Wednesday, November 9, 2016

Donald John Trump ashangaza ulimwengu wa Siasa, Achaguliwa kuwa rais wa Marekani

Donaldo John Trump achaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani

New York, Marekani - 09/10/2016.  Donald John Trump, amechaguliwa kuwa rais wa 45 Marekani baada ya kupata vit vya kura 289 zidi ya mpinzani wake Hillary Clinton aliyepata viti vya kura 218.

Donald Trump akiongea mbele ya wapenzi na washabiki wake walikuwa katika hotel yake inayo julikana kama The Trump alisema. " Hillary Clinton amenipigia simu na kutupongeza na ninampongeza kwa jitihada zake wakati wa harakati wa uchaguzi huu."

"Ushindi wa leo, ni harakati na hazikuwa kampeni za uchaguzi, hivyo hizi harakati ndio sasa zimeanza kazi."

Vilevile rais mteule Donald Trup, aliwaomba watu wote kuwa wamoja na kwa kusema kuwa wale waliomchagua na wasionipigia kura wote wawe kitu kimoja na kuwa atakuwa rais wa Wamarekani wote.  "Nawaomba wote walio umia kutokana na uchaguzi tuwe wamoja ili kujenga Marekani mpya."

Rais mteule, Donald Trump, alikumbana na vikwazo vya kila namna katika kampeni za kuwania urais wa Marekani, kwa kudaiwa kuwa mbaguzi, msemaji wa vitu na mambo ambayo si yakiutu an pia kudaiwa kuwa alikuwa anadhalilisha wanawake.

Ushindi wa Donald Trup unatafsiliwa kuwa ni jibu kwa wanasiasa kwamba wabadirike kwa kuwa wa watu wamechoka na siasa zisizo eleweka na haadi wazizotimiza.

No comments: