Wakazi wa Kigali wastuliwa na milipuko ya mabomu.
Kigali, Rwanda - 20/20/2010. Milipuko ya mabomu imetokea sehemu tatu tofauti katika jiji la Kigali na kusababisha kifo cha mtu mmoja na watu zaidi ya 18 kujeruhiwa na watano kati ya majeruhi hao vibaya.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, watu wawili wamekamatwa "hawa watu walio kamatwa ni kati ya wale watu wanaotaka kuleta vurugu kwa kutishia amani na ni watu wa kundi la Interahamwe" alisema msemaji huyo.
Hata hivyo serikali ya Rwanda imeanza uchunguzi mara moja kuhusiana na milipuko hiyo ya mabomu.
Milipuko hiyo imekuja wakati wananchi wa Rwanda wanajiaanda kufanya uchaguzi wa kumchagua rais mnamo mwezi wa August.
Picha hapo juu ni ya bendara ya Rwanda nchi ambayo miaka kumi na nane iliyo pita kulitokea mauaji kati ya watu jamii ya Watutsi na watu jamii ya Wahutu na watu wengi welipoteza maisha.
Matokea ya uchaguzi Ukrain shwali.
Kiev, Ukrain - 20/02/2010. Mgombea wa chama pinzani katika kiti cha urai wa Ukrain bi Yulia Tymoshenko amefuta kesi ya malalamiko ya madai ya kutaka matokeo ya uchaguzi kurudiwa kuhesabiwa, baada ya mpinzani wake Victor Yanukovych kushinda katika uchaguzi wa urais ulio fanyika mapema mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari bi Yulia Tymoshenko alisema "Haina haja ya kuendela na kesi kwa hali halisi ya koti inajionyesha yakwa hakuna kitu kitabadilisha matokeo."
Bi Yulia Tymoshenko, alifungua kesi kwa madai ya kuwa kulikuwa kunaukiukwaji wa sheria wakati wa uchaguzi na wakati wa kuzihesabu kura.
Picha hapo juu anaonekana, bi Yulia Tymoshenko akiondoka ndani ya mahakama baada ya kusikia kesi ya madai aliyo yaleta mbele ya koti inayo shughulika kesi za sheria ya uchaguzi.
Rais wa Niger angolewa madarakani na jeshi.
Niamey, Niger - 20/02/2010. Malfu ya wananchi wameandamana jijini Niamey kuunga mkono kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mamadou Tandja.
Maandamano hayo ambayo yaliishia katika majengo ya ukumbi wa bunge la Niger kwa kuonyesha shukurani kwa jeshi kwa uamuzi wa kumtoa madarakani rais huyo, ambaye alijiongezea muda wa kuongoza nchi.
Hata hivyo jeshi la nchi hiyo limehaidi kuanda uchaguzi muda si mrefu na kurudisha madaka kwa serikali ya kiraia..
Picha hapo juu wanaonekana wanajeshi wakiwa wanaangalia usalama wakati wa maandamano.
Saga la Afghanistan lasababisha kuvunjika kwa serikali.