Monday, February 8, 2010

Kosta Rika yapata rais mwanmke kwa mara ya kwanza.

Kosta Rika yapata rais mwanamke kwa mara ya kwanza. Santa Jose, Kosta Rika - 08/02/2010. Matokea ya uchaguzi mkuu wa Kosta Rika yamempa ushindi mkuwa mgombea uchaguzi wa kiti cha urais Bi, Laura Chinchila kwa ushindi wa asilimia 47% dhidi ya wapinzani wake. Bi, Laura Chinchila, amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Kosta Rika, aligombea kiti hicho kupitia chama tawala. Picha hapo juu anaonekana, rais mtalajiwa wa Kosta Rika,Bi, Laura Chinchila, akiwaonyesha kidole gumba juu baada ya kutangazwa kuongoza matokeo ya uchaguzi.

Irani kuanza kurutubisha madini ya nyuklia.
Tehran, Iran - 08/02/2010. Serikali ya Iran imekabidhi waraka kwa shirika linalo shughulikia ukaguaji wa nguvu za nyuklia na kusema ya kuwa itaendelea kurutubisha madini ya nyuklia kufikia 20% kuanzia jumanne.
Barua hii imekabidhiwa, baada ya rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad kuagiza yakuwa kazi ya kurutubisha madini ya nyuklia kuanza mara moja.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, katikati akikagua maendeleo ya moja ya mtambo wa kinyukli hivi karibuni.
Kiongozi wa upinzani nchini Sri Lanka akamatwa.
Kolombo, Sri Lanka - 08/02/2010. Aliyekuwa mgombea mpinzani wa kiti cha urais wa Sri La, General Fonseka ametiwa kizuizini na askari wa kijeshi.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, General Prasad Samarasinghe,alisema " General amekamatwa kutokana na makosa aliyo yafanya wakati alipo kuwa kazini kama mkuu wa jeshi.
Hata hivyo, kiongozi mmoja wa cha kisiasa, Sri Lanka Muslim Congress Rauff Hakeem, alisema "General Fonseka alikamatwa mbele yetu kwa kudhalilihswa."
Picha hapo juu ni ya General Fonseka, ambaye yupo kizuizini kwa sasa.

No comments: