Sunday, April 13, 2008

Kenya yaweka rekodi ya dunia kwenye karne ya 21, kwa kuwa na baraza kubwa la mawaziri.

Je wapenzi wa Nou Camp kukusa uhondo wa Kibrazil na kuhamia Itali?

Milan , Itali -Aliyekuwa mchezaji bora wa dunia Ronadinho kwa upande wa soka, (kabumbu) ambayeni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na Barcelona, amekubali kimsingi kuamia timu ya AC Milan ya Itali, kwa mujibu wa wakala wake, ambaye ni kaka ya mchezaji huyu bwana Robert de Assis.
Ronadinho mwenye miaka 28, amekuwa na wakati mgumu kwenye uwanja wa Nou Camp, kutokana ma maumivu ya liyo mkumba kwa kipindi kisicho pungua miezi michache iliyopita.
Picha hapo juu anaonekana Ronadinho akiwa unjanjani anafanya vitu vyake.
Ron akama anavyo julikana kwa mavitu ya kuchezea mpira kama kwa wake wanao jua kula samaki mwenye miiba mingi mdomoni , anaonekana akiwa ndani ya jezi ya Basca.
Picha nyingine wanaonekana manyota wa soka wa dunia Zinedin Zidane kushoto na Ronadinho kulia wakigombania gombe la gozo wakati timu hizo zilipo kutana.
Kenya yaweka rekodi ya dunia kwenye karne ya 21,kwa kuwa na baraza kubwa la mawaziri.
Nairobi, Kenya - Mgogoro wa kisiasa nchini Kenya, umefikia tamati baada ya rais Mwai Kibaki kutangaza baraza jipya la mawaziri wapatao 40.
Kiongozi wa chama pinzani bwana Raila Odinga, amechukua nafasi ya waziri mkuu, wizara ambayo imeanzishwa ili kugawana madaraka.
Baraza hili litajumuisha vyama vya upinzani , hata hivyo baraza hili limepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi wa Kenya.
Pichani hapo juu wanaonekana waziri mkuu mpya , Raila Odinga na rais Mwai Kibaki wakipongezana baada ya kutangaza baraza la mawaziri.
Picha nyingine anaonekana rais Mwai Kibaki akitangaza baraza la mawaziri mbele ya waandishi wa habari.
Waziri wa zamani wa Itali kurudi madarakani?
Rome, Itali - Wananchi wa Itali wameanza na kupiga kura kuwachagua kuchagua wabunge wa bunge la Itali.
Uchaguzi huu unafanyika wakati viongozi wa wanao tazamiwa kuchuana vikali ni aliye kuwa waziri mkuu wa zamani wa Itali bwana Silvio Berlusconi na Veltroni.
Hata hivyo wachunguzi wa maswala ya kisiasa wanasema huenda bwana Berlusconi akarudi madarakani ikiwa chama chake kitaongoza.
Pichani anaonekana Veltroni akihutubia wakati wakampeni za uchaguzi.
Picha nyingine anaonekana waziri mkuu wa zamani wa Itali akiwa anongea na waandishi wa habari hivi karibuni.
Serikali ya Libya yatoa msamahaa kwa wapinzani walio taka kumtoa Muhamar Gaddaf miaka ya 1995.
Tripol, Libya - Serikali ya Libya imewaachia zaidi ya watu wapatao 90, ambao wengi wao ni wanachama wa Islamic Group, chama ambacho kinapingana na serikali inayo ongozwa na rais Muhamar Gaddaf.
Kuachiwa huko kumesaidiwa na chama kisicho cha kiserikali kinacho ongozwa kaka wa rais wa Libya.
Chama hiki ambacho kiliibuka mwaka 1995, kikiwa na madhumini ya kumtoa madarakani rais wa Libya Muhamar Gaddafi.
Pichani wanaonekana baadhi ya wafungwa ambao wame achiwa hivi karibuni.
Wanachi wa Rwanda wakumbuka siku ya mauaji ya vita vya wenyewe vya kikabila vilivyo tokea 1994.
Kigali, Rwanda - Wananchi wa Rwanda wameadhimisha hivi karibuni, kukumbuka vifo vya watu wapatao milion moja ambao walipoteza maisha yao wakati wa vita vya kikabila vilivyo zuka nchini Rwanda 1994.
Vita hivyo vya kikabila kati ya watu jamiii ya kihutu na kitutsi, wakati vita hivyo idadi kubwa ya waru jamii ya kitutsi kuuwa kinyama kwa kukwatwa na mapanga na siraha nyingine za jadi.
Vita hivi ambavyo vilichukua miezi mitatu na siku kadhaa, na vilikwisha baada ya kikosi cha jeshi la upinzani ( RPF ) Rwandise Patriotic Front kikiongozwa na rais wa sasa bwana Poul Kagame, kushinda na kukiondoa madaraka chama na MRND, kilicho kuwa kikiongozwa na hayati rais , Juvenail Habyalimana.
Pichani wanaonekana baadhi ya watuhumiwa waliohusika na mauaji vita wakiwa wamevalia magwanda ya serikali na kujenga nchi kwa kufanya kazi ya kilimo.
Picha nyingine hapo chini, anaonekana mmoja wa watuhumiwa akiwa anasikiliza makosa kwenye koti ya ijulikanayo kama Gachacha.
Picha nyingine, hapo nchini ni picha linaonekana moja ya fuvu la watu waliopoteza maisha yao wakati wa vita vya wenyewe vya kikabila nchini Rwanda.
Janga la njaa, laleta msuko suko na kiongozi wa nchi apigwa chini na bunge.
Port Au Prince, Haiti - Bunge la nchi ya Haiti limepiga kura na kukubaliana kwa pamoja ya kuwa waziri mkuu bwana Jacque Edouard Alexis kuondolewa madarakani.
Hii ina kuja baada ya kuzuka kwa huaba wa lishe au chakula na kuongezeka kwa huaba wa kazi.
Kufuatia hali hii ya kiuchumi kuwa mbaya, ilisababisha raia wa Haiti kuandamana na kupambana na wanajeshi wa wa jeshi la kumoja wa mataifa.
Pichani hapo wanaoneka wanainchi wa Haiti, wakiwa wamekaa chini kwa shahuku kubwa kwa kutaka kujua nini jeshi hili litafanya kuwapatia lishe na Kazi.
Lakini wanajeshi wa umoja wa Mataifa wapo nchi Haiti kwa ajili ya kulinda usalama.
Hali ya utata kuzuka na kuwacha watu kuwa na butwaa baada ya bomu kulipuka msikitini.
Teheran, Iran - Kusini mwa Iran kwenye mji ujulikanao Shiraz, kumetokea mlipuko wa bomu ndani ya msikiti na kusababisha vifo vya watu 11.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, alisema ya kuwa, mlipuko huo umetokana na bomu la kutengenezwa kihuria au mabomu ya kutengenezwa nyumbani.
Hata hivyo kunahabari ya kuwa huenda vifo vya watu vikaongezeka.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa wameshikwa na mshangaokuhusu tukio hili kutokea ndani ya msikiti.
Picha chini, linaonekana gari la kubeba wagonjwa likitoka kwenya sehemu ya tukio hili.
Wanaume watakiwa kufanyiwa kujitokeza zaidi kwa kuwa tayari kutairiwa.
Nairobi, Kenya - Katika kupambana na ugonjwa hatari wa ukimwi nchini Kenya, serikali ya nchi hiyo imeandaa mikakati ya kujaribu kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi kwa kutoa mafunzo ya kitaaluma kwa watumishi wake wate wanaohusika na kujua ni jinsi gani ya kutairi na kujaribu kuwaelimisha wananchi njia bora ya kujikinga na ugonjwa huu.
Picha hapo juu anaonekana baadhi ya wananchi wa Kenya wakiwa wamashikiria mabango kuhimiza serikali yao kuwapatia dawa wagonjwa walio athirika na ugonjwa wa ukimwi.
imepitishwa kisheria kutairiwa kwa wanaume, ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na ugonjwa.

1 comment:

Anonymous said...

Hello. This post is likeable, and your blog is very interesting, congratulations :-). I will add in my blogroll =). If possible gives a last there on my blog, it is about the Notebook, I hope you enjoy. The address is http://notebooks-brasil.blogspot.com. A hug.