Sunday, February 1, 2015

Mmoja wa waandishi wa habari wa Aljazeera aachiwa.

Rais Robert Mugabe mwenyekiti wa AU.


Adis Ababa, Ethiopia - 01/02/2015. Rais Robert Mugabe , amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya muungano wa nchi za Afrika  AU, baada ya mwenyekiti wa sasa rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kumaliza muda wake.

Akiongea mara baada ya kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti, rais Mugabe alisema " kazi yangu ni kuhakikisha yote yaliyo azimiwa yanatimizwa, hivyo kama nchi za Ulaya na washiriki wake watasema kuhusu kuchaguliwa kwangu, hilo haliniusu."

"Lengo ni kuhakikisha tunatumikia wananchi wa Afrika, na hasa kuinua hali ya wanawake, japo tupo tofauti kimaumbile, wanawake wanaweza fanya kazi fulani na kuna kazi nyingine wanaume hawawezi kufanya kama kubeba motto tumboni, hivyo tunaangalia ni njinsi gani wanawake wasaidiwe katika jamii ili kuchangia ujenzi wa bara hili kiuchumi."

"Zimbawe leo tuna majaji na marubani wanawake, hivyo tunajua umuhimu wa wanawake katika jamii nzima ya kiaafrika."

Rais Robert Mugabe, ndiye rais mkubwa kiumri, na ambaye amekuwa akisifiwa na kupendwa sana katika bara la Afrika kama mginaji halisi wa Wafrika, na hasa kwa kupinga na kufokea hadharani  tabia za baadhi ya nchi zinazo taka kuleta muvurugo na kuiba mali zilizopo katika bara la Afrika kiujanja ujanja.

Mmoja wa waandishi wa habari wa Aljazeera aachiwa.
 
Kairo, Misri - 01/02/2015. Peter Greste, mwandishi wa habari wa shirika la habari la Aljazeera, ameachiwa huru na kusafirishwa kwao nchini Australia, wakati waandishi wenzake Baher Mohamed, na Mohamed Fanny wakiwa bado jela.

Greste Muaustralia na wenzake Baher na Fanny, wamekaa jela siku 400, tangu mahakama jijini Kairo kuwahukumu vifungo, baada ya kushatakiwa kukisaidia kihabari chama kilicho tolewa madarakani cha Muslim Brotherhood  kwa nguvu na rais wake Mohammed Mosri kukamatwa.

Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema kuwa " Greste alipakizwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Misri leo hasubuhi, akiwa na kaka yake.

Mostefa Soug, mkuurugenzi mkuu wa  Aljazeera akiongea kuachiwa kwa Peter Grste alisema "tunafurahi kuwachiwa kwa Peter Greste, lakini hata hivyo bado tunasisitiza Baher na Fanny lazima waachiwe huru, na hatuta pumzika mpaka waachiwe."

Kuachiwa huko kwa Greste kumekuja kutokana na msukomo wa kimataifa unao isukuma serikali ya Misri ya kutaka kuachiwa kwa waandishi wa habari wa Aljazeera waliopo ambo mmoja wao Peter Greste kuachiwa  huru na wenzake Beher Mohammed na Mohamed Fanny bado wapo jela.

Wakwepa kodi nchini Ugiriki walikuwa kitisho kwa serikali.

Athens, Ugiriki - 01/02/2015. Mkuu wa umiliki na ukusanyaji wa kodi nchini Ugiriki Nikos Karavitis Theoharis, alilazimika kujiudhuru, baada ya kupokea vitisho kutoka kwa wakwepa kodi.

Akiongea, mara baada ya kuchaguliwa kwa serikali mpya ya Siryiza,  Theoharis alisema " Nilikuwa napokea  simu za vitisho ofisini kwangu na ujumbe kupitia mitandao yakuwa ni Euro 5,000 zitatumika kuvunja miguu yangu."

"Vitisho nilivyo kuwa nikipokea, vinaonyesha ni kwa kiasi gani wakwepa kodi walivyo kuwa wanaibia nchi bila uwoga, na hivyo baada ya kuona nipo imara ndipo walipo nitisha na kwa usalama ikabidi  nijiudhuru."
"
 
"Lakini naamini serikali iliyo ingingia madarakani, itakuwa shubiri kwa wakwepa kodi. kwani vitisho walivyo kuwa wakivitumia havita saidia"

Theohari,s aliyaongea haya baada ya kushinda kuwa kama mbuge, na ambaye anaunga mkono serikali mpya iliyo chaguliwa nchini Ugiriki, inayo pinga mbinyo na makato ya serikali kwa wananchi ili kulipa madeni ya nchi. Hatua ambayo inadhaniwa huenda ikaleta mtafaruku katika jumuiya ya umoja wa Ulaya.




No comments: