Hatuta pindishwa na kupigishwa magoti na nchi za Ulaya"Ayatollah"

Kiongozi huyo alisema yakuwa Amerika na washiriki wake wasiwaze kabisa ya kuwa Iran, itapindishwa na kupigishwa magoti, kataika mradi huu wa nguvu za nyuklia.
Na ametaka swala hili liachiwe chombo kinacho simamia maswala haya kifanya kazi yake kama kawaida na siyo kukipangia.
Hadi hivi sasa, Iran imekuwa inasisitiza ya kuwa, mitambo ya nyuklia iliyo nayo ni kwaajili ya matumizi ya umeme na siyo kwa ajili ya kutengeneza siraha za kinyuklia.
Pichani anaonekana kiongozi mkuu wa Iran,Ayatollah Ali Kamenei akiongea hivi karibuni miji Teheren.
Hatumo tena kwenye mazungumzo"Hali ya usalama siyo nzuri kwetu"


Kivu, DRC - Kiongozi wa kijeshi , na aneye ongoza mapambano ya kutete jamii watutsi chini Kongo, Gen,Laurent Nkunda, amesema ya kuwa wamesimamisha mazungumzo na serikali ya Kinshasa kwa sababu za kiusalama.
Akiongea ,msemaji wa kundi la Gen Laurent Nkunda, bwana Jean Desire Muiti,alisema ya kuwa wamechukua uhamuzi huu , baada ya mmoja ya wa mmsemaji wa kikindi hicho bi Milindi kutishiwa kukamatwa.
Akiongezea, bwana Jean Desire Muiti, alisema ,ilibidi wajumbe waingilie kumuokoa , bi Milindi asikamatwe na kikosi cha askari wapatao kumi, amabo ni kikisi maalumu cha serikali ya Kinshasa, inayo ongozwa na rais Joseph Kabila.
Picha ya hapo juu anaonekana Gen Laurent Nkunda, akiongea na waandishi habari hapo siku za nyuma.
Picha nyingine anaonekana,mmoja ya wajumbe wa mukutano akiwa amekaaa hajui la kufanya,baada ya mkutano kuvunjika.
Senegel, yapotelewa na mmoja ya viongozi wake"Alikuwa na ushauri mzuri"


Bwana Bara Falilou aliyekuwa na miaka 92, alikuwa ni mjukuu wa mwanzilishi wa chama hiki Islamic Brotherhood amabcho kilianzishwa mnamo mwaka 1883.
Chama hiki Islamic Brotherhood, kimekuwa muhimili wa ushauri wa serikali ya Senegel.
Mmoja ya watu walio huzuria maombelezi ya kifo cha bwana, Bara Falilou, ni rais wa Senegel, bwana Abdoulaye Wade.
Kutokana na kifo cha bwana Bara Falilou, serikali ilitangaza maombelezo ya siku tatu
Pichani anonekana marehemu Bara Falilou, alipokuwa akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi waserikali.
Picha ya chini ni picha ya mwanzilishi wa chama cha Islamic Brotherhood, bwana Ahmadou Bamba.
Askari wa Irak, awaua askari wenzake kwa makusudi"Wakuu wa jeshi"

Tukio hili ni laina yake tangu Amerika, ivamie Irak mwaka 2003.
Askari huyo aliwapiga risasi askari wa amerika mmnamo tarehe 26/12, walisema wakuu wa jeshi ya kuwa tukio hilo lilitokea wakati askari hawa walipopo kuwa wakila doria moja ya vitongoji vya mji wa Mosul.
Hata hivyo wakuu wa vikosi hivi walisema mauaji haya yalifanyika kwa makusudi na askari huyu, anasemekana alijipenyeza na kujiunga na jeshi, na anatokea kwenye jamii ya Wasunni.
Pichani wanaonekana wanajeshi wa jeshi la shirikisho la Irak wakiwa tayari kuanza doria, na nyuma yao ni helikopta ikiondoka baada ya kuwashusha.
Kesi ya rais wa zamani wa Liberia yaingia awamu mpya"Ushahidi waanza kutolewa"
Hague, Netherland - Kesi ya aliyekuwa rais wa zamani wa Liberia,bwana Charles Taylor mwenye miaka 59, imeingia kataika hatua za mwanzo, baada ya mmoja wa mashahidi kuelezea mahakama,uhusianao uliokuwepo kati ya bwana Charles Taylor na baadhi ya viongozi wa vita vya wenyewe kwawenye, nchini Liberia na Sierra Leone.



Maelezo haya yalitolewa na mmoja wa aliyekuwa mkuu wa ulinzi wa bwana Taylor,bwana Varmuyan Sherif.
Bwan Sherif, alisema yakuwa alitumwa na ,bwana Taylor, kwenda kuonana na mmoja wa kiongozi wa kikundi cha kivita bwana Sam Bockarie .
Kikundi cha bwana Bockarie ndicho kinasadikiwa kuhusika katika vita vya Sierra Leone.
Hata hivyo mwanasheria kwa upande wa bwana Taylor,amesema ya kwamba, bwana Sherif alikuwa na matatizo ya akili wakati wote alipo kuwa akifanya kazi wakati ule.
Pichani hapo juu wanaonekana dada wa bwana Charles Taylor,bi Ann Payne Tayrol na Thelma Tayrol wakisikiliza na kuangalia kwenye runinga njinsi gani kesi ya kaka yao inavyo kwenda.
Picha ya pili anaonekana bwana Tayrol, alipokuwa mahakamani kusikiliza kesi yake.
Na picha nyingine ni ya bwana Sam Bockarie,amabye anasadikiwa kuwa ndiye aliyeongoza vita vya Sierrra Leone.
No comments:
Post a Comment