Monday, February 11, 2008

Rais avamiwa Ikulu, waasi wa Mashariki wa Timor wataka kuleta machafuko.

Kosa la kaptain wetu, humtokea kila mchezaji, kwani mpira unazunguka"Wachezaji wa Kamerooni"

Younde, Kameroon - Wachezaji watimu ya taifa ya Kameroon, wamesema yakuwa kushindwa kwao kubeba kombe la maifa ya Afrika nchini Ghana, sikwasababu ya kosa la kaptain wao Rigobert Song,bali haikuwa siku yao ya kushinda kombe hilo.
Wakiongea kwa wakati tofauti, wachezaji wa timu ya taifa ya Kameroon, walisema kosa ambalo amefanya Song , humtokea mchezaji yoyote, na kwa wale wanao jua au wamesha wahi kucheza mpira wanajua yakuwa mpira huwa wakati mwingine unafanya mchezaji asifanye alivyo tarajiwa na mpira unazunguka, hivyo ulimzunguka kaptaini wao mara moja na hapo mchezaji wa Misri timu ya taifa ya Misri Zidan, akaupata mpira na kumpasia Boutrika aliyefunga goli lililo wapa ushindi Wamisri.
Hivyo sisi wachezaji wote tupo pamoja nae, bado tutazidi kuichezea Kamerooon mpaka hapo miguu ikikataa, aliongea haya Geremi Ndjitap, huku akipewa sapoti na Samuel Eto'o.Kwani tuna kombe la Afrika nchini Angola ,na badye kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini, hivyo kwa sasa tutaanza panga mikakati ya kuweza kucheza vizuri ili tuweze kushindana kwenye mashindano haya ya 2010 nchini Angola na Afrika ya kusini.
Picha hapo juu anaonekana kaptain wa timu ya taifa ya Kamerooni Rigobert Song, akiwa ndani ya jezi ya timu yake ya taifa ya Kameroon, na huku mguu wake wa kushoto ukiwa umefungwa bandaji,hivyo maumivu ya mwili wake yapo ndani ya mapenzi ya nchi yake.
Picha ya pili anaonekana Rigobert Song, akiwa kazini kutetea nchi yake siku ya mwisho ya mishindano ya kombe la Afrika,wakati Kamerooni ilipo cheza na Misri na kufungwa goli moja kwa nungu.
Picha ya chini ni picha ambayo wapenzi wasoka wa Kamerooni hawataisahau, kwani anaonekana kaptain wa timu ya taifa ya Kamerooni Rigobert Song,akigombea mpira na Mohammed Zidan, baada ya mpira kumzunguka Song, na hatimayake Zidan, aliupata mpira na kutoa pasi mwanana kwa Boutrika aliye wanyima ushindi wa kombe la Afrika Wakamerooni kwa kufunga bao la pekee.
Eddy Murphy King of Zamunda, aowa nakuacha kwa kipindi kifupi.
Los Angeles, USA - Mcheza sinema na mwana vitimbwi, Eddy Murphy, ameachana na mkewe ,bi Tracey Edmond, baada ya kufunga ndoa kwa kipindi cha wiki mbili.
Eddy Murphy mwenye umri wa miaka 46 na bi Tracey Edmond mwenye miaka 40, walifunga ndoa kwenye kisiwa cha Bora Bora.
Eddy Murphy mwenye watoto sita, kutoka kwa ndoa ya zamani, amecheza sinema nyingi, na moja ya sinema ambazo zimempa umaharufu ni ile ijulikanayo Coming to America.
Picha juu anaonekana bwana Eddy Murphy akiwa kazini kataika harakati za kucheza sinema, amabzo huwa kivutio kwa wapenzi wa sinema.
Picha ya pili anaonekana bwana Eddy Murphy, akiwa amekula kodo,mbela ya wapenzi wake baaday ya kumaliza kufanya mavitu yakeya sinema.
Picha ya mwisho anaonekana Eddy Murphy, akiwa na aliyekuwa mkewe, bi Tracey Edmond siku zakaribuni kabla ya kufunga ndoa yao iliyodumu wiki mbili tu.
Misri yawa bingwa wa kombe la Afrika,Kamerooni yakosa kombe kwa kosa la beki.
Accra, Ghana - Timu ya taifa ya Misri imeibuka na ubingwa kwa mara ya sita, baada ya kuzaba bao moja kwa nunge timu ya taifa ya Kamerooni.
Bao hilo la ushindi lilifunngwa na mshambuliaji hatari Mohammed Aboutrika, baada ya kupata pasi kutoka kwa Zidan, ambaye aliweza kufaidika kutokana na makosa ya beki mzoefu wa Kamerooni rigobert Song.
Ushindi huu wa the FARAOS, unakuja kwa kujumisha wachezaji wanao cheza ligi ya Misri,na wachezaji wawili wanao cheza nje ya ligi ya Misri ndiyo walioitwa kujiunga na timu hiyo ya taifa.Hii ni mara ya pili kwa the Farao, kuwafunga Simba wa Kamerooni, kwani katika mzunguko wa kwanza wakati wakigombania kuingia awamu ya pili Misri iliifunga Kamerooni goli 4-2.
Pichani anaonekana timu kamptain wa Misri, Ahamed Hassan akinyanyua kombe la ubingwa la mataifa ya Afrika. Misri imeshinda kome hili kwa mara ya sita.
Picha ya chini anaonekana Mohammed Zidan, akishangilia huku amebebwa na mchezaji mwenzake baaday ya kumzidi maarifa beki wa Kamerooni, Rigobert Song na kumpasia Mohammed Aboutrika, ambaye bila makosa alifanya vitu vyake kwa kuona nyavu za mlinda mlango wa Kamerooni Idriss Kameni, nakuwa bao la ushindi.
Chini ni picha ya wachezaji wa Misri wakishangilia baada ya kukabidhiwa Kombe lao.
Mgombea mwenza wa ZANU-PF afutwa uanachama"Huyu ni kibaraka ZANU -PF ya dai"
Harare, Zimbabwe - Chama tawala cha ZANU - PF, kimemfukuza uanachama bwana, Simba Makoni, baada ya kuamua kugombania kiti cha urais kama mgombea wa kujitegemea.
Bwana Makoni. alitangaza hivi karibuni ya kuwa atagombania kiti cha urais wakati wa uchaguzi wa rais mapema mwishoni mwa mwezi wa tatu, na bwana Makoni alishwa wahi kuwa waziri wa faranga wa Zimbabwe, lakini alitolewa kwenye wizara hiyo .
Akiongea na waandishi wa habari,makamu wa chama tawala ZANU-PF, bwana, Joseph Chinotimba, aliseama ya kuwa bwana Makoni,amekuwa kibaraka wa serikali za magharibi, Amerika na Uingereza, nakuwa hataweza kuigawa ZANU-PF,hivyo atashindwa na kuumbuka, baada ya uchaguzi, hivyo nasikitika sana, kwani alikuwa mmoja wa wapiganaji wenzetu wakati wa kumpiga mkoloni, lakini sasa kawa kibaraka wao.
Pichani anaonekana bwana Simba Makoni,enzi zake akiwa kama waziri wa faranga wa Zimbabwe akielekea bungeni kutoa miswada.
Hapo chini ni picha ya bwana Simba Makoni,akiongea na waandishi wa habari baada ya kutangaza kugombea urais kama mgombea wa kujitegemea.
Mahaka ya Hague yapata mshitakiwa mwingine,ashutumiwa na mauaji ya Ituri.
Hague, Holland - Aliyekuwa kiongozi wa jeshi la waasi lijulikanalo kama(DRC)Democratic Republican of Congo bwana Mathieu Ngdjolo amekamatwa na mjini Kinshasa na kuletwa nchini Holland, kujibu mashitaka ya mauaji ya mamia ya watu.Alisema wakili mmoja wa mahakama ya mjini Hague, ICC (International Criminal Court), bwana Luis Moreno Ocampo.
Bwana, Mathieu Ngdjolo anashitakiwa kwa kutoa amri ya kutekateza zaidi ya wana vijiji wapatao 200 mwaka 2003 wakatia aliipo kuwa mkuu wa usalama wa taifa.
Tuhuma hizo ambazo zinamkabili ni mauaji yaliyo tokea maeneo ya Ituri na kijiji cha Bogoro.
Kutokana na watetezi wa haki zabinadamu na kuhudumia watu waliopata matatizo, wanadai zaidi ya watu wapatao 600,000 wamakimbia makazi yao tangu machafuko ya Ituri yaanze mapema kwenye mwaka ya 1999. Pichani kulia ni picha ya bwana Mathieu Ngdjolo,alipo kuwa kazini enzi zake kama afisa usalama wa taifa, miaka ya 2003.
Waasi wadai wageni wasaidia serikali, wasiwasi waongezeka "roho zipo nyengema"
Ndjamena, Chad - Wakimbizi amabo walikimbilia nchni Kameroni, wakati wa majaribu ya kiipindua serikali ya rais Idriss Deby, wamaeanza kurudishwa nyumbani kwao.
Hii ionakuja baada ya wapinzani wa serikali kushindwa kumuondoa madarakani rais Idriss Deby.
Kutokana wa msemaji mmoja wa kuhudunia watu waliokumbwa na maafa, alisema yakuwa, hali bado ya mashaka mjini Ndjamena, ijapokuwa watu wamekuwa wakiambiwa ya kuwa waasi hawatarudi tena kushambulia jiji la Ndjamena.
Japokuwa kunahabari ya kuwa waasi hawa wanajijenga tayari kwa mashambulizi mengine, na wamedai yakuwa wanashikiria miji ya n Momgo na Bitkine iliyopo katikati ya nchi ya Chad.
Hata hivyo waasi wa serikali wamezidi ilaumu serikali ya Ufaransa kwa kuisidia serikali ya rais Idriss Deby.
Pichani wanaonekana wanajeshi wa serikali wakila doria mjini Ndjamena, baada ya kuyarudisha majeshi ya waasi nyuma ya jiji na vitongoji vyake.
Chini wanaonekana wanajeshi wa Ufaransa wakiwa wanalinda maeneo muhimu ya kusaidi huduma za binadamu jijini Ndjamena.
Chni nim picha ya kina mama wakiwa wamekaa bila kujua ni nini kinafuata kataiaka kambi moja ya wakimbizi.
Mtuhumiwa wa septemba 11/2001, afunguliwa mashitaka, akabiliwa na kinyongo.
Washington,USA - Serikali ya Amerika imetangaza na kumfungulia mashitaka, aliye kuwa kiongozi wa ugaidi wa sempemba 11/2001 bwana Khalid Sheikh Mohammed.
Akiongea haya Brigedia,General Thomas Hartmann, alisema ya kuwa bwana, Khalid Sheikh Mohammed, anatuhumiwa kwa kuhusika kutumia ujuzi wa hali juu, kwa kusaidiana wa magaidi wengine wa Alqaeda walitumia ndege kashambulia ,kulipua na kuharibu majengo yajulikanayo kama World Trade Centle mjini New York na majengo mengini njini Washington, ambapo zidi ya
watu wapatao 3000 walipoteza maisha yao.
Hata hivyo inasadikiwa bwana Khalid Sheikh Mohammed, alikiri makosa baada ya kuteswa kwa kutumia mbinu ijulikanayo kama " Water Boarding" ambayo watetezi wa haki za binadamu wanasema ni kinyume na sheria za haki za binadamu na sheria za nchi.
Inaamini ka ikiwa bwana Khalid Sheikh Mohammed akikutwa na hatia, anaweza kuhukumiwa kifo Hapo juu ni njia tofauti au mojawapo ambayo watetezi wa haki za binadamu wanadai yakuwa ni kunyume cha haki zabinadamu kutumia njia hii kupata ushahidi au ukweli kutoka kwa mtuhumiwa. Picha ya chini ni picha ya Khalid Sheikh Mohammed, ambaye anashutumiwa kwa kuhusika na uigaidi na mauaji ya semptemba 2001
Rais avamiwa Ikulu ,Waasi wa Mashariki wa Timor wataka kuleta machafuko.
Dili, Mashariki ya Timor - Rais wa Mashariki ya Tomor, bwana Jose Ramos Horta, amenusurika kuuwawa na risasi, baada ya waasi wa Mashariki ya Tomor kuvamia nyumbani kwakwe siku ya jumatatu 11/02/08 na kumpiga risasi za tumbo.
Mapambano hayo yaliongozwa na mmoja wa wanajeshi waasi wa Mashariki ya Timor, bwana Afredo Reinado ambaye waliuwawa wakati wa kutupiana risasi na walinzi wa rais.
Rais Jose Ramos Horta, alikimbizwa hospitali ya jeshi iliyopo mjini Dili, nabaadaye kupelekwa Australia kwa matibabu zaidi.
Picha juu ni kiongozi wa waasi wa Mashariki ya Timor, bwana Afredo Reinado, ambaye aliyeongoza kujaribu kuleta mapinduzi ya kijeshi.
Picha ya pili anaonekana rais Jose Horta, akiwa katika hali mbaya kukimbiziwa hospitali kwa matibabu.
Hapo juu ni picha ya rais Jose Ramos Horta, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.

No comments: