Sunday, February 3, 2008

Rais wa Tanzania achaguliwa kuwa mwenyekiti wa AU - Afrikani Union.

Mashindano ya Magari ya Paris Dakar yasimamishwa'Manazi wa kigaidi wawakikwazo"

Paris, Ufaransa - Shirikisho la mbio za magari ya Paris kueleka Dakar Senegel, yamesimamishwa baadaya kutokea tishio la kutekwa na kutokuwa na huakika wa usalama wa washiriki wa mbio hizo.
Uamuzi huo umetolewa na serikali ya Ufaransa, baada ya watu wenye urai wa Ufaransa kuuwawa na watu wanaodaiwa kuwa wanazi wa ugadi na utekaji nyara, katika nchi ya Mauritania. Kwenye nchi ya Mauritania,mbio hizi huwa na vituo visivyo pungua vinane kati ya kumi natano.
Hata hivyo msemaji mmoja wa serikali amesema ya kuwa, hali ya usalama kwa washirki wa mbio hizo ilikuwa katika hali nzuri,na hivyo uamuzi wa kusimamisha mashindano hayo ni pigo kwa wana nchi wa Mauritania kiutalii na kibiashara kwa kuzingatia raia wengi huza vitu vyao kwa wingi wakatio wa mbio hizo.
Picha hapo juu ni picha za pikipiki gari ndogo na roli ambazo hushiriki kwenye mashindano haya, na kwa kiasi kikubwa hupitaia maeneo ya jangani.
Chad yawa kidonda kingine cha vita kwa nchi za Afrika.
Ndjamena, Chad - Wapiganaji wa jeshi la upinzani nchini Chad, wamesimamisha mapambano kwa muda ili kuwapa wananchi kutoka ndani ya jiji la ndjamena, kabla ya kuanza kushambulia jiji hilo upya.
Hatua hii imekuja baadaya mapambano makubwana na makali ambayo wapinzani waliweza kuingia hadi ikiru.
Wapinzani hawa wanapingana na rais wa Idriss Deby ambaye alichuwa madaraka ya urais 1990 .
Kufuatia tukio hilo, serikali ya Ufaransa inasaidia kuwapeleka nje ya nchi raia wote amabo si wa Chad wapatao 600.
Picha hapo juu ni gari iliyo lipuliwa kwa bomu jiji Ndjamena wakati wamapambano, kati ya majeshi ya serikali na wapinzani.
Chini ni picha ya raia wasio wa Chad wakikimbia mapambano, kwa kusaidiwa na wanajeshi wa Ufaransa.
Tetemeko la ardhi la sababisha maafa makubwa nchini zilizo zungukwa na maziwa makuu.
Kigali, Rwanda - Tetemeko kubwa la ardhi limelikumba maeneo ya maziwa makuu.
Maafafa ya tetemeko hilo yameleta mstuko mkubwa kwa wananchi wa Kongo DRC na Rwanda .
Tetemeko hilo, ambalo kimetokea nchini Rwanda na kuua zaidi ya watu wapatao 33 na mamia kujeruhiwa limekuja baada ya kusababisha maafa makubwa nchini Kongo DRC, ambapo tetemeko lilitokea mapema kabla ya tetemoko lililo tokea nchni Rwanda, hata hivyo msemaji wa serikali ya Rwanda Mary Gahonzire, amesema ya kuwa serikali inatoa kilamsaada ili kuwaokoa wananchi kutoka maeneo yaliyo kumbwa na maafa ya tetemeko hilo.
Tete meko hilo lilitokea muda wa saa saaba mchana na wakati nchini Kongo DRC, tetemeko lilitokea saa nne hasubuhi.
Pichani hapo juu ni maafa yaliyo sababishwa na tetemeko la ardhi nchini Kongo DRC.
Picha nyingine inaonyesha ramani ya maeneo yaliyo kumbwa na tetemeko la ardhi hivi karibuni.
Rais wa Tanzania, achaguliwa kuwa mwenyekiti wa AU- African Union.
Addis Ababa, Etheopia- Umoja wa Afrika (AU- Afrikani Union) umemchagua rais wa Tanzania bwana Jakaya M Kikwete kuwa mwenyekiti wa uongozi huo kuchukua nafasi iliyo achwa wazi na rais wa Ghana bwana John Kufuor.
Katika kikao chake cha 53, AU imekuwa na migongano ya kichwa jinsi gani wanaweza kutatua migogo ya kivita na kisiasa ambayo inazikumba nchi za Afrika tangu vugu vugu la mageuzi ya kisiasa kuingia Afrika.
Pichani anaonekana rais Jakaya Kikwete, akisoma baadhi ya mambo muhimu wakati alipo hudhulia mkutanao wa kujenga dunia kiuchumi nchini Uswisi hivi karibuni.
Picha ya chini aanaonekana rais Kikwete, akiongea na wakatia wa mkutano wa kujenga dunia kiuchumi, nchini Uswisi
Mbwa asaidia kukamata faranga zilizo potea bila kujulikana.
Soweto, Afrika ya Kusini - Watu wapatao wanne wamekamatwa na polisi nchini Afrika ya Kusini, kwa kosa la kukutwa na pesa zipatazo R2,8 milion.
Ukamatwaji wa pesa hizo ulifanya na mbwa wa pilisi,ambaye amefunzwa kunusa pesa.
Polisi walianza uchunguzi wao baada ya gari la kubebe pesa kupotea katika mazingira ya utata, na hadi walipo pata pesa hizo ndani ya mmoja wa wakazi wa mji wa Soweto.
Watu hao waliokamatwa na kushukiwa na wizi huu watafikishwa mahakamani hivi karibuni.
Picha hapo juu ni picha ya polisi akiwa na mbwa, ambao husaidia kufuatilia makosa na kukumata wahalifu.
Hapo chini ni picha ya mbwa wa polisi akiwa mfunzoni.
Wizi wachangia mgongano wa kisiasa, mapambo ya kumwenzi kiongozi wa UNITA ya ibiwa.
Luanda, Angola - Kaburi la marehemu kiongozi wa zamani wa UNITA Jonas Savimbi limebomolewa na kuibiwa wa baadhi ya mapambo ambayo yalikuwa yamepambwa ili kumuenzi.
Jonas Savimbi, ambaye alikuwa kiongozi aliye kuwa akiongoza UNITA, kupamabana na serikali ya Angola chini ya chama MPLA kwa kipindi kisicho pungua robo karne..
Hata hivyo viongozi wa NITA wamekuwa wakidai ya kuwa wizi huu umefanya na wanachama wa MPLA.
Pichani hapo juu ni picha ya Jonas Savimbi enzi hizo za uhahi wake, huku akiwa ndani ya magwanda ya kiafande.
Jitiada za Kofi Annan, bado kuzaa matunda, watu wazidi poteza maisha yao nchini Kenya.
Nairobi, Kenya - Mazungumzo kati ya viongozi wa Kenya Bwana Mwai Kibaki na Laila Odinga, bado yapo mashakani.
Vijana wakiwa mitaani na mapanga na malungu na vyombo vya dola vikiwa na siraha kali kama bunduki na mabomu ya kutoa machozi, ndiyo hali ambayo wanchi wa Kenya kwa sasa wanavyo ishi katika maisha yao ya kila siku.
Kiongozi mmoja wa vijana wanao andamana aliseamaya kuwa wacha waongee na Kofi Annan, lakini "sisi bado tuna tete haki zetu "
Kufuatia wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini Kenya, wanasema ya kuwa hali yakufikia makubaliano bado ipo tata, hii inakuja baada ya baadhi ya makubaliano kuwa ya kusimamisha malumbano ya kisiasa amabyo yanasababisha umwagaji wa damu.
Akiongea mmoja wa wazee wa jadi mjini Nivasha alisema, hadi viongozi hawa bwana Laila na Kibaki, watakapo jua ya kuwa hali hii itakuwa ni moja ya historia ambayo itakuwa inawafuata kila wananapo kwenda, hivyo ni vizuri wakae wakubaliane, ili kuleta amani nchini mwetu (Kenya) Hadi sasa maisha ya wananchi walio wengi nchini Kenya wanapoteza maisha kwa kilile wasicho kijua,bali wanakumbwa na mauaji ya kikabila au chuki za umaskini zilizo kuwa zikiwaleme, na sasa wanaona ni njia pekee ya kutoa hasira zao ni kulipa kwa kupitia njia ya kufanya ualifu au mauaji, alimalizia mzee huyu wa jadi ambaye anaisha mjini Naivasha.
Pichani hapo juu ni picha ya wananchi wa Kenya wakiama maeneo ambayo hawatakiwi kuishi kutokana na kutokuwa kabila la wakazi.
Picha nyingine anaonekana mtoto akiwa amekaa kenya taruma la reli, hajui la kufanya baada ya wazazi wake,kupoteana na mtoto wa kati wa machafuko ya kikabila nchini Kenya

No comments: