Saturday, February 13, 2010

Rais wa zamani wa Amerika aruhusiwa kutoka hospitai.

Rais wa zamani wa Amerika aruhusiwa kutoka hospitali.

New York, Amerika - 13/02/2010. Aliyekuwa rais wa Amerika, Billy Clinton ameruhusiwa kutoka hospital baada ya kufanyiwa operasheni ndogo ya ili kuruhusu damu iweze kufanya kazi yake mwilini vizuri.
Operasheni hiyo iliyo fanywa kwenye moyo, ilifanyikia katika hospital New York.
Billy Clinton, aliyekuwa rais wa Amerika kwa miaka minane 1993-2001, alionekana akitokea hospitali kuelekea nyumbani.
Picha hapo juu, ni yaaliye kuwa rais wa amerika Billy Clinton,ambaye amefanyiwa operasheni wa moyo hivi karibuni.
Picha hapo juu,ni ya Dr Schwartz akiongea na wandishi wa habari, mara baada ya kumaliza operasheni ya aliyekuwa rais wa Amerika Billy Clinton.
Wasudan kuanza kampeni ya kumchagua rais nchi.
Khartoum, Sudan - 13/02/2010. Kampeni za uchachaguzi zimeanza nchini Sudan kugombea kiti cha urais wa Sudan.
Wagomea urais wapatao 12 wanafanya kampeni ya kugomea kiti hicho ambacho kwa sasa kina shikliwa na rais Omar Al Bashir.
Uchaguzi huo utakaofanyika April 11,utafungua njia ya kupiga kura ya maoni mnamo mwaka 2011.
Mpinzani mkubwa wa rais, Omar Al Bashir,ni Yasser Arman 49, ambaye alisha wahi kuwa waziri mkuu na mwanacham wa Umma Party.
Picha hapo juu wanaonekana kulia rais wa sasa wa Sudan Omar Al Bashir na mpinzani wake mkuu Yasser Arman, ambaowatachuana vikali kugombe kiti cha urais wa Sudan.
NATO yapania kuukomboa mjiwa Marjah.
Marjah, Afghanistan-13/02/2010. Jeshi la NATO na jeshi la Afghanistan, chini ya uongozi wa US limeanza kampeni ya kuukomboa mji wa Marhaj kutoka mikononi mwa kundi la Taliban.
Kampeni hiyo iliyo anza rasmi mapema leo alfajiri,inajulikana kama Operasheni Moshtarak ,amboyi nia ni kuukomboa mji hua na kukukabidhi chini ya serikali.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa kundi la Taliban, alisema ya kuwa wapiganaji wake watapigana hadi mtu wa mwisho ili kuilinda nchi yao iliyo vamiwa na jeshi la kigeni.
Picha hapo juu wanaonekana wanajeshi wakielekea mstari wa mbele na huku mbwa wa kunusa mabomu akiwa kazini tayari kupambana kundi la Taliban.

No comments: