Sunday, February 24, 2008

Iran yaitaka Amerika na washiriki wake waiombe radhi

Nyota ya kabumbu ya zamani ya Uingereza kupata matibabu ya kuepuka kilevi.

London , Uingereza - Nyota ya zamni katika mchezo wa mpira wa miguu nchini Uingereza Poul Gascoine, au kwa jina maarufu Gazza, amewekwa kwenye kituo maalumu cha kutibia watu wenye matatizo ya kilevi.
Gazza ambaye alikuwa chuchu ya mafaniko ya timu ya taifa ya Uingereza miaka ya 80 mwishoni na ya 90,kwa umaili wake wakujua kulisakata kabumbu na kutoa mapande mazuri kwa washambuliji wake wa timu taifa ta Uingereza.
Pichani hapo juu anaonekana Gazza akisoma kikaratsi jinsi gani ya kuwakumbusha vijana wa timu yake la kufanya ili kutorudia makosa wakati alaipo kuwa kocha wa timu Kattering Town.
Picha ya pili anaonekana Gaza katika hali tofauti, siku za mwisho kabla ya kutundika daruga za kabumbu.
Picha ya tatu anaonekana Gazza, alipo kuwa kazini hakuwa na mchezo, mis the ball, get the man, enzi hizo sheria za mpira zilikuwa zinaruhusu kukandamizana uwanjani.
Picha ya nne na ya tano anaonekana Gazza, akili kwa uchungu baada ya timu yake ya taifa kukuso kuendela na mashindano kwa kutolewa na wapinzani wao wakuu Ujerumani wakati wa mashindano ya mataifa ya Ulaya yaliyo fanyaika Uingereza.
Mungu ni chanzo cha mafanikio yangu,Kaka atoa sadaka kombe lake la dhahabu.
Sao Poulo, Brazil - Mchezaji bora wa dunia kwa upande wa soka, Kaka kombe lake la dhahabu kama mchango kwa kanisa ambalo ni muumini wa kanisa hilo.
Kaka amabye ni amabye ni mmoja ya wachezaji walokole, (born again) alisema ya kuwa nalileta kombe hili hapa mbele ya Mungu, kwani mafanikio yangu yote yamekuwa ni baraka za kutoka kwa Mungu kwa kupitia mwana ye mpendwa Yesu Kristu.
Na kombe hili litakaa hapa Kanisani, alimalizia kwa kusema haya mbela ya waumini wasio pungua 5000.
Hivi karibuni Kaka alishinda kwa kuwa kijana, ambaye ameamua yakuto kuwa na msichana mpaka hapo atakapo oa.
Kaka, ambaye jina lake kamili ni Ricardo Izecson dos Santos Leite, amesema ukifika wakati wa kuacha kucheza mpira atapendelea kuwa mchungaji, ili kumtumikia Mungu.
Uturuki yadai ya kuwa Iraq imeshindwa,basi Uturuki itaendelea mpaka wamalize kazi yao.
Ankara, Uturuki - Helikopta moja ya jeshi la Uturuki, ililipuliwa hivi karibuni na kikosi cha askari na kuleta maafa bmakubwa kwa upande wa jeshi la Uturuki.
Mmoja wa wasemaji wa PKK, alisema ya kuwa waliitungua helikopta hiyo muda wa saa za magharibi karibu na mji kimoja uitwacho Chamsku.
Kuthibitisha habari hizi msemaji wa jeshi la Uturuki, alisema ya kuwa kuna helikopta moja ilianguka na hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na msemaji huyo.
Wakati huo huo , serikali ya Iraq imeitaka serikali ya Uturuki, kuyatoa majeshi yake nchini Iraq na karibu namipaka yake kwani mapambano hayo yanahatarisha usalama wa Iraki.
Hata hivyo serikali ya Uturuku ,inadai ya kuwa imeamua kufanya hivyo baada ya serikali ya Iraq kushindwa kuwazuia wapiganaji wa PKK, kshambulia nchini Uturuki.
Picha ya juu anaonaekana, mmoja wa askari wa Kituruki akiwa kataika uwajna wa mapambano.
Na chini pi picha ya inaonyesha baadhi ya wanajeshi waliiopoteaz maisha kwa kupigania nchi yao wakirejeshwa nyumbani.
Angola yaongoza kwa vifo vya watoto wadogo katika nchi za duina ya tatu.
Luanda, Angola - Nchi ya Angola imekuwa moja ya nchi ambayo inaongoza kwa vifo vya watoto wadogo kulinganisha na nchi nyingine zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.
Maelezo haya yaliotolewa na shirika moja la kutoa misaada nchini Uingereza.
Angola ambayo inautajiri wa asili kama mafuta na almasi, lakini wananchi walio wengi wanaishi maisha ya hali ya chini kulinganiasha na uchumi uliopo, ilimalizia ripoti hii ya shirika hili.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Angola akiutubia Umoja wa mataifa siku za karibuni alipo hudhulia mkutano wa viongozi wa umoja huo.
Picha ya katikati wanaonekana watoto wa kiangola ambao wanakabiriwa na magonjwa yanayo weza kutibiwa au kuzuiwa ya siwadhulu ikiwa watapewa kinga.
Chini anaonekana mtoto akipewa dawa ya kinga na mmoja ya wahudumu wa dhahanati nchini Angola.
Serikali ya Eritrea ya iwekea ngumu UN kusambaza misaada kiuraisi
UN - Umoja wa mataifa umeilaumu serikali ya Eritrea, kwa kitendo chake cha kuzuia misada kuingizwa nchini Ethiopia kwa kupitia nchini Eritrea.]
Akiongea hay msemaji mmoja wa UN bi Marie Okebe, alisema ya kuwa imekuwa ni vugumu kuingia nchini Ethiopia, kwani serikali ya Eritrea imakuwa ikiwapa wakati mgumu,na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa mataifa kutishiwa nanguvu za dola na mitutu.
Hata hivyo uhusiano kati ya serikali ya Ethiopia na Eritrea umekuwa wa mashaka kwa kipindi kilefu sasa, hivyo ni vigumu hali kuwa nyepesi , alisema msemaji mmoja wa serikali ya Eritrea.
Pichani anaonekana rais Isaias Afewerki wa Eritrea, akiongea na wahandidhi wa habari siku za karibuni.
Picha chini wanaonekana askari wa Eritrea wakifungua kizuizi tayari kulikagua gari UN lililo beba misaada.
Amani kupatikana nchini Uganda?Mkataba wa Amani utafikiwa tu msemaji wa serikali.
Kampala, Uganda - Serikali ya Uganda na kikoso cha jeshi la upinzani kinacho ongozwa na bwana Joseph Kony,wametiliana sahii ya makubaliano kusimamisha mapigano na kuelekea njia ya kuleta amani nchini Uganda.
Vita hivi kati ya serikali na wapinzani wanaoongozwa na bwana Joseph Kony , vimechukua karibu ya robo karne, vimekuwa vikileta maafa makubwa kwa wananchi wa kaskazini mwa Uganda.
Hata hivyo mmoja wa wasemaji wa serikali alisema ya kuwa mkataba huu ni njia na ishara nzuri ya kuwa amani itapatikana tu.
Picha hapo juu anaoneka rais Yoweri Mseveni , akiwa amepumzika baada ya kazi ngumu za kiofisi.
Picha ya katikati anaonekana rais Yoweri Kaguta Museveni, akihutubia wapiganaji wake enzi hizo alipo kuwa bado yumo ndani ya magwanda ya kijeshi.
Chini ni picha ya bwana Joseph Kony akiongea na waandishi wa habari hapo siku za nyuma.
Amerika na washiriki wake watakiwa watuombe radhi,serikali ya Irani yaagiza.
Teheran, Iran - Rais wa Iran bwana Mahmoud Ahamadinejad, ameitaka serikali ya Amerika na washiriki wake, kuomba msamahaa kwa wananchi wa Iran, kwa kuishutumu serikali ya Iran yakuwa inampango wa kutengeneza mabomu ya nuklia.
Rais Mahmoud Ahamadinejad, aliyasema haya sikuya jumamos ,baada ya ripoti ya shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia (IAEA) kueleza ya kuwa Iran,imekuwa ikionyesha ni jinsi gani nchi hii inavyo fatilia umakini wa kutengeneza umeme unaotokana na nguvu za nyuklia na siyo kutengeneza siraha za nuklia.
Hata hivyo Amerika na washiriki wake bado, wanasisitiza ya kuwa serikali ya Iran lazima iwekewe vikwazo na mbinyo ili kuacha kuendelea na mpango wake wa kuendeleza nguvu za kinuklia.
Picha hapo juu ni rais wa Iran bwana Mahmoud Amadinejad, akiongea hivi karibuni kusissitizia msimamo wa serikali ya Iran kuhusu uhalari wake.
Picha ya katikati anaonekana rais Mahmoud Ahamadinejad,wakati waenzi zile za kuongoza mapinduzi ya Iran, anavyo onekana kwa sasa.
Chini ni sehemu ya mitambo ya kutengeneza nguvu za nuklia,na anaonekana mmoja ya wafanya kazi wa idara fulani akiwa anaangalia kwa makini jinsi gani uzalishaji unavyo kwenda.

2 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

See HERE