Thursday, February 26, 2009

Fedha za rais wa Gabon zafilisiwa nchini Ufaransa.

Fedha za rais wa Gabon zafilisiwa nchini Ufaransa.

Paris,Ufaransa - 27/02/09. Uongozi wa serikali ya Ufaransa, umefirisi fedha za rais wa Gabon, Omar Bongo Ondimba,
Uamuzi wa kufirisi fedha zake umekuja baada ya koti iliyopo Bordeaux kutoa uamuzi wa kutaka rais, Omar Bongo, kulipa fedha zilizo ingia kwenye akaunti yake, ili mfanya biashara wa Kifaransa, Rene Cardona aachiliwe kutoka jela.
Pesa zipatazo Us-$580,000, zilitolewa na mtoto wa mfanya biashara huyo, ili babayake aachiwe kutoka jela.
lakini hata hivyo koti, iliamua ya kuwa fedha hizo zilitolewa kinyume cha sheria, na kuamuliwa zirudishwe mara moja.
Picha hapo juu anaonekana rais, wa Gaboni, Omar Bongo Ondimba, akicheza muziki kusherekea miaka 70, tangu kuzaliwa kweke.
Picha ya pili anaonekana,rais, Omar Bongo, alipo kuwa moja ya mikutano ya kimataifa hivi karibuni.
Syria na Amerika kuanza mazungumzo hivi karibuni.
Washington, Amerika 27/02/09 - Ofisi ya Syria kwenye umoja wa Mataifa, imesema yakuwa serikali ya Amerika na Syria zitaanza mazungumzo hivi karibuni ili kujadiri hali ilivyo mashariki ya Kati.
Mazungumzo hayo yata wakutanisha balozi wa Syria wa nchini Amerika na viongozi wa Amerika wanaoshughulikia maswala ya mashariki ya Kati.
Katika mkutano hu watazungumzia swala la amani na hali halisi ya Mashariki ya kati kwa ujumla.
Picha hapo juu inaonekana bendera ya nchi ya Syria, nchi ambayo imekuwa inalaumiwa na Amerika kwa kujihusisha na kuyumba kwa hali ya usalama katika eneo hilo, hasa kwa kuunga mkono makundi ya Wapalestina ya nayo pingana wa Waizrael.
Picha ya pili, ni ya bendera ya Amerika, nchi ambayo imekuwa haina uhusiano mzuri na nchi ya Syiria.
CIA yasema Kim Jongo Il, bado ashikilia uskani.
Pyongyang,Korea ya Kaskazini - 27/02/09.Shirika la Kijasusi la Amerika -CIA- limesema ya kuwa kiongozi wa Jamuhuri ya Korea ya Kaskazini,Kim Jong Il, bado anaongoza nchi, japokuwa imeripotiwa hali yake ya afya siyo nzuri.
Haya yalisemwa na Leon Panetta wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari, kuhusu nia ya Korea ya kaskazini, kutaka kurusha mizimga ya ke ya masafa marefu kwa majaribio.
Picha hapo juu anaonekana kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong Il,akiongea na baadhi ya viongozi wa Korea ya Kaskazini,kabla ya kuwa kwenye matibu kwa kipindi kilefu sasa.
Vyama vya Wapalestina kukubaliana kushirikiana kimsingi.
Kairo,Misri - 27/02/09. Makubaliano ya kimsingi yamefikiwa kati ya vyama pinzani vya Fatah na Hamas ambayo vinaongoza Wapalestina ili kujadili jinsi gani vinaweza shirikiana.
Baada ya mkutano huo uliofanyika Misri, mmoja ya kiongozi wa Fatah,Ahamed Qurei, alisema uamuzi huo ni kwa ajili ya Wapalestina wote waishio Ukanda wa Gaza na West Bank.
Hata hivyo, kiongozi huyo akuelezea kiundani zaidi nini makubaliano yapi watajadili.
Picha hapo juu, ni ngao ya bendera ya Fatah, chama ambacho kimekuwa kikipigania haki za Wapalestina tangu kianzishwe mwaka 1954.
Picha ya pili ni ya ngao ya chama cha Hamas, chama ambacho kimekuwa kikipigania Wapalestina, huku kikiwa na mwelekeo tofauti na Fatah.

Wednesday, February 25, 2009

Ajari ya ndege yatokea nchini Uhollanzi.

Amani ya Somalia ni mthiani mgumu kwa Jamii ya kimataifa.

Mogadishu, Somalia - 25/02/09.Watu wapatao 48, wameuwawa,huku vita vikendelea katika maeneo ya jiji Somalia kati ya makundi ya kijeshi kwa kushirikiana na jeshi la Muungano la Afrika na kundi kubwa la Al Shabab.
Katika vita hivyo wanajeshi wa muungano wa jeshi la Afrika, pia limewapoteza wanajeshi wake sita ambao wanatokea nchini Burundi.
Kufuatia hali hii, inampa wakati mgumu, rais mpya wa Somalia, Sharif Ahmed, kuweza kuunda serikali ya muungano.
Picha ya hapo juu wanonekana, baadhi ya wanajeshi wa wa muungano wa Afrika, wakiwa katika doria.
Picha ya pili wanonekana baadhi ya wapiganaji wa moja ya kikundi kinacho pinga serikali ya ya Somalia wakiwa katika moja ya maeneo yao,huku wakiwa wamebeba siraha tayari kwa vita pindipo vikitokea.
Ajari ya ndege yatokea nchini Uhollanzi.
Amsterdam,Uhollanzi-2/02/09.Watu wapatao tisa, wamepoteza maisha baada ya ndege ya shirika la Usafiri la Uturuki kuanguka,nchini Uhollanzi karibu na kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Amsterdam.
Katika ajari hiyo, watu wengine wapatao 50, wamajeruhiwa vibaya kati ya abiria 135 walio kuwemo kwenye ndege hiyo.
Ndenge hiyo namba TK1951, iliyo kuwa ikitokea jijini Instambul kuelekea Amsterdam, ilipotea njia ya kutulia na kuanguka na kukatika vipande vitatu.
Hata hivyo, wataalaam wa mambo ya usalama wa ndege wanaendelea na uchunguzi kujua nini chanzo cha ajali hiyo.
Picha hapo juu, inaonekana ndege ya shirika la ndege la Uturuki, ikiwa imeharibika vibaya sehemu za nyuma ya ndege hiyo.
Picha ya pili ineonesha, ndege ikiwa imeanguka karibu na maeneo ya makazi ya wanachini

Friday, February 20, 2009

Kesi ya aliyemrushia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika ya hairishwa.

Papa wapunguza mashambulizi kwa binadamu"Wasema wataalaamu".

Frolida, Amerika - 20/02/09.Wataalamu wa tabia ya viumbe viishivyo baharini ,wamesema mashambuli ya papa kwa binadadmu yamepungua kwa kiasi kikubwa katika mwaka 2008kwa kulinganisha miaka mitano iliyo pita.
Akiongea hayo, mwanasayansi anayeshughulikia tabia za papa, alisema mwaka 2008, papa walipunguza mashambuli kwa binadamu,kwani ni watu wawili walipoteza maisha kutokana na kujeruhiwa na papa, nchini Mexico, Amerika mmoja na Australia mmoja.
Picha hapo juu anaonekana papa, akiwa amemza binadamu maara baada ya kushambulia.
Picha ya pili, anaonekna papa, akiluka juu ya maji tayari kushambua kitu chochote anacho hisi kipo mbele yake.
Kesi ya aliye mrushia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika ya hairishwa.
Baghdad,Irak-20/02/09. Wanachi wa Irak, wamshuhudia Muntedar al Zaidi mwenye miaka 30, akifikishwa mahakamani kwa kosa la kumtupia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika, George Bush, wakati alipo fanya ziara nchini Irak, kabla ya muda wake wa kuwa rais wa Amerika kuisha.
Muntader al Zaidi, alifika mahakamani, hasubuhi ya siku ya alkhamis 19/02/09, huku akishuhudiwa na ndugu ,jamaa, marafiki, wanasheria, wanasiasa na wanchi wengine.
Katika kesi hiyo,watu walisikika wakipiga kelele, ambazo zilimpa wakati mgumu hakimu na kuchukua muda zaidi ya saa na dakika 15.
Hata hivyo, hakimu alihairisha kesi hadi 12/machi/2009
Zimbabwe yaitaji billion 5$- dola,"Asema waziri mkuu"
Harare,Zimbabwe - 20/02/09. Waziri mkuu mpya wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amesema,ili kujenga na kunyanyua uchumi wa Zimbabwe,kunaitajika zaidi ya billion 5$ - dola.
Na hii inaitakuja kutoka na vitega uchumi vitakavyo wekwa na wawekezaji.
Waziri mkuu, huyo wa Zimbabwe, aliyasema haya wakati alipo kuwa baada ya kukutana na rais wa Afrika ya Kusini na waziri wa fedha,ili kujadili ni njia zipi zita tumika kusaidia kunyanyua haraka uchumi wa Zimbabwe.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Zimbabwe, nchi ambayo imekuwa katika hali mbaya ya kiuchumi tangu kuanza matatizo ya kisiasa,baada ya uchaguzi mkuu wa uliofanyka mapema mwaka 2008.
Picha ya pili anaonekana waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, akiongea huku akiangali kwenya faili lake lililo juu ya kijukwaa, nakujaribu kuafafanua kwa undani, huku akionyesha mikono juu, kuashiria hali ya uchumi ya Zimbabwe, inahitaji kujengwa upya.
Kiongozi wa Likud, Benjamin, Netanyahu, atakiwa kuunga serikali.
Jerusalem, Izrael- 20/02/09 - Rai wa Izrael, Shimon Peres, amembomba kiongozi wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu kuunga serikali ya muungano kwa muda usiopungua wiki sita.
Rais, Shimon Peres, alimuomba, bwana Benjamin Netanyahu, wakati walipo kutana, na baadaye kuongea katika mkutano uliofanyika Jerusalem.
Katika, mkutano huo, bwana, Benjamini Netanyahu, aliwaomba viongozi wa vyama pinzani kuungana kwa pamoja, ili kuweza kuunda serikali kwa ajili ya wana nchi Izrael.
Picha ya hapo juu wanaonekana, rais, Shimon Peres na kiongozi wa chama cha Likud, bwana Benjamin Netanyahu, wakisalimiana muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo.
Picha ya pili, anaonekana, kiongozi wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu, akiongea kwa kusisitiza lazima waungane ili kujenga Izrael.
Tamil Tager washambulia ndani ya jiji la Kolombo"Hali si swali Sri Lanka"
Kolombo, Sri Lanka - 20/02/09. Watu wapatao 50 wamjeruhiwa vibaya na wengine wawili kuuwawa baada ya ndege za kijeshi la kundi la Timil Tiger, kushambulia ndani ya jiji la Kolombo.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Sri Lanka,Kaheliy Rambukwella, alisema yakuwa ndege hizo zilishambulia majengo ya serikali.
Hata hivyo moja ya ndege hizo za kijeshi, ilishambuliwa na ndege za jeshi la serikali.
Mapambano kati ya jeshi la serikali na kundi la Tamil Tiger ambalo linagombani kujitenga na serikali.
Picha hapo juu, zinaonekna gari zikiendeshwa kwa kasi ili kuepuka milipuko, mara ya milipuko kusikika karibu na mojo ya majengo yenye ofisi za serikali.
Picha ya pili ni ramani ya Sri Lanka, nchi amboyo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, tangu mwazo wa mwaka 1983.

Thursday, February 19, 2009

Rais, Baraka Obama, afanya ziara yake ya kwanza nje ya Amerika tangu kuapishwa kuwa rais wa Amerika.

Hakuna amani mpaka askari wetu aachiliwe huru"Serikali ya Izrael ya dai"

Cairo, Misri - 19/02/09. Makataba wa makubaliano wa kuleta amani katika ukanda wa Gaza,umeingia katika hatua nyingine ya utata.
Habari kutoka katika serikali ya Misri, zimesema, jambo la serikali ya Izrael kusema ya kuwa, ili pawepo na amani, ni lazima askari wa Izrael aliye kamatwa mwaka 2006, aachiwe huru na kundi la hamas, litaleta ugumu wa kuwepo na amani ya kudumu katika maeneo ya Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa habari hizo zina sema, katika mkataba huo hakukua na makubaliano au maelezo ya aina yoyote yanayo husu kuachiwa kwa askari huyo ndipo kutaleta amani katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza.
Askari huyo, Gilad Shalit aliyekamatwa mwaka 2006 mwezi wasita karibu na mpaka wa Gaza.
Picha hapo juu ni Izrael, nchi ambayo imekuwa na wakati mgumu hasa kwa wanasiasa, ni njia gani watatumia kumpata askari Gilad Shalit, kutoka mikononi mwa kundi la Hamas.
Picha ya pili, ni ya moja ya bendera ya Hamas,kundi ambalo limekuwa likimshikilia askari Gilad Shalit tangu mwaka 2006.
Picha ya chini ni ya nchi ya Misri,nchi ambayo imekuwa ikijitahidi kuleta maelewano na mapatano kati ya Izrael na kundi la Hamas na uongozi wa Wapalestina kwa jumla.
Rais, Baraka Obama, afanya ziara yake ya kwanza nje ya Amerika tangu kuapishwa kuwa rais wa Amerika.
Ottawa, Kanada-19/02/09. Rais wa Maerika, Baraka Omaba, amefanya ziara ya kwanza ya kimataifa nchini Kanada tangu ahapishwe kuwa rais wa Amerika.
Rais, Obama, katika ziara hiyo, anatarajiwa kuzungumzia kiundani zaidi ushirikiano wa karibu wa nchi hizi mbili na na wenyeji wake viongozi wa Kanada.
Picha hapo juu, wanaonekna baadhi ya watu, wakiwa wamebeba mabango ya kumkaribisha rais wa Amerika, Baraka Obama, nchini Kanada ikiwa ndiyo ziara yake ya kwanza ya kiserikali tangu awe rais wa Amerika.
Picha ya pili, anaonekna rais wa Amerika ,Baraka Obama, akipewa saruti na mmoja ya wanajeshi wa Kanada, wakati alipo wasili kwenye uwanja wa ndege.
Picha ya tatu, wanaonekana, rais wa Amerika , Baraka Omaba, na mwenyeji wake,Mkuu wa jimbo la Ottawa,Michelle Jean, wakikagua gwaride la heshi lililo andaliwa na kwa ajili ya rais Baraka Obama.
Muungano wa Ulaya wakosolewa na rais wa Czech.
Brussel, Belgium-19/02/09.Rais wa Czech, Vaclav Klaus,amekosoa utendaji wa Muungana wa nchi za Ulaya kwa kufanya baadhi ya kazi ambazo zinaenda kinyume na Muungano huo.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge na wengine kutoka nje, rais Vaclav Klaus, alisema yakuwa umoja huo umekuwa na muundo ambao hautoi nafasi zaidi, kwani wale wanaotoa mawazo yao tofauti wamekuwa wakiitwa wana pinga Muungano wa Ulaya.
Picha hapo juu, anaonekna rai wa Czech, akinyoosha kidole kusisitizia nini anamaaanisha, wakati alipo hutubiwa bunge la Muungano wa nchi za Ulaya.
Bunge lapiga kura, kufunga kambi ya jeshi inayo tumiwa na Amerika.
Manas,Kirgizstan-19/02/09.Bunge la Kirgizstan limepiga kura kwa wingi kufunga kambi na uwanja wa ndege uliopo nchini humo kwa matumizi ya jeshi la Amerika.
Katika kura hizo zilizo pigwa,kura zilizo kubali kufungwa kwa kambi na kiwanja hicho cha ndege zilikuwa 78 na zilizo kataa kufungwa kwa kiwanja hicho ni kura 1.
Kambi hiyo iliyo kuwa muhimu kwa jeshi la Amerika katika kuendeleza vita vyake nchini Afghanistan,imetakiwa kufungwa kwa kipindi kisicho pungua miezi sita.
Picha hapo juu zina onekana ndege za kijeshi za Amerika, zikiwa zimesimama kwenye uwanja huo uliopo Manas na ndege nyingine inaonekna ikikaribia kutua uwanjani.
Picha ya tatu, anaonekana mmoja ya wanajeshi wa Amerika, akiwa amebeba zana zake, na miezi michache hatakuwa tena katika eneo la Manas kama kambi yake (yao) ya kijeshi.

Tuesday, February 17, 2009

NATO kuangalia kwa makini makubaliano ya Taliban na Pakistan.

Venezuela wapiga kura ya maoni" Rais ataweza kutawala zaidi ya miula miwili"Wakubali wanachi wa Venezuela".

Caracas,Venezuela - 17/02/09. Wananchi wa Venezuela, wamepiga kura ya maoni kupitisha mswaada wa kumruhusu mwanachi yoyote ambaye atakuwa rais, kuweza kutawala zaidi miula miwili iliyo kuwa imewekwa hapo mwanzo katika katiba ya Venezuela.
Kura zilizo kubali mswada huo zilifikia asilimia 54, na kukubaliana na mswada huo ulio pendekezwa na rais Hugo Chavez.
Kufuatia kura hiyo rais, wa sasa wa Venezuela, Rais, Hugo Chavez ataweza kugombania tena urais pindipo kipindi chake cha urais kitakapo kwisha mwaka 2012.
Picha hapo juu anaonekna , rais Hugo Chavez, akiongea na wanchama na wanchi walio kuja kumsikiliza baada ya matokeao ya kura ya maoni.
Picha ya pili, wanaonekana melfu ya wananchi wakishangilia, baada ya ya matokeo ya kura ya maoni kutangazwa.
NATO kuangali kwa makini makubaliano ya Taliban na Pakistan.
Mingora, Pakistan - 17/02/09.Nchi wanachama wa NATO, wa wameonya kuhusu serikali ya Pakistan kuanza kuongea na kundi la Taliban.
Onyo ilimekuja baada ya serikali ya Pakistan, kukubali kuwepo kwa sheria za kidini katika jimbo la Swat.
Kwa mujibu wa NATO, wanaangali kwa makini sana hali hii.
NATO ambayo inawanajeshi zaidi ya 55,000 katika maeneo tofauti kati ya mipaka ya Afghanistan na Pakistani katika vita vya kupambana na ugaidi.
Picha hapo juu ni bendera ya NATO na bendera zanchi wanchama wake.
Iran na Urusi zafanya mazungumzo ya ushirikiano wa kijeshi.
Teheran,Iran - 17/02/09.Serikali ya Iran inafanya mazungumzo na serikali ya Urusi, katika jitihada za Iran kuweza kushirikiana na Urusi katika nyanja za kijeshi
Mazungumzo hayo yaliyo wakutanisha waziri wa ulinzi wa Urusi, Anatoly Serdyukov na waziri wa ulinzi wa Iran, Mostaf Najar, yalilenga hasa ji jinsi gani serikali ya Irani itaweza kupata mizinga ya kijeshi ya kuzuia ushambuli wa anga.
Picha hapo juu ni picha ya ya moja ya mitambo ya kijeshi ya Iran,ambayo ipo kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya anga.
Serikali ya Amerika yaionya Korea ya kaskazini.
Tokyo,Japan - 17/02/09. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi, Hillary Clinton ameionya serikali ya Korea ya Kaskazini, ya kwamba mpango wake wa kutaka kujaribu kurusha mabomu ya nyukili kitakuwa ni kitendo ambacho jumuia ya kimataifa haitakikubali.
Bi, Hillary Clinton,aliyaongea haya wakati alipo kutana na viongozi wa serikali ya Japan, ambapo yupo ziarani nchini humo Japan.
Picha ya hapo juu anaonekana , Bi Hillary Clinton,akisalimiana na waziri wa mabo ya nchi za nje wa Japan Hirofumi Nakasone,mapema walipo kutana mjini Tokyo.

Thursday, February 12, 2009

Hakuna kesi zidi ya rais wa Sudan"Mahakama ya kataa"

Sheyi Emanuel Adebayo, achaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa msimu wa 2008 - 2009.

Lagos,Nigria-10/02/09.Shirikisho la chama cha mpira la Afrika.,limemchagua mchezaji wa timu ya taifa ya Togo na Arsenal, Sheyi Emanuel Abebayo kuwa mchezaji bora wa bara la Afrika wa ,baadaya kuwashinda kwa kura wachezaji wengini walioshirikishwa katika uchaguzi huo.
Picha hapo juu anaonekana Emanuel Adebayo,akiwa ameshikilia zawadi aliyo pewa baada ya kushinda kuwa mchezaji bora wa Afrika.
Picha ya pili anaonekana Solmon Kalou akiwa ameshikilia zawadi aliyo pewa baada ya kuchaguliwa kuwa mchezai bora mwenye umri mdogo.
Kadima ya shinda uchaguzi nchini Israel "Bi Tzipi Livni huenda akawa waziri mkuu mpya".
Jerusalem,Israel - 12/02/09.Waziri wa mambo yanchi za nje wa Israel, Tzipi Livni,ameshinda uchaguzi mkuu ulio fanyika nchini Israel kwa kuranyingi zaidi kuliko vyama vyote vilivyo shiriki katika uchaguzi huo kwa chama chake kupata viti 28.
Bi, Tzipi Livni ambaye aligombani kupitia chama cha Kadima, aliweza kuwashinda wapinzani wake, hasa mpinzani wake mkuu Benjamini Netanyahu, ambaye aligombani kupitia chama cha Likud.
Hata hivyo kwa mujibu wa katiba ya Israel, itakuwa vigumu kwa Kazima kuongoza nchi kwani ni lazima kishilikiliane na vyama vingine ili kuweza kufikisha idadi kamili ya viti katika bunge ili kuweza kuongoza nchi.
Picha hapo juu anaonekna waziri wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni, akionyesha mikono yake miwili kuonyesha ishara ya ushindi kwa wanachama na wakereketwa wa chama chake cha Kadima.
Picha ya pili, ni ya Benjamini Netanyahu, ambaye chamchake cha Likud,kimekuwa cha pili kwa kimepata viti vingi, hivyo huenda kikashirikishwa kuunda serikali mpya ya Israel.
Moto mkubwa waleta maafa nchini Australia."Wawili wakamatwa"
Sydney,Australia-12/02/09. Polosi nchini Australia wamawakamatwa watu wawili, kwa kushukiwa kuanzisha moto ambao umeleta maafa makubwa na kupoteaz maisha ya watu wapatao 200.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi,Christine Nixon, alisema yakuwa uchunguzi bado unaendelea.
Kufuatia moto huo, serikali ya Australia imetangaza siku moja ya maombelezi kwa maafa yaliyo letwa na moto huo.
Picha hapo juu, anaoneknana polisi akiangalia ni kiasi gani gari lilivyo ungua kutokana na moto ambao umeshutua mamilioni ya wa Australia.
Meli yenye siraha yaachiwa na wateka nyara wa Kisomalia.
Nairobi, Kenya- 12/02/09.Kundi lililo kuwa likishikilia meli ya Ukraine kwa muda wa miezi mitano, wameiachia na sasa ipo mikononi mwa serikali ya Kenya.
Meli hiyo MV Faina, mabayo ilikuwa imebeba zana za kijeshi, iliwasili katika bandali ya Mombasa na wafanyakazi wake wote.
Picha hapo juu, wanaonekna baazi ya watu wakiangali kwa mbali meli iliyo kuwa imetekwa ikiwa imepiga nanga katika bandari ya Mombasa.
Hakukua na kesi zidi ya rais wa Sudan"Mahakama yakataa".
The Hague,Netherland - 11/02/09.Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia kesi za makosa ya jinai iliyopo mjini the Hague, imesema yakuwa hakukua na kibali cha kukamatwa kwa rais wa Sudan, Omar Al Bashir.
Kwa mujibu wa mujibu wa masemaji wa mahakama hiyo iliyopo nchini Netherland,Sonia Robla, alisema hakuna kibali kilichotolewa kwa kukamtwa kwa rais, Omar Al bashir, msemaji huyo,alisema haya alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.
Picha hapo juu anaonekna rais wa Sudan,akiongea na wandishi wahabari, kuhusu hali halisi ya nchi yake.
Picha ya pili anaonekana raia Omar Al bashir, wa Sudan akiwasili katika moja ya mikoa iliyopo nchini Sudan, ili kukagua maendeleo.
Zimbabwe yapata Waziri Mkuu Mpya.Morgan Tsvangirai awa Waziri Mkuu .
Harare, Zimbabwe - 12/02/09.Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, amaehaidi kurudisha hali ya uchumi na jamii katika hali yake ya kawaida, baada ya kuapishwa kuchukua ofisi kama waziri mkuu mpya wa Zimbabwe.
Waziri Mkuu, Morgani Tsvangirai, ambaye ni kiongozi wa chama cha MDC (Movement of Democratic Change), amekuwa akivutana na rais Robert Mugabe, baada ya uchaguzi mkuu ulio fanyika mapema mwaka 2008.
Picha hapo juu anaonekana, kiongozi wa MDC, Morgan Tsvangirai, akiapishwa kuwa waziri mkuu, na rais wa Zimbabwe,rais Robert Mugabe 11/02/09.
Picha ya chini wanaonekana,kutoka kushoto ni rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kati ni Morgan Tsvangirai na aliyekuwa rais wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki,wakipeana mikono mara baada ya kumaliza kukubaliana kutia sahii mkataba wa kuongoza serikali pamoja.

Tuesday, February 3, 2009

Muungano wa nchi za Afrika wamchagua rais wa Libya kuwa Mwenyekiti.

Muungano wa nchi za Afrika wamchagua rais wa Libya kuwa Mwenyekiti.

Adis Ababa,Ethiopia - 03/02/09 - Muungano wa nchi za Afrika, umemchagua rais wa Libya Muammar Gadafi kuwa mwenyekiti wa muungano huo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia februari 2- 2009.
Rais Muamaar Gadafi,ambaye amekuwa akisisitiza kuungana kwa nchi za Afrika ndiyo njia pekee ya itakayo iponya Afrika na kutaweka heshima ya Afrika.
Katika ufunguzi wa mkutano huo, muungano wa nchi za Afrika, zilitaka vikwazo vilivyowekwa zidi ya Zimbabwe viondolewe, kwani viongozi wa nchi hiyo wamekubali kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga Zimbabwe.
Picha hapo juu, anaonekna rais wa Tanzania Jakaya . M. Kikwete,ambaye muda wake wakuwa mwenyekiti wa wa muungano wa nchi za Afrika umekwisha akihutubia katika moja ya mikuta ya kuwakaribisha viongozi wa Afrika walipo tembelea nchi yake.
Picha ya pili,ni ya rais wa Libya, Muammar Gadafi,ambaye ndiye mwenyekiti aliyechukua kiti cha uwenyekiti wa muungano wa nchi za Afrika kutoka kwa rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akisikiliza kwa makini wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ulio fanyaka Adis Ababa Ethiopia.
Kundi la FARC nchini Kolombia, la achia mateka wengine.
Bogota, Kolombia - 03/02/09. Kundi linalo pingana na serikali ya Kolombia, FARC, limewaachia mateka wanne lililo kuwa likiwashikilia kwa muda mrefu.
Baadhi ya watu waliochiwa huru ni gavana wa zamani, Aran Jara, mwenye umri wa miaka 51, aliyetekwa nyara mwaka 2001.
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la la msalaba mwekundu,Yves Heller,alisema Alan Jara, aliachiliwa huru, katika eneo lililopo kusini mwa Kolombia kwenye jimbo la Guaviere.
Picha hapo juu , wanaonekana wapiganaji wa FARC, wakiwa wanafanya doria, katika maeneo yao. Picha ya pili, anaonekana mmoja ya mateka walioachiwa na kundi la FARC, akiwasalimia ndugu na jamaa na marafiki waliokuja kumlaki.
Urusi na Belarus kudumisha ulinzi kati ya nchi zao.
Moscow,Urusi - 03/02/09. Serilikali ya Belarus na serikali ya Urusi, zimetiliana mkataba wa makubaliano ya kiulinzi, ili kudumisha ubola wa ulinzi kati ya nchi hizi mbili.
Makubaliano hayo yalifanyika nchini Urusi wakati rais wa Belarus, Alexander Lukashenko na mwenyeji wake, rais wa Urusi,Dmitry Medvedev.
Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo yaliyo chukua muda mrefu kati ya nchi hizi mbili.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Urusi, Dmitry Medvedev, akimkaribisha mgeni wake rais wa Belarus, rais Alexander Lukashenko, alipo wasili nchini kwa ziara ya kiserikali.
Picha ya pili, wanaonekana viongozi wa nchi zote mbili, Urusi na Belarus, wakiongea katika mkutano mara baada ya kutiliana sahii mkataba wa makubaliano ya kiulinzi mjini Moscow.
Picha ya tatu, anaoneka rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, akisalimiana na waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin, wakati alipo wasili nchini Urusi kwa ziara ya kiserikali.
Al-Shabab ya ahaidi kupigana na Majeshi ya Muungano wa Afrika.
Mogadishu,Somalia - 03/02/09.Kundi la Al-Shabab,linalo pingana na serikali ya Somalia, limesema ya kuwa litaanza kupigana namajeshi ya (AU African Union) majeshi ya Muungano wa Afrika. Akiongea hayo, mkuu wa kundi la Al-Shabab,Sheik Mukhtar Robow, alisema ya kuwa watawaimiza wananchi wote wa Somalia, kujiunga no kupigana na jeshi hilo, kwani wanauwa wanchi Wasomalia.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, watu wapatao 18, wali uwawa, baada ya basi walilo kuwa wame panda kushambuliwa na jeshi la muungano wa Afrika, inakuja baada ya jeshi hilo kushambuliwa na bomu lililo kuwa limetegwa barabarani kusini mwa Mogadishu.
Picha hapo juu wanaonekana wapiganaji wa kundi la Al-Shabab wakiwa wanafanya mazoezi ya kulenga kwa kutumia siraha.
Picha ya pili,anaonekana mmoja wa kina mama akilia kuonyesha kuomba msaada, kwani hali ya usalama nchini Somalia imekuwa ni ya kutisha.
Iran yarusha chombo Angani"Nimafanikio makubwa kwa Wairani"Asema rais wa Iran".
Tehran,Iran - 03/02/09. Iran imezindua na kurusha rasmi chombo cha kwenda angani.
Uzinduzi huo na urushwaji wa chombo hicho, kilichopewa jina Omid au Matumaini,ulishuhudiwa na rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad.
Akiongea mara ya chombo hicho kuruka angani, rais, Mohmoud Ahmadinejad, alisema hii ni mafanikio makubwa kwa Wairan wote.
Chombo hicho Omid, kitakaa angani kwa muda wa miezi mitatu, na madhumuni yake ni kuimarisha mawasiliano na kuangalia matukio ya asili.
Picha ya hapo juu wanaonekana Wanasayansi wa Kiirani wakiwa karibu na roketi iliyo tumika kurushia Omid.
Picha ya pili anaonekana rais wa Iran, Mohmoud Ahmadinejad,akipokea maelezo toka kwa mwana sayansi, wakati alipo tembelea eneo hilo kabla ya Omid kwenda angani.