Wednesday, September 29, 2010

Maafisa usalama wagundua mpango na njama za magidi

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini ampa madaraka ya chama mtoto wake.

Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 29/09/2010. Kiongozi wa serikali ya Korea ya Kaskazini amemteua mtoto wake wa kiume kushika nyazifa zake za uongozi wa chama nchi humo.
Kim Jong -Il, alimteaua mtoto wake huyo Kim Jong-Un ambaye inasemekana alipata elimu yake kwenye nchi za Ulaya Magharibi.
Kiongozi huyo Kim Jong-Il ambaye inasadikiwa ya kuwa hali yake ya afya inazidi kudholota alifanya uteuzi huo hivi karibuni na kutangaza katika mkutano mkuu wa chama chake uliofanyika jiji Pyongyang.
Picha hapo anaonekana kiongozi mkuu wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Il akiongoza mkutano mkuu wa chama uliofanyika hivi karibuni.
Picha ya pili wanaonekana wajumbe walioudhulia mkutano ambapo mtoto wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong-Un alikabiziwa uongozi.
Waafisa usalama wagundua mpango na njama za magaidi.
London, Uingereza- 29/09/2010. Maafisa usalama wa nchi za Ulaya wamegundua na njama ambazo zilikuwa zimepangwa na makundi ya kigaidi hivi karibuni.
Kwa mujbu wa habari zilizo patikana zilisema "kundi la wapigana la Pakistan lilikuwa limepanga mashambulizi kwenya miji mikuu ya Ujeruman, Uingereza na Ufaransa na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na mpango huo."
Habari hizo zinasema kundi hilo lilipanga mashambuliza kama ya le yaliyo fanyika nchini India mwaka 2008 Novermba.
Picha hpo juu wanaonekana polisi wakiwa wana chunga mnara maarufu nchini Ufaransa mara baada ya watu kuamriwa waondoke kutokana na tishio la bomu.
Sheria za jumuia ya Ulaya kupambana na Ufaransa.
Paris, Ufaransa - 29/09/2010. Ofisi ya kamishna wa sheria wa jumuia ya Ulaya imeitaka serikali ya Ufaransa kujibu haraka kwanini ilivuluga sheria za umoja wa Ulaya.
Majibu ya barua hiyo yanatakiwa baada ya serikali ya Ufaransa kuwafukuza watu wa jamii ya Waroma hivi karibuni.
Akisisitiza, kamishna wa sheria wa jumuia ya Ulaya Viviane Reding alisema "Ufarance imevunja sheria ambayo ina mruhusu kila raia wa nchi mwanachama wa jumuia ya Ulaya yupo huru kutembea na kuishi katika nchi wanchama wa jumuia hiy."
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Ufaransa Bernard Valero ilisema " serikali ya Ufaransa inafanya hivyo ili kukabiliana na uarifu unaondelea katika jamii nchini humo"
Picha hapo juu anaonekana kamishana wa sheria wa jumuia ya Ulaya Viviane Reding akiongea kuhusu swala la raia wa Ulaya wa jamii ya Waroma.
Wimbi la maandamano laikumba jumuia ya Ulaya.
Brussel, Umoja wa Ulaya - 29/09/2010. Maelfu ya wafanyakazi wamendamani ili kupinga ubanaji wa bajeti za serikali na mpango wa kupunguza matumizi.
Akiongea kwa kama mwakilishi wa jumuia ya wafanyakazi nchini Ufaransa Bernard Thibault alisema "tupo hapa kutoka kila nchi mwanacham wa jumuia ya Ulaya ili kunyesha mshikamano wetu kupinga mpango mzima unaochukuliwa na serikali za umoja huu, kwani utaleta matatizo katika jamii."
Maandamano hayo yamekuja baada ya serikali za jumuia ya Ulaya kungalia upya bajeti zake jambo ambalo sekta za umma huenda zikaathirika kwa kiwango kikubwa.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wafanyakazi jijini Manchester wakiandamana kupinga mpango huo.

Monday, September 27, 2010

Abbas atoa muda kwa viongozi wa Izrael kusimamisha ujenzi

Rais Robert Mugabe ataka Afrika ipewe kiti cha kudumu. UN, New York 27/09/2010. Rais wa Zimbabwe ametaka bara la Afrika lipewe kiti katika baraza la usalama la umoja wa Mataifa.cha kudumu Rais Robert Mugabe alisema "ni kitu kisichokubalika na wala kueleweka kwa bara la Afrika kuwa nara pekee lisilokuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa matifa na ihii inaleta kutokuwa na usawa kihistoria" Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa ina wakilishwa na Uingereza, Marekani, China, Urussi,France na wawakilishi kumi ambao uchaguliwa kila baada ya miaka miwili na watano kubadilishwa kila mwaka. Picha hapo juu anaonekana rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa katika kikao cha 65 cha umoja huo wa mataifa 2010. Serikali ya Ufaransa ya haidi kuwaokoa raia wake waliotekwa nyara. Bamako, Mali - 27/09/2010. Serikali ya Ufaransa iko mbioni iki kuwaokoa raia wa Ufaransa ambao wametekwa nyara na kundi la Maghreb ambao linashirikiana na kundi la Alqaeda. Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya rais alisema" tunaamimini ya kuwa raia waliotekwa na kundi hilo bado wazima na niwajibu wa serikali kuokoa maisha ya raia wake" Pichani anaonekana rais wa Ufaransa ambaye serikali yake inafanya kila mbinu kuwaokoa raia wake waliotekwa nyara na kundi la Maghreb.

Abbas atoa muda kwa viongozi wa Izrael kusimamisha ujenzi.
Paris, Ufaransa - 27/09/2010. Rais wa taifa la Wapalestina amesema ya kuwa hatasimamisha mazungumzo na serikali ya Izrael kwa sasa ili kutoa muda wa kusimamishwa ujenzi wa makao mapya ya Waizrael.
Rais Mahamoud Abbas alisema " itakuwa ni vyema kwa serikali ya Izrael kusimamisha ujenzi badala ya kukataa na kundelea na ujenzi huo"
Pia rais Abbas aliongezea kwa kusema "wakati ninatoa muda kwa serikali ya Izrael kusimamisha ujenzi wake katika maeneo walio kalia kinguvu, nitajaribu kuwasiliana na viongozi wengine wa nchi za Kiaarabu ili kupata ushauri"
Picha hapo juu anaonekana rais wa Taifa la Wapalestina akiwa ameinama wakati wa moja ya mikutano ya kutaka kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael.

Thursday, September 23, 2010

Baraka Obama asisitiza ushirikiano kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati.

Baraka Obama asisitiza ushirikiano kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati.

New York, Amerika- 23/09/2010. Rais wa Amerika amezitaka jumuia za kimataifa kushirikiana ili kuleta amani kati ya Waisrael na Wapalestina.
Rais Baraka Obama aliyasema hayo mbele ya viongozi na wakuu wanchi walioudhulia kikao cha 65 cha umoja wa Mataifa "yakuwa kama tukishirikiana kwa pamoja katika kutatua mgogoro kati ya Wapalestina na Waizrael, basi kwenye mkutano mwingine wa umoja wa mataifa 2011 tutakuwa na mwanacham mpya wa umoja wa mataifa ambayo itakuwa Palestina."
Vilevile rais Obama, alisema mlango uko wazi kwa mazungumzo na Iran ikiwa nchi hiyo itaonyesha nia".
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wakimsikiliza katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akiwakaribisha kabla ya kuanza kikao cha 65 cha umoja wa Mataifa.
Picha ya pili anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama akisisitiza baadhi ya mipango wakati alipo akihutubia viongozi kwenywe mkutano wa 65 wa Umoja wa Mataifa.
Rais wa Iran ashambulia sera za kibepari.
UN,New-York - 23/09/2010. Rais wa Iran imeitaka dunia kutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa kuhangamiza na kuharibu siraha zote za mabomu ya kinyuklia kote duniani.
Rais Mahmoud Ahmadinejad alisema ya kuwa "dunia haitakuwa na usalama ikiwa siriha za nyuklia hazita agamizwa kwani zinakwenda kinyume na maadili ya Mitume ambao walikuja kutangaza amani na upendo"
Kwa kuongeza, rais Ahmadnejad alitaka "heshima lazima iwepo katika dini zote na vitabu ambavyo vinatumika katika kufundishia imani ya kumwamini Mungu" Rais Ahmadinejad, alisema ya kuwa" mashambulizi ya Septemba 11 yalikuwa ni mipango ya ambayo ilipangwa kuhujumu uchumi wa Amerika ili kusaidia mbinu za mabepari"
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran, akihutubia kwenye mkutano wa 65 wa Umoja wa mataifa jijini New York.

Sunday, September 19, 2010

Mzozo wa kidini waleta hali ya wasiwasi Indonesia

Mzozo wa kidini waleta hali ya wasiwasi Indonesia. Jakarta, Indonesia - 19/09/2010. Mamia ya waumini wa dini ya Kikristu wame kiuka amri iliyo wekwa na polisi kuwataka wasiudhulia misa kutokana na sababu za kiusalama. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa kanisa la Batak Christian Church alisema "tunataka haki ya kuomba Mungu, kwani tukikataliwa tutakuwa tunanyimwa haki zetu." Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu ambao walikusanyika pamoja kumuomba Mola.

Nchi za Sahara ya Kusini mwa Afrika zapambana kikamilifu na ukimwi.

New York, UN - 19/09/2010. Umoja wa Mataifa umetoa ropoti ya kuwa nchi zilizopo kusinu mwa jangwa la Sahaha zimejitahidi kupambana na usaambaa wa ugonjwa wa ukimwi.

Kwamujibu wa hahabiri UN zinasema "uambukizwaji wa ugonjwa huo umepungua kwa asilimia 25 katika nchi ambazo zilikuwa zinaongoza kwa kusambaa kwa ugonjwa huo."

UN ilisisitiza haya ni matokeo ya kampeni na mipango mbinu ambayo imesaidia katika kupunguza uasambaaji wa ugonjwa huo.

Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa katika kampeni ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi.

Tuesday, September 14, 2010

Viongozi wa Palestina na wa Izrael wakutana tena

Viongozi wa Iran wakutana na viongozi wa Afrika. Tehran, Iran - 14/09/2010. Rais wa Iran amezitaka nchi za Afrika "kutafuata uhuru kamili iki kuepukana na uchumi tegemezi ambao unakuja kwa masharti. Rais Mahmoud Ahmadinejad aliyaongea hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano uanawakutanisha viongozi wa Afrika na wa Iran ili kujadili ushirikiano wa karibu. Picha hapo huu inawaonyesha viongozi wa Afrika wakiwa na rais wa Irani mara wakati wa mkutano.

Viongozi wa Palestina na wa Izrael wakuatana tena.
Sharm el Sheikh. Misri-14/09/2010. Viongozi wa Izrael na Palestina wamekutana leo ili kwa mara ya pili tangu kuanza kwa mazungumzo kujadili swala zima la usalama la eneo hilo.
Viongozi hao, Benjamin Netanyahu Waizrael na Mahmud Abbas wa Wapalestina walikutana wakati serikali ya Amerika ikiwa inasisitiza kuwepo na mazungumzo yatakayo fikia fuaka.
Mazungumzo hayo yalisimamiwa na waziri wa mambo ya nje wa Amerika Bi Hillary Clinton.
Picha hapo juu wanaonekana waziri mkuu wa Izrael Benjamini Netanyahu akipeana mkono na kiongozi wa Wapalestina Mahmud Abbas mara baada ya mkutano.

Saturday, September 11, 2010

Waamerika wawakumbuka waliopoteza maisha Septemba 11

Waamerika wawakumbuka waliopeteza maisha Septemba 11.

New York, Amerika - 11/09/2010. Wananchi wa Amerika leo wamekusanyika jijini New York na Washington na kufanya maombi ya kuwakumbuka watu wote walio uwawa wakati wa mashambulizi ya kigaidi yaliyo fanywa na kundi la Alqaeda miaka tisa ilyo pita.
Picha hpo juu inaonekana moja ya ndege ikielekea kulipua jengo maarufu lililo kuwa linajulikana kama Trade Centre.
Picha ya pili ni ya eneo ambalo majengo yaliyo angushwa baada ya mashambuli ya Alqaeda, yakionekana kwa juu.
Picha ya tatu wanaonekana rais wa Amerika Baraka Obama na mkewe Michelle Obama wakiwa wamesimama kuwakumbuka wale wote walio poteza maisha yao wakati wa mashambulizi ya Septemba 11 2010.
Serikali ya JD Kongo yapiga marufuku uchimbaji haramu wa madini.
Kinshasa, JDK- 11/09/2010. Rais wa Kongo (JDK) amepiga marufuku uchimbaji wa madini yaiona yote kwenye majimbo matatu likiwemo jimbo la Kivu ya Kusini.
Rais Joseph Kabila, alitoa amri hiyo mapema alipo tembelea mjini wa Mashariki wa wa Walikale, mji ambao unashutumiwa kwa kuongoza matendo ya ubakaji wa wanawake, kwa mujibu wa UN repoti.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya vijana wakiwa wamebeba siraha amabzo hununliwa baada ya uuzaji haramu wa madini yanayo chimbwa katika maeneo yaliyo pigwa marufuku.

Tuesday, September 7, 2010

Bi, Julia Gillard kuiongoza Australia.

Bi, Julia Gillard kuiongoza Australia.

Sydney, Australia - 07/09/2010. Wanchi wa Australia wataendelea kuongozwa na Bi, Julia Gillard baada ya kuungwa mkono na vyama vingine.
Bi, Julia Gillard atakuwa waziri mkuu wa Australia baada ya uchaguzi mku ulio fanyika mwisho wa mwezi wa nane mwaka huu chni ya chama cha Labor Party.
Picha hapo juu anaonekana, Bi Jullia Gillard akiongea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Monday, September 6, 2010

Paul Kagame aapishwa kuwa rais wa Rwanda kwa muhula wa pili.

Paul Kagame aapishwa kuwa rais wa Rwanda kwa muhula wa pili. Kigali, Rwanda - 06/09/2010. Wanachi wa Rwanda wameshuhudia kwa mara nyingine tena kuapishwa kwa rais aliyechaguliwa baada ya uchaguzi mkuu kumaliziaka tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994. Paul Kagame 52, ameapishwa kuwa rais wa Rwanda kwa mara ya nyingine tena, baada ya kushsinda uchaguzi mkuu iliyo shirikisha vyama vingi. Akiongea baada ya kuapishwa, rais Paul Kagame, alisema "umefikia wakati wa Afrika kujisimamia wenyewe na hakuna kipya cha kujifunza kutoka nchi za Ulaya." Sherehe hizo ziliuzuliwa na vingozi wa nchi jirani, Afrika na wageni wengine waaalikwa. Pichas hapo juu anaonekana rais Paul Kagame akiapa kuwa rais wa Rwanda kwa mara ya pili.

Amani kati ya Waizrael na Wapalestina mjadala tata.
Tel-Aviv, Izrael - 06/09/2010. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael, Avigdor Lieberman, amesema mazungumzo na makubaliano ya kuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina yatachukua miaka au kufikia kizazi kijacho.
Avigdor Lieberman alisema "siamini ya kuwa makubaliano ya amani na Wapalestina yanawezekana kwa sasa na yatachukua miaka na hata kufukia kizazi kijacho."
Maoni hayo ya waziri wa mamba oa nje wa Izrael, yamekuja wakati viongozi wa Palestina na Izrael chini ya usimamizi wa serikali ya Amerika wanakutana ilikutafuta mbini mbadala za kuleta amani kati ya majirani hao.
Picha hapo juu anaonekana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael Vigdor Lieberman, ambaye amesema swala la amani halita fikiwa kwa sasa.
Waziri mkuu wa Lebanon akili kufanya makosa.
Beiruti, Lebanon - 06/09/2010. Waziri mkuu wa Lebanon amesema "kuishutumu Syria kuhusika na kifo cha marehemu baba yake Rafik al Hariri, aliyefariki kwa mlipuko wa bomu mwka 2005 kuliletwa na mivutano ya kisiasa."
Saad al Hariri,aliyasema hayo wakati alipo kuwa anaongea na mwandishi wa habari wa Asharq-Awsat lenye makao yake jijini London.
Tangu kifo cha Rafikia al Hariri, Syria imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa kwa kuhusika na kifo chake.
Picha hapo juu waneonekana waziri mkuu wa Lebanon, Saad al Hariri akiongea ana rais wa Syria Bashar al Assad wakati walipo kutana.

Sunday, September 5, 2010

Fidel Castro ataadhari dunia na nguvu za kinyuklia.

Fidel Castro ataadharisha dunia na nguvu za nyuklia. Havana, Kuba - 05/09/2010. Rais wa zamani wa Kuba Fidel Castro, ameitaadhalisha dunia kuhusu hali iliyopo ambayo nchini zenye nguvu za kinyuklia zitaendelea kusukumana na Iran basi huenda zikaamua kutumia nguvu za kinyuklia jambo ambalo litahatarisha dunia kwa ujumla. Fidel Castro 84, akihutubia mbele ya watu wapatao 11,000 alisema " ikiwa Amerika na washirki wake wataendele kuiwekea Iran vikwazo kutokana na nchi ya Iran kutokubaliana na matakwa yao ( Amerika) na washiriki wake kunaleta wakati mgumu na hivyo wakati umefika watu wote duniani washirikiane kuzuia matumizi ya nguvu za kinyuklia yasitumike." Picha hapo juuanaonekana Fidel Castro akiwasalimia baadhi ya watu waliohudhulia wakati wa hotuba yake.

Bei ya vyakula yaleta mashaka nchini Mozambili.
Mozambiki, Msumbiji - 05/09/2010. Maelfu ya wanachi wa Mozambiki wamepambana na polisi wakati wa maandamano ya kupinga kupanda bei ya vyakula nchini humo.
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la msalaba mwekundu polisi walitumia risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi ili kuwasambaza watu waliokuwa wanaandamana.
Msemaji huyo alisema "kutokana na maandamano hayo viongozi wa serikali wamakuwa wakiwatembelea wananchi na kueleza hali halisi ili kupunguza ghasia."
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa wapo katika mstari ili kununu chakula.
Ugonjwa wa kipindupindu waleta maafa Afrika ya Kati.
Njdamena, Chad - 05/09/2010. Ugonjwa wa kipindupindu umeua watu wapatao 41 nchini Chad
Msemaji wa wizara ya afya ya Chad Mohamat Mamadou alisema "hadi kufikia sasa kuna watu wapato 600 wamepata maradhi hayo ya kipindupindu."
Msemaji huyo wa wizara ya afya ya Chad, alisisitiza kwa kuongeza ya kuwa karibu eneo zima la Afrika ya Kati limekumbwa na ugonjwa huo.
Ugonjwa wa kipindupindu, humsababisha mtu kuarisha na kupungua maji mwilini na hata kusababisha kifo.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wagonjwa wakiwa wamelazwa katika hospitali moja nchni Chad kwa ajili ya kupata matibabu.

Wednesday, September 1, 2010

Hali ya usalama nchini Somalia yazidi kushutua dunia

Hali ya usalama nchini Somalia yazidi kushutua dunia. Mogadishu,Somalia - 01/09.2010. Wakazi wa mji wa Mogadishu wamekuwa katika hali ya wasiwasi tangu kundi la al-Shabaab kuaendelea kushambulia mji la Mogadishu Kundi la al Shabaab lilitangaza hivi karibuni ya kuwa linaanza mashambulizi rasmi kushambulia majeshi yote ya kigeni ambayo yamo nchini humo. Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa wanamsaidia mama mmoja ambaye alipata mshituko mara baada ya kundi la al Shabaab kuanzisha mashambulizi.