Thursday, February 4, 2016

Shirika la utangazaji la RT la Urusi lawa tishio.

Shirika la utangazaji la RT la Urusi lawa tishio.


Shirika la utafiti wa masuala ya kiusalama la Marekani CEPA, limemlaumu George Galloway mtangazaji na mwanasiasa mkongwe wa Uingereza ya kuwa kipindi chake  Sputnik kinacho tangazwa katika luninga ya Kirusi - RT kuwa kinahatarisha na kuzidharaulisha serikali za nchi za Magaharibi na NATO.

CEPA Center for European Policy Analysis yenye makao ya ke makuu jijini Washington, limesema kutokana na kuwepo na RT  inayo tangaza kiingereza, kipindi cha Sputnik, kimekuwa kikitumika kama sehemu ya kukuza na kundesha  juhudi za Urusi dunia kwa kuponda mipango na mikakati ya Marekani na washirika wake.

Ripoti ya hiyo ambayo ilitolewa January 2016, iliandaliwa ili kufanya utafiti ni kwa jinsi gani amshirika ya habari yanavyo fanya kazi na shirika la utangazaji wa luninga RT likanonekana kuwa linazidi kukua na kuwa tishio kwa mashirika ta utangazaji ya nchi za Ulaya Mgharibi na Marekani.




No comments: