Friday, August 27, 2010

Kenya yazaliwa upya. Nairobi, Kenya 27/08/2010. Wananchi wa Kenya, leo hii wameshuhudia kutiwa sahii katiba mpaya ya nchi hiyo. Kwenye sherehe hiyo iliyo udhuliwa na viongozi na marais wa nchi jirani, rais wa Kenya Mwai Kibaki, aliapishwa tena ilikuiongoza Kenya chini ya katiba mpya. Kukubalika kwa mabadiliko ya katiba ya Kenya ni matokeo ya kura za maoni zilizo pigwa hapo awali na ambapo wananchi wa Kenya waliowengi walikubali katiba ya nchi ifanyiwe mabadiliko. Picha hpo juu anaonekana rais wa Kenya Mwai Kibaki, akinyanyua juu katiba mpya ya Kenya, mara baada ya kutia sahii kupitishwa kwa katiba hiyo mpya.

Saturday, August 21, 2010

Wairani washangilia uzinduzi wa nguvu za kinyuklia. Tehran, Iran 21/08/2010. urussi na Iran zimeanza kwa pamoja urutubishaji wa madini kwa aajili ya kuimarisha na kuongeza nguvu za siahati ya kinyuklia. Akiongea katika ufunguzi huo makamu wa rais wa usimamizi wa nyuklia, Ali Akbar Salehi, alisema " mradi huu umesimamiwa na serikali ya Iran na serikali ya Urussi na nihatua ya kimaendeleo kwa wanachi wa Iran." Naye waziri wa mabo ya nje wa Urussi Sergi Lavrov alisema, uzinduzi wa mradi huu wa kinyuklia ni muhimu kwa Iran kwani wanachi wa Iran watafaidika kimaendeleo." Picha hapo juu anaonekana mwanamama wanasayansi wa mabo ya kinyuklia akikagua kwa makini ni jinsi gani mashine zinavyo fanya kazi.

Wednesday, August 11, 2010

Wanyarwanda wamchagua tena Paul Kagame

Wanyarwanda wa mchagua tena Paul Kagame.

Kigali, Rwanda - 11/09/2010. Matokeo ya uchaguzi nchini Rwanda yamempa ushindi mkubwa aliyekuwa rais wa Rwanda Paul Kagame.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka kwa kamati iliyosimamia uchaguzi huo ilisema "Paul Kagame alishinda kwa kupata wingi wa kura ziadi ya asilimia 90.
Poul Kagame ambaye aligombea uchaguzi wa rais kupitia chama cha (RPF- Rwanda Partiotic Front) na amekuwa kiongozi wake tangu 1994 baada kuchukua madaraka kwa kuiondoa serikali rais Juvenal Abyarimana ambayo ilisadikiwa ilisimamia mauaji ya kikabila yaliyotokea nchini humo.
Hata hivyo wagombea wavyama vya upinzani walidai yakuwa uchaguzi huo ulikuwa na mazingira magumu kwao.
Pichani anaonekana rais Paul Kagame akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Sunday, August 8, 2010

Pentagon wataka Wikileaks kurudisha nyaraka za siri.

Pentagon wataka Wikileaks kurudisha nyaraka za siri.

Washington, Amerika- 08/08/2010. Amerika imetaka chombo cha habari kilicho toa maelezo ya siri kuhusu mpango mzima wa kivita zidi ya kundi la Al-qaeda na Taliban kurudisha nyaraka zote kwa serikali ya Amerika. Wikileaks chombo ch a habari ambacho ndicho kilicho andika habari hizo, kimedai ya kuwa bado kina nyaraka za siri zipatazo 15,000 na huenda wakazitoa habari hizo muda wowote kwenye mitandao. Msemaji wa Pentagon Geoff Morrell alisema "tungeomba wikileaks watukabidhi karatasi hizo kwa ni watakuwa wamefanya jambo la busara na ninamatumaini watakubaliana na sisi katika swala hilo." Hata hivyo Wikileaks kuna tetesi ya kuwa "Wikileaks watachapisha siri zote ikiwa wafanyazai wa chombo hicho watasumbuliwa au kukamatwa." Picha hapo juu ni ya alama ya Wikileaks chombo cha habari ambacho kilitchapisha hivi karibuni nyaraka za siri za pipango ya kivita vinavyo endelea zidi ya Al-qaeda na washiriki wake nchini Afghanistan na kote duniani. Tarik Aziz ataka Amerika isawazishe makoso kabla ya kuondoka.
Baghdad, Iraq- 08/08/2010. Aliyekuwa waziri kiongozi wa serikali, wakati wa utawala wa Saadam Hussein, amesema kuondoka mapema kwa jeshi la Amerika nchini Iraq ni kuicha nchi hiyo katika hali ya hatari kubwa. Tarek Azizi ambaye kwa sasa anatumikia kifungo, alisema "Iraki haitakuwa Irak tena, na Amerika inatakiwa kubaki na kuijenga Irak kama walivyo ikuta, kwani Amerika imefanya makosa na hivyo lazima isahiishe makosa kabla ya kuondoka." Tarek Azizi, pia aliisifu serikali ya Saadam Hussein kwa kusema " Saadam hakuwa mwongo na hakubadilisha ukweli, ni mtu ambaye nilimweshimu na kumpenda na nimtu ambaye historia itatoa jibi wakati utakapo fika, kwani alijenga nchi, alitumika nchi yake na watu wake, na nchi za Magharibi zilimwelewa vibaya kutokana na sababu fulani." Pichani hapo juu anaonekana Tarik Azizi enzi za uongozi wake akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya uongozi wa serikali yake. Fidel Castro aonya kuzuka kwa vita vya matumizi ya nyuklia.
Havana, Kuba - 08/08/2010. Rais wa zamani wa Kuba Fidel Castro, amehutubia taifa kwa mara ya kwanza tangu alipo achia madaraka ya uongozi.
Fidel Castro 83 amabye mpaka sasa ni kiongozi wa chama Commnist alionya ya kuwa dunia inaelekea kwenye mashindano ya kivita ambapo matumizi ya nyuklia huenda ya katumika.
Na alisema "Uongozi wa serikali ya Amerika unampango wa kuzishambulia Iran na Korea ya Kaskazini, vilevile ikiwa rais wa Amerika Baraka Obama atatoa ruhusa ya kuanza vita,basi watu wengi watateketea wakiwemo Waamerika wanao fanya kazi katika maeneoya Mashariki ya Kati,na huo utakuwa ndiyo mwisho wa kuwa na amri moja ya kidunia na kuleta mgongano mkubwa kwenye maeneo ya Mashariki ya Kati na kwingine kote duniani."
Vilelevile Fidel Castro alisema " swala la mkubwa mmoja kutoa amri litafikia mwisho na baadhi ya miundo mbinu ya kibiashara na fedha zita hathirika na kuangamia."
Pichani anaonekana aliye kuwa rais wa Kuba Fidel Castro akihutubia mkutano hivi karibuni jijini Havana.

Thursday, August 5, 2010

Wakenya wakubali mabadiko ya katiba ya nchi.

Wakenya wakubali mabadiliko ya Katiba ya nchi.

Nairobi, Kenya - 05/08/2010. Matokeo ya uchaguzi wa kura ya maono yaliyolenga kubadirisha katiba ya nchi yamekubaliwa kwa asilimia kubwa.
Matokeo hayo ambayo yataleta mabadiliko makubwa katika katiba ya Kenya hasa kiuongozi na kisiasa.
Akiongea kwa furaha, kiongozi wa kampeni ya ndiyo, Kiraitu Murungi amabaye ni waziri wa nishati alisema "Wakenya wamekubali kwa pamoja na Kenya mpya imezaliwa"Wapigakura ya kukubali walipata asilimia 67.
Akiongea mara baada kiongozi aliye kuwa akiongoza kampeni za kupinga mabadiliko hayo Williamu Ruto ambaye ni waziri wa Elimu ya juu, aliseama "tumekubali matokeo ya kura."
Picha hpo juu ni bendera ya Kenya,nchi ambayo inatarajia kufanya mabadiriko ya kikatiba mara ya kura za wananchi walio wengi kukubali mabadiliko yafanyike.
Picha ya pili anaonekana mmoja wa raia wa Kenya akiwa ameshikilia karatasi iliyo andikwa 'ndiyo' kukubali mabadiliko ya katiba wakati wa kampeni.
Rais wa zamani wa Uganda aiga dunia.
Kampala, Uganda - 05/08/2010. Aliyekuwa rais wa Uganda Godfrey Binaisa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa masemaji wa familia alisema " Mzee Godfrey Binaisa alifariki usiku wa manane nyumbani kwake."
Binaisa ambaye alitawala Uganda mara baada ya kuangushwa utawala wa Idi Amini Dada, aliwai pia kuwa mwanasheria wakatiwa uhamishoni nchini Amerika.
Picha hapo juu anaonekana Godfrey Binaisa enzi za uhai wake akihutubia moja ya mkutono kama mgeni rasmi.
Naomi Campbell akili mbele ya mahakama.
Hague,Uhollanzi-05/08/2010. Mahakama inayoshughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za kibinadmu duniani leo imemuhoji mwanamitindo maharufu duniani Naomi Campbell.
Naonmi Campbell, aliongea katika mahakama hiyo, ili kutoa ushahidi kama alipokea alhmasi iliyo katwa kutoka kwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor mwaka 1997, wakati walipo kutana kweney chakula kilicho anadaliwa na aliyekuwa rais Afrika ya Kusini, Nelson Mandela.
Mwana mitindo huyo alikili yakuwa alipokea zawadi ya mawe kutoka kwa wanaume wawili waliokuja kumgongea wakati akiwa chumbani amalala na zawadi hizo alizichangia katika mfuku wa maradi wa Mandela ambao husaidia jamii.
Picha hapo juu anaonekana Naomi Campbell akitoa ushahidi mbele ya mahakama jijini Hague.
Picha ya pili anaonekana Naomi watatu kutoka kushoto wakati walipo pigwa picha ya pamoja na aliye kuwa rais wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela.

Tuesday, August 3, 2010

Izrael na Lebanoni zatupiana sisasi.

Mkuu wa polisi ahukumiwa jela miaka 15.

Mahakama nchini Afrika ya Kusini imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela aliyekuwa mkuu wa polisi nchini Afrika ya Kusini baada ya kukutwa na hatia ya kupokea rushwa na zawadi kinyume cha sheria.. Jack Selebi ambaye amkuwa na hatia ya kuchukua rushwa aliwahi kuwa mkuu wa jeshi la polisi na hata kufanyakazi na Interpol. Picha hapo juu anaonekana aliyekuwa mkuu wa polisi nchini Afriak ya Kusini Jack Selebi akiwa kizimbani kuisikiliza hukumu ya kesi yake. Izrael na Lebanoni zatupiana risasi. Beiruti, Lebanon - 03/08/2010. Jeshi la Lebanoni na jeshi la Izrael wametupiana risasi na kusababisha majeruhi ya wanajeshi wanne wa Lebanoni na vifo vya watu watono mmoja wapao akiwemo mwandishi wa habari. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema mashambulizi hayo yalianza wakati jeshi la Izrael lilipo kuwa lina jaribu kukata miti iliyopo mpakani na Lebanoni. Picha hapo juu wanaonekana wahudunu wa huduma ya kwanza wakimkimbiza mmoja wa majeruhi mara baada ya kujeruhiwa.

Sunday, August 1, 2010

Desmond Tutu kujihudhuru kazi za kiofisi.

Desmond Tutu kujihudhuru kazi za kiofisi. Cape -Town, Afrika ya Kusini - 01/08/2010. Aliyekuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Agrikan nchini Afrika ya Kusini na mshindi wa zawadi ya Amani ya Laureate Desmond Tutu ametangaza ya kuwa atajihudhuru na kutumia muda mwingi na familia yake. Akiongea hayo Askofu mstahafu alisema, "Nita kuwa nasiku moja ya kiofisi hadi hapo mwaka 2011 Februari. Askofu Desmond Tutu alikuwa mmoja wa viongozi waliopinga ubaguzi wa rangi. Picha hapo juu anaonekana Askofu mstahafu, ambaye ifikapo 2011 Februari atakuwa na muda mwingi wa kukaa na familia yake na kusimulia hadithi kwa wajukuu. Washukiwa wa mauaji ya Kampala kizimbani.

Kampala,Uganda - 01/08/2010. Mahakama nchini Uganda imeanza kusikiliza kesi inayo wakabili raia watatu kutoka nchini Kenya kwa kuhusika na mauaji ya watu wapatao 76.
Mauaji hayo yalitokea wakati mamia ya watu walikuwa wamekusanyika kuangalia fainali ya kombe la dunia July 11/ 2010 jiji Kampala.
Watuhumiwa hao ni Hussein Hassan Agad, Mohamed Adan Abdow na Idris Mogandu.
Picha hapo juu wanaonekana washitakiwa wakiwa mbele ya hakimu kusikiliza mashitaka zidi yao.
Jeshi la Kiholanzi la rudi nyumbani.
Kabul, Afghanistan - 01/08/2010. Jeshi la Kiholanzi limeanza rasmi kuondoka nchini Afghanistan, na kuwa jeshi la kwanza kutoka shirikisho la NATO kuondoka.
Jeshi hilo ambalo lilikuwa nchini humo kwa kipndi cha miaka minne.
Katika kipindi hicho chote nchini Afghanistan, jeshi hilo lime wapoteza wanajeshi wapatao 24.
Akiongelea kuondoka kwa jeshi hilo, katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen, alisema "kuondoka kwa jeshi la Kiholanzi siyo mwisho kwani jeshi jingine litakuja kuendeleza kazi.
Jeshi hilo ambalo lili anza kazi yake mwaka 2006, lilikuwa na kazi ya kutoa misaada ya kibinadamu na kusaidia kujenga uhusiano kati ya jamii nchini Afghanistan.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanajeshi wa jeshi la Kiholanzi wakiwa kazini wakati walipo kuwa nchini Afghanistan.