Sunday, November 24, 2013

Mabaki ya mwanzilishi wa Kanisa Katoliki dunia yaonyeshwa.


Mabaki ya mwanzilishi wa Kanisa Katoliki dunia yaonyeshwa.


Vatican City, Vatican - 24/11/2013. Waumini wa Kanisa Katoliki duniani wameonyeshwa kwa mara ya kwanza mabaki  ya aliyekuwa mwanzilishi wa kanisa Katoliki Mtakatifu  Peter.

Mabaki hayo ya Mtakatifu Peter, yalionyeshwa kwa waumini hao huku yakiwa yamewekwa katika kisanduku katika misa  iliyo ongozwa na Papa Fransisco.

Kuonyeshwa kwa mabaki hayo kwa waumini wa Kikristu na hasa kwa waumini wa kanisa Katoliki inaaminika kutaongeza kukuza imani ya waumini wa kanisa la Katoliki, hasa baada ya kukubwa na  mikasa na utovu wa nidhamu ya kimaadili kwa wafanyakazi na wahudumu wa kanisa hilo katika sehemu tofauti duniani

Iran yafikia makubaliano na 5+1 juu ya Nyuklia.

Geneva, Uswis - 24/11/2013. Nchi 5+1 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa,  China na Urusi, zimefikia makubaliano na Iran  kwa mara ya kwanza tangu kuanza mazungumzo kwa miaka kumi iliyo pita.

Katika makubaliano hayo Iran imekubali kusimamisha baadhi ya mikakati yake ya kuendelea kuzalisha madini ya kinyuklia na badala yake itapewa  kiasi cha $ dola za Kimarekani 7 billion ikiwa ni moja ya afuheni katika vikwazo ambavyo Iran ilikuwa imewekewa na jumuiya ya kimataifa kutokana na mpango wake wa kuzalisha madini ya kinyuklia ambao unashukiwa huenda yakatuka  katika kuunda siraha za sumu.


Akongea baada ya makubaliano hayo, rais wa Iran Hassan Rouhani amesema " hii ni historia na kwa wale ambao walikuwa wana nia tofauti na Iran, sasa watafahamu ya kuwa Iran inahaki ya kuuendelea na mpango wake wa amani wa kuzalisha nyuklia kwa matumizi ya  kisayansi na kijamii."


Kwenye makubaliano hayo ni kwamba Iran imekubali "kutokuzalisha madini ya Uraniam kupita kiasi cha asilimia 5% na kutoa ruhusa ya wakaguzi kutembelea na kukagua katika viwanda vya kufulia madini ya kinyuklia katika miji ya Natanz, Fordo na hakutakuwa na uendelevu wa uzalishaji wa na ufuaji wa madini ya kinyuklia katika kiwanda cha Arak."

Hata hivyo serikali ya Izrael haikupendezwa na makubaliano hayo na  waziri mkuu wa Benyamin Netanyahu amesema ya kuwa " kitendo cha kufikia makubaliano na Iran ni makosa ya kihistoria na Izrael haina imani na Iran, kwani tangu mwanzo Iran Ilisha sema yakuwa inataka kuifuta Izrael katika ramani ya dunia."

Makubaliano hayo hayataifanya Iran kusimamisha mpango wake wa kuzalisha nyuklia ambao imekuwa ikipigania toka kuanza kwa mazungumzo miaka kumi iliyo pita na vile vile makubaliano hayo yatakuwa katika mtazamo katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

No comments: