Tuesday, December 28, 2010

Laurent Gbagbo akutana na viongozi wa ECOWAS.

Laurent Gbagbo akutana na viongozi wa ECOWAS.

Abidjan, Ivory Coast- 28/12/2010. Marais watatu wa jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi wamekutana na rais wa Ivoty Coast ili kujadili hali ya kisiasa nchini humo na kumtaka aachie madaraka. Marais hao ni Boni Yayi wa Benin, Ernest Bai wa Sierra Leone, na Pedro Pires wa Kape Verde walikutana na rais wa sasa Laurant Gbagbo kuzungumzia hali halisi ya myumbo wa kisiasa uliopo katika nchi hiyo. Marais hao kabla ya kuonana na Gbagbo, waliongea na Alassane Ouattara ambaye jumuia ya kimataifa inamtambua kama ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni. Hata hivyo hakuna habari zilizo tolewa kwa undani ili kwa pamoja walisema mkutano ulikuwa wa mafanikio. Picha hapo juu wanaonekana marais wa Laurent Gbagbo kushoto, Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone na Boni Yayi wa Benin wakiongea na waandishi wahabari mara baada ya kukutana kwao.
Urussi yazitaka nchi nyingine kuangalia mambo yao.
Moscow, Urussi - 28/12/2010. Serikali ya Urussi imezitaka serikali za nchi nyingine kutoingilia mambo yake na nchi hizo zitizame maswala ya nchi zao.
Uamuzi wa serikali ya Urussi kutoa tamko hilo umekuja mara baada ya baadhi ya nchi zikiongozwa na Amerika kulaumu kitendo cha mahakama nchini Urussi kumkuta na hatia Mikhail Khodorkovsky kwa kosa la kutumia mali na pesa za nchi kinyume cha sheria .
Waziri wa mambo ya nje wa Amerika Hillary Clinton, alisema " kitendo cha kuhukumiwa kwa Mikhail kinaleta mashaka kutokana na jinsi kesi hiyo ilivyo endesshwa."
Picha hapo juu anaonekana Mikhail Khodorkovsky akisikiliza hukumu ilipo kuwa inatolewa mbele yake.

Friday, December 24, 2010

Korea ya Kusini na Kaskazini wasiwasi wazidi kukuwa.

Makampuni ya Amerika yafanya biashara za kijamii na Iran.

New York, Amerika - 24/12/2010. Wizara ya biashara ya Amerika imetoa vibali kwa makampuni ili kufanya biashara nchini Iran kwa kipindi cha miaka kumi iliyo pita.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana vibali vipatavyo 10,000 vilitolewa kwa makampuni maalumu ili kufanya biashara za kusaidia jamii. Moja ya makampuni hayo ni Kraft Food, Pepsi na baadhi ya biashara za kibenki ambazo zilikuwa zinasaidia jamii katika maendeleo. Stuart Levey, msimamizi wa maswala ya vikwazo alisema " hii inafanyika kuhakikisha ya kuwa vikwazo visiathili watu hata wakafikia kukusa vyakula ambapo haitakuwa jambo la kiutu." Serikali ya Amerika iwekea Iran vikwazo ili nchi hiyo iweke wazi ukweli wake kuhusu mpango mzima wa mradi wake wa kinyuklia jambo ambalo Iran inalipinga na kukataa katakata kufanya hivyo. Picha hapo juu ni picha ya moja ya kampuni ambayo imewekeza kibiashara nchini Iran. Korea ya Kusini na Kaskazini wasiwasi wazidi kukuwa. Seoul, Korea ya Kusini 24/12/2010. Serikali ya Korea ya Kusini inaamini ya kuwa serikali ya Korea ya Kaskazini huenda ikafanya majaribio ya bomu la nyuklia mapema mwakani. Kutikana na ripoti kutoka wizara ya mabo ya nje ya Korea ya Kusini zinasema "majaribio hayo yatafanywa na Korea ya Kaskazini ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza na kuangalia uwezo wa wake wa nguvu za Kinyuklia. Na majaribio hayo yatasababisha hali kuwa ya wasiwasi zaidi kati nchi hizo mbili." Korea ya Kaskazini ilifanya majaribio tofauti ya kinyuklia mwaka 2006 na 2009 kwa mujibu wa habari zinazoeleweka kimataifa, lakini Korea ya Kaskazini yanyewe haijawai kutamka kuhusu swala hilo. Picha hapo juu anaonekana mmoja wa mwanajeshi wa Korea ya Kaskazini akiwa katika moja ya vituo vilivyopo mpakani na Korea ya Kusini tayari kwa kazi ya ulinzi huku akiwa ameelekeza bundiki tayari. ECOWAS uenda ikatumia nguvu nchini Ivory Coast. Abidjan, Ivory Coast - 24/12/2010. Viongozi wa shirikisho la uchumi wa Afrika ya Magharibi (ECOWAS) wamemtaka rais wa sasa wa nchi hiyo kuachia madaraka mara moja. Viongozi wa shirikisho la ECOWAS walisema "ikiwa rais Gbagbo hatafanya hivyo basi itabidi nguvu zaidi itumike." Agizo hilo lilitolewa na viongozi wa ECOWAS lenye nchi wanachama 15 wakati walipo kutana jijini Abuja kujadili hali halisi ya Ivory Coast. Vurugu za kisiasa nchi Ivory Coast zilizidi mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa na rais Laurant Gbagbo kudai ya kuwa ameshinda na huku mpinzani wake Alassane Ouattara akidai yeye ndiye aliye shida uchaguzi wa rais. Picha hapo juu anaonekana rais wa sasa wa Ivory Coast Laurent Gbagbo akiongea wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa rias.

Tuesday, December 21, 2010

Irak yapata serikali mpya.

India na Urussi kushirikiana kwa ukaribu zaidi. New Delhi, India - 21/12/2010. Serikali ya India na Urussi zimekubaliana kwa pamoja kushirikiana katika nyanja za kiusalama na kutiliana mikataba ya kibiashara uchumi na sayansi. Rais wa Urussi Dmirty Medvedev na waziri mkuu wa India Manmohan Singh walikubaliana mikataba hiyo wakati walipo kutana na kuzungumza ili kudumisha uhusiano zaidi. Ziara hiyo wa rais wa Urussi imekuja baada ya ziara za kufuatana za viongozi wa Uingereza, Amerika, China na Ufaransa kufanya ziarani nchini India ili kudumisha ushirikiano wakaribu. Picha hapo juu wanaonekana rais wa Urussi Dmirty Medvedev kushoto akipeana mkono na waziri mkuu wa India Manmouhan Singh mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao. Irak yapata serikali mpya.

Bagdad, Irak - 21/12/2010. Bunge la Iraki limekubaliana kwa pamoja kupitisha uteuzi wa waziri mkuu wa Irak na serikali yake na kutegua kitendawili cha kisiasa kilicho dumu zaid ya miezi tisa. Nouri al Maliki, ataiongoza serikali serikali ya Irak kwa kushirikisha makundi yote ya kisiasa ya Shia Sunn na Kurdi. Akiongea mara baada ya kupitishwa kwa serikali yake Nouri al Maliki alisema, serikali yake itajitahidi kwa kwa kila hali kuongoza wananchi wa Irak na ingawaje kwa sasa kunawakati mgumu ambao utasababisha baadhi ya mambo kuto fikiwa malengo kama ya livyo pangwa ili kuinua maisha ya wa Irak. Picha hapo juu anaonekana Nouri al Maliki kushoto akiwa na Ayad Allawi ambao hapo mwazo misimamo yao tofauti ilisababisha mvutano wa kisiasa kwa muda mrefu na kuleta wasiwasi mkubwa. Jeshi la umoja wa mataifa kuendelea kuwepo Ivory Coast.
Abidjan, Ivory Coast. 21/12/2010. Umoja wa Mataifa umekibaliana kwa pamoja kuendelea kuwepo kwa jeshi la Umoja la kulinda amani nchini Ivory Coast kwa kipindi zaidi cha miezi sita.
Jeshi hili lenye wapiganaji wapatao 10,000 litakuwa na majukumu mengine ya ziada, ikiwa ni kulinda wanchi na kupambana na mashambulizi ya aiana yoyote.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya rais wasasa Laurent Gbagbo, kulitaka jeshi hilo kutoka nchini humo mara muda wa makubaliana yaliyo wekwa utakapo kwisha.
Pia umija wa Ulaya na washiriki wake wamemwekea vikwazo rais Gbagbo na washirki wake wakaribu.
Msemaji wa Ikulu ya Amerika, Robert Gibbs alisema "inabidi Gbagbo aondoke madarakani mara moja."
Hata hivyo rais Laurent Gbagbo, bado anashikilia kiti cha urais huku akiungwa mkono na jeshi kwa kusaidiwa na wadau wake.
Picha hapo juu vinaonekana vifaru vya umoja wa mataifa vikiwa vimesimamishwa nje ya ofisi ya umoja wa mataifa iliyopo jiji Abidjan.

Thursday, December 16, 2010

Baraka Obama atangaza hali halisi ya Afghanistan.

Baraka Obama atangaza hali halisi ya Afghanistan. Washington, Amerika 15/12/2010 - Serikali na washiriki wake wanafanya kazi nzuri katika kuijengaAfghanistan na kuwaanda wananchi wa Afghanistan kuijenga nchi yao. Rais Baraka Obama, alisema "ingawaje hali ni ngumu lakini hii siyo kikwazo kwani, na nashukuru wale wote waliojitolea na kuendelea kujitolea pamoja na wapiganaji wetu ambao wanafanya kazi usiku na mchana ili kuijenga Aghanistan." Akiongezea rais alisema, "maendeleo yanaonekana na maendeleo haya ndiyo msingi mkubwa wa kuwafanya wananchi wa Afghanistan kuamini yakuwa kazi iliyo fanywa na jumuiya ya kimataifa ilikuwa ni kwa ajili ya wanachi wa Afghanistan." Baraka Obama, ameongea hayo ili kuwahakikishia wanachi wa Afghanistan ya kuwa Amerika ipo pamoja nao. Picha hapo juu anaonekana rais Baraka Obama, akiongea na waandishi wa habari ili kuzungumzia hali halisi ya Afghanistan na mipango ya kuisadia nchi hiyo kimaendeleo. Hatimaye mwanzilishi wa Wiki Leaks akubaliwa dhamana

London, Uingereza - 15/12/2010. Mahakama kuu jijini London imemwachia huru mwanzilishi wa Wiki Leaks baada ya mahakama ya mwanzo kukataa kumwachia huru kutokana na rufaa iliyo mtaka aendelee kukaa mahabusu.
Julian Assange 39 aliachiwa na kusema ya kuwa "anawashukuru wale wote walio changia kwa kiasi kikubwa hadi kuachiwa kwake na akasema ataendelea na kazi yake kama kawaida.
Assange anatakiwa Sweden kwa kosa la kufanya mapenzi ya kuchutukiza na moja ya wanamama wakati alipo kuwa nchini Sweden. Picha hapo juu anaonekana Julian Assange aliyeshikilia karatasi akitokea ndani ya mahakamani mara baada ya masharti ya dhamana kutimilizwa.
Serikali ya Amerika kuishitaki kampuni ya mafuta ya BP.
Washington, Amerika - 15/12/2010. Serikali ya Amerika imefungua kesi dhidi ya kampuni ya mafuta BP kutokana na uharibifu iliotokea baada ya mafuta machafu kuharibu mazingira katika pwani za Ghuba ya Mexico.
Mwanasheria mkuu wa Amerika, Erik Holder alisema, "uchafuzi wa mazingira ulio tokea ulisababishwa na BP kutofatilia sheria na kukamilisha maswala ya kiafya na usalama katika uchimbaji wa mafuta na tunaangalia ni kwa njia za kufanya ili kuhakikisha BP inawajibika kwa kuvunja sheria ya kuweka maji kuwa safi ( Clean Water Act )."
Uamuzi wa serikali ya Amerika kufuangua kesi dhidi ya BP, baada ya moja ya visima vyake kuvuja na kusambaza mafuta machafu katika Ghuba ya Mexico.
Picha hapo juu inaonyesha moja ya machafuko yaliyo sababishwa na mafuta machafu katika moja ya eneo la pwani ya Ghuba ya Mexico.
China na India kushirikiana kwa karibu zaidi.
New Dheli, India - 15/12/2010. Waziri mkuu wa China amefanya ziara nchini India ili kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili.
Wen Jiabao amekutana na waziri mkuu wa Manmohan Singh na kujadili maswala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hasa katika kukuza biashara ambapo huenda ikafikiwa kiasi cha $ 100 Billion.
Ziara hiyo ya waziri mkuu wa China nchini India inatafsiliwa kuwa imekuja wakati muafaka kwani India ni nchi ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi. Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, akikagua gwaride lililo andaliwa wakati alipo wasili nchini India.
Hakimu, Duncan Ouseley alikataa maombi ya mwana sheria wa serikali ya Sweden ya kutaka Julian Assange aendelee kukaa mahabusu kwa madai ya kuwa "anaweza kukumbia."
Kuachiwa kwa Julian Assange, kumewezekana mara baada ya wadau wake kuchangisha kiasi cha US dollar zipatazo laki tatu na robo, chini ya uongozi wa watu mashuhuri kama Jemina Khan,Bianca Jagger, Ken LOach na John Pilger.
Picha hapo juu anaonekana Julian Assange akiingia mahakamani kusikiliza ombi la dhamana yake ambapo hapo mwanzo alikataliwa na mahakama ya mwanzo.

Wednesday, December 15, 2010

Ghana kuanza kuzalisha mafuta.

Irak yaondolewa vikwazo na Umoja wa Mataifa. New York, Amerika - 15/12/2010.Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imeiondolea vikwaza nchi ya Irak iliyo kuwa imeviweka kwa muda wa zaidi ya miaka 19. Akiongea katika mjadala wa kutaka kuiondolea vikwazo Irak, makamu wa rais wa Amerika Joe Biden alisema "Irak inahitaji kuwa katika kiwango cha kimataifa kwa kujitegemea yenyewe na demokrasi ndiyo msingi mkubwa ambo utifanya nchi hiyo imeze kuendelea na Wairak wameonyesha uwezo huo. Pia ni muhimu kwa Irak kuwa na uhusiano mzuri na majirani zake kwani bado Wairak wanamthian mkubwa mbeleni." Katika kikao hicho, kamati ya usalama iliondo vikwazo vyote ilivyoviweka kwa Irak na kupitisha mswada ambao umeiruhusu Irak kuweza kujenga mtambo wa nyuklia kwa matumizi ya kawaida. Vikwazo kwa Irak viliwekwa mwaka 1991 na umoja wa Mataifa mara baada ya Irak kuivamia Kuwait mwaka 1990 enzi ya utawala wa rais Saddam Huissen ambaye alitolewa madarakani na serikali ya Amerika mwaka 2003 baada ya kushukiwa kuwa na siraha za kuangamiza jamii. Ghana kuanza kuzalisha mafuta. Akrah, Ghana - 15/12/2010.Wananchi wa Ghana kwa mara ya kwanza wameungana na nchi nyingine dunia katika kuzalisha mafuta kutoka kwenye Ghuba ya Guinea. Akifungua kuanza kwa uzalishaji huo rais wa Ghana John Atta Mills alisema "kuzalishwa kwa mafuta hayo ni baraka na siyo laaana kwa wananchi wa Ghana, na mafuta yatakayo patikana yataisaidia Ghana kuinua uchumi wake zaidi kulio ilivyo sasa." Kiasi cha mapipa 55.000 yanatarajiwa kuzalishwa kwa siku. Eneo hilo liligunduliwa kuwa linamafuta miaka mitatu iliyo pita na kampuni moja ya Uingreza Tullow Oil PLC. Picha hapo juu ni ya ramani ya nchi ya Ghana ikiwa imefunikwa na rangi za bendera ya nchi hiyo ambayo kwa sasa inatambulika rasmi kuwa mzalishaji wa mafuta na kujiungana na nchi nyingine zilizopo katika bara la Afrika. Wanasiasa maarufu Kenya wahusishwa katika machafuko ya 2007

Nairobi, Kenya - 15/12/2010. Mwanasheria mkuu wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ametangaza rasmi majina ya watu walioshukiwa kuhusika na machafuko wakati na kabla uchaguzi mkuu uliofanyika 2007.
Moreno Ocampo, alitangaza majina hayo "Uhuru Kenyatta ambaye ni waziri wa fedha, William Ruto, Fransis Muthaura, Joshua Arap Sango mwandishi wa habari, Henry Kosgey na mkuu wa polisi wa zamani Mohamed Hussein."
Akiongea mara baada ya kumaliza kutaja majina hayo, Moreno alisema watu hawa washukiwa hawa bado hawana makosa mpaka hapo mahakama itakapo wakuta na hatia.
Uamuzi huo wa mahakama ya kimataifa kuingilia kati swala hilo la kutafuta ukweli ni watu gani walikuwa vinara wa kuongoza machafuko ulikuja kutokana na serikali ya Kenya kuchukua muda kuwatambua watu hawa waliotajwa.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Kenya nchi ambayo ilikuwa na machafuko makubwa ya kihistoria katika nchi hiyo tangu kupata uhuru kutokana na mvutano wa kisiasa na itikadi zilizopo kati ya wananchi wake.

Tuesday, December 14, 2010

Dunia ya mpoteza mtetezi wa amani.

Mahakama ya kubali maombi ya dhamana ya Julian Assange. London, Uingereza - 14/12/2010. Mahakama jijini London imekubali kumwachia kwa masharti mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks kwa dhamana ya dola za Kiamerika $ 317,400.

Julian Assange 39,ambaye anashitakiwa nchini Sweden kwa kosa la kufanya mapenzi ya kustukiza ambayo nimakosa nchini Sweden. Assange alijipeleka mwenyewe polisi mara ya karatasi ya kutaka kukamatwa kwake kutolewa na Interpol baada ya serikali ya Sweden kumfungulia mashitaka. Hata hivyo upo uwezekano wa serikali ya Sweden kupinga rufaaa hiyo. Picha hapo juu anaonekana Julian Assange ambaye anashukiwa na makosa ya kufanya mapenzi ya kushtukiza na moja ya mwanadada hivi karibuni nchini Sweden. Wanasheria wa Kenya wafikiria mara mbili mkataba wa Roma. Nairobi,Kenya - 14/12/2010. Kundi la wanasheria nchni Kenya wametishia kuandika barua kwa bunge la Kenya kufuta uanachama wake katika Mahakama ya Kimataifa (International Criminal Court-ICC). Kundi hilo la wanasheria walisema " tulitaka haki itendeke na mahakama ya kimataifa lakini haikuwa hivyo kutokana na uchunguzi wao. Na tunaangalia ni njia gani tutatumia kupitia bunge kujitoa katika matakaba wa Roma ( RomeStatute)." Mjadara huo umekuja baada ya ICC kusema inamajina sita ya watu waliohusika kuleta machafuko ya kisiasa kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika 2007. Machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 1500 na wengine 300,000 kuachwa bila makazi. Picha hapo juu anaonekana mmoja wa kijana akikimbia kuepusha maisha yake kutokana na machafuko yaliyo tokea kabla na baada ya uchaguzi nchini Kenya 2007 ambapo hali ya kiusalama ilikuwa imechafuka, kutisha kwa kilahali. Waziri mkuu wa Itali ashinda kura za maoni kwa mara nyingine. Roma, Itali - 14/12/2010. Waziri mkuu wa Itali ameshinda kura za maoni ambazo zilikuwa zimeitishwa zidi yake kutokana na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali kutokwa na imani naye. Silvio Berlusconi,ameshida kura hizo za maoni kwa kiasi cha uchache wa kura dhidi ya wale wanaopinga uongozi wake. Ushindi huo aliopata Berlusconi, siyo wa mara ya kwanza kwani alishida kura kama hiyo siku za nyuma. Hata hivyo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema Berlusconi atakuwa na wakati mgumu kuongoza serikali kutokana na upinzani mkubwa katika bunge na serikalini. Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Itali,Silvio Berlusconi akionyesha dole baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa kuwa ameshinda tena kura za maoni ambazo ziliitishwa na vyama vya upinzani hivi karibuni. Dunia ya mpoteza mtetezi wa amani.
Washington, Amerika - 14/12/2010. Mshauri mkuu wa serikali ya Amerika katika maswala na hali halisi ya nchi za Pakistan na Afghanistan amefariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa mara ya pili.
Habari kutoka Ikulu ya Amerika zimesema "Richard Holbrooke 69 alikuwa amelazwa katika hospital ya rufaa George Washington kwa ajili ya matibabu mara baada ya kupata matatizo ya moyo."
Rais wa Amerika Baraka Obama alisema " ameshutushwa na kifo cha Richard Holbrooke, na alikuwa mwananchi mwaminifu aliyependa nchi yake na kuitumikia kwa hali na mali, wanachi wa Amerika tomepoteza shujaa ambaye alikuwa mlinzi na mtetezi wa Amerika katika nyanja za kimataifa na kuhakikisha amani inapatikana kwa hali na mali."
Richard Holbrooke, alikuwa kinara katika kutetea na kuleta amani hasa katika nchi za Ulaya ya Mashariki zijulikanazo kama nchi za Balkans, pia kutumia mbinu zote kusimamisha vita vya Bosnia na alikuwa ni mmoja wa washauri wa rais Obama katika vita vinavyo endelea nchini Afghanista ili kujadili mbinu za kukabidhi madaraka kwa Waafghanistan.
Picha hapo juu anaonekana marehemu Richard Holbrooke, akiongea katika moja ya mikutano ya kimataifa enzi za uhai wake.

Sunday, December 12, 2010

Waziri mkuu wa Itali kuwekwa kwenye boksi la maoni na wabunge.

Waziri mkuu wa Itali kuwekwa kenye boksi la maoni na wabunge. Roma, Itali - 12/12/2010. Wachunguzi wa serikali wameanza uchunguzi kufuatia kuwepo na habari ya kuwa waziri mkuu wa Itali ametoa milungula ili ashinde kura za maoni kuuhusu uongozi wake. Malalamiko hayo yalifunguliwa na kiongozi wa upinzani Antonia Di Puerto ambaye akikosoa uongozi wa waziri mkuu wa sasa Silvio Berluscon. Naye kiongozi mwingine wa chama cha upinzani Luigi De Magistris alisema "tumeona rushwa inatumika kati ya wabunge ili kumuunga mkono Berluscon." Hata hivyo Berluscon alisema "sidhani kama kutakuwa na wasaliti wengi na naimani serikali itashinda." Uamuzi wa kutaka kura za maoni zipigwe kumekuja kutokana na baadhi ya wabunge hasa wa upande wa upinzani kutokuwa na inami na waziri mkuu kutokana na habari za matukio ambayo yanamuhusisha moja kwa moja. Picha hapo juu ni picha waziri mkuu wa Itali, Silvio Berluscon ambaye serikali yake imekuwa na mvutano sana na vyama pinzani na kutaka kura za maoni zipigwe zidi ya uongozi wake.

Uchaguzi wa wabunge Misri waleta mvutano upya.
Kairo, Misri - 12/12/2010. Mamia ya watu wameaandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge kwa kudai ya kuwa haukuwa wea haki na kutaka mwanasheria mkuu kufuta matokeo.
Katika matokeo hayo chama tawala kinacho ongozwa na rais Housein Mubarak kimeshinda kwa kupata vitu vingi katika bunge. Naye msemaji wa mmoja wa chama cha upinzani George Ishak alisema "watu wanaandamana kupinga matokeo hayo na tutapinga kwa kufungua kesi ili kuonyesha ya kuwa uchaguzi haukuwa wa halali." Kufuatia matokeo hayo Mohamed ElBaradei aliyekuwa mkuu wa maswala ya Atomi amevitaka vyama vya upinzani kupinga kwa pamoja kushiriki katika uchaguzi wa urai uanaotarajiwa kufanyika mwaka ujao. Picha hapo juu wanaonekana polisi wa kuzuia ghasia wakiwa wanawazuia wananchi walioandamana mbele ya mahakama kuu kutoleta maafa na kuhakikisha usalama na amani unakuwepo. Japana kuweka mitambo ya kuzuia mashambulizi ya anga. Tokyo, Japan - 12/12/2010. Serikali ya Japan inajiandaa kuweka mitambo ya kuzuia
mashambulizi ya anga kutokana na kukua kwa mgogoro katika eneo zima la Asia Pasifiki. Habari zilizo patikana zinasema "mitambo aina ya Patriot Advavced Capabilty 3 itawekwa kuzuia mashambulizi ya anga pindipo kutatokea mashambulizi." Kitendo cha serikali ya Japan kuamua kuweka mitambo hiyo kinakuja kutokana na matukio ya Korea ya Kaskazini kuishambulia Korea ya Kusini hivi karibuni, jambo ambalo limezidi kuleta myumbo na mashaka katika eneo hilo la Asia Pasifiki. Picha hapo juu inaonekana moja ya mitambo ya kijeshi ambayo serikali ya Japan ina mpango wa kuiweka mitambo ya kivita ilikuzuia mashambulizi yoyote ya anga pindipo yatakapo fanyika. Wabunge wapinga malipo ya kiafya ya Septemba 11. Washington, Amerika 12/12/2010. Wabunge wa chama cha Republikan nchini Amerika wamepinga mswaada wa serikali kutaka kutoa malipo ya huduma za kiafya kwa wale wote walio athirika wakati wa mashambulizi ya Septemba 11/2001. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "kukataliwa kwa maswaada huo wa kuwasaidia malipo ya kiafya kutawaathiri pia wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi katika eneo hilo na wakazi wa vitingoji vya karibu na Ground Zero." Tangu tukio la Septemba 11/2001, wanasiasa wamekuwa wakipishana kimawazo kuhusu swala hili. Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika harakati za kusafisha mabaki ya majengo yaliyo bomoka, mara baada ya kulipuliwa na ndege zilizo tekwa nyara na magaidi.
Bomu lalipuka katikati ya jiji la Stockholm.
Stockholm, Sweden - 12/12/2010. Maofisa wa upelelezinchini Sweden wameanza rasmi kuchunguza tukio la bomu ambalo lililipuliwa katikati ya jiji la Stockholm jana.
Anders Thornberg ambaye ni afisa wa upelelezi alisema "tumeanza uchunguzi wa tukio hilo na tunalichukulia kama ni la kigaidi."
Katika mlipuko wa bomu hilo watu walijeruhiwa kutokana na mlipuko huo uliotokea jana wakati baadhi ya watu wakiwa mbioni kununua vitu kwa ajili ya kujianda na sherehe za Krismas
Hata hivyo shirika la habari la Sweden lilipata email iliyokuwa imeeleza kuwa huenda kukatokea tukio hilo kutokana na Sweden kujishirikisha katika vita vya Afghanistan na kitendo cha mchoraji mmoja raia wa Sweden kuchora picha ya kumkashifu Mtume Mohamed S.W.A.
Picha hapo juu wanaonekana wafanyakazi wa zima moto wakiwa wanazima moto uliotokana na mlipuko wa bomu kabla ya kuleta maafa makubwa.

Friday, December 10, 2010

Ujerumani na Ufaransa zasema tutailinda sarafu ya Euro.

Ujeruman na Ufaransa zasema tutailinda sarafu ya Euro.

Freiburg, Ujerumani -10/12/2010. Kansela wa Ujerumani na rais wa Ufaransa wamekuta mjini Freiburg kujadili njia mbadala za kuimarisha sarafu ya Ulaya (EURO). Kansela Angela Markel na Nikolas Sarkozy walikutana na kuangalia kiundani njia ambazo zitaifanya sarafu ya Euro kuimarika zaidi hasa katika wakati uhu mgumu wa myumbo wa uchumi duniani. Viongozi hao kwapamoja walisema "tuta ilinda Eoro, kwani ni sarafu ya Euro ndiyo Ulaya yenyewe."

Kukutana kwa viongozi hao kunakuja kabla ya mkutan wa viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya kufanyika siku chache zijazo. Picha hapo juu anaonekana rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy kushoto akiongea huku Kansela Angela Markel akimsikiliza kwa makini sana na kutathmini nini hasa anaongea wakati walipo kutana hivi karibuni kujadili nini la kufanya ili sarafu ya Euro kuwa imara zaidi kimataifa. Zawadi ya Nobel yawekwa kwenye kiti cha mtarajiwa.

Oslo, Norway -10/12/2010. Sherehe za kumzawadia mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel mwaka 2010 imefanyika jijini Oslo bila ya mzawadiwa kuwepo. Liu Xiaobo ambaye ni raia na mazaliwa wa China ndiye aliyekuwa mshindi wa zawadi ya amani ya mwaka 2010, lakini hakuweza kuudhulia sherehe hiyokwani anatunikia kifungo cha miaka 11 jela kwa kosa la uhani kwa mujibu wa sheria za China. Hata hivyo zawadi yake iliwekwa kwenye kiti ambacho alitarajiwa kukalia wakati wa kupokea zawadi hiyo. Thorbjoern Jagland ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya kutoa zawadi alisema " Liu hajafanya kitu au jambo baya yeye ni mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu." Msemaji wa serikali ya Chini Jiang Yu, alimesema "kutolewa kwa zawadi hiyo kwa Liu ni siasa iliyo shinikiza, ambayo ni zao la wakati wa vita vita vya baridi, na hivyo China haitakukubali kuingiliwa katika maamuzi yake." Picha hapo juu wanaonekana wageni waalikwa wakiangalia picha ya Liu Xiaobo aliye tunikiwa zawadi ya amani ya Nobel 2010 lakini hauwepo kwenye sherehe hizo na zawadi yake kuwekwa kwenye kiti alicho tarajiwa kukikalia.

Tuesday, December 7, 2010

Urussi kuwa mwanachama wa World Trade Organazations

Mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks awekwa kizuizini

London, Uingereza -07/12/2010. Mahakama ya jijini London imemkatalia dhamana mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks ambaye alijipeleka mwenyewe polisi.
Julian Assange 39, aliwasili kwenye kituo cha polisi na baadaye kufikishwa mahakamani kutokana na kesi ya kufanya mapenzi ya kushutukiza iliyofunguliwa juu yake nchni Sweden.
Mwanasheria wa serikali wa Sweden aliomba mahaka kutompa dhamana Julian Assange kwa kuwa hajulikani anapoishi."
Hata hivyo mwanasheria Mark Stephens,ambaye anamwakilisha Julian Assange alisema " tutakata rufaa siku ya Jumanne wiki ijayo na ikiwezekana tutaenda mahamaka kuu na nina amini ya kuwa mahakama ya Uingereza itataua swala hili bila matatizo. "
Picha hapo juu ni ya Julian Assange ambaye mtandao wake umetikisa ulimwengu wa siasa na wa kidiplomasia baada ya kuchapisha habari za siri.
Waziri mkuu wa Uingereza afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan.
Kabul, Afghanistan - 07/12/2010. Waziri mkuu wa Uingereza amefanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan na kukutana na rais wa nchi hiyo.
Waziri mkuu David Cameron, aliongea mbele ya waandishi wa habari alisema " uhusiano wa wanchi wa Afghanistani na Uingereza utazidi kudumishwa na jumuiya ya kimataifa ishirikiane kuijenge Afghanistan."
Hata hivyo David Cameron, aliongezea kwa kusema " natumaiini hali itazidi kuwa nzuri na itaturuhusi kuanza kufikiria kuondoa majeshi yetu ifikikapo mwakani."
Kabla ya kuongea na rais Hamid Karzai, David Cameron alitembelea wanajeshi wa Uingereza waliopo katika jimbo la Helmond.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kushoto akiwa na mwenyeji wake rais wa Afghanistan Hamid Karzai kulia wakati walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Urussi kuwa mwanachama wa World Trade Organazations 2011.
Brussels, Ubelgiji - 07/12/2010. Jumuiya ya Ulaya imekubali na kuunga mkono kwa Urussi kuwa nchi mwana chama World Trade Organizatio, (WTO) ifikapo mwaka 2011.
John Clancy mbaye ni msemaji wa jumuiya ya Ulaya alisema "tumetia sahihi mkataba huo na Urussi baada ya kufikia maafikiano kwa pamoja."
Kukubaliwa huko kwaUrussi kuwa mwanachama wa WTO kutainua kwa kiasi kikubwa uchumi kati ya nchi wanachama na inakakadiliwa kufika kiasi cha asilimia 3.3 na hata kuongezeka katika siku za mbele.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa Urussi na jumuiya ya nchi za Ulaya wakiwa katika mkutano ili kujadili nini cha kufanya ili kudumisha uhusiano wa karibu.
Mazungumzo ya kinyuklia na Iran bado kitendawili.
Geneva,Uswis - 07/12/2010.Mkutano wa mazungumzo kati ya Iran na nchi za jumuia ya Ulaya, nchi wanachama wa kudumu wa kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa
Urussia,China,France, Uingereza, Ujerumani na Amerika umekwisha bila lengo la mkutano huo kufikiwa.
Saeed Jalili ambaye ni mkuuwa wa maswala ya kinyuklia ya Iran,alisema "hatutazungumzia maswala ya maendeleo yetu ya kinyuklia na uzalishaji wake katika kikao kijacho amabcho kinatarajiwa kufanyika Instambul nchini Uturuki na kuhusu swala hilo basi lazima kuwepo na ushirikiano kutoka pande zote mbili."
Naye mmoja wa wajumbe toka Amerika alisema "matarajio ya mkutano wetu hayakufikiwa na kuleteta matoke finyu."
Dhumuni la mkutano huo, ilikuwa ni kuzungumzia hali halisi ya maswala ya kinyukli yanavyoendeshwa nchini Iran, lakini hakuna ufumbuzi uliofikiwa.
Picha hapo juu anaonekana Saeed Jalili mkuu wa maswala ya kinyuklia wa Iran, akitoka katika ukumbi wa mkutano, mara baada ya kumaliza mazungumzo.

Monday, December 6, 2010

Mazungumzo ya Iran na Umoja wa Matifa yaanza nchini Uswisi.

Mazungumzo ya Iran na Umoja wa Mataifa yaanza nchini Uswisi.

Geneva, Uswis - 06/12/2010. Shirika linalo simamia na kudhibiti uzalishaji nishati za kinyuklia limeanza mazungumzo na serikali ya Iran ili kujadili mpango mzima wa kinyuklia uliopo nchini Iran. Mazungumzo hayo ambayo yameudhuliwa na viongozi wa jumuiya ya Ulaya,Urussi, Amerika, Uingereza, China na Ujeruman nchi wanachama katika kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wataongelea kiundani na kujadili na serikali ya Iran kuhusu undeleaji wa mpango mzima wa nyuklia.
Picha hapo juu anaonekana Saeed Jalili kiongozi kutoka serikali ya Iran anaye shughulikia mswala ya nyuklia kulia akiongea na mkuu wa maswala ya mambo ya nje wa jumuiya ya Ulaya Cathirine Ashton kabla ya kuanza mazungumzo.
Argentina yaunga mkono kuwepo kwa taifa la Palestina.
Buenos Aires, Argentina -06/12/2010. Serikali ya Argentina imefuatia msimamo wa Brazil kwa kukubali kuunga mkono kuwepo kwa Taifa la Wapalestina walio huru.
Katika barua iliyo tumwa kwa rais wa Wapalestina Mohmoud Abbas na uongozi wa Argentina ilisema " tunaitambua Palestina kama taifa huru kutokana na makubaliano ya mipaka ya mwaka 1967."
Kuungwa mkono huko kwa serikali ya Wapalestina na nchi za Amerika ya Kusini umekuwa wakaribu sana hasa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Wapalestina Mahmoud Abbs akisalimiana na rais wa Argentina Cristina Kirchner wakati walipo kutana katika moja ya mikutano kujadili hali halisi ya Wapalestina.
Mmiliki wa ndege za Konkodi atozwa faini.
Paris,France - 06/12/201. Shirika la ndege lilio kuwa mmiliki wa aina ya ndege Concorde limetozwa faini baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na kutokuwajibika katika usalama wa ndege hiyo ambayo iliungua moto.
Shirika hilo Continental Air lines lilitozwa faini kiasi cha $ US dollor 268,400 na mahakama nchini Ufaransa baada ya ndege yake aina ya Concorde kushika moto wakati inaanza kupaa na kuanguka na kupoteza maisha ya abiria 113.
Picha hpo juu ni ya ndege ya aina ya Concorde ikiwa imeshika moto mara baada ya kuanza kupaa.

Sunday, December 5, 2010

Umoja wa Afrika watuma mjumbe kuleta suruhu za kisiasa nchini Ivory Coast

Umoja wa Afrika watuma mjumbe kuleta suruhu za kisiasa nchini Ivory Coast. Abidjan,Ivory Coast - 05/12/2010. Rais wa pili wa Afrika ya Kusini tangu kushindwa kwa utawala wa kibaguzi wa rangi, Thabo Mbeki amewasili jijini Abidjan ili kuleta suruhisho la matokeo ya uchaguzi wa rais. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "Thabo Mbeki ameteuliwa na Umoja wa Afrika (UA) kushughulikia swala la matokeo ya uchaguzi wa Ivory Coast, ambapo rais mtetezi Laurent Gbagbo waliapishwa kuwa rais, ingawaje apo awali kamati ya uchaguzi ilimtangaza mpizani wake Allasane Ouattara kuwa mshindi kwa kupata kura nyingi zaidi." Kuwasili huko kwa Thabo Mbeki kunatarajiwa kuleta suruhisho ili kuepuka mvutano wa kisiasa. Uchaguzi nchini Ivory Coast uliwahi kuhairishwa zaidi ya mara tano kutokana na mvutano wa kisiasa. Picha hapo juu ni ya aliyekuwa rais wa Afrika ya Kusini Thabo mbeki, ambaye anatarajiwa kuleta suruhisho la kisiasa nchini Ivory Coast.

Jeshi la Umoja wa Afrika kuwa na wakati mgumu.
Mogadishu, Somalia - 05/12/2010. Kundi la Al-Shabab lililopo nchini Somalia limesema litaendelea kupambana na majeshi ya wageni waliovamia nchi yao.
Maelezo hayo yalitolewa na mmoja wa kiongozi wa wapiganaji kwa kusema " wamevamia nchi yetu na hatuna budu kuitetea."
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu zinasema "zaidi ya watu mia moja wamefariki katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza mapambano kati ya Al-Shabab na jeshi la UA ."
Picha hpo juu wanaonekana wanajeshi wa Umoja wa Afika wakiwa katika mazoezi ya kijeshi ili kupambana na kundi la Al-shabab.
Picha ya pili ni ya kundi la Al-Shabab kundi ambalo limekuwa ilikiendeleza mashambulizi zidi ya wanajeshi wa umoja wa Afrika na raia ambao wanakwenda kinyume na Al-Shabab.
Iran yatangaza kuzalisha madini ya kinyuklia.
Tehran, Iran 05/12/2010. Serikali ya Iran imetangaza ya kuwa wanasanyansi wake wameweza kuzalisha kwa mara ya kwanza madini ya ambayo yanatumika katika kuzalisha nguvu za nyuklia.
Akiongea mkuu huyo wa maswala ya kinyuklia Ali Akbar Salehi alisema "Iran itaanza kutumia madini yake hayo kwa mara ya kwanza ambayo yamezalishwa hapa nyumbani na kutotegemea kuagiza toka nchi za nje."
Kitendo cha Iran kutangaza uwezo wake huo, kutazidi kuleta vichwa kuuma kwa Amerika na nchi nyingine ambazo haziamini ya kuwa Iran haina mpamgo wa kutengeneza siraha za kinyuklia.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanasayansi wa Irani wakiwa kazini katika kiwanda cha kuzalishia nguvu za kinyukli.
Wamisri wapiga kura tena kuwachagua viongozi wao.
Kairo,Misri - 05/12/2010. Wanachi wa Misri wamepiga kura kwa mara ya pili ili kuwachagua wabunge.
Uchaguzi huo wa mara ya pili wa kuchagua wabunge unafanyika huku vyama vya upinzani vikiwa vimejitoa kwa kupinga ya kuwa uchaguzi huo si harali.
Uchaguzi huo ambao chama tawala (NDP)-National Democratic Party) kinatarajiwa kushinda viti vingi kutokana na kujitoa kwa vyama vya upinzani.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wadau wa vyama vya upinzani wakiwa wametawanywa na polisi wa kuzuia ghasia wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa awali.

Friday, December 3, 2010

Baraka Obama afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan.

Baraka Obama afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan. Kabul, Afghanistan - 03/12/2010. Rais wa Amerika amefanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan na kuongea na wanajeshi na raia wa Amerika wanaoshiriki kwa katika vita zidi ya Taliban na washirkia wake. Akiongea katika hotuba hiyo rais Baraka Obama alisema "Amerika itaendelea na kupambana na wale wote ambao wanapinga maendeleo ya Amerika au kutishia usalama wa Amerika na watu wake, na hatutashindwa kamwe kuwasaka popote walipo." Hata hivyo katika ziara hiyo rais Baraka Obama, hakuweza kukutana na rais wa Afghanistan kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya. Picha hapo anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama akishuka kutoka kwenye ndenge mara baada ya kuwasili nchini Afghanistan kwa mara ya pili akiwa kama rais wa Amerika ili kuwapa salamu za sikuku wanajeshi na kuelezea ni kwa jinsi gani Waamerika wote wapo pamoja nao. Ulaya ya kumbwa na mporomoko wa barafu. London, Uingereza - 03/12/2011. Bara la Ulaya limekumbwa na mporomoko wa barafu ambao umesababisha hali ya utoaji wa huduma kuyumba. Barafu hizo ambazo zinaendelea kugubika karibuni Ulaya kote tokea Urussi hadi Spain limekuwa gumzo kwa wakazi wengi wa eneo hili. Siku ya Jumanne barafu nyingi ilipolomoka na kusababisha hali ya hewa kuwa barisi hadi kufikia kati ya hasi 20 na 22. Picha hapo juu linaonekana moja ya gari la kusafisha njia likijaribu kutoa barafu ili huduma ziweze kuendelea zilishindikana kutokana na wingi wa barafu iliyo poromoka toka angani

Thursday, December 2, 2010

Kombe la dunia mwenyeji ni Urussi 2018 na Katar 2022.

Kombe la Dunia wenyeji ni Urussi 2018 na Katar 2022.

Zuriki,Swizland-02/12/2010. Shirkisho la soka duniani limepiga kura na kuchagua nchi ambazo zita kuwa wenyeji wa fainali ya mchezo wa soka wa mwaka 2018 na 2022.
Akitangaza wenyeji wa fainali wa soka hizo ambazo ni Urusi 2010 na Katar 2022.
Wakiongea kwa wakati tofauti viongozi wa kampeni wa za kutaka nchi zao kuwa wenyeji wa soka
" Tunawahakikishia mtafurahi na kuondoka na kumbukumbu za furaha" naye kiongozi wa Katar alisema " nawashukuru kwa kutupatia wananchi wa Katar uaminifu wenu na yote tuliyo haidi yatakamilishwa na kila atakaye hudhulia 2022 fasinali za soka, basi atomndoka na kumbukumbu ambazo zitakuwa na milele."
Picha ya hapo juu ni ya bendera ya Urussi nchi ambayo imechaguliwa kuwa mwenyeji wa kombe la fainali za soka mwaka 2022.
Picha ya pili anaonekana kiongozi wa kampeni ya kutaka kombe la dunia lichezwe nchini mwaka akilinyanyua kombe la dunia mara baada ya nchi yake kutangazwa kuwa mwnyeji wa kombe la dunia 2022 na kushoto ni rais wa FIFA Sepp Blatter.
Picha ya tatu ni ya bendera ya Katar nchi ya kwanza ya kiarabu kuandaa kombe la dunia.
Picha ya nne wanaonekana baadi ya wajumbe wa Katar wakipokea kombe la dunia kama ishara ya kukubaliwa kuwa mwenyeji wa mchezo wa soka 2022 mara baada ya Katar kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa fainal hiyo.
Mahakama ya kataa rufaa ya mwanzilishi wa WIKI leaks.
Stockholm, Sweden-02/12/2010.Mahakama kuu nchini Sweden imekataa rufaa ya mwanzilishi wa mtandao WIKI leaks ambaye anakabiliwa ya ubakaji.
Kwa mujibu wa msemaji wa mahakama Kerstin Norman alisema " mahakama imeamua kukataa rufani ya Julian Assange."
Julian Assange mwanzilishi wa WIKI Leaks mtandao ambao umetoa habari nyingi za kushutusha na hasa zile za nyaraka za siri za serikali tofauti.
Picha hapo juu anaoeneka Julian Assange, ambaye rufani yake imekataliwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya mtandao wake.
Picha ya pili ni nembo ya mtandao wa WIKI leaks ambao umehusika katika kutoa habari za nyaraka za siri.
Kampuni ya ndege ya Qantas yafungua kesi dhidi Rolls-Royce.
Sydney,Australia-02/12/2010. Kampuni inayohusika katika matengenezo ya injini za ndege ambazo zimekuwa zikileta matatizo na kusababisha baadhi ya injini za ndege kufanyiwa uchunguzi.
Kampuni hiyo Rolls-Royce ambayo ndiyo mtengenezaji wa injini hizo imetakiwa kulipa fidia kutokana na usumbufu uliofanywa na injini zake kwa kampuni ya ndege ya Qantas.
Hata hivyo kampuni ya Rolls-Royce imesema huwa inafanya uchunguzi wa hali ya juu katika injini zake kila wakati.
Picha hapo juu inaonekana moja ya injini ya shirika la ndege la Qantas ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya kushika moto.
Rais wa Sri Lanka ashutumiwa kwa kuhusika na mauaji dhidi ya TAMIL Tigers.
London, Uingereza - 02/12/2010. Rais wa Sri Lanka ambaye yupo ziarani nchini Uingereza ametajwa ya kuwa anahusika kwa kiasi kikubwa katika mauaji yaliotokea wakati wa vita zidi ya kundi ta TAMIL Tigers.
Habari hizi ambazo ni moja ya mlolongo wa habari ambazo zimetolewa na mtandao wa WIKI Leaks zina eleza ya kuwa "rais wa Mahinda Rajapaska na washiriki wake wanahusika katika mauji wakati wa vita vyawenyewe kwa wenyewe (Kati ya serikali iliyopo madarakani na kundi la TAMIL Tigers ambalo linapingana na serikali."
Hata hivyo wapinzani wa Mahinda Rajapaska na serikali yake waliweza kuzuia kuendelea na mpango wa rais huyo kuhutubia katika mkutano uliopangwa ambapo kwa sasa yupo ziarani nchini UIngereza.

Tuesday, November 30, 2010

Mkutano wa utunzaji wa mazingira waanza kwa mashaka.

Google kufanyiwa uchunguzi na jumuia ya Ulaya. Brussel, Umoja wa Ulaya - 30/11/2010. Kitengo cha uchunguzi cha jumuia ya muungano wa umoja wa Ulaya kinachunguza malalamiko yaliyo tolewa dhidi ya Google kwa kukutumia vibaya umezo wake. Kwa mujibu wa makampuni mengine ya kimtando yamsema "google inavunja ushindani wa kiimtandao dhidi ya makampuni washindani." PIcha hapo juu inaonekana picha ya mtandao wa Google ambao unalalamikiwa na washindani wake kwa kuvunja ushindani. Mkutano wa kutunza mazingira waanza kwa mashaka. Cancun,Mexico - 30/11/2010. Mkutano wa kutunza mazingira unaofanyika nchini Mexico umeamza kwa vishindo huku kila nchi muhusika akitaka matakwa yake yatimizwe. Akiongea katika mkutano huo mwakilishi wa serikali ya Amerik Jonathan Pershinga alisema " tunataka kuwepo na makubaliano ya pamoja katika kudhibiti uaribifu wa mazingira duniani" Hata hivyo msimamo huo wa Amerika umeonekana kutiliwa mashaka na baadhi ya washiriki kwa kudai kuwa hakutaleta matokeo mazuri. Pichani hapo juu aanonekana mmoja ya washiriki wa mkutano wa mazingira unaofanyika Mexico akichora kapicha kuashiria ishara kuhusu matokeo ya mikutano iliyo fanyika hapo awali kabla wa sasa unaofanyika Cancun Mexico ambapo wajumbe wa nchi tofauti wanakutana kujadili mazingira. Venezuela yapewa mkopo na Urussi kwa ajili ya kuimarisha maswala ya kiulinzi. Carakas, Venezuela 30/11/2010. Serikali ya Venezuela imesema ya kuwa serikali ya Urussi itaipa mkopo wa $4 billion ambazo zitaiwezesha nchi hiyo kukuawa siraha ili kuimarisha maswala ya kijeshi na ulinzi. Akiongea katika sherehe ya miaka 90 ya jeshi la anga rais wa Venezuela Hugo Chavez alisema " Tumeamua kufanya hivyo ili kuendelea kulinda nchi yetu na maadui." Picha hapo anaonekana rais wa Venezuela Hugo Chavez wakati wa kuadhimisha sherehe za maiaka 90 ya jeshi la anga ambalo ilitaongezewa nguvu. Radi yaleta maafa na vifo ya watu nchi Afrika ya Kusini. Kwa Zulu Natali, Afrika ya Kusini - 30/11/2010.Watu wapatao saba na wengine kujeruhiwa baada ya radi kuwashambulia wakati wakiangali jengo lilijenge kwa turubai kwaajili ya Krismas. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali anayeshughulikia maafa Mthokozisi Duza alisema "watu walio jeruhiwa apo hospitali kwa matibabu." Picha hapo juu inaonyesha miali ya moto iliyo tokana na radi ikishambulia Kwa zulu Natal na kusababisha maafa ya kijamii na kwa mazingira. Rais wa Urussi atoa onyo ikiwa hakuna makubaliano na NATO.

Moscow, Urussi - 30/11/2010. Rais wa Urussi Dimtri Medvedev amesema ikiwa nchi yake aitafikiana makubaliano na NATO katika swala la kujenga mitambo ya kiulinzi basi nchi yake itajihami zaidi kiulinzi. Akilihutubuua taifa, rais Medvedev alisema "swali lililopo ni kwa NATO kukubaliana nasi katika swala zima la ujenzi wa mitambo ya ulinzi au ikiwa hakuna makubaliano basi katika kipindi cha miongo ijayao basi tutaamua kuweka mitambo yetu wenyewe ya kiulinzi na kufufua mashindano ya kisiraha." Pia rais Medvedev, aliwataka wanachi kuongeza kizazi kwa katika kipindi cha miaka ijayo taifa litakuwa na watu wachache na haitakuwa vizuri kwa ujenzi wa taifa." Picha hpo juu anaonekana rais wa Urusi Dimri Medvedev akihutubia taifa na kuongelea maswala ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla. China inamatumaini ya kuwa ipo siku kutakuwa na Korea moja.
Beijing China 30/11/2010. Habari zilizo patikana kutoka kwa mtandao wa Wiki Leaks zinasema ya kuwa baadhi ya viongozi wa serikali ya China wanapendelea kuunga mkono na kuungana kwa Korea ya Kusini na ya Kaskazini.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "balozi wa China nchini Kazakhstan alisema wanamatumaini siku za mbaleni kutakuwa na Korea moja ingawa kwa sasa bado nchi hizo zinajulikana kama zilivyo Korea ya Kusini na Korea ya Kaskazini."
Picha hapo juu ni bendera ya Korea ya Kaskazini nchi ambayo imekuwa ina vutana na jumuia ya Kimataifa kuhusu ukweli wa swala la kinyuklia na mshiriki wa karibu wa China.
Picha ya pili ni ya bendera ya Kora ya Kusini nchi ambayo imekuwa haina ushirikiano mzuri na serikali ya Korea ya Kaskazini.