Sunday, February 28, 2016

Urusi yazidi kujiimarisha kijeshi.


Urusi yazidi kujiimarisha kijeshi.

Urusi imeonyesha rasmi gari mpya  aina ya Batmobile ambayo itatumika katika mapambano ya kivita na vurugu za aina yoyote. Gari hiyo ambayo hapo awali ilijulikana kama  Punisher, inasemekana ni jibu kwa gari la kijeshi la Kimarekani Humvee.


Akiongea wakati wa kukagua gari hii mpya ya kijeshi, rais wa Urusi, Vladmir Putin alisema "nawashukuru kwa jitihada  na hii inahakikishia kuwa Urusi ipo tiyari kujibu mashambulizi ya aina yoyote pindipo tutakapo shambuliwa."

Kwa mujibu wa shirikala la habari la Urusi RT, gari hii mpya ya Kirusi, inauwezo wa kuchua watu kumi na ndani gari hii ina muundo wa V ambao inatoa kinga kubwa kwa watumiaji wa gari hii pindipo wakishambuliwa au gari kushambuliwa na bomu na vilevile hili gari lina mitambo ya kurushia mizinga.

Uzinduzi wa gari hili, unatarajiwa kuleta vichwa kuuma kwa Marekani na washiriki wake, kwani Urusi tangu iingilie vita vya Syria, nguvu zake za kijeshi zimefanya kuwepo na mabadiriko makubwa ya kivita kati ya serikali ya Syria inayo ungwa mkono na Urusi na wapinzani wa serikali wanao ungwa mkono na nchi za magharibi.

No comments: