Thursday, January 31, 2013

Izrael yaishambulia Syria.

Harakati za uchaguzi zaanza rasmi nchini Kenya.

Nairobi, Kenya - 31/01/2013. Viongozi wa siasa nchini Kenya wameanza kampeni za uchaguzi kupitia vyama vyao tayari kujiandaa kwa uchaguzi mkuu utakao fanyika Machi 4/ 2013.
Harakati kubwa za uchaguzi zitakuwa ni katika kinyang'anyiro cha kiti cha urais ambapo kamati ya uchaguzi imeyapitisha majina ya  waziri mkuu Raila Odinga na Uhuru Kenyatta  kuwa baadhi ya wagombea wa kiti cha urais.
Uchaguzi wa viongozi hao umekuja baada ya rais wa sasa Mwai Kibaki kumaliza muda wake kama rais wa Kenya.
Odinga amemchagua makamu wa rais Kalonzo Musyoka kuwa makamu wake na Uhuru Kenyatta amemchagua waziri wa elimu William Ruto kuwa makamu wake.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Raila Odinga na Uhuru Kenyatta walisema " tunatumaini uchaguzi utakuwa wa haki na yale yaliyo tokea 2007/2008 hayatatokea tena."

Izrael yaishambulia Syria.

Damascus, Syria - 31/01/2013. Serikali ya Syria imetishia kuchukua hatua kali dhizi ya Izrael.
Tishio hilo la serikali ya Syria limekuja baada ya ndege za kijeshi za Izrael kufanya mashambulizi ndani ya Syria.
Kwa mujibu wa serikali ya Syria, ndege nne za kijeshi za Izrael zimefanya mashambulizi karibu na jiji la Damascus na kuua watu wawili na watano kujeruhiwa.
Kufuatia mashambulizi hayo, jumuiya ya nchi za kiarabu limelaani kitendo hicho kwa kusema ni kinyume  na sheria za kimataifa na kuizaraurisha jumuiya hiyo.
Hata hivyo habari kutoka Washington zimethibitisha yakuwa ndege za Izrael zimeshambulia msafara wa kijeshi nchini Syria.
Nayo Iran imeunga mkono serikali ya Syria kwa kudai ya kuwa ipo bega kwa bega na serikali ya Syria na  ipo tayari kutoa msaada wa kila hali kwa Syria.
Hata hivyo serikali ya Izrael haijathibitisha mashambulizi hayo.

No comments: