Sunday, November 27, 2016

Rais Fidel Castro hatupo naye tena

Rais wa kwanza wa Kuba aaga dunia.


Havana, Kuba - 26/11/2016. Fidel Castro 90 rais wa kwanza wa Kuba na mwana mapinduzi amaefariki dunia.
Akitangaza kupitia luninga ya nchi hiyo, rais was sasa wa Kuba Raul Castro, alisema kuwa "rais wetu wa kwanza na kiongozi na mwanamapinduzi Komrade Fidel Castro amefariki leo 25/11/2016."
Kufuatia kifo cha rais Castro, Kuba itakuwa katika maombelezo ya siku tisa. Mazishi ya rais huyo wa Kuba yanatarajiwa kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa dunia.
Fidel Castro alikuwa mpinzani wa siasa za kibepari na alikuwa akipenda kusema "Uwanamapinduzi ni ni mapambano mpaka kufa ya wakati uliyo pita na wakati ujao."
"Wanaongea kushindwa kwa ujamaaa, lakini yapo wapi mafanikio ya siasa za kibepari katika bara la Afrika Asia na Latin Amerika?
" Sikubaliani na ubepari, ni mbaya auvutii na unatenganisha unaleta vita vitna na mashindano yasiyo na tija katika jamii."
Marehemu rais mstaafu wa Kuba Fidel Castro alizaliwa mwaka 31/08/1926 mjini Biran Kuba.

No comments: