Sunday, December 30, 2007

Kijana wa miaka 19 apewa kazi ya kufuata nyayo za mama Bhutto.

Alex Ferguson awapiga faini wachezaji wake kwa kukuso maadili mema kwa jamii.

Manchester, Uingereza - Kocha mkuu wa timu ya Man United, bwana Alex Ferguson, amepiga marufuku shereha zote hasa wakati wa Kri-Max, zinazo husisha klabu na wachezaji bila viongozi kuwepo.
Akiongea na wachezaji wake , kocha Alex Ferguson, alionya na kusema hatavumilia tena kitendo hicho na anawapiga faini wachezaji wote walio kuwepo kwenye sherehe hiyo.
Onyo hilo limekuja baada ya kujulina yakuwa wachezaji hawa walikwenda kwenye sherehe hiyo bila wake zao, wala marafiki zao wa kike,bali waliandaliwa wadada wapatao 100, kuwapoza na kuwastaresha.
Katika sherehe hizo, wachezaji walilewa na kufanya vitu vya ajabu, na mmmoja ya wachezaji wa timu hiyo, anachutumiwa kwa kumjamii mwanadada wakati wamelewa.
Pichani anaonekana kocha Alex Ferguson akiongea na vijana wake,na picha nyingine wanaonekana baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo walio sadikiwa kuwepo kwenye sherhe hiyo.
Mwamuzi wa zamani wa soka (The Sheriff) Upara apewa ulinzi .
Rome, Itali - Mwamuzi wa zamani na maarufu duniani katika mchezo wa soka, au mpira wa miguu, bwana Pierluigi Collina ameongezewa ulinzi na polisi baada ya kupata tishio.
Hali ya vitisho imekuwa ikizidi, na zimekuwa zikiongezeka kwa kupita mtandao wake.
Bwana Collina, ambaye amechaguliwa kuwa msimamizi wa wamuzi wa soka nchini Itali, ndiye anaye husika na upangaji wa wamuzi wa mechi zote za ligi daraja la kwanza na lapili nchini Itali.
Mwamuzi huyu wa zamani wa soka, au gozi la ng'ombe, bwana Collina au The Sheriff) mwenye upara, alikuwa maarufu kwa kujua kazi yake ya uamuzi wa soka, naalikuwa anaheshimika na wachezaji wote wa soka duniani.
Picha ya kwanza, anaonekana bwana Collina, akiwa amevalia mavazi ya kawaida baada ya kuacha kazi ya urefa miaka ya karibuni.
Picha ya pili anaonekana Pierluigi Collina, pamoja na wachezaji maarufu duniani walipo kuwa wakicheza mechi kwa ajili ya michango wa umoja wa Mataifa kusaidia Maendeleo.UNDP - Unated Nations Development Programme.
Picha ya tatu, anaonekana the Sharrif, Collina akimpa onyo mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Klose, baada ya kufanya manyago uwanjani.
Mchezaji anapo kosa maadili ya mchezo wa soka, basi kwa the Sheriff ( Upara) Collina alikuwa hana simile hata kiduchu, kadi nyekundu hukuonyesha, Fabian Barthez ahamini macho yake.
Naikiwa mchezaji hujisahahu, basi The Upara ( Sheriff) humkumbusha kwa kumuelekeza ya kuwa hii ni soka, na lazima ufate maadili yake.Hivyo anaonekana akimkumbusha mchezaji wa Argentina Gabriel Batistuta ya kuwa nakuona mwenendo wako uwanjani hivyo kaa chonjo.
Wapenzi wa sadamu wasema watamkumbuka daima kiongozi wao, yupo miyooni mwao daima"Ni mwaka sasa watimia"
Awja, Iraq - Mamia wa wapenzi na wanchi walio kuwa wakimenda Saddam Hussein kama kiongozi wa nchini Iraq, walifanya maombelezi ya kumkumbuka kiongozi wao ambaye alinyongwa kwa kutumia kitanzi, 30/12/2006.Baada ya kukutwa na kosa la kukiuka haki za kibinadamu.
Maombelezi hayo yaliongozwa na viongozi wa jamii ya Kisuni pamoja na viongozi wa makabila,yaliuzuliwa na wanafunzi na watu wengine alipozikwa hayati Saddam Hussseni kwenye mjiwa Awja. Huku wakiombelza kwa kusoma Koran, mmoja wa ndugu wa familia ya hayati rais Saddam Hussein, bwana Ghalib Hammud,alisema yakuwa kiongozi hwao wapo pamoja naye kiroho na watamkumbuka kila mwaka.
Picha ya kwanza anaonekana kijana akiombeleza mbele ya picha na kaburi la rais Saddam Hussein.
Pichani anonekana enzi zake rais wa Iraq, Saddam Hussein akihutubia wananchi wa Iraq.
Picha ya pili wanaoneka mabwana wawili walimvisha kitanzi, Saddam Hussein, tayari kuaga dunia.
Picha ya tatu wanaonekana wanfunzi wa shule ya msingi wakiombeleza mbele ya kabuei la hayati rais Saddam Hussein.
Picha ya mwisho anaonekana rais Saddam Hussein, akisikiliza hukumu yake toka kwa jaji.
Dunia nzima yalia na mama asilia, Tsunami bado kuwa tukio la kutisha.
Java, Indonesia - Tukio kubwa ambalo walimwengu mzima ulisikitika na kushangaazwa kwa unyonge paka leo hii na jibu lake bado ni kitendawili kwa wana sayansi,dini na wahenga ni lile tikio la watu zaidi ya nusu million kupoteza maisha kwa kipindi kifupi, kwa ajili ya mgivu za mama asilia amabye alipewa jina la Tsunami.
Hivi karibuni wakazi wa maeneo ambayao yalikumwa na tsunami ya 26/12/2004 na duniani kote, na kuleta maafa makubwa kwa binadamu na mazimgira yake yaliadhimishwa.
Tukio hili la tsunami, lilikumba karibu kila jamii hapa duniani, hapo pichani juu wanaonekana wanachi wakitafuta sehemu ya kujificha kuepuka madhara ya maji yanayo kuja kutoka baharini.
Picha ya pili chini ni siku chache baada ya tsunami kuleta madhara, na picha nyingine wanaonekana wakina mama wakilia kwa uchungu baada ya kuona madhara ya tsunami.Pcha ya chini wanoneka baadhi ya watu waliokuwepo kwenye ufukwe wa bahari,hawamini wanacho kiona kwani ilikuwa ghafla bahari imepandisha maji kwanguvi hadi kwenye nyumba zao.
Kijana wa miaka 19, apewa kazi ya kufuata nyayo za mama Bhotto.
Rawalpindi, Pakistani - Chama cha - PPP ( Pakistani Peoples Party) kilicho kuwa kikiongozwa na marahemu bi Benazir Bhutto, kimefanya uteuzi wake mpya wa uongozi.
Katika mkutano huo ambao ulikuwa namadhumuni kumchagua kiongozi wa chama hiki (PPP) na kuangalia ni jinsi gani watashiriki katika uchaguzi
Kwa pamoja uongizi wa chama cha PPP, umepitisha bila kipingamizi ya kuwa mtoto wa marehemu bi, Bhutto kuwa kiongozi wa chama cha Pakistani People Party na kukubali kushiriki katika uchaguzi ujao, na kuomba vyama vyote vya upinzani kushiriki katika uchaguzi huo.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, bwana wa bi Bhutto, bwana Zardari, alisema ya kuwa mtoto wao wa kiume, bwana Bilawal Bhutto Zardari,ndiye atakeye kuwa kiongozi wa chama hicho.
Bilawal Bhutto,mwenye miaka 19, ambaye bado nimwanafunzi wa chuo cha Oxford nchini Uingereza,amesema yakuwa kwa sasa,baba yake ndiye atakaye kuwa akiongoza chama hiki katika shughulizake za kila siku, mpaka hapo atakapo kuwa tayari kukiongoza chama hicho. Bilawal alizaliwa mwezi mmoja kabla ya marehemu mama yake kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa Pakistani mwaka 1988, alipewa jina hili lenye maana ya kuwa hakuna wa kulingana naye.
Pichani anaoneka , mume wa marehemu bi, Bhuotto ,bwana Asif Ali Zardari, akiongea na waandishi wa habari,na picha nyingine anaonekana bwana Bilawal ambaye ndiye kiongozi mkuu wa chama cha PPP.
Balozi wa Tanzania ajeruhiwa vibaya na majambazi na kuporwa vitu.
Pretoria, Afrika ya Kusini - Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, bwana Emannuel Mwambulukutu, amjeruhiwa vibaya na majambazi waliovamia ubalozi wakati wa sherehe za kumuaga balozi huyo na familia yake.
Tukio hilo lilitokea mida ya saa mbili usiku wa tarehe 29, na hali ya balozi Mwambulukutu,inasemekana ya kuwa bado siyo nzuri.
Hata hivyo polisi wamesema ya kuwa wamemkamata mtu mmoja ambaye anashukiwa mmoja ya watu walio kuja kuvamia na kuleta maafa makubwa kwenye ofisi za ubalozi.
Pichani anaonekana balozi Mwambulukutu, akiwa kazini.
Uchaguzi wa Kenya, matokeo yaleta utata, Mwai Kibaki awa rais tena wa Kenya.
Nairobi, Kenya - Matokeo ya uchaguzi nchini Kenya, hatimayake yamepatikana, rais Mwai Kibaki, apita tena kuwa rais wa Kenya kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Rais Kibaki inasemekana amemshinda mpinzani wake mkuu bwana Raila Odinga kwa kiasi kidogo cha kura zote zilizopigwa.
Matokeo haya ya uchaguzi yalimpa bwana Kibaki kura zipatazo 4,584,721 zidi ya bwana Odinga.
Bwana Mwai Kibaki, aliapishwa kuwa rais wa Kenya, mara tu ya kutangazwa mshindi, nainadadikika ni kati ya dakika sitini baada ya matokeo, bwana Kibaki akikabidhiwa ofisi kama rais wa Kenya.
Hadi kufikia leo jiono hali ilikuwa ya hatari, na vyombo vya habari vyote vimefungwa na hakuna matangazo ya yaina yoyote ya luninga, hii ni kwa ajili ya manufaa kwa taifa msemaji mmoja wa serikali alisema.
Pichani, anaonekana bwana Mwai Kibaki, akipokea biblia,tayari kula kiapo kama rais wa Kenya.
Chini ni picha ya bwana Raila Odinga, akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya uchaguzi nchini Kenya, nakudai kuwa bwana Mwai Kibaki na chama chake wameiba kura, na kutaka kura ziridiwe kuhesabiwa.
Chini anaonekana rais, Mwai Kibaki akiongea baada ya kuapishwa kuwa rais.

No comments: