Tuesday, January 20, 2009

Baraka Hussein Obama,aapishwa rasmi kuwa rais wa 44 wa Amerika."Amerika ya pata rais wa kwanza Mwafrika ( Mweusi), ukurasa mpya umefunguliwa.

Baraka Hussein Obama, aapishwa rasmi kuwa rais wa 44 wa Amerika. "Amerika ya pata rais wa kwanza Mwafrika (Mweusi) na ukurasa mpya umefunguliwa, na ndoto imetimia.

Washington,Amerika. 20/01/09 - Baraka Hussein Obama, ameapishwa rasmi kuwa Rais wa 44 wa Amerika.
Rais, Baraka Hussein Obama, ambaye alishinda uchaguzi kwa kura nyingi zidi ya mpinzani wake kutoka chama cha upinzani cha Republikan bwana, Jonny MacCain.
Kuapishwa kwa na kukabiziwa ofisi, kumeleta msisimko mkubwa kwa jumuia ya kimataifa, kwa kuzingatia ya kuwa ni rais wa kwanza mweusi - Afrikan Amerikan, na kutimiza zile ndoto za viongozi waliopita.
Akiongea katika hutuba yake ya kwanza, baadada ya kuapishwa, rais Baraka Hussein Obama, aliiakikishia jumuia ya mataifa ya kuwa Amerika, ipo kwa kuleta amani na utulivu, na Amerika ni rafiki wa kila nchi na wananchi wake, na kuhaidi kuleta mabadiliko ndani ya Amerika na kwa jumuia ya kimataifa.
Picha ya hapo juu anaonekana rais mpya wa Amerika, Baraka Husseina Obama, akihutubia taifa mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa 44 wa Amerika.
Picha ya pili, wanaonekana baba na mama yake rais, mwafrika wa kwanza ( mweusi), Baraka Hussein Obama kuwa rais wa Amerika tangu taifa la Amerika kuundwa wakiwa wamepiga picha ya pamoja wakati wa ujana wao.
Picha ya tatu,anaonekana, rais mpya wa Amerika rais, Baraka Hussein Obama, akiwa na baba yake, Hussein Obama, wakati wa utoto wa rais Baraka Obama.
Picha ya nne, wanaonekana, wananchi wakiwa wameshikilia, kitambaa kikubwa, kilicho andikwa, hatimaye tumeshinda, (Tumevuka).
Picha ya tano anaonekana, rais wa zamani wa amerika, George Bush, akiwa ndani ya helkopta tayari kuondoka, kuelekea nyumbani, baada ya kazi ngumu ya miaka minane ya kuongoza nchi.
Picha ya sita, wanaonekana, rais mpya wa Amerika, Baraka Hussein Obama kushoto, mke wa rais wa zamani wa Amerika, Laura Bush kati kushoto, rais wazamani wa Amerika George .W. Bush, kati kulia na mke wa rais mpya wa Amerika Michelle Obama, walipo piga picha ya mwisho, kabla ya rais wa zamani wa Amerika, George Bush, kuondoka rasmi Ikulu ya Amerika.
Picha ya saba, wanaonekana, rais wa zamani wa Amerika George Bush na rais mpya wa Amerika Baraka Hussein Obama, wakikumbatiana mara baada ya rais,Baraka Hussein Obama, kuapishwa kuwa rais wa 44 wa Amerika.
Picha ya nane, ni mikono ya bwana na bibi Baraka Hussein Obama, wakila kiapo mbele ya Mungu,na wananchi wa Amerika huku wakiwa wameshikilia Biblia, na Biblia hii ilitumiwa na rais wa kumi na sita wa Amerika, Abraham Linconi.
Picha ya tisa, anaonekana rais mpya wa Amerika, Baraka Hussein Obama,akila kiapo kuwa rais wa Amerika, huku mke wake akiwa ameshikilia Biblia.
Picha ya kumi, wanaonekana, rais mpya wa Amerika, Baraka Obama, na familia yake wakiwasalimia wananchi baada ya kuapishwa kuwa rais.
Picha ya kumi na moja,anaonekana, mke wa rais mpya wa Amerika, akisalimia huku ameshikilia Biblia, ambayo mume wake,ameitumia kuapa mbela ya Mungu, ili kuwa rais wa Amerika.
Picha ya kumi na mbili, wanaonekana, rais mpya wa Amerika, Baraka Obama, na John Kerry wakiwa wanaongea mara baada ya Baraka Obama, kumaliza kuongea katika mkutanao wa kumuunga mkono, John Kerry wakati alipokuwa anaaanza kampeni ya kutaka kugombea urais mwaka 2004.
Picha ya kumi na tatu anaonekana, Baraka Obama, enzi ya toto wake, akiwa ameshikilia, fimbo ya kupigia mpira, kuonyesha ni jinsi gani alivyo kuwa tayari kupambana na kushinda.
Picha ya kumi nanne, Barka Obama, akionyesha ni jinsi gani,anaweza tawala hata kwenye maji,hii inaonekanakwenye picha hapo chini, akiwa amezungukwa na maji ya bahari.
Picha ya mwisho, anaonekana, Baraka Obama, na mama yake, Stanley Anna Dunham, wakiwa pamoja katika sehemu moja ya kuchezea watoto.

No comments: