Wednesday, March 5, 2008

Polisi atoa siri ya serikali"Serikali ya kanusha" Ushwari kuanza kurejea.

Nyota ya timu ya Barcelona yapata majeraha kwa mara nyingine.

Barcelona, Uispania - Mchezaji nyota wa timu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, hataweza kucheza kwenye mechi au mazoezi kwa kipindi kisicho pungua wiki sita, baada ya kuchanika misuri ya mguu wake wa kushoto.
Messi,amekuwa akisumbuliwa na majeraha tofauti ambayo yamekuwa yakimkuta kila mara.
Akisema haya mganga wa timu ,aongezea yakuwa itambidi apumzike kwa kipindi na siyo vyema kumharakisha kuanza mazoezi.
Akiongezea haya kaptaini wa timu ya Barcelona, Chales Puyol alisema ya kuwa wapenzi wa timu yao wamakuwa wanadai Messi achezeshwe, pindipo akionekana ana nafuu kidogo, na akashauri wawe wavumilivu na kuacha kazi hii iwe ya waganga wa timu.
Pichani hapo juu anaonekana Lionel Messi akiwa na nyota ya soka Diego Armando Maradona.
Picha ya pili anaonekana Messi akiwa anafanya mavitus kabla ya kupata majeraha ya misuri wakati wa pambano la marudiano na timu ya Celtic ya Schotland.
Picha nyingine naonekana Mesi akiwa anagaaga chini, baada ya kupata maumivu,na picha ya chini anaoneka Lionel Messi akiwa anatolewa nje ya uwanja na mmoja wa viongozi wa timu ya Barcelona.
Bi, Madona atoa album mpya, wapenzi wake kukonga roho.
London, Uingereza - Malkia wa muziki wa pop, bi Madonna amezindua rasmi album mpya ijulikanayo kama Hard Candy.
Album hiyo ambayo imekuwa ikingojewa kwa hamu saana, imeanza rasmi kupataikana tangu tarehe, 29/april/2008.
Madonna ambaye kila anapotoa album yake huwa ana kujas na kitu kipya, hivyo kwenye album hii, amesema ya kuwa hii albumu ni kwa ajili ya wale wanaopenda lawalawa.
Picha hapo juu anaonekana bi Madonna , akiwa ame mwaga tabasamu ya hali ya juu, kuashiria ya kuwa wapenzi msiwe na shaka album hii ita konga roho zenu.
Picha ya pili na ya tatu anaonekana bi Madonna anapo kuwa kazini hataki mchezo, huwa anafanya kweli kwa kila zana za muziki.
Picha ya bhapo chini anonekana bi Madonna akiwatumbwiza wapenzi wake huku akiwa amavalia vazi lenye rangi ya mapenzi.
Mafuriko yaleta madhara makubwa kwa wakazi wa Kusini mwa Afrika.
Windhoek, Namibia - Mvua kubwa ambayo inaendelea kunyesha maeneo ya Kusini mwa Afrika, inasababisha uharibifu mkubwa na kuleta madhala makubwa kwa wakazi wamaeneo haya,haya ni kwa mujibu wa msemaji wa msemaji wa kamati ya uokoji na kusaidia kwenye maeneo yaliyo dhurika na mvua hizi bwana Gabriel Kangowa.
Kwa mijibu wa msemaji wa UN, kwa upande wa kusaidia watoto alisema kunazaidi ya watoto wapatao 15000, ambao wanahitaji msaada wa haraka zaidi kwenye maeneo haya..
Mafuriko haya yameleta madhara maeneo tofauti ya nchi za Namibia, Zambia,Zimbabwe, Mozambiki na Malawi.
Picha hapo juu zinaonekana sehemu tofauti amabazo zimekumbwa na mafuriko na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wa maeneo ya kusini mwa Afrika.
Polisi atoa siri ya serikali "Serikali yakanusha" ushwari kuanza kurejea.
Nairobi, Kenya - Serikali ya Kenya imekanusha ya kuwa haijawahi kuwa na mkutano wa siri na kundi la Mungiki, kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Akiongea, msemaji wa serikali alikanusha ya kuwa hakukuwepo na mkutano waina yoyote kati ya serikali na kundi hilo.
Inasadikiwa mkutano huo ulifanyika kwa siri, ili kuweza kupanga ni jinsigani kundi hili linaweza kulinda watu wa kabila la Wakikuyu na mali zao hasa maeneo ya Lift Valley.
Siri hii imefichuka baada ya moja wa askari wa polisi kuongea na shirika moja la habari,na kueleza ni kwanini kwenye baadhi ya maeneo, watu wenye siraha waliruhusiwa kuvivuka vizuizi vya polisi bila kuzuiliwa kuelekea maeneo yaliyo tokea fujo.
Picha hapo juu, wanaonekana polisi wa Kenya wakipambana na moja ya watu amabo wanashutumiwa kuleta vurugu na machafuko.
Picha nyingine wanaonekana wananchi wenye huruma wakimsaidia mmoja wa majeruhi, aliye pata majeraha kutokana na vurugu hizi.
Picha ya chini anaonekana, aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Matifa bwana Kofi Annan, akiongea na waandishi wa habari baada ya viongozi wa pinzani wa Kenya, bwana Mwai Kibaki na Laila Odinga kukubaliana kuongoza nchi kwa pamoja.

Ukanda wa Gaza, bado waleta kichwa kuuma kwa serikali ya Amerika.
Gaza, Palestina - Rais wa Palestina bwana Mahmoud Abbas, ameseama ya kuwa hataendelea na mazungumzo ya kuleta amani kati ya Israeli na Palestina.
Rais Mahamoud Abbas aliyasema haya wakati alipo kuatana na waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Amerika bi, Condoleeze Rice, wakati alipo kwenda kumuona kujadili ni jinsigani utulivu unaweza kurudi, baada ya machafuko yaliyo tokea siku za karibu, kati ya kundi la Hamas na na Jeshi la Israel.
Waziri wa mambo ya nje wa Amerika, yupo ziarani kwenye maeneo haya, kuendeleza mazungumzo ya amani katai ya Israeli na Palestina.
Machafuko haya ambayo yameanza tena kwenye ukanda wa Gaza yamekuwa ya kuwa, yakivuruga upatikanaji wa amani katika eneo hili kwa muda mrefu.
Picha hapo juu anaoneka arais Mahamoud Abbas, akimkaribisha bi, Condoleeze Ricealipo kwenda kumtembelea hivi karibuni.
Picha chini anaonekana bi,akikaribishwa na mmoja wa viongozi wa Israeli, alipokwenda kuongea na viongozi wa Israeli
Viongozi wa dini zote kukutana mjini Rome, kuunga dalaja la imani kwa waumini wao.
Rome Itali - Kiongozi wa Kanisa Katoliki diniani Pop Benedict,ataongoza mkutano kati ya Waumini wa Kikristu na Waumuni wa Kiislamu utakao fanyika mwezi wa November mwaka huu.
Akiongea haya msemaji wa wa Vatican alisema ya kuwa mkutano wa kwanza utafanyika november 4 mpaka 6 mjini Rome.
Mkutano huu utaudhuliwa na viongozi wa dini wa wapatao 24 na walimu wa dini zote.
Moja ya mazungumzo yatakayo watakayo zingatia na kujadili kwa undani ni Upendo wa Mungu,n upendo kwa jirani , utu na kuheshimiana kwa watu na imani zao.
Picha hapo juu ni alama inaonekana alama ya mwezi na nyota kama alama ya Uislamu, kati ni alama ya Msalaba ikiwa ni ishara ya kuamini Ukristu
Chini ni picha ya Pop Benedict, akiwa ameshikilia na kukinyanyua kitabu kitakatifu juu.
Rais,Hugo Chavez aionya, serikali ya Kolombia kaeni chonjo, kazi mbaya si mchezo mwema.
Cucuta,Vanezuela - Serikali ya Venezuela, imeaanza kupeleka majeshi yake pamoja na vifaru kwenye mpaka na nchi ya Kolombia,haya ni kwa mujibu wa msemaji wiraza ya ulinzi.
Kupelekwa kwa wanajeshi hawa mpakani, kuna kuja baada ya jeshi la Kolombia, kuingia kinyume cha sheria nchini Ekuado na kumua kiongozi wa kundi la FARC,bwana Raul reyes.
Kuwepo kwa majeshi haya mpakani mwa Kolombia na Venezuela, ni kuwa seriakli ya Venezuela inajiandaa kuzuia uwezekano wa majeshi ya Kolombia kuvuka mpaka na kuingia nchini Venezuela, ambapo inadaiwa ya kuwa, mipakani humo ndipo wapinzani wa serikali ya Kolombia FARC, wanaishi.
Picha ya juu, anaonekana rais Hugo Chavez, akiongea na waandishi wa habari kuhusu maswala ya ulinzi nchini Venezuela.
Picha nyingine anaonekana, rais Hugo Chavez, akijaribu siraha amabyo ni moja ya siraha zitakazo tumika, pindipo vita vikianza kati ya Venezuela na Kolombia.
Picha ya chini wanaonekana wanajeshi wa Venezuela wakiealeka mpakani mwa Venezuela na Kolombia.

2 comments:

Anonymous said...

Nice post and this post helped me alot in my college assignement. Say thank you you seeking your information.

Anonymous said...

Sorry for my bad english. Thank you so much for your good post. Your post helped me in my college assignment, If you can provide me more details please email me.