Thursday, February 18, 2010

Hali ya usalama wa rais wa Niger mashakani.

Hali ya usalama wa rais wa Niger mashakani. Niamey,Niger - 19/02/2010. Jeshi nchini Niger limemteka nyara rais wa Niger Mamadou Tandja, baada ya kuvami makazi yake. Kwa mujibu wa watu waliona tukio hilo walisema" walisikia milio ya risas wakti inaaminika rais alikuwa akiongoza mkutano. Habari zinasema jeshi limemchukua rais ili atangaze kujiudhulu urais. Niger imekuwa katika mvutano wa kisiasa, tangu rais Tandja alipo jitangazia kujiongezea madaraka, jambo ambalo halikukaribishwa na jumuia ya kimataifa. Picha hapo juu anaonekana rais wa Niger, Mamadou Tandja, akihutubuia wanachi hivi karibuni kabla ya kukamatwa. Rais wa Amerika akutana na Dalai Lama. Washington, Amerika - 19/02/2010. Rais wa Amerika Baraka Obama, amekutana na kiongozi mwana harakati wa kutetet haki za Watibeti katika Ikulu ya Amerika leo. Viongozi hawa wawili walikutana licha ya China kupinga mkutano huo wa kiongozi wa Watibeti na rais wa Amerika. Picha hapo juu, kulia ni kiongozi wa Watibeti Dalai Lama na kulia ni rais Baraka Obama, ambao wamekuta kwa mazungumzo ya faragha katika ofisi za Ikulu. Interpol watoa picha za washukiwa. Riyadh, Saudi Arabia - 18/02/2010.Police wa kimataifa Interpol imetoa picha na majina ya watu ambao wanashukiwa kuhusika katika mauaji ya aliyekuwa kamanda masaidizi wa kundi la Hamas, Mahmoud al Mabhouh wakati alipo kuwa nchini Dubai. Kwa mujibu wa Intarpol "watu walio husika na mauaji hayo watakamwa kutokana na ushirikiano wa nchi tofauti." Hata hivyo watu hao wanashukiwa kwa kutumia paspoti zisizo halisi na inasadiwa paspoti hizo ziliibiwa au kutolewa kinyume cha sheria. Picha hapo juu ni zawatu wanaoshukiwa katika mauaji ya aliyekuwa kamanda wa wa kundi la Hamas hivi karibuni.

No comments: