Iss yatangaza vita zidi ya Marekani.
Tikrit, Iraq - 19/08/2014. Wapiganaji wa kundi la ISS la Irak wamebakia wakilishirilia mji wa Tirkit, baada ya jeshi la Iraq kushindwa kuendelea na mashambulizi kutokana na kukosa vifaaa vya kijeshi.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi ambaye hakutaja jina lake alisema '' imebidi tusimamishe mashambulizi yetu, kwani wapiganaji wa ISS wapo na vifaa vya kisasa na pia hatuna vifaa ya kutegua mabomu ambayo yametegwa karibu kila eneo la kuingia mji wa Tikrit.''
Mji wa Tikrit ambao ni makazi na alipo zaliwa na kuzikiwa aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein, umekuwa chini ya wapiganaji wa kundi ISS, ambalo lina pingana na serikali ya Irak.
Kundi la ISS limetangaza kuwa ''litafanya mashambulizi kwa Marekani na washiriki wake wakati wowote na mahali popote kuanzia sasa.''
Kundi la ISS linapambana na jeshi la Irak, jeshi la Wakurdi ambapo yanapata msaada kutoka kwa Marekani na washiriki wake, jambo ambalo limefanya hali ya usalama nchi Irak kuzidi kuwa tete zaidi.
Kenya kuwe ugumu kuingia nchini humo.
Nairobi, Kenya - 19/08/2014. Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itasimamisha usafiri wa anga kutoka nchi ambazo zimekumbwa na ugonjwa wa ebola.Uamuzi huo umekuja baada ya utafiti kufanywa na wataalamu wa afya nchini Kenya na kuonekana kuwa kuna hatari ya Kenya kukumbwa na ugonjwa huo kutokana na kuwa kiungo cha ndege nyingi zitokazo na kuingia nchini humo kutoka sehemu tofauti katika bara la Afrika.
Nchi ambazo zitahathirika na kusimamishwa kwa usafiri wa anga ni pamoja na ''Liberia na Nigeria''
Ugonjwa wa ebola umekuwa tishio hasa kwa nchi za Afrika ya Magharibi na kusabibisha vifo vya watu 1000 mpaka sasa, na kufanya shirika la afya dunia WHO kutangaza vita rasmi zidi ya ugonjwa huu.
No comments:
Post a Comment