Thursday, January 8, 2009

Mashoga wafungwa miaka kwa kuwa mashoga.

Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi zachafua jina la letu"China ya dai"

Beijing,China-08/01/09.Waziri wa mambo ya nje ya China Quin Gang, ameziliaumu nchi za Magharibi kwa kutumia vyombo vya habari kuharibu jina la nchi yake China.
Akisisitiza ya kuwa nchi kama Zimbabwe na Jamuhuri ya Kongo (DRC) ya kuwa zina fanya biashara na China kinyume cha sheria katika ununuzi wa siraha, hii siyo kweli.
Waziri, Quin Gang, alisema kwa mtu au shirika lolote likichunguza kwa undani, wataona yakuwa yote wanayo sema siyo ya kweli.
Picha ya hapo juu, ni ya bendera ya China, nchi ambayo inasema vyombo vya habari ya Magharibi vina chafua jina la nchi ya China.
Picha ya pili ni ya moja ya vyombo vya habari,ambavyo vinadaiwa kuchafua jina la China, kwa kutangaza mambo yasiyo ya kweli.
Mashoga wafungwa miaka kwa kuwa mashoga.
Dakar, Senegal-08/01/09- Watu tisa wamehukumiwa kwenda jela miaka minane, baadada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na maswala ya ushoga.Kwa mujibu wa mwanasheria wa watuhumiwa hao,Diadji Diouf.
Picha hapo juu ni ya bendera ya nchi ya Senegal,nchi ambayo ushoga ni kinyume na sheria ya nchi.Picha ya pili ni ya bendera ya jumuiya ya mashoga.
Picha ya tatu wanaonekana mashoga wakibusiana,kuwepo kwa mashoga katika nchi nyingi za Afrika ni kinyume na sheria, lakini mashoga waishio Ulaya, wamekuwa wanapata haki sawa kama binadamu wengine.
Jumuiya ya Ulaya na Urusi bado kukubalina kuhusu swala la gasi.
Brussel,Belgium-08/01/09.Jumuiya ya Ulaya imekuwa na mazungumzo na kampuni ya mafuta ya Urusi Gazprom, ambayo imefunga usambazaji wa gasi katika nchi za jumia ya Ulaya.
Ufungaji wa usambazaji wa gas, umekuja baada ya Urusi kudai ya kuwa Ukrein imefungua bomba linali sambaza gas Ulaya, na kusamba za gasi hiyo nchini Ukrein.
Mvutano huo wa gasi, umekuja baada ya serikali ya Ukrein kushindwa kukubaliana kimsingi juu ya bei ya gasi.
Picha hapo juu ni moja ya mitambo ya kusambazia gasi,ikikaguliwa na mmoja ya wafanyakazi, hasa kwa kipindi hiki cha baridi katika nchi za Ulaya.
Picha ya pili ni ya bendera ya Urusi nchi ambayo ndiyo msambazaji mkuu wa gasi katika nchi nyingi za Ulaya.
Picha ya tatu, ni ya bendera nchi za jumuiya ya Ulaya, nchi hutegemea gasi kwa matumizi kutoka Urusi.
UN- Umoja wa Mataifa wanyanyua mikono juu, kutokuendelea kutoa misaada Gaza."Hadi hapo hali ya usalama itakapo kuwepo"
Gaza, Ukanda wa Gaza-08/01/09.Shirika la kutoa misaada la Umoja wa Mataifa, limesimamisha misaada yake yote kuelekea eneo la Gaza.
Uamuzi huuo umekuja baada ya mmoja ya wafanyakazi wake kushambuliwa na kupoteza maisha wakati jeshi la Isreal lilipo shambulia msafara wa misaada ya vyakula na madawa vilivyokuwa vikielekea Gaza.
Picha hapo juu linaonekana moja ya gari la kubebea wagonjwa likiwa njiani kuwapeleka majeruhi ambao wamajeruhiwa katika vita vinavyo endelea kati ya Israel na Palestina katika eneo la Gaza.
Picha ya pili, linaonekana lori likiwa limebeba shehena kuelekea Gaza, lakini hata hivyo magari hayao yamekuwa yakukutwa na misukosuko na mengine kutokufika yanapo takiwa kupeleka misaada.
Picha ya tatu, zinaonekana baadhi ya majengo yakiwa yamezunguka mosho unaotoka katikati, baadaya ya eneo hilo kushambuliwa na jeshi la Israel.

No comments: