Wednesday, January 7, 2009

Ghana yapata rais mpya

Ghana yapata rais mpya.

Accra Ghana -7/01/09. John Atta Mills, mwenye miaka 64, ameapishwa kuwa rais wa Ghana, baada ya kushinda uchaguzi wa urais zidi ya mpinzani wake Nana Akufo Addo.
Rais John Atta Mills,ambaye aligombea urais kwa kupitia chama cha NDC - National Demokratik Kongresi, aliweza kushinda kura kwa kupata asilimia 50.23% zidi ya mpinzani wake Nana Akufo Addo aliyepata asilimia 49.77%.
Picha hapo juu anaonekana rais mpya wa Ghana, John Atta Mills, akiapa mbele ya Mungu na wananchi wa Ghana, ili kuwa rais wa Ghana.
Picha ya pili, anaonekana, rais mpya wa Ghana John Atta Mills, akiangalia kwa makini, wakati wa uchaguzi ukindelea kabla ya matokeo kutoka yakuwa, John Atta Mills ameshinda uchaguzi wa rais.
Picha ya tatu, anaonekana rais, John Atta Mills, akiwasalimia wanchama na wapenzi waliompigia kura kuwa rais.
UN - Umoja Wamataifa washikwa kigugumizi kutatua mgogoro wa Israel na Palestina.
Gaza,Ukanda wa Gaza - 4/01/09.Vita vinavyo endelea kati ya Israel na Kundi la Hamas, zimefikia hatua ya kugonisha vichwa jumuiya za kimataifa.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kisiasa katika eneo hili la mashariki ya kati,wanasema yakuwa mvutano uliopo kati ya Wapalestina na Israel,umefikia kiwango cha kuzifanya nchi za jumuiya za kimataifa kushindwa kuamua,kwa kwa kuzingatia uhusiano uliopo kati ya nchi hizi zikiongozwa na Amerika.
Hali hii imefika kutoangalia haki za binadamu kwa pande zote mbili , Israel na Wapalstina na jumuiaya ya kimataifa inaangalia huku wakitupiana maneno nani aanze kusimamisha vita.
Kwa upande wa Israel, inasema ni lazima Hamas isimamishe kabisa kutumia roket kwa kubomu ndani ya Israel,na wakati uhuo huo, Palestina chini ya Hamas na Fatah,zinadai lazima Israel, iondoke katika maeneo inayo yakalia kwa nguvu.
Picha hap juu, ianaonyesha moshi ulio jaa moto ukilipuka baada ya jeshi la Israel,kutupa mabomu yake ndani ya maene ya liyopo Gaza.
Picha ya pili wanonekana wanachama wa Hamas na na Wapalestina kwa ujumla wakiandamana kupinga kitendo cha Israel kuvamia Gaza.
Picha ya tatu, wanaonekana wanajeshi wa Israel wakimsaidia askari mwenzao, baada ya ku jeruhiwa katika mapambano na Hamas.
Picha ya nne , linaonekana jengo likilipuka baada ya kushambuliwa na mabomu kutoka kwenye helkopta za kijeshi za Israel.

No comments: