Wednesday, March 9, 2016

Iran yarusha makombora.


Tehran, Iran 09/03/2016. Jeshi la Iran limefanikiwa kurusha makombora mawili  (Ballist missiles)  Urushaji wa makombora hayo yaliyo pewa majina ya Qadr -H na Qadr F ulifanyika kaskazini mwa nchi hiyo katika eneo lijulikanao Alborz Mashariki. Makombora hayo yanauwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 1500 hadi 2000.

Kamanda wa kitengo cha usalama wa anga wa Iran, Brigedia, Amirali Hajizadeh amesema kuwa. "Kombora aina ya Qadr H linuwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 1700 na jingine Qadr F linaweza haribu na kuchakaza kabisa kitu chochote kilichopo umbali wa kilomita 2000."

Tamko la Iran kuhusu kurusha makombora yake, limekuja baada ya msemaji  wa serikala ya Marekani Mark Toner kukosoa kitendo hicho nakusema " Kufuatia kitendo hicho cha Iran, Marekani italifikisha suala hilo katika balaza la usalama la umoja wa mataifa."

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, amesema kuwa " Iran haitaji ruhusa yoyote katika masuala yake ya kiulinzi wa nchi, na tulisha sema kuwa hatuta ulizia wala  omba ruhusa katika kushughulikia masuala yetu ya kiulinzi."

Iran nchi ambayo ilikuwa imewekewa  vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu na Marekani na washiriki wake, imekuwa kwa miaka mingi ikijitengenezea mitambo ya kiulinzi ya kijeshi na pia kuhakikishia jumuia ya kimataifa kuwa utengenezaji wa zana za kiulinzi  ni harakati za kujiimarisha katika suala la ulinzi wa nchi.




No comments: