Thursday, April 3, 2008

Ufaransa yaanza mikakati ya kutaka kuachiwa kwa bi, Ingrid Betencourt's

WTA, Miami yaonyesha ya kuwa Serena bado kiboko kwa kila anaye kuja.

Miami, Amerika - Mwana dada Serena Williams, ameweza kuendelea kwenya mashindano ya tenis kwa upande wa wanawake (WTA) baada ya kufika nusu fainali.
Bi, Serena Williams, ambaye kufika kwake nusu fainali kumekuja baada ya kumnyanyasa bi Justine Henin.
Bi Serena, alishinda kwa pointi 6-2, 6-0, kwenye mpambano wa kukata na choka uliofanyika mjini Miami.
Bi, Justine Henin na bi Serena Williams wamekuwa wapinzani wa jadi tangu walipo anza kukutana kiprofecheni miaka isiyo pungua mitano iliyo pita.
Waziri mkuu ajiuzuru kwa kufuatwa na kashfa za mafaranga.
Dublin, Irland(Irish) - Waziri mkuu wa Irland ( Irish) bwana Bertie Ahern , amaetangaza ya kuwa atajiuzuru wadhifa wake ifikapo mwezi wa mei tarehe 6, baadha ya kudhuka kwa kashfa juu yake.
Bwana, Bertie Ahern mwenye umri wa miaka 56, anashutumiwa kwa kuchukua pesa kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara kwa vipindi tofauti kati ta miaka ya 1989 na 1992.
Lakini bwana Bertie Ahern, amekanusha kashfa hii na kudai yakuwa hana hatia wa wasiwasi wa swala hili.
Hata hivyo, waziri Bertie Ahern, anasifika kwa kuinua uchumi wa kisiwa hiki cha Irish.
Pichani hapo juu anaonekana bwana Bertie Ahern akitangaza tarehe ya kujiudhuru kwake.
Picha ya chini anaonekana waziri, Bertie Ahern akwaaga baadhi ya watu aliokuja kusikiliza yale aliyo yasema.
Mambo si shwali tena nchini Somalia, wapinzani wateka baadhi ya maeneo.
Mogadishu, Somalia - Mapigano mapya yamezuka tena nchini Somalia, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 19, mapigano hayo ambayo yamesababisha hali ya wasiwasi kurudi tena jiji Mogadishu.
Mapambano haya yaliongozwa na kundi la Islamic Courts Union, amablo pia limedai ya kuwa limeteka mji wa Baidoa na kuteka vifaa vingi vya kijeshi kutoka kwenye kundi la wanajeshi wa serikali.
Pichani wanaonekana baadhi ya wananchi wakiwa hawajui la kufanya , mmoja wa wapiganaji akiwa ameshikilia bunduki tayari kwa lolote litakalo tokea.
Wazimbabwe tuwepamoja kujenga nchi yetu, tuachane na siasa," Mfanya biashara aomba".
Harare, Zimbabwe - Baadhi wa wakazi wa jamii ya ulaya au wazungu ambao ni wazaliwa wa nchi ya Zimbabwe wamekuwa na maoni tofauti kuhusu hali halisi ya uchaguzi nchini humo.
Mmoja wa wakazi hawa bwana Mercer, ambaye ni mfanyabiashara, alisema ya kuwa inabidi sisi kama Wazimbabwe tuungana kujenga nchi yetu, na maswala ya siasa yasituvuluge vichwa vyetu, kwani siasa ndio chombo pekee ambacho siku zote kinaleta migogoro kataika jamii, na matatokeo yake hivi leo ni vikwazo kila kukicha , na juu ya vikwazo hivi ni vigumu kwetu kufanya biashara na ndio maana hatuagizi, wala hakuna wateja, kutokana na migogoro ya siasa.
Hivyo Wazimbabwe tujenge nchi yetu na kuwa pamoja.
Ufaransa yaanza mikakati ya kutaka kuachiwa kwa bi, Ingrid Betancourt's.
Bogota, Kolombia - Serikali ya Ufaransa na washiriki wake Spain na Uswisi wanafanaya mkakati wa kutaka kuachiwa kwa mwana siasa na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, bi Ingrid Batancourt's, ambaye ameshikiliwa na wanajeshi wa kundi la FARC.
Kundi hili la FARC, linapingana na serikali ya Kolombia kwa kipindi kisicho pungua miongo miwili.
Bi Ingrid Betancourt's ambaye ana uraia wa Ufaransa na Kolombia, na alisha wahi kuwa mgombea wa Urais kipindi cha nyuma kabla ya kukamatwa kwake na waaasi wa FARC.
Kutokana na habari kutoka kwa ndugu na familia , zinasema yakuwa bi, Betancourt's anamatatizo ya kiafya na huenda yakahatarisha maisha yake.
Picha hapo juu anaonekana mama wa bi Ingrid Betancourt's , akiongea kwa uchungu na majonzi kuhusu hali ya afya ya mwanae bi Ingrid.
Picha nyingine anaonekana, bi Ingrid Betancourt's akiwa kwenye kambi ya wapinzani wa FARC , ambao wanamchikilia hadi sasa.
Picha ya chini anaonekana na mtoto wa bi, Ingrid Betancourt's, Lorenzo akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya kiafya ya mama yake, ambaye amashikiliwa na waasi wa FARC.
Waumini wa dini ya Bodee, watafikishwa mbele ya Pilato kujibu mashitaka.
Beijing, China - Zaidi ya watu wasiopungua 1000, watafikishwa mahakamani katika jimbo la Tibeti, mapema mwezi wa mei mwaka huu. .
Mmsemaji mmoja wa serikali ya Beijing, amesema ya kuwa , watuhumiwa hawa wana husika na machafuku ya kisiasa na kijamii katika jimbo la Tibeti.
Mmsemaji huyo alisema ya kuwa machafuko haya yalikuwa yamepangwa na waumini wa dini ya Mabodee ambao wanaongozwa na Dalai Lama.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waumini wa dini ya Bodee, wakiwa wanasoma vitabu vya dini yao.
Mvutano kati ya NATO na Urusi bado kitendawili, wapewa matumaini hapo baadaeye.
Bucharest, Romania - Shirikisho la Umoja wa Kijeshi la nchi za Ulaya (NATO) limekubaliana kwa pamoja ya kuwa nchi za Georgia na Ukreini kusubiri kuwa mwanachama wa shirikisho la NATO.
Hali ya uamuzi huu inakuja baada ya kuwekewa ngumu na nchi ya Rusia ( Urusi), kwani nchi hii ina ona ya kuwa nchi hizi kuwa mwanachama wa shirikisho hili litahatarisha usalama wa nchi ya Urusi, kwa kuzingatia nchi hizi zipo karibu na Urusi.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa NATO wamesema nchi hizi zisiwe na wasiwasi ipo siku zitajiunga na shirikisho hili.
Vile vile Rusia ( Urusi) ina pinga mpango wa Amerika kuweka mizinga ya ke karibu na mipaka ya Urusi, ama nchi ambayo ipo karibu na nchi hii ya Urusi.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi vinara wa NATO, waziri mkuu wa Uingereza bwa Gordon Brawn na rais wa Amerika bwana George Bush.

1 comment:

Anonymous said...

I do not even know the way I ended up right here,

but I assumed this post used to be great. I

don't recognise who you might be however

certainly you are going to a well-known blogger should you are not already ;) Cheers!

Check out my weblog jackson sun jobs classifieds