Wednesday, March 2, 2016

Osama bin Laden alitaka mirathi yake itumike kundeleza mapambano. 


Aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden, alikuwa ameandika kuwa mirathi yake  ya kifedha zipatazo $29 millioni, kwa kiasi kikubwa zitumike takika kusaidia kuendeleza "Jihad" mapambano,  na kiasi kidogo kigawiwe kwa ndugu wa familia, ijapokuwa mpaka hazijulikani hizo fedha zipo wapi.

Zikiwa zimeandikwa kwa mkono wa Osama bin Laden, habari hizi, zimetolewa na serikali ya Marekani wiki hii, baada ya kuruhusu mafaili yaliyo kamatwa na kikosi maalumu cha kijeshi cha Marekani wakati walipo kuvamia makazi na  maficho  ya Osama bin Laden yaliyo kuwepo kwenye mji wa Abbottabad  Pakistan siku ya 1. Mai 2011 na kufanikiwa kumua.

"Nivyema kwa jamii kufahamu nini kiongozi wa Al Qaeda alipanga"  Alisema Brian Hale Mkurugenzi wa mambo ya jamii kutoka idara ya upelelezi ya taifa ya Marekani huku akiwa anaonyesha makaratasi yaliyo chukuliwa kutoka katika makazi wa Osama bin Laden

Karatasi hiyo ambayo inaonyesha nini kiongozi wa Al Qaeda alitaka kifanyike katika mirathi yake, ni moja ya makatasi 100 ambayo yameruhusiwa kuwekwa hadharani, baada ya kamati ya ulinzi na usalama kuyapitia kwa uangalifu.



No comments: