Thursday, January 1, 2015

Mamilioni washerekea kuanza kwa mwaka mpya.

Mamilioni washerekea kuanza kwa mwaka mpya.

 Mungu Baba tunakushukuru, utubariki, utulinde, utuzidishie kwa kila jambo tulifanyalo na utufanye tuzidi kukuomba na kukutegemea wewe Muumba kwa kila jambo. Amina.


 Wapalestina wajiunga na Mahamakama ya Kimataifa.
Ramalhah, Palestina - 01/01/2015. Rais wa Palestina Mahamoud Abbas, ametia siani mkataba wa makubaliano wa kujiunga rasmi kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa inayo shughulikia  makosa ya jina na ukiukwaji wa haki za binadamu ICC, masaa machache baada ya kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kushindwa kupitisha ombi la uhuru wa Wapalestina.

Akiongea baada ya kumaliza kusaini kujiunga na ICC, rais Mahmoud Abbas alisema " wanatushambulia kila siku, angani, majini na kila sehemu, wapi tutapeleka malalamiko yatu? Ikiwa kakati ya usalama ya umoja wa mataifa imetukataa."

Akiunga mkoni kitendo cha rais Abbas kusaini kujiunga na ICC, Hanan Ashrawi, ambaye  ni mwanadiplomasia alisema " tumekuwa watu wapole katika majadiliano tangu 1991, wakati mpango wa kuwa na mataifa mawili ya Kipalestina na la Kizrael kuzikwa, hivyo hiki kitendo cha leo ni muhimu kwa Wapalestina."

Kufuatia kujiunga kwa Wapalestina na ICC, kumetoa uwezo kwa mahakama ya kimataifa kuweza kuchunguza mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yamefanyika katika maeneo ya Wapalestina.

Kufuatia kujiunga kwa Wapalestina kwenye koti ya ICC, waziri mkuu wa Izrael, Benjamin Netanyahu amesema " Kitendo cha Abbas, kutawafanya Wapalestina kushitakiwa, kutokana na vitendo vyao vya kigaidi na hasa kwa kuunga mkono kundi la Hamas.
"Sisi kwa upande wa Izrael hatukubaliani na uamuzi wa Wapalestina, na tutalinda haki za Waizrael."

Uamuzi huu wa Wapalestina kujiunga na ICC, kumekuja baada ya kamati ya Usalama ya umoja wa mataifa kushindwa kupitisha muswaada ulioletwa na Wapalestina, baada ya Marekani na Australia kupinga muswaada huo, ambao ulikuwa unadai Izrael kusimamisha kitendo cha kuchukua ardhi ya Wapalestina kwa nguvu na kurudisha wanazo kalia kwa kufuata mipaka ya makubaliano ya mwaka 1967.