Thursday, August 28, 2014

Hamas na Izrael wa kubaliana suruhu.

Hamas na Izrael wa kubaliana suruhu.

Gaza/Jerusalem - Makshariki ya Kati - 28/08/2014. Izrael na wapiganaji wa kundi la Palestina wafikia makubaliano ya kusimamisha mapigano.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, viongozi wa pande zote mbili walidaikuwa kila upande umepata ushindi.

Akiongea kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa makubaliano hayo 26/08/2012 jiji Kairo, waziri mkuu wa Izrael Benjamin Netanyahu alisema '' tumelitia adabu kundi la Hamas, na Izrael haikukubaliana na masharti yaliyo tolewa na kundi la Hamas katika mazungumzo yaliyo fanyika Misri Kairo.''

'' Na hatutafungu bandari au kiwanja cha ndege au kuondoa vizuizi na hatuta kubali au kuruhusu kundi la Hamas kurusha roketi zake ndani ya Izrael.''Aliongezea waziri Netanyahu.

Nalo kundi la Hamas limesema kupitia msemaji wake Sami Abu Zuhri '' Huu ni ushindi kwa Wapalestina wote, na bila kupambana hii hali isingetokea, bado tuendeleza mapambano mpaka Palestina itakapo pata haki yake.''

Vita kati ya Hamas na Izrael vimechukua siku 50, ambapo Wapalestina  2,139 walifariki dunia kutokana na mashambulizi ya kutoka jeshi la Izrael, na kwa upande wa watu 70 walipoteza maisha yao kati yao 64 wanaj
wanajeshi wa Izrael na raia sita.

Kwa mujibu wa habari kutoka katika kikao cha makubaliano, pande zote mbili zimekubaliana kusimamisha mapigano kwa muda wa mwaka.

3 comments: