Tuesday, January 13, 2009

Guantanamo bay,kufungwa, Obama akichukua ofisi.

Ethiopia ya ondoa majeshi yake nchini Somalia,"Wasiwasi wazidi". Addis Ababa,Ethiopia-13/01/09. Serikali ya Ethiopia, imetangaza rasmi, jeshi lake lililo kuwa linasaidia kulinda usalama nchini Somalia, limeanza rasmi kuondoka nchini Somalia kuelekea nyumbani. Kufuatia kuondoka kwa jeshi la Ethiopia,hali ya usalama nchini Somalia imekuwa katika hali ya wasiwasi kwa mujibu wa mmoja wa makzi wa mji wa Mogadishu Hata hivyo, kuna habari ya kuwa umoja wa Mataifa, upombioni kupitisha mswada wa kupeleka jeshi la kimataifa ili kulinda amani,kwani kuondoka kwa jeshi la Ethiopia, kumeacha majeshi ya Burundi na Uganda kuwa majeshi pekee ambayo yanasaidia kulinda amani kwa serikali ya Somalia. Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza awa na kazi ngumu na mgogoro wa Mashariki ya Kati.

London,Uingereza-13/01/09.Vita vinavyo endelea katia ya Izrael na Palestina,vimeleta utata na kazi kuwa ngumu kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Brair, ambaye anashughulikia swala la kuleta amani katia ya Waizrael na Wapalestina.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Brair,ambaye anashughulikia kuinua maendeleo ya Wapalestina kwa ujumla waishio wa Gaza na West Bank, amekuwa akikumbana na wakati mgumu kwa kuzingatia vita vinavyo endelea kati ya kati ya Izrael na Palestina.aliyaongea haya Mustafa Barghouti amabye ni mmoja ya viongozi wa serikali ya Wapalestina.
Picha ya pili anaonekana Tony Brair,akiwa anasikiliza kwa makini waswali anayo ulizwa kuhusu mgogoro kati ya Izrael na Palestina katika moja ya mikutano na waandishi wa habari.
Picha ya pili wanaonekana , Tony Brair na rais wa Wapalestina, Mahamoud Abbas walipo kutana hivi karibuni kujadiri maendeleo ya Wapalestina.
Guantanamo Bay kufungwa, Obama akianza kazi.
Washington, Amerika-13/01/09.Rais mchaguliwa wa Amerika, Baraka Obama,atatia sahii kufungwa mara moja kwa gereza la Guantanamo Bay, mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Amerika, Gantanamo Bay, imekuwa jela ya kuwafungia watuhumiwa wanao shukiwa kuhusika na ugaidi.
Baraka Obama, ataapishwa kuwa rais, siku ya jumanne 20/01/09.
Picha hapo juu anaonekna , rais mtarajiwa wa Amerika, Baraka Obama, akiongea katika moja ya mikutano, na amekuwa akisisitiza kufungwa kwa gereza la Guantanamo Bay, kwani linailetea sura mbaya Amerika.
Picha ya pili wanaonekana watuhumiwa ( wafungwa) wakiwa ndani ya jela ya Guantanamo Bay, ambamo wengi wa wafungwa hawa wamekaa muda mrefu katika jela hiyo bila kuhukumiwa.
Picha ya tatu, wanaonakana, wanajeshi wa Amerika, wakiwa wana wachunga baadhi ya watuhumiwa wanao shutumiwa kuhusika na ugaidi.
Simu ya waziri mkuu ya fanya kura kutopigwa "jibu ni mgogoro wa Izrael na Palestina".
Jerusalem,Israel-13/01/09. Waziri Mkuu wa Izrael, Ehud Olmert, amesema yakuwa alimpigia simu rais George Bush, kuomba Amerika isipige kura kupitisha kura ya kutaka kusimamisha mapigano kati ya Izrael na Palestina.
Kufuatia hatiua hiyo, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika,Condoeezza Rice, aliacha kupiga kura na kutoka katika kikao cha kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
Picha hapo juu, wanaonekana, Condoleezza Rice akisalimiana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, mapema walipo kutana nchini Izrael, kujadiri mgogoro wa Izrael na Palestina.
Picha ya pili, wanaonekana wajumbe wa kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa, wakiwa katika moja ya kikao ili kujadili maswala ya kiusalama yanayo ikabili swala la Mashariki ya Kati.
Picha ya tatu, anaonekana,Condoleezza Rice, akiwa katika kikao cha kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa, wiki iliyo pita kujadili swala la amani ya Mashariki ya Kati.
Mkutano wa nchi za Kiaarabu,utakao fanyika Doha, wawa na mvutano.
Doha, Katar-13/01/09. Serikali ya Misri,imekataa kukubaliana na jumuia ya nchi za Kiaarabu kutumia mkutano unao tarajiwa kufanyika mjini Doha,tarehe 18/01/09,kujadiri swala la vita vinavyoendelea katia ya Israel na Palestina.
Kikao hicho, hicho cha jumuia ya Kiaarabu, ambao unatarajia kuzungumzia maswala ya kiuchumi, huenda ukakumbwa na mvutano mkubwa, kati ya nchi wanachama wa jumuia hiyo.
Picha hapo juu ni ya nchi ya Misri, nchi ambayo ina shughulika, swala la kuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina kwa Muda mrefu,bila mafanikio ya kusimamisha vita hivi milelel.
Picha ya pili ni ya Katibu wa jumuia ya Kiaarabu, Amr Moussa akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kikao kuhusu swala la mgogoro wa mashariki ya kati nadi ya UN- Umoja wa Mataifa

No comments: