Monday, March 24, 2008

Pope John Poul II aonekana katika umbile la moto"Adai aliye piga picha"

Nyota ya the Green Eagles yataka weka daruga za soka muda si mrefu.

London, Uingereza - Mchezaji na nyota ya timu ya taifa ya Nigeria Jay Jay Okacha, amesema ya kuwa msimu wa soka wa 2007-2008, huenda ukawa mwisho wake wa kucheza soka la kulipwa.
Ja Jay Okacha, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Hull, amekuwa kivutio kikubwa kila awapo uwanjani kulisakata gozi la ngombe,hasa alipo kuwa amevalia jezi ya timu yake ya taifa ya Nigeria na kufunga magori 59 mpka hapo malipo jiudhuru kuchezea timu hii ya taifa.
Jay Jay Okacha, ambaye ameanzia kucheza timu ya Ujerumani Franfrut, Uturuki Fenebasche,PSG Ufaransa na Bolton ya Uingerea, amekuwa chachandu kwa kila timu aliyo chezea.
Pichani hapo juu anaonekana Jay Jay akiwa nanafanya vitu vyake ndani ya jezi ya the Green Eagles.
Picha ya pili anaonekana,Jay Jay Okacha akiuliza ya kuwa vipi, kwani kila aje kwangu ajue nipo kazini, lazima wawe fiti.
Picha ya tatu anaonekana Jay Jay Okacha, anaonekana akitoa kitu ambacho makipa huwa ni vigumu kutabiri ni jinsi gani wanaweza kuzuia kitu hiki.
Pope John II aonekana katika umbile la moto" adai mpiga picha hii".
Rome, Itali - Picha ambayo ipo katika umbile la moto, imeoneka hivi karibuni wakati wa kuazimisha miaka miwili toka kiongozi wa kanisa Katoriki Duniani hayati Pope John Poul II aiage dunia
Picha hii ilipigwa na polisi mmoja ambaye alipiga picha hii aliseama alikuja kuitambua picha hii baada ya ya muda fulani.
Maadhimisho haya yalifanyika karibu na eneo alilozaliwa Pope John II, kwenye mji wa Beskid Zywiecki.
Pichani hapo juu ni picha ya hayati Pope John II, akitoa salamu na baraka kila alipo kuwa akiwa ziarani, na upande wa pili ni picha ya umbile la moto ambayo ilipigwa siku ya kuadhimisha miaka miwili toka aage dunia.
Miaka mitano ya vita vya Irak, bado utata, " nani zidi".
Baghdad, Iraq - Dunia nzima hivi karibuni imeazimisha miaka mitano tangu vita vya Iraq vianze vikiongozwa na Amerika.
Haki hii imekuwa ya maoni tofauti na mabadiliko makubwa kijamii na kisiasa, aliongea haya , mmoja ya wafanyakazi wa zamani wa shirika la msaraba mwekundu bwana Roland H Benjanin ambaye alikuwa nchini Iraq, wakati wa vita vinaanza.
Shirika la msaraba mwekundu lilitoa wafanayakazi wake wote baada ya jengo lao kulipuliwa na na kusababisha vifo vya wafanayakazi wake. Hata hivyo vita hivi vmeleta maafa ya kupoteza maisha ya watu kutoka jamii tofauti,kuanzia wanajeshi na raia pia
Vita hivi mpaka sasa inasemekana idadi ya wanajeshi 4000, wa Amerika wamepoteza maisha yao, hii ni kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa mambo ya kivita nchi Amerika.
Picha hapo juu anaonekana mmoja wa raia wa Iraq akiwa ameshikiliwa na wenzake huku akiwa na uchungu na majonzi baada ya mmoja wa familia yake kuuwawa na bomu hivi karibuni.
Picha pili chini anaonekana mwanajeshi wa jeshi la Amerika akiwa kazini huku raia wa Iraq,wakimwangalia kwa walakini.
Hatuelewi wanamuomba nani msamaha," kwani wanatakiwa kutimiza walicho haidi, mmoja wa wanajeshi waliopigana vita vya Iraq".
New York, Amerika - Harakati za kupata walichokuwa wakipigani imefika hali ya kuwa usumbufu kwa wanajeshi waliopigania nakutetea nchi ambayo walikuwa wanajua ya kuwa wakimaliza kutimiza kazi waliyo tumwa na hawatakuwa na wasiwasi wakuwa raia wa nchi amabyo walipigania na nchi ambayo ilikuwa ndoto yao, haya yalisemwa na mmoja wa wapiganaji ambao walikuwa mstari wa mbele kataika vita vya kumng'oa madarakani rais wa Iraq hayati Saadam Hussein.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wapiganaji hawa, bwana Abdool Habibullah mwenye miaka 27, ambaye ni mzaliwa wa Guyana, alisema yakuwa aliomba urai wa amerika semptemba 2005, baada ya kurudi kwenye mambano ya Iraq,na mpaka sasa 2008, bado anangojea majibu, nas inaelekea alicho ongea rais Bush ya kuwa hali itakuwa nzuri na kila kitu kitakuwa sawa tutakapo rudi kutoka vitani. Sasa hatuelewi nani wanaomba msamaha,kwani wanatakiwa kutimiza hahadi waliohaidi.
Akiongezea yakuwa hali hii ni kuto kuwajibika kwa baadhi ya watu waliopo maofisini, mmoja ya wapiganaji walio rudi kutoka vitani Krzsztof Matejqowasqi mwenya miaka 22, ambaye amekaa Iraq kwa kipindi cha miezi 15 alipo rudi alikuta yakuwa karatasi za maombi yake ya kuwa raia wa Amerika zimepotea.
Picha hapo juu ni moja ya wanajeshi ambao wamepigana vita vya Iraq, na mpaka sasa wanasubiri uraia wao kupitishwa.
Kamati ya Usalama na Ulinzi ya Umoja wa mataifa, inakiuka miiko yake,na Darfur wanateketea.
New York - Amerika -Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan, amesema ya kuwa kamati ya ulinzi na usala ya Umoja wa Mataifa ina kiuka( miiko)wajibu wake kwa kufungia macho matatizo yanayao tokea Darfur.
Akiongea haya wakati alipo kuwa amealikwa kwenye chakula, bwana Kofi alisema ya kuwa dunia nzima imekuwa ikitegemea kamati hii ya ulinzi na usalama kufanya maamuzi ambayo yana manufaa kwa wanadamu wote, lakini sivyo kamati hii inavyo fanya.
Aliongozea ya kuwa kupelekwa kwa jeshi la Umoja wa Afrika Darfur, imekuwa ni kitendawili kwa kamati hii, na wakati huo huo watu wanazidi teketea kwa kipindi kirefu sasa.
Bwana Annan, ingawa hakutaja nchi, lakini inaeleweka ni nchi zipi zipo kwenye kamati hii, aliongea haya mmoja ya wageni walioalikwa kwenye chakula hiki kula pamoja na bwana Annan
Wa Cyprus wataka kuwa kitu kimoja, viongozi wao wasisitiza.
Nicosia, Cyprus - Viongozi wapinzani wa kisiwa cha Cyprus, bwana Mehmet Ali Tarat na Demetris Christofias, walikutana na kuongea chini ya usimamizi wa umoja wa Mataifa.
Mkutano huu ulifanyaiaka kwenye eneo ambalo lipo chini ya Umoja wa mataifa.
hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hawa kukutana baada ya bwana kuwa rais wa Cyprus ambayo ipo upanda wa Greeki.
Viongozi hawa walisema ya kuwa wanataka kufungua kitabu kipya, na kuleta mabadiriko ya kisiasa kisiwani hapo.
Kisiwa cha Cyprus, kimegawanyika sehemu mbili, moja ipo chini ya serikali ya Uturuki na nyingine ipo chnini ya serikali ya Greesi.
Talibani, wasema bado wapo ngangali, waja na mbinu mpya za mapigano.
Kabul, Afghanistani - Kiongozi wa kundi la Talinani bwana Jalaluddini Haqqani, ametangata ya kuwa kundi lake litaanz mashambulizi umpya ya kupigana na wanajeshi wa NATO amabao wapo nchini Afghanistani.
Akiongea katika runinga ambayo ememuonyesha bwana, Jalaluddini Haqqani akiwa amepauka kwa kiasi,aliendelea kusema ya kuwa. kupotea kwao ilikuwa ni moja ya mbinu za kujijenga upya, na hivyo vita hivi hawakuwa wameshindwa, na sasa wamekuja na mbinu mpya ya kushambulia kwa kutumia mbinu za kuvuizia na kushusha.
Picha hapo juu anaonekana kiongozi wa Talibani, bwana Jalaluddini Haqqani akiwa ndani ya gani moja nchini Aghanistani.
Picha nyingine ni picha ambayo inaonyesha jinsi gani Talibani wanavyosumbua vichwa ya jumuia ya kimataifa,kwani hapo katika picha ni moja uaribifu uliotokea baada ya bomu kulipuka na kuuwa baadhi ya wanajeshi wa NATO na wakazi wa eneo hili.
Jeshi la Umoja wa Afrika kuanza kuonyesha misuri yake katika kutatua matatizo ya bara la Afrika?
Njuani, Komoro - Kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika, kimewasili kwenye kisiwa cha Njuani, tayari kupamabana kurudisha kisiwa hicho mikononi mwa serikari.
Inaaminika zaidi ya wanajeshi wasiopungua 1000, kutoka Tanzania, Sudani, na Senegali wapo tayari kukiweka kisiwa hicho mikononi mwa serikali, aliongea haya msemaji wa jeshi hilo la umoja wa Afrika, kamanda Yahaya Abdalhah.
Serikali ya Libya ndiyo itakayo toa kila aina ya misaada ya kiufundi na kitaaluma.
Kisiwa cha Komoro kimekuwa na mgogoro wa kisiasa tangu ulipo fanyika uchaguzi 2002.
Pichani hapo juu wanaonekana wanajeshi wa jeshi la jeshi la Umoja wa Afrika wakiwasili kwenya kisiwa cha Juani nchini Moroko.

No comments: