Papa Benedikti XVI atangaza kujiudhulu.
Vatican, Vatican City - 11/02/2013.Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani ametangaza kujiudhulu wazifa wake kutokana na hali ya kiafya kuto mruhusu kuendelea na kazi za kiinjili.
Akitangaza kuhusu habari hizi, Federico Lombardi ambaye ni msemaji wa Vatican alisema Papa Benedikti wa XVI atajiudhulu wadhifa wake kama mkuu wa kanisa Katoliki duniani tarehe 28/02/2013.
Papa Benedikti mwenye miaka 85, ambaye alitawazwa kuwa mkuu wa kanisa Katoliki April 19, 2005 amekuwa ni kiongozi wa kanisa Katoliki wa 265.
Kufuatia kujiudhulu huko kwa Papa Benedikti, Makadinali watakutana katika ya mwezi Machi ili kumchagua kiongozi mpya wa kanisa hilo.
Libya yavutana na ICC juu ya washitakiwa kutoka nchini Libya
Tripol, Libya - 11/03/2013. Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia makosa ya jinai (ICC) imeitaka serikali ya Libya kumkabidhisha mikonino mwa mahakama hiyo aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Libya wakati wa utawala wa rais Muammar Gaddafi.
Abdullah Senussi ambaye alikamatwa nchini Mauritania mwezi Machi mwaka jana, hadi sasa yupo mikononi mwa serikali ya Libya, na anakabiliwa na mashitaka ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa kama mkuu wa upelelezi wa Libya.
Kwa mujibu wa habari kutoka makao makuu ya koti (ICC) iliyopo Hague nchini Netherlands, zinasema " serikali ya Libya inatakiwa kumkabidhi haraka iwezekanavyo Abdulah Senussi mikononi mwa ICC kabla sheria haijachukua mkondo wake"
Kesi zidi ya Senussi imekuwa inaleta mvutano kati ya ICC na serikali ya Libya jambo ambalo limeifanya ICC kutishia kutumia mbinu mbadala baada ya serikali ya Libya kuzidi ng'ang'ania azma yake ya kumzuia mtuhumiwa huyo.
Wagombea urais Kenya wawekwa kiti moto kupitia Luninga.
Nairobi, Kenya - 11/02/2013. Wananchi na kaaazi wa Kenya watapata kwa mara ya kwanza fursa ya kuwa ona wanasiasa wanaogombania urais wakijadili na kuongea sera zao za kisiasa na kiuchumi kwa kutangazwa moja kwa moja kupitia luninga na redio za kitaifa.
Mdaharo huo wa kisiasa ambao utachukua muda wa masaa mawili, utawakutanisha wanasiasa ambao ni viongozi wa vyama wanagombania kiti cha urais kupitia vyama hivyo ili kuelezea wananchi wa Kenya ni kwa kiasi watainua maisha ya Wakenya kiiuchumi na kijamii.
Wananchi nchini Kenya watapiga kura 4 mwezi Machi 2013, ili kumchagua rais na wabunge.
No comments:
Post a Comment