na utawala wa Assad utazidi kuwa na wakati mgumu kwani serikali nyingi zipo tayari kufanya kazi na viongozi wa upinzani." alimaliza waziri Hague.
Katika mazungumzo hayo, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria, aliwataka viongozi hao waige mfano wa viongozi wa upinzani wa Libya walioungana kumng'oa Muammar Gaddafi.
Syria imekumbwa na maandamano ambapo wananchi wanadai mabadiliko ya siasa lazima yafanyike na rais Assad ajitoe katika maadaraka.
Maandamano yafanya waziri mkuu kujiudhuru.
Kairo. Misri - 21/11/2011. Waziri mkuu anayeliongoza baraza la mawaziri wa serikali ya mpito wa Misri ameandika barua ya kujiudhuru kutokana na maamndamano yanayo endelea nchi humo.
Essam Sharaf aliandika barua hiyo na kuikabidhisha kwa kamati ya kijeshi ya nchi hiyo kufuatia mauaji ya watu 33 yaliyo tokea baada ya polisi na wanajeshi kupigina na waandamanaji wakati wa kutuliza ghasia.
Habari kutoka ofisi ya wizara ya afya zinasema " watu wapatao 33 wameuwawa na 1,500 kujeruhiwa tangu maandamano hayo yaanze hivi karibu."
Maandamano haya ambayo nimakubwa tangu kuangushwa kwa rais Husni Mubaraka, yaliitishwa ili kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko ya kisiasa haraka.
Kufuatia kujiudhuru huko kwa waziri mkuu ssam Sharaf, wasiwasi mkubwa umetanda nchi humo, kwani ni siku chache zimebakia kabla ya uchaguzi wa bunge kuanza.

Sunday, November 20, 2011

Rais wa Syria asema yupo tayari kufa kutetea nchi yake.

Jeshi la Ethiopia ladaiwa kuingia nchini Somalia.

Gurel, Somalia - 20/11/2011. Wanajeshi wa Ethiopia wameonekana wakiingia nchini Somalia kwa kutumia Maroli na baadhi ya magari ya kijeshi.
Mzee mmoja wa kijiji Abdi Ibrahim alisema "nimeona magari ya kijeshi na maroli yakiwa yamebeba wanajeshi wa Ethiopia kuelekea eneo linaloshikiliwa na Shebab lililopo Galgudud."
Hata hivyo serikali ya Ethiopia imekanusha uvumi huo.
Kuonekana huko kwa wanajeshi wa Ethiopia nchini Somalia kumekuja baada ya jeshi hilo kuivamia Somalia mwaka 2006 kwa masaada wa Marakani na baadaye kujitoa kwa kushindwa kuleta amani nchini Somali.
Rais wa Syria asema yupo tayari kufa kutetea nchi yake.
Dumascus, Syria - 20/11/2011. Rais wa Syria amehaidi kupambana na wale wote ambao wanavuruga amaani nchini Syria baada ya makao makuu ya chama tawala kushambuliwa na mabomu.
Rais Bashar al Assad alisema " nipo tayari kufa kwa ajili ya nchi yangu, na nitahakikisha ya kuwa wale wote wanao vuruga amani wamekamatwa na ikiwa tutashambuliwa na jeshi lolote kutika nje basi itakuwa hali ya kutisha katika eneo zima la nchi za Kiarabu."
"ajisikia vibaya saana napo ona damu za watu wa Syria zinamwagika kwa sababu ya kundi fulani ambalo linavuruga amani, hivyo nilazima sheria zifuatwe ili kuweza kuleta amani nchini Syiria."
Na uamuzi wa nchi za jumuiya ya Kiarabu kuisimamisha Syria uanachama ni moja yaa nchi ya kuidhinisha uvamizi wa kijeshi ambao utaleta maafa makubwa." alisema rais Bashar Assad.
Nazo serikali za Uturuki naa Marekani zimebashiri ya kuwa huenda kukawa na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchi Syria na huku Urussi ikisisitiza kuwepo na mazungumzo ya amani yaanze mara moja.
Kundi la FARC lapata kiongozi mpya.
Bogota, Kolombia -20/11/2011. Kundi la FARC linalo pingana na serikali ya Kolombia limetangaza jina la kiongozi mwingine baada ya kiongozi wao mkuu wazamani Alfonso Cano kuuwawa na jeshi la Kolombia.
Timoleo Jimenez 52 amechaguliwa kushika madara hayo kufuatia kuwawa kwa Alfonso Cano mapema mwezi wa November mwaka 2011.
Wakitangaza FARC walisema " Komredi Timoleo Jiminez amechaguliwa kwa hali moja kuwa kiongozi wa FARC."
Mkuu huyo mpya wa FARC alipata mafunzo ya kijeshi nchini Kuba na Urussi naa amekuwa katika kundi la FARC tangu 1970.
Kundi la FARC limekuwa likipigana na serikali ya Kolombia inatosaidiwa na Marekani na inaaminika FARC inawapiganaji wapato 20,000.
Alqaida wadai kufaidika na vita vya Libya.
Algers, Algeria - 20/11/2011. Kiongozi wa kundi la Alqaida lililopo kaskazini mwa Afrika ameliambia gazeti moja la Nouakchott lililopo Mauritania ya kuwa kundi lake limefaidika kutokana na kuangushwa kwa serikali ya Muammar Gaddafi.
Mokhtar Belmokhtar aalisema " tumefaidika kwa kupata siraha nyingi ambazo zilikuwa zimefichwa na serikali ya Muammar Gaddafi na kundi letu litazidi kuimarika."
Tangu kuangushwa kwa Muammar Gaddafi, serikali za Magharibi zimekuwa na wasiwasi huenda baadhi ya siraha zimeangukia kwenye mikono ya kundi la Alqaeda na kuitaka serikali ya mpito ya Libya kufanya kila juhudi kuzifuatilia siraha hizo.
Amani ya kisiasa bado kupatikana nchini Misri.
Kairo, Misri-20/11/2011. Hali ya wasiwasi imezidi kuongezeaka nchini Misri, huku polisi wakiendelea kupambana na waandamanaji wanao pinga kuwepo kwa serikali ya kijeshi.
Polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mipira walikumbana na wakati mgumu wa kuwatawanya maaelfu ya watu waliokusanyika kwenye eneo lijulikananio kama Tahrir lililopo katikati ya jiji la Kairo.
Waandamanaji hao ambao walikuwa wakisema "hatutaki utwala wa kijeshi na Tantawi aondoke."
Kwa mujibu wa mmoja ya wafanyakazi wa huduma ya kwaza mtu mmoja alikufa hapo hapo baada ya kupigwa risasi ya plastiki na alikuwa anaitwa "Ahmed Mahmoud 23."
Waandamanaji hao wamekuwa wanatumia, fimbo, mbao na matofari ili kupamabana na polisi.
Misri imekuwa na myumbo wa amani tangu kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Husni Mubbaraka mapema mwezi wa pili mwaka huu.

Saturday, November 19, 2011

Pope Benedikt awasili nchini Benin.

Mtoto wa Muammar Gaddafi akamatwa.

Obari, Libya - 19/11/2011. Mtoto wa aliye kuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amekamatwa katika mji wa Obari uliyopo kusini mwa nchi hiyo.
Saif al-Islam, ambaye alikuwa mafichoni tangu serikali ya baba yake kuangusha na kuwawa na kundi la National Transitional Council (NTC) chini ya msaada wa jeshi la NATO mapema mwezi wa kumi 2011.
Waziri wa sheria wa Libya Mohammed al Allagui alisema "Saif atawasilishwa Tripol."
Hata hivyo, kiongozi aliye ongozwa kukamatwa kwa Saif alisema " Tutamweka hapa Zintan hadi hapo serikali itakapo undwa na ndiyo hapo tutamkabidhi mikononi mwa serikali."
Saif al-Islam amesha funguliwa kesi na mahakama ya kimataifa inayo shughulikia makosa ya kibinadamu iliyopo nchini Uhollanzi ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Papa Benedikt awasili nchini Benin.
Benin, Katounou - 19/11/2011. Papa Benedikt XVI amewasiili nchini Benin kwa mara ya pili huku maelfu ya wananchi wakimshangilia kwa shwangwe.
Msemaji wa ofisi ya Vatikani alisema "katika ziara yake Pope Benedikt, atatembelea sehemu tofauti na kusisitiza umoja na ushirikiano ili kukuza amani hasa katika bara la Afrika, huenda akakutana na wakati mgumu wa kujibu maswali juu ya matumizi ya kondom."
Nchi ya Benin ambayo waumini wa kanisa Katoliki wanazidi kuongezeka tangu kuwasili kwa mapadri wa Kikatoliki miaka 150 iliyo pita kuanzisha seminari kubwa ya kikatoliki katika eneo la Afrika ya Magharibi.
Vatikan yakasirishwa na picha zilizo chapishwa zidi ya kiongozi wa kanisa Katoliki.
Vatican, Vatican City -19/11/2011. Kanisa Katoliki limelaani kitendo cha wanakampeni zidi ya ushoga kuchapisha picha za kiongozi wa kanisa hilo akipigana busu na kiongozi mmoja wa dini ya kiislaam.
Habari kutoka kanisa hili zimesema "picha hizo lazima ziziuliwe na kuwekwe sheria kuzuia picha kama hizo."
Picha hizo za Papa Benedikt akibususiana na kiongozi mwingine wa dini, ni moja ya picha ambazo zimesambazwa na kuonyeshwa ni za waziri mkuu wa Izrael Benyamini Netanyahu akimbusu rais wa Wapalestina Mahamoud Abbas, na huku rais Sarkoz akibusiana na Kansela Angel Markel wa Ujerumani.
Meya akutwa nahatia ya kuhusika na mauaji ya kimbali na ahukumiwa kwenda jela.
Kigali, Rwanda - 19/11/2011. Mahakama ya kimataifa inayo shughulikia haki za binadamu iliyopo nchini Rwanda imemuhukumu aliyekuwa meya wa mji wa Kivuma kwa kuhusika katika mauaji ya kimbali yaliyo tokea mwaka 1994.
Gregoire Ndahimana ambaye alikutwa na makosa ya kusaidia " mauaji ya watu wasio pungua 4,000 wenye asili ya Kitutsi."
Kwa mujibu wa mahakama "Ndahimana alikuwepo kama kiongozi wa serikali wakati wa mauaji yaliyo tokea katika kanisa Katoliki lililopo Nyange."
Gregoire Ndahimana atatumikia kifungo cha miaka 15 jela, japo kwa sasa ameshatumikia miaka miwili kutokana yanayo husika na maswala ya mauaji ya kimbali yaliyo tokea Rwanda 1994.

Wednesday, November 16, 2011

Mario Monti aapishwa kuwa waziri kuwa mkuu wa Itali.

Mario Monti aapishwa kuwa waziri mkuu wa Itali.

Roma, Itali - 16/11/2011. Mario Monti ameapishwa kuwa waziri mkuu wa Itali, siku chache baada Silvio Beruscon kujiudhulu.
Mario Monti ambaye alishawahi kuwa kamishna katika jumuiya ya Ulaya.
Baada ya kuapishwa waziri mkuu Monti aliunda baraza la mawaziri tayari kuandaa mkakati wa kupambana naamyumbo wa uchumi uliyoikumba Itali.
Jumuiya ya nchi za Kiarabu yatoa onyo kwa Syria.
Rabat, Morokko - 16/11/2011. Jumuiya ya nchi za Kiarabu imetoa siku tatu kwa nchhi ya Syria kusimamisha vurugu zinazotokea kati ya serikali na wapinzani au hatua nyingine zitachukuliwa.
Msemaji wa katika mkutano huo alisema " tunataka serikali ya Syria kusimamisha umwagaji wa damu unao endelea na ukandamizwaji kwa wapinzani usimamishwe."
Onyo hilo limetolewa baada ya jumuiya hiyo kuiwekea vikwazo serikali ya Syria hivi karibuni.

Tuesday, November 8, 2011

Obama na Sarkozy watiwa wasiwasi na kauli za Benjamin Netanyahu.

Aliyekuwa bingwa wa ngumi wa uzito wa juu wa dunia afariki dunia.

Philadelphia, Marekani - 08/11/2011. Aliye kuwa bingwa wa ngumi za uzito wa juu dunia amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ya ini.
Joe Frazier 67 aliyejulikana kama "Smokin Joe" ambaye aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya ini na kulazwa hospital kwa matibabu. Joe the Smokin ambaye alikuwa bingwa wa ngumi za uzito wa juu mwaka 1970 hadi 1973.
Bingwa mwenzake wa dunia kwa muda wote Mohamed Ali alisema " dunia imempoteza bingwa na mpiganaji ambaye hatatokea kama yeye."
Kwani niaba ya launite.blogspot.com Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
Obama na Sarkozy watiwa wasiwasi na kauli za Benjamin Netanyahu.
Paris, Ufaransa - 08/11/2011. Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amemwita waziri mkuu wa Izrael Benjamin Netanyahu ya kuwa ni "mwongo" wakati alipo kutana na rais wa Marekani Baraka Obama.
Rais Sarkozy alisikika alisema "siwezi hata kumwelewa na nimechoka naye kwani ni mwongo."
Naye rasi wa Marekani Baraka Obama alisikika akisema "wewe umechoka naye, je mimi mwenzako karibu kila siku na husika naye kwa njia moja au nyingine."
Kauli za viongozi hao zilisikika wakati walipo kutana kabla ya kuanza mkutano wa wakuu wa nchi tajiri G20 uliyo fanyika nchini Ufaransa ili kujadili hali ya uchumi wa dunia ambao unayumba.
Mwana wa Mfalme wa Uingereza atembelea Tanzania.
Dar es Salaam, Tanzania - 08/11/2011. Mwana wa Malkia wa Uingereza na mkwe wamefanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni moja ya nchini ambazo walipewa mwaliko na serikali ya nchi hiyo.
Prinsi Charles na mkewe Kamilla katika ziara hiyo wamekutana na rais wa Jakaya Kikwete pia na viongozi mbalimbali wa nchi ya Tanzania na kujadili ni kwa jinsi gani uhusiano uliopo katia ya Tanzania na Uingereza unaweza kudumishwa kwa ukaribu zaidi.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alisema "Tanzania na Uingereza tunashirikiana katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii na ziara hii ya mwana wa Malkia wa Uingereza inaonyesha uhusiano uliopo kati ya kati yetu ni mzuri na utaendelea kudumishwa."
Mwana wa Malkia Prinsi Charles na mkewe Kamilla watakuwa Tanzania kwa muda wa siku tatu.

Monday, November 7, 2011

Mganga aliyekuwa akimuhudumia Michael Jackoson akutwa na makosa.

Mganga aliyekuwa akimuhudumia Michael Jackoson akutwa na makosa.

Los Angeles, Marekani - 07/11/2011. Mganga ambaye alikuwa anamuhudumia bingwa wa musiki wa pops amekutwa na makosa ya kumwua bingwa huyo wa muziki bila kukusudia 25. June,2009.
Dr Conrad Murray, ambaye alikuwa ndiye aliye kuwa anamwangalia kiafya bingwa huyo wa musiki wa pops Michael Jackson, alikutwa na makosa hayo na mahakama ya jiji la Los Angeles na hukumu ya kesi yake itafanyika 28/11/2011.
Michael Jackson, ambaye alifariki kutokana na dawa alizo meza chini ya uandishi na usimamizi wa Dr Conrad Murray.
Kifo cha Michael kilisitua na kuleta mshituko dunia nzima hasa kwa wapenzi wake wa musiki.

Mahajaji wafanya Hija ya kila mwaka.

Mahujaji wafanya Hija ya kila mwaka.

Makka, Saudi Arabia - 07/11/2011. Mamilion ya waumini wa dini ya Kiislaam duniani wamefanya Hijja ikiwa ni nguzo mojawapo ya dini ya Kiisalaam.
Mahujaji hao ambao hukutana kila mwaka, ili kutubu dhambi zao na kuomba msamaha kwa Mungu ili wasamehewe yale waliyo yafanya kutokana na udhaifu wa kibinadamu huku wakisema Rabeka Alhaahaa Rabeka Alhaahaa.
Waziri mkuu wa Ugiriki aachia madaraka ya kuongoza nchi.
Athens, Ugiriki - 07/11/2011. Waziri mkuu wa Ugiriki amejiudhulu uongozi wa nchi hiyo na kutoa nafasi ya kuundwa serikali ya muungano itakayo ongoza kutatua uchumi wa nchi hiyo.
George Papandreou alisema alitangaza kujihudhulu baada ya kukutana na rais wa Ugiriki Karolos Papoulias ili mkuzungumzia hali halisi nini kinatakiwa ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Kufuatia kujiudhulu huko serikali ya muungano itaundwa na inatarajiwa kutangazwa siku ya Jumanne.
Rusia yaonya mashambulizi zidi ya Iran
Moscow, Urusi, 07/11/2011. Waziri wa mambo nje wa Urusi, ameonya ya kuwa kitendo cha kutaka kuishambulia Iran kitaleta madhara makubwa na kufanya eneo zima la Mashariki ya Kati kuwa na vurugu kubwa.
Waziri Sergei Lavrov alisema " swala la nyuklia la nchi ya Iran lazima litatuliwe kwa mazungumzo ya kidiplomasia na siyo kwa ushambulizi wa mabomu."
Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Urusi aliya sema hayo baada ya rais wa Izrael Shimon Perez kusema "mashambulizi zidi ya Iran yanaweza kutokea."
Mvutano huu wa swala la Iran na nyuklia, umekuwa zaidi huku shirika la kimataifa linalo shughulikia maswala ya kinyuklia kukaribia kutoa ripoti yake kuhusu mradi mzima wa kinyuklia wa Iran.
Hata hivyo Iran, imekuwa ikidai ya kuwa mpango wake wa kinyuklia ni kwa ajili ya kuendeleza maswala ya utafiti na sayansi na kusema ya kuwa pindipo itakapo shambuliwa basi haita kaaa kimya itafanya mashambulizi pia.
Polisi wapambana na waandamanaji jiji Monrovia Liberia
Monrovia, Liberia - 07/11.2011. Jiji la Monrovia nchini Liberia limekumbwa na machafuko baaday police kupambana na waandamanaji wanaounga chama cha upinzani kinacho ongozwa na Winton Tubman.
Maandamano hayo yamefanyika ili kupinga ya kuwa uchaguzi unaotaka kufanyika utakuwa si wa haki na wanaupinga.
Kwa mujibu wa mashaidi "polisi walitumia siraha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano hayo."
Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa aliyepo nchini Liberia Yasmin Bouziane alipo ulizwa kuhusu matukio ya mauaji akukana wala kukubali.
Liberia nchi ambayo ilikuwa na machafuko na mauaji miaka michache iliyo pita, imekuwa na mvutano wa kisiasa ambao umeibuka hivi karibuni kati ya chama cha kisiasa kinacho ongozwa na Bi Ellen Johnson Sirleaf na vile vya wapinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 2003.

Saturday, November 5, 2011

Mkutano wa G20 washindwa kutengua kitendawili cha uchumi.

Mkuu wa jeshi la Kenya aonya uuzaji na utumizi wa punda nchini Somalia.

Nairobi, Kenya - 05/11/2011. Jeshi la Kenya limetoa onyo kwa watu ambao wanatumia punda nchini Somalia, kwa madai punda hao wanatumika na kundi la Al Shabab.
Meja Emmanuel Chirchir ambaye alitumia mtandao wa twiter kwa kuonya " nimarufuku kwa wanchi wa Kenya kuuza punda kwa Wasomalia ambao wengi wa punda hao huishia kwenye mikono ya kundi la Al Shabab."
Bei ya punda kati ya mpaka wa Somalia na Kenya imefika dola za Kimarekani $150 hadi 200 kutokana na punda hao kuwa ndiyo njia pekee ya kusafirishia mizigo.
Meja Chirchir alisha wahi kuwaonya wanchi wa Somalia waishio katika mikoa 10 ya kuwa waondoke kwani miji hiyo inatumiwa na kundi la Al Shabab na kunauwezekano wa miji hiyo kushambuliwa.
Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna ushaidi ya kuwa kuna punda ambao wamehusika katika kubeba siraha za kundi la Al Shabab.
Mkutano wa G20 washindwa kutengua kitendawili cha uchumi.
Cannes, France - 05/11/2011. Mkutano ulio wakutanisha viongozi wa kuu wa nchi 20 wa zenye uchumi uliyotengemaa umekwisha bila kuweka mkakati madhubuti wa kutafuta myumbo wa uchumi dunia.
Mkutano huo ambao ulikuwa umetawaliwa na deni la Greek na mashaka ya kiuchumi yanayo endelea nchini Itali, na kuhadi kuungana katika kutatua mgogoro wa kiuchumi wa dunia kwa kutoa maoni tofauti.
Kufuatia mkutano huo wa viongozi wa G20 umalizika, waziri mkuu wa Greek George Papandreous alilazimika kuitisha kura ya maoni ndani ya bunge la nchi hiyo kuhusu uongozi wake na uamuzi wake kusitisha mpango wa wananchi wa Greek kupiga kura ya maoni yao juu ya mkopo ambao Greek inahitaji ili kuinua uchumi wake na kushinada kura hiyo na huku vyama vya upinzani vikishinikiza ajiudhuru uongozi wake wa nchi.
Nigeria yakumbwa na milipuko ya mabomu.
Damaturu, Nigeria- 05/11/2011. Milipuko ya mabomu imetokea nchini Nigeria kwenye mji wa Damaturu na kusababisha mauaji na kuleta uharibifu mkubwa.
Milipuko hiyo ambayo imetokea huku miliyo ya risasi ikisikika na kusababisha zaidi ya watu 60 kupoteza maisha huku wakazi wa mji huo wakiwa wameshikwa na wasiwasi mkubwa.
Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na milipuko hiyo, ingiwa serikali bado inaendelea kufanya msako wa siraha nyumba hadi nyumba katika maeneo ya mji wa Damaturu.
Kiongozi wa FARC nchini Kolombia auwawa.
Bogota, Kolombia - 05/11/2011. Serikali ya Kolombia imetangaza ya kuwa imefanikiwa kumua aliyekuwa kiongozi wa kundi la FARC, kundi ambalo limekuwa likipingana na serikali ya nchi hiyo kwa miaka mingi.
Waziri wa ulinzi Juan Carlos Pinzon alisema " jeshi la Kolombia limefanikiwa kumua kiongozi wa wa kundia la FARC Alfonso Cano 63, baada ya kuvamia makazi aliyokuwa amejificha kusini mwa mwa mji wa Kauka."
"Na hili ni pigo kubwa kwa kundi hilo na tunapenda kutoa onyo ya kuwa wavuruga amani nchini hawatapewa nafasi kwani tunataka Kolombia kuwa nchi ya amani." Alimalizia waziri wa ulinzi.
Kifo cha kiongozi huyo wa FARC kumekuja baada ya serikali ya Kolombia kutangaza zawadi ya dolla za Kimarekani million 5, kwa mtu atakaye toa habari kuhusu alipo kiongozi huyo wa FARC.

Thursday, November 3, 2011

Rwanda yarudisha madini ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rwanda yarudisha madini ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kigali, Rwanda - 03/11/2011. Serikali ya Rwanda imerudisha madini zaidi ya tani 82 yaliokamatwa na polisi nchini Rwanda na kurudishawa Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo.
Naibu mkurugenzi wa mali ya asili wa Rwanda " Michael Biryaberema alisema " Rwanda inataka kukomesha uchimbaji huo haramu na kufuta fira ya kuwa Rwanda inafaidika na kutokana na madini yanayo toka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zitashirikiana kwa pamoja katika kuimarisha sekta ya madini."
Madini ambayo yamerudishwa ni pamoja na yale ya cassiterite, bati na vile vile coltan, ambayo hutumiwa kujenga vifaa kama vile simu za mkononi. Kurejeshwa kwa madini hayo kunafuatia sheria za kimataifa zinazonuiwa kusafisha sekta hiyo inayokabiliwa na ufisadi wa hali ya juu. Utajiri wa madini wa Congo Kinshasa umekuwa kichocheo kikuu cha mzozo wa miaka mingi nchini humo.
Eritrea yakanusha kusaidia kundi la Al Shabab.
Asmara, Eritrea -03/11/2011. Serikali ya Eritrea imekanusha ya kuwa inawasaidia kijeshi na kisiraha kundi la Al Shabab lililopo nchini Somalia.
Habari zilizo patikana kutoka serikali ya Kenya na Somalia zimesema " serikali ya Eritrea imetuma ndege yenye dhana za kijeshi kwa kundi la Al Shabab."
Hata hivyo serikali ya Eritrea ilisisitiza yakuwa habari hizo ni za uongo, hazina ukweli na hazina ushahidi."
"Na tumekuwa tukisema nguvu za kijeshi hazita leta amani nchini Somalia."
Somalia nchi ambayo ipo kwenye kona ya Afrika Mashari na imekuwa na vita vya wenye kwa wenyewe kwamuda usiopungua miaka 20.
Iran yaonya mpango wa kutaka kuishambulia kijeshi.
Tehran, Iran - 03/11/2011. Mkuu wa jeshi la Iran ameonya kitendo au jaribio la kuishambulia Iran, kitakuwa ni kitendo ambacho kitasababisha majuto makubwa.
Amir Ali Hajizadeh alisema " Iran inauwezo wa kutengeneza siraha na mizinga ya aina yoyote japo kunatishio kutoka nchi za Magharibi."
Na siraha hizo zinauwezo wa kwenda km 2,000 jambo ambalo hatuoni haja ya kufanya hivyo."
Mkuu huyo wa jeshi aliyasema hayo baada ya jeshi la Izrael kufanya majaribio ya mizinga yake yenye uwezo wa kufika hadi Iran.
Hadi sasa kuna habari zinasema "waziri mkuu wa Izrael Benyamin Netanyahu na washiriki wake wakuu wanajaribu kusisitiza nguvu za kijeshi zitumike zidi ya Iran ili kuharibu mitambo ya kinyuklia iliyopo humo."
Iran imekuwa ikishinikizwa nchi za Magharibi kusimamisha miradi yake ya kinyukli kwa madai ya kuwa Iran inampango wa kutengeneza siraha za kinyuklia, jambo ambalo Iran imekuwa ikilikana na kudai miradi yake ya kinyuklia ni kwa ajili ya kusaidia ukuzaji wa kisayansi.
Waziri mkuu wa Ugiriki akumbwa na wakati mgumu wa maamuzi.
Athense, Ugiriki - 03/11/2011. Waziri mkuu wa Ugiriki amekuwa na wakati mgumu kiuamuzi baada ya kutangaza yakuwa nchi yake haitapiga tena kura ya maoni kuhusu mkopo ambao nchi hiyo inauhitaji.
George Papandreou alisema "tumeanza kuzumngumza na vyama vipanzani ili kupata muafaka wa swala zima la kifedha tunazo hitaji."
Naomba tuungane katika swala hili ili kuikwamua nchi yetu kiuchumi."
Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walishikwa na mshangao baada ya waziri mkuu wa Giriki kutangaza ya mkuwa ataitisha kura ya maoni ilikujua maoni ya wanchi juu ya mkopo unaotarajiwa kupewa nchi ya Giriki ili kujikwamua kiuchumi.