Sunday, January 20, 2008

Putin na Kremlin wazidi kutanua misuri ya kiuchumi barani Ulaya.

London, Uingereza - Mchezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid , Man United na aliyekuwa kaptain wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham, amejiunga na timu ya Arsenal kwa ajili ya kuijiweka fiti.
David Beckham, ambaye kwa sasa anachezea timu ya LA Galxy ya Amerika, yupo nchini Uingereza, baada ya ligi ya Amerika kuisha kipindi chake cha 2007.
Kufanya mazoezi na timu ya Arsenal, kutamsaidia David Beckham, kuwa fit pindipo ataitwa kujiunga na timu ya taifa ya Uingereza, ambayo ina kocha mpya bwana Fabio Kapello.
Picha hapo juu anaonekana, David Beckham, Kolo Ture, na wachezaji wengine wakielekea mazoezini.
Chini pichani anaonekana David Beckham, akipasha viungo moto tayari kula ufundi wa kisoka kutoka kwa Wenger .
Thabo Mbeki,awasili Zimbabwe , ''Kitendawili bado kuteguka?''
Harare, Zimbabwe - Rais wa Afrika ya Kusini bwana Thabo Mbeki, amewasili nchini Zimbabwe, ilikujaribu kuzungumza na viongozi wa serikali na viongozi wa vyama vya upinzani.
Hata hivyo viongozi wa chama cha upinzani wamepanga maandamano makubwa yatakayo fanyika hivi karibuni kudai mabadiliko ya katiba.
Ziara ya rais,Mbeki ni moja ya harakati za kutaka kusuruhisha mgogoro wa kisiasa uliopo kati ya chama cha ZANU-PF,na wapinzani.
Ufaransa yaiwekea ngumu Rwanda,mtuhumiwa hatasafirishwa"Mahakama"
Paris, Ufaransa - Mahakama ya serikali ya Ufaransa, imesimamisha kuhamishwa kwa mtuhumuiwa ambaye inasadikiwa alihusika katika mauaji ya watu wengi, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye nchini Rwanda.
Mtuhumiwa huyu,bwana Dominique Ntawukuriryayo, anashutumiwa kwa kuhusika na mauaji ya watu jamii ya tutsi wapatao 25,00 wakati wa mauaji yaliyo stua dunia 1994.
Akiongea kwa niaba ya mtuhumiwa, mwanasheria anaye mwakilisha bwana Dominique, bwana Thiery Mausis, alisema uhamuzi huu umekuja baada ya kugundulikaya kuwa kuna baadhi ya sheria zilikiukwa.
Pichani ni rais wa Rwanda, bwana Poul Kagame, ambaye aliongoza kuleta utulivu nchini Rwanda, kuhakikisha kila aliye husika katika mauaji ya watu wasio na hatia, lazima wakumbane na vyombo vya sheria kujibu mashtaka.
Putin na Kremlin wazidi kutanua misuri ya kiuchumi barani Ulaya.
Sofia,Bulgaria - Serikali ya Urusi na Serikali ya Bulgaria zimetiliana makubaliano ya kuwa serikali ya Urusi itajenga mabomba ya kupitisha gasi nchini Bulgaria.
Kujengwa kwa mabomba haya kutaiwezesha Urusi, kuwa ndiyo nchi pekee kwenye bara la Ulaya itakayo kuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza gasi.
Wakati huo huo huo,serikali ya Urusi ,imeseamaya kuwa serikali ya Uingereza inapoteza ukweli wa hali halisi,wa matukio yaliyo tokea kati ya London na Moscow.
Hali hii inatokana na serikali ya Urusi kufunga ofisi za muhimu ambazo zilikuwa zinatumiwa na mashirika na watu binafsi kuweza kufanya kazi na Uingereza.
Pichani wanaonekana viongozi wa Urusi na Bulgaria wakiwa pamoja wakati wakijiandaa kuongea na waandishi wa habari baada ya kukubaliana kimikataba.
China kuwa mkombozi wa uhaba wa lishe kwa wananchi.
Harare,Zimbabwe - Serikali ya China imehaidi kuisaidia serikali ya Zimbabwe,ili iweze kujinyakua kwenye hali ya uhaba wa chakula kwa kuipatia kiasi cha toni 5000 za chakula..
Ahadi hii ilitolewa na makamu msaidizi wa balozi wa China nchini Zimbabwe bwana Ma Deyun.
Akiongea,wakati alipo kutana na viongozi wa serikali ya Zimbabwe,kaimu balozi huyu bwana, Ma Deyun, alisema nchi hizi mbili zitaongeza ushirikiano wa kijamii na kibiashara kwenye msimu wa mwaka 2008.
2007, biashara kati ya China na Zimbabwe, ili ongezeka kwa kiasi kikibwa, na kwa mwaka 2008, huusianao wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili utagharimu kiasi cha $500million.
Serikali ya China,imekuwa ikijenga uhusiano na serikali nyingi za Afrika.
Hapo juu ni picha ya bendera ya Zimbabwe na chini ni picha ya bendera ya China.

No comments: