Je unajua mwanasiasa wa Afrika,anaishi kwa mashaka "Namashaka haya ndiyo chanzo cha matatizo"




Demokrasi ambayo Wafrika wengi waliipokea, haikuwa kama ilivyo tarajiwa, kwani wakati wa mageuzi yalipoanza vuguvugu lake, siyo Waafrika wengi walijua ya kuwa hali hii itakuwa kinyume na matarajio yao.
Waafrika wengi walitarajia maendeleo ya jamii na ya kiuchumi, na walitarajia yakuwa, kuja kwa vyama vingi au kwa mageuzi ya kisiasa yangeleta neema, kwa kila jamii.
Lakini ukweli ni kwamba sivyo ulivyo, kwani hakuna hata mwanasiasa mmoja ambaye aliweza kuueza ukweli kuhusu hali halisi ya mageuzi .
Bali wale wanasiasa ambao walikuwa wapo kabla ya mageuzi,, walishikwa na wasiwasi, na kuanza kupanga mikakati ya kukabiliana na mageuzi haya, nawakati huo huo chimbuko la wanasiasa ambao hawakupata nafasi ya kushiriki katika serikali ya awali, iliwabidi waanzishe vyama vya upinzani ambavyo vitakabiliana na chama tawala, si kwa kujenga bali kwa kulumbana na kusahahu kupanga mipango ya kujenga nchi kwa pamoja.
Jambo jingine ambalo naomba ni wafahamishe ndugu zangu, yakuwa mwanasiasa ni binadamu wa kawaida tu, ambaye ni mfanyakazi kama wewe au mimi, bali tofauti tulio nayo ni katika utendaji wa kazi, ni kwamba mwanasiasa anakuwa na mkataba wa muda fulani, kuongoza jamii kwa kipindi fulani, kufuatia katiba ya nchi iliyo wekwa na kipindi hiki kinaweza kuwa miaka mitano au zaidi, lakini tukae tukijua hii nikazi ya muda tu kwa mwanasiasa huyu.
Kama tunavyo jua wanasiasa wengi wa Afrika hawana huakika wa maisha baadaye pindipo watokapo madarakani, au chama chao kushindwa na chama pinzani, kutokana na hali hii, hujikusanyia kipato na kutumia fursa hii ya madaraka walio nayo kwa kufanya kila njia kujiandaa na hali ya baadaye pindipo hali ikienda kinyume,na wakati huo huo kupanga mikakati ya kubaki madarakani,
Kwani hadi hivi sasa karibu nchi zote za Afrika ambazo zimefanya uchaguzi wa kushindanisha vyama vingi, zimekumbwa na matatizo karibu yanayo fanana,na yale yaliyo tokea nchini Kenya, hasa kwa matokeo ya uchaguzi kuwa na mashaka mengi na mauaji ya kutisha ambayo jumui za kimataifa huwa hazijui ama hazifuatilii kuindani hali hizo.
Hii inategemea ni kwa kiasi gani chama kilicho shinda kinakubalika vipi kwenye jumuia ya kimataifa, hata kama chama hicho kimeshinda kwa mashaka makubwa.
Hali ya jumuia ya kimataifa kutofatilia malalamiko haya, yamekuwa ndiyo chanzo cha jeuri anayoendelea sehemu zote katika Afrika,kwani hadi hivi sasa kuna nchi zimefanya uchaguzi, na mauaji yametokea hakuna hata kiongozi mmoja wa serikali ambaye ameulizwa au kushitakiwa.
Hii siyo tu,inaonekana ya kuwa Waafrika bado tunawakati mgumu wa kukabiliana na hali hii, bali pia kuna baadhi ya viongozi ambao wanagombania kuongoza nchi hizi hawana mapenzi na watu wao wala kizazi kijacho cha nchi hizi.
Viongozi hawa wamekuwa wakigombania kuongoza nchi kwa kutumia mbinu za kila namna na hasa ukabila, dini na hali ya ufukara, kwa kuwarubuni wananchi yakuwa watasawazisha matatizo hayo, na kuwapa matumaini makubwa.
Lakini wanapo ingia madarakani wanakuta hali sivyo walivyo haidi, na kushindwa kuwaelezea wanchi ukweli ya kuwa hali sivyo ilivyo kama walivyo haidi.
Ukweli ni kwamba uchumi na siasa ni sawa na baba na mama, kwani baba anapokuwa hatekelezi majukumu yake, basi mama hataangaika pekeyake kujenga nyumba, na kama mama hataonyesha mapenzi kwa baba na kushirikiana kumsaidia baba kujenga nyumba, basi hali huwa mbaya kifamilia.
Hivyo basi uchumi wa Afrika kiasilia ni mwingi hauna mfano wa kulingana, lakini jinsi ya kuboresha uchuni huu ndiyo mashaka makubwa,kwani nchi nyingi za Afrika katika bajeti ya kila mwaka haziweki fungu la fedha la kuhimiza au kusaidia watu kugungua nyezo bora za kujenga na nyezo kusaidia au kurahisisha kazi za kila siku.
Fedha nyingi hupotea bila kujulikana matumizi yake na wala hazijulikani zimewekwa kwenye mabenki gani?
Bali utasikia kila kiongozi wa Afrika, anasema ya kuwa hatuna fedha za kusaidia kuboresha maisha ya wanainchi, lakini wakati huo huo utaona ya kuwa matumizi ya wanasiasa ya nakuwa makubwa kupindukia, nampaka kuwashangaza wana nchi na jumuia za kimataifa.
Vile vile jumuia za kimataifa zina changia kwa kiasi kikubwa kuleta hali hii,kwani baadhi ya mikataba inayo wekwa huwa haina manufaa kwa pande zote mbili, na 10% huwa ndiyo kiungo cha kumbana mwanasiasa wa Afrika.
10% na mambo mengine ya kiundani ambayo jumuia ya kimatifa inajua kuhusu viongozi hawa wa Afrika, ambao wapo madarakani, huwa ndiyo siraha kubwa ya kuwabana wasiwe na sauti wanapo kuja kukubaliana kuhusu mikataba na kutetea haki za wanachi wao,hivyo huwafanya viongozi hawa kuwa wazee wa ndiyo ndiyo kwa kila wanacho ambiwa.
Demokrasi na Afrika ni kitu kigeni saana, kwani wananchiwalio wengi wa Afrika, wanaishi kwa kila kukicha na kukizama hawajui nini la kesho, bali wale wachache, alio jaaliwa kupata homa ya demokrasi, basi hutumia kuwaambukiza Waafrika wenzao na matokeo yake ni kama yalio tokea nchini Kenya hivi karibuni.
Ikiwa kama mwananchi hawana matumaini na serikali na serikali haisemi ukweli kuhusu hali halisi, basi wananchi wanakuwa wanageuzwa geuzwa kama pia kwa kufuata wapi kunatoka maneno matamu, nakusahau ya kuwa wanacho hitaji siyo maneno matamu bali ni maendeleo ya kijamiii na kiuchumi, lakini hali ya rushwa na udanganyifu inapo fikia kiwango cha kuwa ndiyo njia ya kipato kwa mwananchi basi, ndipo kila mtu ujiangalia nafsi yake na kusahahu mwingine na kuangalia atamsaidia vipi ndugu yake, ili aweze kupambana na maisha ya lila siku, na ndugu yake akipata basi ataangalia ndugu yake, na ndugu yake kwa ndugu yake na itakuwa hivyo, mpaka yatapo tokea mabadiliko ya uongozi, na huyu kiongozi atakaye ingia atafatialia mtindo huu, na kiongozi mwingine akifatilia mtindi huu, basi nchi huishia kugawanyika kimakabila au kidini.
Na hii ni sumu moja kubwa ya kuua jamii fulani na kuinua jamii fulani, na hatimayake ikifikia tamati ni punje moja ya baruti itawasha mbunga nzima, kwani mbuga nzima ilikuwa majani yake yalikuwa yamekauka tayari.
Swali la kujiuliza je wakati mbuga nzima ina kauka jumuia ya kimataifa ilikuwa haioni?
Ukweli ni kwamba jumuia ya kimataifa ilikuwa inaona, kwani kila usikiapo maoni ya wanasiasa na wa tafsili wa mambo wanazungumzia ya kuwa hali hii ilikuwepo tangu zamani.
Je, hawakujua yakuwa mbuga inapo kauka ni chembe moja ya baruti ikiwaka iataunguza mbuga mzima?
Ukweli ni kwamba walijua, nasema haya kutokana na historia ya wanadamu, ya kuwa huwa anavumulia kwa kiasi fulani lakini uvumulivu ukishindwa basi, ni uadui hufuata na huasama.
Hivyo basi hali ya nchi ya Kenya, ilikuwa inajulikana kwa kiasi kikubwa ya kuwa yapo mataba na matatizo ya ukabila, lakini kwa sababu fulani na manufaa ya liyokuwa yanapatikana kutokana na hali hii, zilifanya jumuia ya kimataifa,kupuuzia, kutofatialia kuindani madhara yatakayo kuja baadaye au kujiuliza je siku ikifikia uvumilivu huu ukaisha kutakuwa nini?
Sasa leo hii, dunia nzima inalia na Wananchi wa Kenya, hasa Afrika,maisha ya watu yanapotea kiunyama.
Viongozi wa siasa,dini na watu tofauti wanajaribu kuomba na kusisitiza utulivu nchini Kenya, lakini inakuwa vigumu kwani nusu ya mbuga imesha kauka na baruti imewaka na kuleta moto ambao kuuzima kunaitaji jitihada zaidi kulikoni ilivyo tarajiwa
Hii ni fundisho jingine kwa jumia ya kimataifa, kwani tujue ya kuwa dunia na walimwengu wa leo tunategemeana kwa kiasi kikubwa sana, japo wapo watu wasioamini hili.
Matatizo ya nchi moja ni matatizo ya dunia nzima kwa ujumla, hivyo naombatushirikiane kutimiza amri za Dini zote Zina himiza tuwe na Upendo.
Kwani kwa wale Wakritu, kama wanakumbuka,"Bwana Yesu Kristu, alisema amri mpya na wapa pendaneni kama nilivyo wapenda mimi, kwani mtu hawezi kumpenda Mungu wakati haumooni, na wakati huo huo unamchukia jirani yako mbaye unamuona. Hivyo basi fumbo hili tukilitimiza basi dunia nzima itakuwa na amani japo kwa dakika moja.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu tunaomba Hekima na Upendo utushushie Afrika
Picha juu inaonyesha ramani jinsi gani nchi ya Kenya ilivyo gawanyika kikabila.
Picha nyingine anaonekana polisi anamwangalia rais jinsi alivyo pata madhara kutokana na vurugu hizo.
Picha, anaonekana mwanajeshi wa Kenya akiwa ameshika bunduki juu, huku wananchi wakiwa wanamwangalia kwa hasira.
Matokea ya uchaguzi nchini Kenya yameleta hali isiyo tabilika, wanaonekana wananchi wenye hasira wakiwa na kila aina ya zana tayari kupamba wao kwa wao.
Siku zote panapo tokea vita au vurugu wanao dhurika zaidi ,ni wakina mama na watoto, pichani wanaonekana wakina mama wakiangalia kwa kiasi gani mali na makazi yao yalivyo haribiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment