Sunday, February 17, 2008

Hatimaye serikali yaomba msamaha

Dhahabu ya muziki wa pop,waadhimisha miaka 25 ya albumu iliyo vunja rekodi ya mauzo.

New York, Amerika - Kinara na nyota wa muziki wa pop na kuruka majoka, Michael Jackson ameadhimisha miaka 25 ya muziki uliotikisa dunia ujulikanao kama Thriller's.
Mwanamuziki huyu,ambaye albamu yake ya Thriller's ilimwingizia faranga(pesa) nyingi na kuvunja rekodi ya mauzo.
Akiongea na kuwashukuru wapenzi wake, kwakutumia mtandao, Michael Jackson, alisema ya kua ni vigumu kuamini ya kuwa tangu siku ile yeye pamoja na msanii na mtunzi bwana Quincy Jones walikaa na kutua albamu ijulikanayo kama Thriller's, na hivi sasa inatimiza miaka 25.
Albamu ya Thriller's, ilitolewa November 1982.
Michael Jackson, amehaidi ya kuwa wapenzi wasife moyo kwani hivi karibuni atatoa muziki, kwa kushirikiana na Kanye West, Akon. Fergie .
Pichani hapo juu anaonekana, Michael Jackson,akiwa amepozi mbele ya jalada la albamu ya Thriller's.
Picha ya pili zinaonekana picha za Michael Jackson, ya kwanza kushoto ni enzi zake baada ya kutoa albamu ya Thrillr's na picha ya upande wa kulia anaonekana Michael Jackson wa sasa.
Picha ya mwisho anaonekana mfalme wa muziki wa pop akiwatumbwiza washabiki wake, miaka ya hivi karibuni.
Baba wa taifa la Kuba, atangaza kujiuzulu uongozi"Ameongoza nchi nusu karne"
Havana, Kuba - Rais wa Kuba bwana Fidel Castro, ametangaza rasmi kuwa hatagombania tena urais wa Kuba, kutokana na afya yake.
Rais Castro ambaye ametawala Kuba kwa muda wa nusu karne, amesema yakuwa hataweza tena kuwa kiongozi wa Kuba kwa kuzingatia umri wake na afya yake kwa ujumla.
Rais Fidel Castro, ambaye amefanyiwa upasuaji wa tumbo, amekuwa hajishuhurishi na kazi za kiserikali tangu afanyiwe upasuaji huu, na alimwachia kiti mdogo wake bwana Raul Castro.
Rais Fidel Castro, ambaye amekoswa ku uwawa mara nyingi, na majasusi wa kila aina zaidi ya mara miasita, kutokana na maelezo ya habari za usalama wa taifa wa Kuba.
Picha hapo juu, wanaoneka Fidel Castro na Che Guevara wakati wa harakati wa kuikomboa Kuba kutoka kwenye utawala wa kizalimu na rushwa wa rais Batista.
Viongozi wa Kuba, ambao wametawala zaidi ya nusu karne, ambao ni ndugu,rais Fidel Castro na mdogo wake Raul Castro.
Hapo anaonekana rais Fidel Castro akihurubia mamia ya wa Kuba enzi hizo kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Picha ya mwisho anaonekana rais Fidel Castro, akishangilia kwa kutumia bendera ya Kuba.
Matunda ya uongozi bora, yaaanza kuonekana,Tanzania yapata kitita kutoka kwa US.
Dar es Salam, Tanzania - Serikali ya Amerika imeipatia serikali ya Tanzania kiasi cha 700 million dola, baada ya kumaliza kutiliana mkataba.
Pesa hizo ambazo zitapatikana katika kipindi cha miaka mitano ni moja ya jitihada za serikali ya Amerika, kusaidia bara la Afrika kupambana na umasikini, magonjwa na kuinua uchumi.
Pesa hizi zimetolewa kwa serikali ya Tanzania, wakati rais George Bush alipo tembelea Tanzania hivi karibuni wakati wa kutembelea baadhi ya mataifa ya Afrika.
Pichani hapo juu wanaonekana rais George Bush akipena mkono na rais wa Tanzania, bwana Jakaya Kikwete baada ya kumaliza kutiliana mkataba kati ya serikali hizi mbili.
Picha chini wanaonekana wakina mama, wakicheza ngoma huku wakiwa wamevalia kanga zenye picha ya rais George Bush.
Ndoto ya kumtumbwiza mwanahaki za binadamu ni za kila mtu.
Pretoria, Afrika ya Kusini - Kundi la musiki lijulikanalo kama Spice Girls, wamesema wangependelea kumtubwiza shujaa na mpigania haki za binadamu, mwanamapinduzi, na kiongozi aliyeongoza kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini, rais wa zamani wa Afrika ya Kusini bwana Nelson Mandela.
Pendekezo hilo lilitolewa na wanamuziki hawa yakuwa itakuwa kama ndoto kwao ya kuwa kutwimbiza siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa bwana Nelson Mandela, atakapo adhimisha miaka 90 ya kuzaliwa siku ya tarehe, 27/ june, mjini London kwenye uwanja wa Hyde Park.
Picha hapo juu anaonekana babu, Mandela akiwa amekula pozi baada ya kazi ngumu wakati wa urais wake.
Chini ni picha ya kundi Spice Girls ambao wanaota usiku na mchana kumtumbwiza baba, babu Nelson Mandela.
Tunaomba msamahaa, hatimayake serikali ya Australia yakubali ya kuwa ilifanya mabaya kwa wazawa.
Sidney,Australia - Serikali ya Australia imeomba msamahaa kwa mara ya kwanza kwa Wakazi wa Asili wa Bara la Australia.
Wakazi hao ambao wanajulikana kama Aboligini, waliobwa msamaha huu na waziri mkuu mpya wa Australia bwana Kevi Rudd.
Waziri mkuu,bwana Kevin Rudd, kwa kuonyesha masikitiko na hudhuni,kwa kitendo hicho, alisema tunaomba msamahaa na tunakili ya kuwa tulikosa.
Waaboligini hawa, waliombwa msamaha huu, baada ya serikali ya Australia kukubali na kuelewa baadhi maafa ambayo waliyaleta tangu wazungu wa kwanza walipo ingia katika bara hili la Australia.
Moja ya maafa yale yaliyo sababishwa na Australia, ni wakati serikali ya Australia, ilipo wateka nyara na kuwachukua kwa nguvu baadhi ya watoto wa jamii ya Akiabolijini na kuwa ingiza katika jamii ya Wazungu.
Kwa kitendo hicho cha serikali ya Australia, kutambua na kukubali maafa ambayo waliyatenda, kimepokelwa kwa furaha na wananchi wa jamii ya Aboligini kwa hisia tofauti.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Australia, bwana Kevin Rudd, alipo kuwa bungeni hivi karibuni kuomba msamahaa kwa wana nchi wa jamii ya Aboligini.
Picha ya kati anaonekana mmoja ya wananchi wa jamii ya abolijini, akitambika kukubali msamahaa kuktoka kwa serikali.
Chini ni picha ya baadhi ya wananchi wa jamii ya Aboligini, wakiwa wamefungwa minyororo kwenye shingo tayari kuelekea sehemu ambayo hawaijui kutumikia kifungo.
Urusi ya toa onyo"Siraha za kulinda Urusi zitaelekezwa nchi Ukraini.
Moscow, Urusi -Rais wa Vladamil Putin wa Urusi, amesemaya kuwa upo uwezekano wa nchi yake kuelekeza mitambo na siraha za nyuklia nchini Ukraini,ikiwa Ukraini itajiunga NATO, (Jumuia ya ushirikiano wa kiulinzi ,kijeshi na usalama wa Ulaya ya Mgharibi na Amerika).
Akiongea haya baada ya kumaliza kuongea na kutiliana mkataba wa kujenga mitambo ya mafuta na gas hivi karibuni, na rais wa Ukraini bwana, Yushchenko.
Akiongezea alisisitizia ya kuwa Urusi, Ukraini, Amerika na Ulaya Magharibi zinawajibika kwa ujumla kuangalia usalama na ulinzi.
Putin amabye anamaliza muda wake wa kumaliza wa kuwa rais wa Urusi mwezi wa Mei,amezilaumu NATO na Amerika kuwa zinaleta utata wa usalama na amani kwa upande wa Urusi.
Wakati huu rais Vladamil Putin, amealikwa kwenye mkutano wa jumuia ya NATO, utakao fanyika mwezi wa nne .Kwa mara ya mwisho rais Putin, aliuzuria mkutano huu mwaka 2002. Pichani anaonekana rais wa Ukraini bwana, Viktor Yushchenko na rais Putini walipo kutana hivi karibuni.

No comments: